Kurdus bin Zuhayr bin Harth al-Taghlibi
Kurdus bin Zuhayr bin Harth al-Taghlibi (Kiarabu: كردوس بن زهير التغلبي) (aliuawa shahidi 61 Hijiria). Yeye ni miongoni mwa mashahidi wa Karbala na masahaba wa Imamu Ali (a.s). Kurdus alikuwa katika jeshi la Imamu Ali (a.s) katika vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan. Akiwa pamoja na kaka zake Muqsit na Qasit aliungana na msafara Imamu Hussein (a.s) wakati wa usiku na aliuawa shahidi katika Siku ya Ashura.
Nasaba
Kurdus bin Zuhayr bin Harth bin al-Taghlibi, alikuwa akinasibishwa na kabila la Taghlib na kwa msingi huo katika kitabu cha Absar al-Ain jina liko katika orodha ya mashahidi wa Kitaghlibi.[1] Katika kitabu cha Waq'at Siffin ametajwa kama "mtoto wa kiongozi wa kabila la Taghlib".[2]
Majina mengine ya Kurdus ni Kursh na Kurdush. Kadhalika imeelezwa kuwa baba yake ni: "Abdallah bin Zuhayr".[3]
Kushiriki Vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan
Muhammad bin Tahir Samawi (1292-1370 Hijiria) anasema katika kitabu cha Ibsar al-Ain kwamba, Kurdus alikuwa miongoni mwa wanajeshi wa Imamu Ali (a.s) katika Vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan na kwa muktadha huo, amenukuliwa maneno kuhusiana na vita hususan vita vya Siffin.[4] Kadhalika Samawi amemtambua Muqsit kuwa ni katika masahaba wa Imamu Hassan.[5]
Kuuawa Shahidi Karbala
Kurdus alikuwa akiishi Kufa na baada ya Imamu Hussein (a.s) kuwasili Karbala, akiwa pamoja na kaka zake Muqsit na Qasit aliungana wakati wa usiku na msafara Imamu Hussein (a.s) na aliuawa shahidi Siku ya Ashura.[6]
Katika Ziyarat al-Shuhadaa, yeye na kaka yake Qasit wanasalimiwa kwa maneno ya: "Assalaam Aal Qasit wa Kurdus Ibn Zuhayr al-Taghlibeyn" na ametajwa kuwa miongoni mwa mashahidi wa Karbala".[7]
Rejea
- ↑ Munqiri, Waqiatu sifiin, 1382 H, uk. 487.
- ↑ Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, uk. 200.
- ↑ Ḥusaynī al-Ḥāʾirī, Dhakhīrat al-dārayn, uk. 545.
- ↑ Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, uk. 200.
- ↑ Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, uk. 200.
- ↑ Samāwī, Ibṣār al-ʿayn, p. 200.
- ↑ Ibn Mashhadī, al-Mazār al-kabīr, uk. 494; Shahid Awal, Al-mizaar, 1410 H, uk. 153.
Vyanzo
- Ḥusaynī al-Ḥāʾirī al-Shīrāzī, al-Sayyid ʿAbd al-Majīd al-. Dhakhīrat al-dārayn fī-mā yataʿallaq bi-maṣāʾib al-Ḥusayn ʿalayhih al-salām wa aṣḥābih. Qom: Nashr-i Zamzam-i Hidāyat, n.d.
- Ibn Mashhadī, Muḥammad b. Jaʿfar. Al-Mazār al-kabīr. Edited by Jawad Qayyūmī Iṣfahānī. Qom: Jāmiʿa-yi Mudarrisīn Hawza ʿIlmīyya Qom, 1419 AH.
- Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār al-jāmiʿa li-durar akhbār al-aʾimma al-aṭhār. 2ned edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403AH.
- Naṣr b. Muzāḥīm al-Minqarī. Waqʿat Ṣiffīn. Edited by ʿAbd al-Salām Muḥammad Hārūn. 2ned edition. Cairo: al-Muʾassisat al-ʿArabīyyat al-Ḥadītha, 1382 AH.
- Samāwī, Muḥammad b. Ṭāhir al-. Ibṣār al-ʿayn fī anṣār al-Husayn ʿalayhi al-salām. Qom: Intishārāt-i Dānishgāh-i Shahīd Mahallātī, 1419 AH.
- Shahīd al-Awwal, Muḥammad b. Makkī al-. Al-Mazār. Edited by Muḥammad Bāqir Muwaḥḥid Abṭaḥī. Qom: Madrisa Imām Mahdī (a), 1410 AH.