Muqsit bin Zuhayr al-Taghlibi
Muqsit bin Zuhayr bin Harth al-Taghlibi (Kiarabu: مقسط بن زُهير بن حرث التغلبي) (aliuawa shahidi 61 Hijria). Huyu ni mmoja wa masahaba wa Imamu Ali (a.s) na ni miongoni mwa mashahidi wa Karbala.
Muqsit alikuwa katika jeshi la Imamu Ali (a.s) katika vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan. Akiwa pamoja na kaka zake Kurdus na Qasit aliungana na msafara Imamu Hussein (a.s) wakati wa usiku na aliuawa shahidi Siku ya Ashura.
Nasaba
Muqsit bin Zuhayr bin Harth bin al-Taghlibi, alikuwa akinasibishwa na kabila la Taghlib na kwa msingi huo katika tukio la Karbala jina lake liko katika orodha ya mashahidi wa Kitaghlibi.[1]
Kushiriki katika Vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan
Muhammad bin Tahir Samawi (1292-1370 Hijiria) anasema katika kitabu cha Ibsar al-Ain kwamba, Muqsit aliikuwa miongoni mwa wanajeshi wa Imamu Ali (a.s) katika vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan na kwa muktadha huo, yamenukuliwa maneno kutoka kwake kuhusiana na vita hususan vita vya Siffin.[2] Kadhalika Samawi amemtambua Muqsit kuwa ni katika masahaba wa Imamu Hassan (a.s).[3]
Kuuawa Shahidi Karbala
Kwa mujibu wa Samawi, Muqsit alikuwa akiishi Kufa na baada ya Imamu Hussein (a.s) kuwasili Karbala, akiwa pamoja na kaka zake Kurdus na Qasit aliungana na msafara Imamu Hussein (a.s) wakati wa usiku na aliuawa shahidi Siku ya Ashura.[4]
Katika Ziyarat al-Shuhadaa, kaka zake Kurdus na Qasit wametajwa kuwa miongoni mwa mashahidi wa Karbala[5], lakini jina lake halijatajwa.
Rejea
Vyanzo
- Ibn Mashhadī, Muḥammad. Al-Mazār al-kabīr. Edited by Jawād Qayyūmī. 1st edition. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1419 AH.
- Ibn Shahrāshūb, Muḥammad b. ʿAlī. Manāqib Āl Abī Ṭālib. Qom: Nashr-i ʿAllāma, 1379 Sh.
- Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. 2nd edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
- Samāwī, Muḥammad b. Ṭāhir al-. Ibṣār al-ʿayn fī anṣār al-Ḥusayn (a). Qom: Dānishgāh-i Shahīd Maḥallātī, 1419 AH.
- Shahīd al-Awwal, Muḥammad b. Makkī. Al-Mazar. Edited by Madrisa-yi Imām Mahdī (a), Muḥammad Bāqir Muwaḥḥidī Iṣfahānī. 1st edition. Qom: Madrisa-yi Imām Mahdī (a), 1410 AH.