Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Dua ya Hamsini na Mbili ya Sahifa Sajjadiya

Kutoka wikishia
Dua ya Hamsini na Mbili ya Sahifa Sajjadiya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa mnamo Sha'ban 1102 AH.

MadaDua iliyokuwa ikitumiwa na Imam Sajjad (a.s), wakati wa kumuombwa Mola wake hifadhi dhidi ya ujanja na njama za maadui zake.
Ina Mapokezi au Haina MapokeziIna Mapokezi
Imenukuliwa Kutoka kwaImamu Sajjad (a.s)
MpokeziMutawakkil ibn Harun
Vyanzo vya KishiaSahifa Sajjadiyah
Dua ya Tawassuli • Dua ya Kumaili • Dua ya Nudba • Dua ya Samati • Dua ya Faraji • Dua ya Abu Hamza Thumali • Ziara ya Ashura • Ziara ya Jamiat Kabira • Ziara ya Warith • Ziara ya Aminu-Llah • Ziara ya Arobaini

Dua ya Hamsini na Mbili ya Sahifa Sajjadiya (Kiarabu: الدعاء الثاني والخمسون من الصحيفة السجادية) ni moja ya dua maarufu itokayo kwa Imamu Sajjad (a.s). Dua hii inalenga kumsihi na kumuomba Mwenye Ezi Mungu kwa bidii ili muombaji aweze kutimiziwa matilaba yake. Katika dua hii, kuna muktadha maalumu unaorejelewa nguvu na uwezo wa Mungu pamoja ambaye elimu Yake imevienea na kuvitawala viumbe vyote. Zaidi ya hayo, pia dua hii inaelezea safari ya lazima ya vimbe inayowakabila kwenye muelekeo wa kurejea kwa Mola. Katika dua hii, baada ya Imam Sajjad (a.s) kuwasilisha mpungufu aliyonayo binadamu mbele ya Mola wake, anaendelea kumwomba Mwenye Ezi Mungu kwa bidii kabisha na bila ya kuchoka, akimtaraji Mola wake kumtimizia mahitaji yake. Miongoni mwa mada nyingine zilizomo duani humo, ni pamoja na sifa za wale wanaovutiwa na ulimwengu, pamoja na hisia hasi alizonazo Imamu Sajjad (a.s) dhidi ya ushirikina.

Tafsi na Ufafanuzi wa Dua ya Hamsini na Mbili unapatikana kwa lugha mbali mbali kupitia vitabu vya tafsiri za kitabu cha Sahifa Sajjadiya. Miongoni mwa vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiajemi, vyenye tafsiri chambuzi za dua ya hamsini na mbili sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya, ni kitabu kiitwacho Shuhud wa Shenakht kilichoandikwa na Hasan Mamduhi Kermanshahi. Aidha kwa upande wa Kiarabi, kitabu maarufu chenye ufafanuzi wa dua hii pamoja na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya, ni kile kitabu kiitwacho Riadhu al-Salikina kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani.

Mafunzo ya Dua ya Hamsini na Mbili ya Sahifa Sajjadiyya

Dua ya Hamsini na Mbili ni miongoni mwa maombi tukufu za kitabu cha Sahifa Sajjadiyya, nayo ni ile dua inayoonesha jinsi ya Imam Sajjad (a.s) alivyokuwa akisisitiza na kudumu katika kutafuta matilaba yake mbele ya Mola wake Mlezi. Kulingana na uchambuzi wa kiuandishi wa Hasan Mamduhi Kermanshahi aliokuja nao wakati wa kufasiri dua hii ni kwamba; hakuna tofauti kati ya sisitizo linalomtaka mja kufikisha ombi lake kwa Mola wake, sisitizo linalomtaka mja kujidhatiti na kudumu katika maombi yake bila ya kuchoka, huku akimtaraji Mola wake kumtimizia haja yake.[1]

Mafundisho ya dua ya hamsini na mbili yamekuja katika vipengele vifuatavyo:

  • Utawala wa elimu ya Mwenye Ezi Mungu uliotanda juu ya uwepo wote kwa jumla (kutokuwepo kwa jambo lolote lisilo dhahiri ndani ya Uungu si lile lililoko ardhini wala mbinguni).
  • Kutowezekana kwa kutoka nje ya mamlaka ya Mwenye Ezi Mungu hali ya kwamba sote ni wenye ufukara wa dhati katika uhitaji wa riziki zake.
  • Watumishi wenye unyenyekevu mkubwa ni wale wenye utendaji kubwa kwenye mchakato wao wa utekelezaji wa maagizo ya Mwenye Ezi Mungu.
  • Mwabudu wa isiye kuwa Mungu huku akiwa ni mlaji (mtumiaji) wa neema Zake, ndiye mtumwa duni zaidi mbele ya Mwenye Ezi Mungu.
  • Kukanusha uwepo wa Mwenye Ezi Mungu kunatokana na dhana zisizo sahihi juu Yake.
  • Kukanusha wajumbe wa Mwenye Ezi Mungu kunahusiana na ushirikina.
  • Kuenea kutanda kwa nguvu za Mwenye Ezi Mungu ulimwenguni mwote.
  • Kutowepo uwezekano wa kupata maisha ya milele kwa yule asiyeridhika na kitendo cha kukutana na Mola Wake
  • Uhakika (uwazi) wa tukio la kifo kwa jamii nzi ya wanadamu waumini pamoja na makafiri.
  • Kujitenga na yeyote atakayemuabudu asiyekuwa Mwenye Ezi Mungu.
  • Kukiri mapungufu na uchache wa vitendo na ukuu wa kosa pamoja na dhambi mbali mbali mbele ya Mwenye Ezi Mungu.
  • Tabia za waliodanganywa na ulimwengu: falsafa ya upuuzi, uzembe, kuzubaika na ulimwenguni na kuhadalika moyo zao kutokana na wingi wa baraka.
  • Matamanio ya nafsi ndiyo kizuizi cha maendeleo ya kibinadamu.
  • Kushikamana na Maombi ya kumuomba Mwenye Ezi Mungu, licha ya kuwepo kwa matarajio ya nafsi juu ya kupata kitu fulani.
  • Kushikamana na Maombi ya kumuomba Mwenye Ezi Mungu, licha ya kuwepo kwa utawala wa ulimwengu dhidi ya binadamu.
  • Kushikamana na Maombi ya kumuomba Mwenye Ezi Mungu, licha ya wingi wa dhambi.
  • Kutafuta matilaba kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu ambaye hakuna Mola mwingine Melzi ispokuwa Yeye peke yake.
  • Taufiki ya kujitenga na uhitaji wa kumhitajia asiyekuwa Mungu, inayopatikana kupitia ibaya ya kumuabudu Mungu wa haki.
  • Ombi la kuondolewa mapenzi ya kidunia kupiti nyenzo ya khofu kwa Mwenye Ezi Mungu
  • Kukimbilia kwa Mwenye Ezi Mungu sambamba na kumwogopa.
  • Umuhimu wa kutawakali (tawakkul) kwa Mwenye Ezi Mungu na kutegemea ukarimu na taadhima Yake (uungwana Wake).
  • Utumwa kamili na kuelekeza fikra zote kwa Mwenye Ezi Mungu ndio shauku kuu ya mwadamu mkamilifu (insan kamil).[2]

Tafsiri Chambuzi za Dua ya Hamsini na Mbili

Dua ya hamsini na mbili kutoka katika kitabu cha Sahifa Sajjadiya imefasiriwa na kufafanuliwa kwa lugha kuptia vita vilivyoshughulikia kutoa tafsiri chambuzi za dua zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni vya vitabu vilivyofanya kazi hiyo kwa lugha ya Kiajemi ni pamoja na; kitabu kiitwacho Diaru Ashiqan kilichoandikwa na Hussein Ansarian,[3] Shuhud wa Shinakht cha Muhammad Hassan Mamdouhi Kermanshahi,[4] pamoja na Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyya kilichoandikwa na Sayyid Ahmad Fahri.[5]

Pia Kuna kazi dhaa zilizoandikwa kwa lugha ya Kiarabu katika juhudi za kuichambua na kuifafanua dua hii ya hamsini na mbili sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiya. Mingoni mwa vitabu vilivyoshughulikia kazi hii ni pamoja na; kitabu kiitwacho Riadh al-Salikin kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani,[6] Fi Dhilali al-Sahifa al-Sajjadiyya kilichoandikwa na Muhammad Jawad Mughniyah,[7] Riadh al-Arifina kilichotungwa na Muhammad bin Muhammad Darabi,[8] pamoja na kitabu kiitwacho Afaq al-Ruh kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[9] Aidha kuna juhudi maalumu zilizofanywa na baadhi ya wanazuoni, katika kukusanya na kutoa uchambuzi wa maneo msamiati wa dua ya hamsini na mbili sambamba na dua nyengine za kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Uchambuzi huu wa kilugha unapatikana katika vitabu kadhaa, kikiwemo; Ta'liqat ala al-Sahifa al-Sajjadiya kilichoandikwa na Faidhu Kashani,[10] pamo na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya kilichoandikwa na Izz al-Din Jaza'iri.[11]

Matini na Tafsiri ya Dua

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الْإِلْحَاحِ عَلَى اللَّهِ تَعَالَى

يَا اللَّهُ الَّذِي‏ لا يَخْفى‏ عَلَيْهِ شَيْ‏ءٌ فِي الْأَرْضِ وَ لا فِي السَّماءِ، وَ كَيْفَ يَخْفَى عَلَيْكَ- يَا إِلَهِي- مَا أَنْتَ خَلَقْتَهُ، وَ كَيْفَ لَا تُحْصِي مَا أَنْتَ صَنَعْتَهُ، أَوْ كَيْفَ يَغِيبُ عَنْكَ مَا أَنْتَ تُدَبِّرُهُ، أَوْ كَيْفَ يَسْتَطِيعُ أَنْ يَهْرُبَ مِنْكَ مَنْ لَا حَيَاةَ لَهُ إِلَّا بِرِزْقِكَ، أَوْ كَيْفَ يَنْجُو مِنْكَ مَنْ لَا مَذْهَبَ لَهُ فِي غيْرِ مُلْكِكَ.

سُبْحَانَكَ! أَخْشَى خَلْقِكَ لَكَ أَعْلَمُهُمْ بِكَ، وَ أَخْضَعُهُمْ لَكَ أَعْمَلُهُمْ بِطَاعَتِكَ، وَ أَهْوَنُهُمْ عَلَيْكَ مَنْ أَنْتَ تَرْزُقُهُ وَ هُوَ يَعْبُدُ غَيْرَكَ

سُبْحَانَكَ! لَا يَنْقُصُ سُلْطَانَكَ مَنْ أَشْرَكَ بِكَ، وَ كَذَّبَ رُسُلَكَ، وَ لَيْسَ يَسْتَطِيعُ مَنْ كَرِهَ قَضَاءَكَ أَنْ يَرُدَّ أَمْرَكَ، وَ لَا يَمْتَنِعُ مِنْكَ مَنْ كَذَّبَ بِقُدْرَتِكَ، وَ لَا يَفُوتُكَ مَنْ عَبَدَ غَيْرَكَ، وَ لَا يُعَمَّرُ فِي الدُّنْيَا مَنْ كَرِهَ لِقَاءَكَ.

سُبْحَانَكَ! مَا أَعْظَمَ شَأْنَكَ، وَ أَقْهَرَ سُلْطَانَكَ، وَ أَشَدَّ قُوَّتَكَ، وَ أَنْفَذَ أَمْرَكَ!

سُبْحَانَكَ! قَضَيْتَ عَلَى جَمِيعِ خَلْقِكَ الْمَوْتَ: مَنْ وَحَّدَكَ وَ مَنْ كَفَرَ بِكَ، وَ كُلٌّ ذَائِقُ الْمَوْتِ، وَ كُلٌّ صَائِرٌ إِلَيْكَ، فَتَبَارَكْتَ وَ تَعَالَيْتَ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ وَحْدَكَ لَا شَرِيكَ لَكَ.

آمَنْتُ بِكَ، وَ صَدَّقْتُ رُسُلَكَ، وَ قَبِلْتُ كِتَابَكَ، وَ كَفَرْتُ بِكُلِّ مَعْبُودٍ غَيْرِكَ، وَ بَرِئْتُ مِمَّنْ عَبَدَ سِوَاكَ.

اللَّهُمَّ إِنِّي أُصْبِحُ وَ أُمْسِي مُسْتَقِلًّا لِعَمَلِي، مُعْتَرِفاً بِذَنْبِي، مُقِرّاً بِخَطَايَايَ، أَنَا بِإِسْرَافِي عَلَى نَفْسِي ذَلِيلٌ، عَمَلِي أَهْلَكَنِي، وَ هَوَايَ أَرْدَانِي، وَ شَهَوَاتِي حَرَمَتْنِي.

فَأَسْأَلُكَ يَا مَوْلَايَ سُؤَالَ مَنْ نَفْسُهُ لَاهِيَةٌ لِطُولِ أَمَلِهِ، وَ بَدَنُهُ غَافِلٌ لِسُكُونِ عُرُوقِهِ، وَ قَلْبُهُ مَفْتُونٌ بِكَثْرَةِ النِّعَمِ عَلَيْهِ، وَ فِكْرُهُ قَلِيلٌ لِمَا هُوَ صَائِرٌ إِلَيْهِ.

سُؤَالَ مَنْ قَدْ غَلَبَ عَلَيْهِ الْأَمَلُ، وَ فَتَنَهُ الْهَوَى، وَ اسْتَمْكَنَتْ مِنْهُ الدُّنْيَا، وَ أَظَلَّهُ الْأَجَلُ، سُؤَالَ مَنِ اسْتَكْثَرَ ذُنُوبَهُ، وَ اعْتَرَفَ بِخَطِيئَتِهِ، سُؤَالَ مَنْ لَا رَبَّ لَهُ غَيْرُكَ، وَ لَا وَلِيَّ لَهُ دُونَكَ، وَ لَا مُنْقِذَ لَهُ مِنْكَ، وَ لَا مَلْجَأَ لَهُ مِنْكَ، إِلَّا إِلَيْكَ.

إِلَهِي أَسْأَلُكَ بِحَقِّكَ الْوَاجِبِ عَلَى جَمِيعِ خَلْقِكَ، وَ بِاسْمِكَ الْعَظِيمِ الَّذِي أَمَرْتَ رَسُولَكَ أَنْ يُسَبِّحَكَ بِهِ، وَ بِجَلَالِ وَجْهِكَ الْكَرِيمِ، الَّذِي لَا يَبْلَى وَ لَا يَتَغَيَّرُ، وَ لَا يَحُولُ وَ لَا يَفْنَى، أَنْ تُصَلِّيَ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِ مُحَمَّدٍ، وَ أَنْ تُغْنِيَنِي عَنْ كُلِّ شَيْ‏ءٍ بِعِبَادَتِكَ، وَ أَنْ تُسَلِّيَ نَفْسِي عَنِ الدُّنْيَا بِمَخَافَتِكَ، وَ أَنْ تُثْنِيَنِي بِالْكَثِيرِ مِنْ كَرَامَتِكَ بِرَحْمَتِكَ.

فَإِلَيْكَ أَفِرُّ، و مِنْكَ أَخَافُ، وَ بِكَ أَسْتَغِيثُ، وَ إِيَّاكَ أَرْجُو، وَ لَكَ أَدْعُو، وَ إِلَيْكَ أَلْجَأُ، وَ بِكَ أَثِقُ، وَ إِيَّاكَ أَسْتَعِينُ، وَ بِكَ أُومِنُ، وَ عَلَيْكَ أَتَوَكَّلُ، وَ عَلَى جُودِكَ وَ كَرَمِكَ أَتَّكِلُ.

Na (ifuatayo) ilikuwa ni miongoni mwa dua zake, (amani iwe juu yake), (aliyokuwa akiitumia) katika juhudi zake za kumsihi Mwenye Ezi Mungu (katika mchakato wa sisitizo la kuomba na kutafuta matilaba yake mbele ya Mola wake).

Ewe Allah (Ewe Mwenye Ezi Mungu) ambaye hakuna kitu kinachofichika kwake si kile kilichomo ardhini wala si cha mbinguni! Na jinsi gani kitu hicho kitaweza kutafichika kwako - Ee Mungu wangu – hali ya kwamba Wewe ndiye muumbaji wake? Na vipi uweze kushindwa kukiingiza ndani ya hisabu Yako kile ulichokitengeneza Wewe mwenyewe? Au ni jinsi gani kitaweza kukupotea kile unachokisimamia (unachokipangia) mipango yake? Au jinsi gani ataweza kukutoroka yule ambaye hana maisha isipokuwa kwa kutegemea riziki yako? Au jinsi ni gani ataepukana Nawe yule ambaye hana mahali penginepo pa kwenda isipokuwa ndani ya ufalme wako (ndani ya mamlaka Yako)?

Umetakasika (utakaso halis ni Wako Wewe)! Wenye khofu zaidi Kwako miongoni mwa waja Wako ni wale wenye maarifa zaidi kuhusiana na Wewe. Na wenye unyenyekevu mkubwa Kwako ni wale wenye utendaji mkubwa zaidi katika mchakato wa kutekelea maamrisho Yako (katika mchakato wa kukutii Wewe). Na mnyonge zaidi Kwako ni yule ambaye Wewe unamruzuku hali yeye anaabudu ghairullah (asiye Wewe).

Umetakasika (utakaso halisi ni Wako Wewe)! Katu Mamlaka Yako hayawezi kupunguzwa na ushirikina wa wale wanaokushirikisha na wengine, kisha wakakanusha Wajumbe Wako. Na wala hana uwezo wa kurudisha amri Yako (maamuzi Yako/Kadari Yako) yule mwenye kuchukia hukumu Zako, wala hana uwezo kujilinda dhidi yako yule mwenye kukanusha uweza Wako. Na hatakuepuka mwenye kuabudu asiyekuwa Wewe, wala hatapewa umri wa daima hapa duniani yule mwenye kuwa na uchukivu wa kukutana Nawe.

Umetakasika (kwa utakaso adhimu ulioje)! Taadhima (hadhi) Yako ni tukufu kupindukia mipaka, na mamlaka Yako ni yenye nguvu kubwa zilizoje, na nguvu Zako ukali kali zilioje, na amri Zako ni zenye mkato wa utekelezekaji ulioje! (na amri Zako ni zenye ukelezekaji usio na pingamizi)

Umetakasika (kwa utakaso adhimu ulioje)! Umehukumu (upepitisha) hukumu ya kifo juu ya viumbe Wako wote; bila kubagua kati ya mwenye kukupwekesha (kwa umoja Wako) na mweye kukufuru, na kila mmoja kati ya viumbe (Wako) ataonja kifo, na kila kimoja atakurudi Kwako. Umebarika na umetukuka, hakuna Mungu ila Wewe peke Yako, na wala huna mshirika.

Nimekuamini Wewe, na nimewasadiki (nimewakubali) mitume Wako, na nimekikubali Kitabu Chako, na nimemkataa kila muabudiwa asiyekuwa Wewe, na nimejitenga na wale wote wanaomuabudu asiyekuwa Wewe.

Ee Mwenye Ezi Mungu! Napitia na asubuhi na jiona nikiwa katika hali ya kuzidharau (kuzidogosha) amali zangu, na (pia asubuhi na jioni) niko katika hali ya kukikiri dhambi zangu, ninakubali makosa yangu (asubuhi na jioni nipo katika hali ya kukubali makosa yangu). Bila shaka Mimi nimekuwa ni mnyonge kutokana na kupindukia mipaka katika kudhulumu nafsi yangu (kwa kutenda dhambi), matendo yangu yameniangamiza, tamaa zangu zimenichafua, na shahawa zangu zimenipunguzia baraka (na matamanio ya nafsi yameniharamishia kheri na fanaka).

Hivyo basi nakuomba, Ewe Mola (bwana) wangu, ombi la mtu mwenye nafsi pumbavu iliyopumbaa kutokana na tamaa ya matumaini ya muda marefu (yasiyo na uhakika), na mwili wake umeghafilika kutokana na utulivu wa mishipa yake, na moyo wake umetekwa na wingi wa neema zilizomjaa, na mawazo yake ni finyu juu yale anayokwenda kuyakutana nayo (juu ya kile anachokielekea, yaani kifo pamoja na malipo ya matendo yako).

(Ewe Mola wangu ninakuomba) Ombi la mtu aliyepinduliwa (aliyepikuliwa) na matumaini (matarajio danganyifu), na (ninakuomba ombi la) aliyefitinishwa na matamanio (ya nafsi yake), na yule aliyetawaliwa na dunia, huku kivuli cha kifo (chake) kikiwa juu yake. (Ninakuomba ombi la) ombi la yule anayeyahisabu na kuyaona makosa yake kuwa ni mengi mno (ninakuomba ombi la yule asiyedogosha dhambi zake), kisha akakiri makosa yake. (Ninakuomba ombi la) ombi la yule asiyekuwa na Mola isipokuwa Wewe, na wala hana mlinzi (msimamizi/kiongozi) isipokuwa Wewe, wala hana mwokozi wa kumuepusha Nawe, wala hana kimbilio la kukutoroka, bali (kimbilio lake ni) Kwako Wewe.

Ewe Mungu wangu, ninakuomba kwa haki Yako iliyoko juu ya viumbe Vyako vyote (iliyowawajibikia viumbe Wako wote), na kwa Jina Lako Kuu ambalo ulimwamuru Mjumbe Wako (Muhammad) (a.sw.w) akutukuze kwalo, na kwa utukufu wa Dhati Yako tukufu, ambayo haichakai (haikongi) wala habadiliki, an ambayo haitoweki (haiuki) wala haifi, kwamba umbariki Muhammad pamoja na Aali Muhammad, na unitosheleza na kila kitu (na uniepushe na aina zote za uhitaji) kupitia ibada yangu Kwako, na uifariji roho yangu kwa kuniondolea fungamano la kufungamana na duniani kupiti hofu ya kukuogopa Wewe, na ninakuomba kupitia rehema Zako, unifadhili kwa wingi wa fadhila kutoka katika (hazina ya) fadhila Zako.

Bila shaka, kwako ndiko ninakimbilia, na (bila shaka) Wewe ndiye ninayekuhofu (ninayekuogopa), na (bila shaka) Wewe ndiye ninayekuomba uowokovu (wokovu). Ni wewe pekee Ndiye ninayekutarajia, na Kwako Wewe ndiko ninakoelekeza maombi yagu. Na Kwako ndiko ninakokimbilia, na Wewe Ndiye ninaye kuamini. Ni wewe peke yako Ndiye ninayekuomba msaada, na ni Wewe pekee Ndiye ninayekuamini. Wewe Ndiye Tegemeo langu (Tegemeo langu lipo Kwako Wewe peke Yako), na matarajio yangu yapo juu ya fadhila Zako na ukarimu Wako.

🌞
🔄
➖
➕

Rejea

  1. ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 341
  2. ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 341-362.
    Sherh Farzahaye Duaye Panjo Dovom Sahife Az Site Irfan.
  3. ↑ Ansarian, Diyar Asheqan, 1373, juz. 7, uk. 611-622.
  4. ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 3, uk. 337-362.
  5. ↑ Fahri, Sherh wa Tafsir Sahifa Sajjadih, 1388, juz. 3, uk. 559-565.
  6. ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 7, uk. 365-394.
  7. ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 647-655.
  8. ↑ Darabi, Riyadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 717-724.
  9. ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 2, uk. 614-629.
  10. ↑ Faydh Kashani, Ta'baqat al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 102-103.
  11. ↑ Jazairi, Sharh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1402 AH, uk. 293-295.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Jazairi, Izu-Din, Sherh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Beirut, Dar al-Taaruf Lil-Matbuat, 1402 AH.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.