Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Dua ya Arubaini na Sita ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Arubaini na Sita ya Sahifa Sajjadiyya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa Mnamo Sha'ban 1102 AH.

MadaDua baada ya kukamilisha ibada ya sala ya Eid al-Fitr na ile ya siku ya Ijumaa.
Ina Mapokezi au Haina MapokeziIna Mapokezi
Imenukuliwa Kutoka kwaImamu Sajjad (a.s)
MpokeziMutawakkil ibn Harun
Vyanzo vya KishiaSahifa Sajjadiyah
Dua ya Tawassuli • Dua ya Kumaili • Dua ya Nudba • Dua ya Samati • Dua ya Faraji • Dua ya Abu Hamza Thumali • Ziara ya Ashura • Ziara ya Jamiat Kabira • Ziara ya Warith • Ziara ya Aminu-Llah • Ziara ya Arobaini

Dua ya Arubaini na Sita ya Sahifa Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء السادس والأربعون من الصحيفة السجادية) ni miongoni mwa dua zilizopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Imeripotiwa kwamba; Imamu Sajjad (a.s) alikuwa na kwaida ya kuisoma baada ya sala ya Eid al-Fitr pamoja na kuitumia dua hii ndani ya siku ya Ijumaa. Katika dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anakiri neema zote za Mwenye Ezi Mungu kwa waja wake huku akitumia lugha (ibara) mbalimbali kwa ajili kutafuta (kuomba) rehema za Mola wake.

Dua ya arubaini na sita ya Sahifa Sajjadiyya imefasiriwa na kufafanuliwa kwa lugha mbali mbali kupita wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu. Miongoni mwa vitabu muhimu vilivyotoa tafsiri chambuzi ya dua hii kwa lugha ya Kifarsi sambamba na daua nyengine za Sahifa Sajjadiyya, ni kama vile; Diare Ashiqan, kilichoandikwa na Hussein Ansarian, Shuhud wa Shenakht, kazi ya Hassan Mamdoohi Kermanshahi. Aidha tafsiri chambuzi ya dua ya arubaini na sita inapatikana kwa lugha ya Kiarabu, inapatikana katika kitabu kiitwacho Riyad as-Salikin, kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani. Kitabu kilichotoa ufafanuzi wa dua hiyo kwa lugha ya Kiarabu, sambamba na dua nyengine zilizoripotiwa ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya.

Mafunzo ya Dua ya Arubaini na Sita

Dua ya arobaini na sita, iliyoandikwa katika Sahifa Sajjadiyya, ni maombi yaliyokuwa yakitolewa na Imam Sajjad (a.s) baada ya kukamilisha ibada ya sala ya Eid al-Fitr na ile ya siku ya Ijumaa. Nyakati hizi mbili zina uzito wa kipekee katika theolojia ya Kiislamu, zikitazamwa kama vipindi vya neema na rehema za kimungu kwa wanadamu. Kwa mantiki hiyo, Imam Zainul Abidin (a.s), kwa kutumia tamathali na semi za kina, anajitahidi kujenga uhusiano wa karibu na Mwenyezi Mungu.[1] Mafundisho yaliomo ndani ya dua ya arubaini na sita yamekuja katika vipengele vifuatavyo:

  • Upendo na Huruma ya Mwenye Ezi Mungu kwa aliyetengwa na watu na miji yote: Fadhili na rehema za Mwenye Ezi Mungu humfikia hata yule anayekataliwa na jamii nzima, na ambaye amefukuzwa kutoka kila mahali.
  • Ungamo la huruma na rehema za Mwenye Ezi Mungu: Ungamo na uthibitisho wa moyo juu ya upole na rehema za Mwenye Ezi Mungu zisizo na kifani.
  • Waja kutokata tamaa na ukarimu wa Mwenye Ezi Mungu: Wanaomwamini Mungu hawatakiwi kukata tamaa kamwe, kwani mlango wa Mwenye Ezi Mungu daima uko wazi kwa waja Wake.
  • Uduni wa viumbe mbele ya uwepo usio na kikomo wa Mwenye Ezi Mungu: Viumbe vyote ni dhaifu na huwa havina thamani yoyote pale vinapolinganishwa na utukufu na uwepo wa Mwenye Ezi Mungu usio na mwisho.
  • Kukubaliwa kwa wanadamu wasio na kimbilio: Mwenye Ezi Mungu huwakumbatia na kuwapokea wale wote ambao hawana pa kukimbilia wala msaada wowote.
  • Kutodharauliwa kwa wahitaji mbele ya Mola wao: Mwenye Ezi Mungu kamwe hawadharau wale wanaomjia kwa unyonge na uhitaji.
  • Kukubaliwa na kuthaminiwa na Mwenye Ezi Mungu yale matendo duni ya waja na kuwalipa maradufu: Mwenye Ezi Mungu huthamini hata juhudi ndogo kabisa za waja Wake na huwalipa thawabu zenye thamani kuliko matendo yao.
  • Mwenye Ezi Mungu kutofanya haraka katika kuwaadhibu waja: Si katika sifa za Mungu kuharakisha adhabu kwa waja Wake wanaokosea, bali huwapa fursa ya kutubia.
  • Kuwaenzi na kuwatukuza wahitaji: Mungu huwapa heshima na hadhi wale wanyonge na wenye mahitaji.
  • Kujibiwa kwa maombi ya waja, hata ya wenye dhambi: Mwenyezi Mungu husikiliza na kujibu dua za waja Wake wote, wakiwemo wale waliozama katika dhambi.
  • Mwaliko kwa waja wenye dhambi kurejea kwa Mola wao: Mungu anawaita na kuwakaribisha waja Wake wenye makosa warudi Kwake kwa toba.
  • Ueneaji wa utawala wa Mwenye Ezi Mungu ulimwengu mzima: Mamlaka na ufalme wa Mwenye Ezi Mungu umetanda katika kila pembe ya ulimwengu.
  • Mwenye Ezi Mungu ndiye Mkuzaji wa wema na Mfutaji wa uovu: Mwenyezi Mungu ndiye anayekuza na kustawisha matendo mema na kufuta kabisa athari za maovu.
  • Hiari ya mwanadamu kama msingi wa mtihani wa Kiungu na mfumo wa malipo: Uhuru wa kuchagua aliopewa mwanadamu ndio msingi unaoweka na Mwenye Ezi Mungu kwa ajili ya majaribio, na ndiyo wa kutoa thawabu na adhabu.
  • Matokeo ya kumwacha Mwenye Ezi Mungu ni kukata tamaa, kuhasirika na kuingia umaskini: Matunda ya Mja kuachana Mola wake, ni kuvunjika moyo, kupata hasara, na kubaki katika ufukara.
  • Milango ya rehema ya Mwenye Ezi Mungu iko wazi daima: Rehema za Mungu hazina kikomo na milango yake iko wazi kwa yeyote anayeielekea.
  • Matumaini na matarajio mema juu ya ukarimu wa Mwenye Ezi Mungu: Mja apaswa kuwa na matumaini thabiti na kutarajia mema kutoka katika fadhili za Mola wake.
  • Muhula wa Mwenye Ezi Mungu wa kuwavumilia wenye dhambi kwa msingi wa ukarimu na hisani Yake: Mwenye Ezi Mungu, kutokana na ukarimu Wake, huwapa muda na huamiliana nao kwa upole wenye dhambi.
  • Udhaifu na unyonge wa wote wanaojidai kuwa na ukuu na heshima mbele ya Mwenyezi Mungu: Mbele ya utukufu wa Mungu, hudogoka na hudunika kila anayejivuna kwa ukuu na cheo alichokuwa nacho.
  • Ufalme wa milele wa Mwenye Ezi Mungu na Hoja thabiti: Mamlaka ya Mwenye Ezi Mungu yamesimama juu ya hoja imara na ufalme Wake ni wa kudumu milele.
  • Haki katika adhabu ya Mwenye Ezi Mungu: Adhabu ya Mwenye Ezi Mungu hutolewa kwa uadilifu kamili, bila dhuluma yoyote.
  • Udhaifu wa mwanadamu katika kuelezea na kushukuru neema: Mwanadamu, kwa upande wake, hana uwezi wa kuorodhesha na kuzishukuru ipasavyo neema zote za Mola wake.
  • Kuomba mwisho mwema: Ni muhimu kumuomba Mungu amjalie mja mwisho mwema wa maisha yake.
  • Kunyimwa na kukata tamaa kama matokeo ya kumgeukia asiyekuwa Mwenye Ezi Mungu: Kumtegemea yeyote au chochote kisichokuwa Mwenye Ezi Mungu, hupelekea kunyimwa fadhili na kuingia katika hali ya kukata tamaa.
  • Hasara kwa wanao muomba asiyekuwa Mwenye Ezi Mungu: Wale wote wanaoacha kumuomba Mwenye Ezi Mungu, na badala yake kuwaomba wengine hupata hasara isiyo na kifani.
  • Milango ya rehema za Mwenye Ezi Mungu iko wazi kwa wenye shauku: Mwenye zi Mungu huwafungulia milango ya rehema Yake wale wote wanaomlilia kwa shauku na kutafuta kwa hamu.
  • Ukarimu wa Mwenye Ezi Mungu unaendelea kuwafikia waombaji: Fadhili za Mwenye Ezi Mungu daima zinawashukia wale wote wanaoinua mikono yao kumuomba Mola wao.
  • Kinga ya msamaha (istighfaru) dhidi ya uovu na bahati mbaya: Kumuomba msamaha Mwenye Ezi Mungu, ndiyo kinga imara inayomlinda mja dhidi ya madhara ya uovu na masaibu mbali mbali.
  • Upana wa riziki ya Mungu kwa wenye dhambi: Mwenye Ezi Mungu huwakunjulia riziki hata waja Wake wote hata wale wenye kutenda dhambi.
  • Upole wa Mwenye Ezi Mungu kuwaenea hata wanaompinga: Upole na uvumilivu wa Mwenye Ezi Mungu unawafikia hata wale wanaompinga na kupigana Naye vita.
  • Ni sunna ya Mwenye Ezi Mungu (desturi ya kuwapa muhula wenye dhambi, watenda jeuri na madhalimu: Mwenye Ezi Mungu ameweka utaratibu wa kuwapa fursa na muda wenye makosa ili warejee wake, wakiwemo madhalimu pamoja na wavukao mipaka.
  • Ulazima wa kufanya toba kwa haraka iwezekanavyo: Inampasa mja kutubia kwa haraka punde tu anapotanabahi na kujua kuwa amefanya kosa.[2]

Tafsiri Chambuzi za Dua ya Arubaini na Sita

Dua ya Arobaini na Sita, kutoka katika kitabu kitakatifu cha As-Sahifa al-Sajjadiyya, ambacho ni mkusanyo wa dua za Imamu Ali ibn al-Hussein Zain al-Abidin (a.s), imefasiriwa na kufafanuliwa na kwa kina kwa lugha ya Kiajemi kupitia vitabu mbalimbali vya wanazuoni mashuhuri. Ufafanuzi huu unalenga kutoa maana na maudhui yaliyokusudiwa katika dua hii tukufu sambamba na dua nyengine za kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu muhimu vilivyochukua jukumu hili ni pamoja na; Diare Ashiqan kazi ya bwana Hussein Ansarian,[3] Shuhud wa Shenakht kilichoandikwa na bwana Muhammad Hassan Mamduhi Kermanshahi,[4] pamoja na kitabu kiitwacho Sharhe wa Tarjomeh Sahifeh Sajjadiyeh, kilichoandikwa na bwana Sayyid Ahmad Fahri.[5]

Aida dua hii ya arubaini na sita imefafnuliwa kwa lugha mama ya Kiarabu, ili kuwarahisishia watumiaji wake kuweza kuelewa makusudio na dhamira zilizomo ndani yake. Miongoni mwa vitabu vilivyotoa tafsiri chambuzi ya dua hii kwa lugha ya Kiarabu, sambamba na dua zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya, ni pamoja na; Riadhu as-Salikina, kitabu kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani,[6] Fi Dhilali as-Sahifat as-Sajjadiya, kitabu kilichoandikwa na Muhammad Jawad Mughniyyah,[7] Riadhu al-Arifina, kitabu kilichoandikwa na Muhammad bin Muhammad Darabi,[8] pamoja na Afaqu ar-Ruh, kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadlullah.[9] Aidha, maneno na misamiati iliyotumika katika dua hii sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya, yamekusanywa na kufafanuliwa kwa mfumo wa fasihi ya kilugha pamoja na fasihi ya kidini. Miongini mwa vitabu vilivyoandikwa kwa ajili ya kazi hiyo ni pamoja na: Ta'liqat 'ala as-Sahifat as-Sajjadiya, kilichoandikwa na Faidhi Kashani,[10] na Sharhu as-Sahifat as-Sajjadiyya, kilichoandikwa na Izzu al-Din al-Jaza'iri.[11]

Matini ya Dua ya Arubaini na Sita Pamoja na Maezo Yake kwa Kiswahili

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي دِفَاعِ كَيْدِ الْأَعْدَاءِ، وَ رَدِّ بَأْسِهِمْ

إِلَهِي هَدَيْتَنِي فَلَهَوْتُ، وَ وَعَظْتَ فَقَسَوْتُ، وَ أَبْلَيْتَ الْجَمِيلَ فَعَصَيْتُ، ثُمَّ عَرَفْتُ مَا أَصْدَرْتَ إِذْ عَرَّفْتَنِيهِ، فَاسْتَغْفَرْتُ فَأَقَلْتَ، فَعُدْتُ فَسَتَرْتَ، فَلَكَ- إِلَهِي- الْحَمْدُ.

تَقَحَّمْتُ أَوْدِيَةَ الْهَلَاكِ، وَ حَلَلْتُ شِعَابَ تَلَفٍ، تَعَرَّضْتُ فِيهَا لِسَطَوَاتِكَ وَ بِحُلُولِهَا عُقُوبَاتِكَ.

وَ وَسِيلَتِي إِلَيْكَ التَّوْحِيدُ، وَ ذَرِيعَتِي أَنِّي لَمْ أُشْرِكْ بِكَ شَيْئاً، وَ لَمْ أَتَّخِذْ مَعَكَ إِلَهاً، وَ قَدْ فَرَرْتُ إِلَيْكَ بِنَفْسِي، وَ إِلَيْكَ مَفَرُّ الْمُسي‏ءِ، وَ مَفْزَعُ الْمُضَيِّعِ لِحَظِّ نَفْسِهِ الْمُلْتَجِئِ.

فَكَمْ مِنْ عَدُوٍّ انْتَضَى عَلَيَّ سَيْفَ عَدَاوَتِهِ، وَ شَحَذَ لِي ظُبَةَ مُدْيَتِهِ، وَ أَرْهَفَ لِي شَبَا حَدِّهِ، وَ دَافَ لِي قَوَاتِلَ سُمُومِهِ، وَ سَدَّدَ نَحْوِي صَوَائِبَ سِهَامِهِ، وَ لَمْ تَنَمْ عَنِّي عَيْنُ حِرَاسَتِهِ، وَ أَضْمَرَ أَنْ يَسُومَنِي الْمَكْرُوهَ، وَ يُجَرِّعَنِي زُعَاقَ مَرَارَتِهِ.

فَنَظَرْتَ- يَا إِلَهِي- إِلَى ضَعْفِي عَنِ احْتِمَالِ الْفَوَادِحِ، وَ عَجْزِي عَنِ الِانْتِصَارِ مِمَّنْ قَصَدَنِي بِمُحَارَبَتِهِ، وَ وَحْدَتِي فِي كَثِيرِ عَدَدِ مَنْ نَاوَانِي، وَ أَرْصَدَ لِي بِالْبَلَاءِ فِيمَا لَمْ أُعْمِلْ فِيهِ فِكْرِي.

فَابْتَدَأْتَنِي بِنَصْرِكَ، وَ شَدَدْتَ أَزْرِي بِقُوَّتِكَ، ثُمَّ فَلَلْتَ لِي حَدَّهُ، وَ صَيَّرْتَهُ مِنْ بَعْدِ جَمْعٍ عَدِيدٍ وَحْدَهُ، وَ أَعْلَيْتَ كَعْبِي عَلَيْهِ، وَ جَعَلْتَ مَا سَدَّدَهُ مَرْدُوداً عَلَيْهِ، فَرَدَدْتَهُ لَمْ يَشْفِ غَيْظَهُ، وَ لَمْ يَسْكُنْ غَلِيلُهُ، قَدْ عَضَّ عَلَى شَوَاهُ وَ أَدْبَرَ مُوَلِّياً قَدْ أَخْلَفَتْ سَرَايَاهُ.

وَ كَمْ مِنْ بَاغٍ بَغَانِي بِمَكَايِدِهِ، وَ نَصَبَ لِي شَرَكَ مَصَايِدِهِ، وَ وَكَّلَ بِي تَفَقُّدَ رِعَايَتِهِ، وَ أَضْبَأَ إِلَيَّ إِضْبَاءَ السَّبُعِ لِطَرِيدَتِهِ انْتِظَاراً لِانْتِهَازِ الْفُرْصَةِ لِفَرِيسَتِهِ، وَ هُوَ يُظْهِرُ لِي بَشَاشَةَ الْمَلَقِ، وَ يَنْظُرُنِي عَلَى شِدَّةِ الْحَنَقِ.

فَلَمَّا رَأَيْتَ- يَا إِلَهِي تَبَاركْتَ وَ تَعَالَيْتَ- دَغَلَ سَرِيرَتِهِ، وَ قُبْحَ مَا انْطَوَى عَلَيهِ، أَرْكَسْتَهُ لِأُمِّ رَأْسِهِ فِي زُبْيَتِهِ، وَ رَدَدْتَهُ فِي مَهْوَى حُفْرَتِهِ، فَانْقَمَعَ بَعْدَ اسْتِطَالَتِهِ ذَلِيلًا فِي رِبَقِ حِبَالَتِهِ الَّتِي كَانَ يُقَدِّرُ أَنْ يَرَانِي فِيهَا، وَ قَدْ كَادَ أَنْ يَحُلَّ بِي لَوْ لَا رَحْمَتُكَ مَا حَلَّ بِسَاحَتِهِ.

وَ كَمْ مِنْ حَاسِدٍ قَدْ شَرِقَ بِي بِغُصَّتِهِ، وَ شَجِيَ مِنِّي بِغَيْظِهِ، وَ سَلَقَنِي بِحَدِّ لِسَانِهِ، وَ وَحَرَنِي بِقَرْفِ عُيُوبِهِ، وَ جَعَلَ عِرْضِي غَرَضاً لِمَرَامِيهِ، وَ قَلَّدَنِي خِلَالًا لَمْ تَزَلْ فِيهِ، وَ وَحَرَنِي بِكَيْدِهِ، وَ قَصَدَنِي بِمَكِيدَتِهِ.

فَنَادَيْتُكَ- يَا إِلَهِي- مُسْتَغِيثاً بِكَ، وَاثِقاً بِسُرْعَةِ إِجَابَتِكَ، عَالِماً أَنَّهُ لَا يُضْطَهَدُ مَنْ أَوَى إِلَى ظِلِّ كَنَفِكَ، وَ لَا يَفْزَعُ مَنْ لَجَأَ إِلَى مَعْقِلِ انْتِصَارِكَ، فَحَصَّنْتَنِي مِنْ بَأْسِهِ بِقُدْرَتِكَ.

وَ كَمْ مِنْ سَحَائِبِ مَكْرُوهٍ جَلَّيْتَهَا عَنِّي، وَ سَحَائِبِ نِعَمٍ أَمْطَرْتَهَا عَلَيَّ، وَ جَدَاوِلِ رَحْمَةٍ نَشَرْتَهَا، وَ عَافِيَةٍ أَلْبَسْتَهَا، وَ أَعْيُنِ أَحْدَاثٍ طَمَسْتَهَا، وَ غَوَاشِي كُرُبَاتٍ كَشَفْتَهَا.

وَ كَمْ مِنْ ظَنٍّ حَسَنٍ حَقَّقْتَ، وَ عَدَمٍ جَبَرْتَ، وَ صَرْعَةٍ أَنْعَشْتَ، وَ مَسْكَنَةٍ حَوَّلْتَ.

كُلُّ ذَلِكَ إِنْعَاماً وَ تَطَوُّلًا مِنْكَ، وَ فِي جَمِيعِهِ انْهِمَاكاً مِنِّي عَلَى مَعَاصِيكَ، لَمْ تَمْنَعْكَ إِسَاءَتِي عَنْ إِتْمَامِ إِحْسَانِكَ، وَ لَا حَجَرَنِي ذَلِكَ عَنِ ارْتِكَابِ مَسَاخِطِكَ، لَا تُسْأَلُ عَمَّا تَفْعَلُ.

وَ لَقَدْ سُئِلْتَ فَأَعْطَيْتَ، وَ لَمْ تُسْأَلْ فَابْتَدَأْتَ، وَ اسْتُمِيحَ فَضْلُكَ فَمَا أَكْدَيْتَ، أَبَيْتَ- يَا مَوْلَايَ- إِلَّا إِحْسَاناً وَ امْتِنَاناً وَ تَطَوُّلًا وَ إِنْعَاماً، وَ أَبَيْتُ إِلَّا تَقَحُّماً لِحُرُمَاتِكَ، وَ تَعَدِّياً لِحُدُودِكَ، وَ غَفْلَةً عَنْ وَعِيدِكَ، فَلَكَ الْحَمْدُ- إِلَهِي- مِنْ مُقْتَدِرٍ لَا يُغْلَبُ، وَ ذِي أَنَاةٍ لَا يَعْجَلُ.

هَذَا مَقَامُ مَنِ اعْتَرَفَ بِسُبُوغِ النِّعَمِ، وَ قَابَلَهَا بِالتَّقْصِيرِ، وَ شَهِدَ عَلَى نَفْسِهِ بِالتَّضْيِيعِ.

اللَّهُمَّ فَإِنِّي أَتَقَرَّبُ إِلَيْكَ بِالْمُحَمَّدِيَّةِ الرَّفِيعَةِ، وَ الْعَلَوِيَّةِ الْبَيْضَاءِ، وَ أَتَوَجَّهُ إِلَيْكَ بِهِمَا أَنْ تُعِيذَنِي مِنْ شَرِّ كَذَا وَ كَذَا، فَإِنَّ ذَلِكَ لَا يَضِيقُ عَلَيْكَ فِي وُجْدِكَ، وَ لَا يَتَكَأَّدُكَ فِي قُدْرَتِكَ وَ أَنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْ‏ءٍ قَدِيرٌ

فَهَبْ لِي- يَا إِلَهِي- مِنْ رَحْمَتِكَ وَ دَوَامِ تَوْفِيقِكَ مَا أَتَّخِذُهُ سُلَّماً أَعْرُجُ بِهِ إِلَى رِضْوَانِكَ، وَ آمَنُ بِهِ مِنْ عِقَابِكَ، يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ.

Na (ifuatayo ilikuwa ni) miongoni mwa dua zake, amani iwe juu yake, (aliyokuwa akiitumia) kwa ajili ya kujilinda dhidi ya njama za maadui, pamoja na kurudisha numa madhara yao.

Ee Mola wangu, Uliniongoza, nami nikajisahau (nikacheza na dunia). Ukaniwaidhi (ukanisemeza), nami nikakaidi (nikajitia ununda). Ukanikirimu kwa fadhila (Zako), nami (badala ya kushukuru) nikaasi. Hatimaye, nilikuja kufahamu yale niliyoyafanya pale Uliponijulisha makasa yangu hayo. Hivyo nikaomba radhi Nawe, ukanikubalia (ukanisamehe). Na ukawa na mwenye kunisitiri hata pale niliporejea katika makosa yangu. Basi shukurani zote ni Zako Wewe, Ee Mungu wangu.

(Ewe Mola wangu! Hakika mimi) nimejivurumisha kwenye mabonde ya maafa, na nikatumbukia ndani ya mapito ya upotevu; ambamo nilihatarika na kukumbwa na (hatari za) nguvu Zako, na kutumbukia kwangu humo, kulinistahikisha kupata adhabu Zako.

Na Tauhidi (upwekeshaji) ndiyo nyenzo yangu kwa ajili ya kukufikia Wewe, na hoja yangu (na kisingizio changu tetezi) ni kwamaba mimi sikuwahi kukushirikisha na kitu chochote, na wala sikuwahi kutwaa (kuchagua au kumtawalisha moyoni mwangu) mungu mwingine (yeyote yule) sambamba Nawe. Hakika, nimekimbilia Kwako kwa maamuzi kamili ya nafsi yangu (Na nimekimbilia Kwako na fafsi yangu ikiwa kibindoni mwangu). (Na bila shaka) kwako Wewe ndio kimbilio la muovu, na kwako Wewe ndio rejeo la yule anayetafuta kimbilio, ambaye amepoteza fungu la nafsi yake (ambaye amepoteza bahati ya nafsi yake).

Ni maadui wangapi walionichomoa panga za uhasama wao (dhidi yangu), na wakanoa makali ya visu vyao (wakavinoa visu vyao dhidi yangu), wakachonga ncha za mishale yao, wakaniandalia sumu ziangamizazo (ziuazo), na wakanilekezea mishale yao yenye kusibu (shabaha zake). Macho yao angalizi kamwe hayapatwi na usinzigi katika ulinzi wake wa kuniangaza mimi, na tayari wameshanuia (wameshadhamiria) kuniletea madhara na kuninywesha machungu ya madhara (ya uadui wao).

Hapo basi, Ewe Mola wangu, uliungalia udhaifu wangu katika kuhimili majanga, na ushindwaji wangu wa kujipatia ushindi katika mapamabano yangu na yule anayenikusudia mabaya. Kadhalika, ukaiangalia hali yangu ya upweke wangu ndani (mbele) ya kundi kubwa la wale wanaonifanyia uadui, na (ukaona) jinsi (maadui zangu) walivyonitegea mitego ya mabalaa, kwa njia ambayo katu sikuwa na fikra nayo.

Hapo basi ukanianzia kwa kunipa msaada Wako (kabla ya mimi kuomba msaada Huo), na ukaniimarishia uwezo wangu kwa nguvu Zako. Baadaye, ukanipunguzia ukali wake (ukali wa maadui zangu hao), na ukawabadilisha kutoka hali ya kuwa na kundi kubwa (mkusanyiko wa nguvu kubwa), hadi kufikia nguvu pweke. Kisha ukaniinua dhidi yake, na ukamuelekezea mwenyewe ile mipango yake mibaya aliyokuwa ameipanga dhidi yangu. Na hatima yake, ukamrejesha bila ya kuponya chuki zake, na bila kuiponya ghadhabu yake. Akaondoka na kujitafuna kidole (kwa hasira), huku majeshi yake yakiwa yameshindwa kutimiza malengo yao.

Ni maadui wangapi walionipangia njama kwa hila zao, na wakanitegea mitego yao. Wakaniwekea mtu maalumu wa kunichunguza kwa makini nyenendo zangu, huku wakinyemelea kama simba anavyomkizia kiwindwa chake, akingoja fursa nzuri ya kumshambulia. Hutabasamu mbele yangu kwa tabasamu ya kinafiki, huku wakinitizama kwa jicho la chuki kupita kiasi.

Na Ewe Mola wangu, Uliyetuka na Muadhamu, baada ya Wewe kubaini ubaya wa nafsi ya daui yangu huyu, pamoja uovu alioficha kifuani mwake, ulimwangusha kifudifudi kwenye mtego wake mwenyewe, kisha ukamrudisha kwenye shimo la maangamizi yake mwenyewe (ayoyatayarisha kwa ajili yangu). Hivyo basi, baada ya majivuno yake, alidhibitiwa na kudhalilishwa vikali ndani ya tanzi za mtego wake ambao alikadiria kuniona mimi nikiwa ndani yake. Na laiti si huruma yako, bila shaka yaliyomfika yeye yangekuwa ndiyo yaliyonifika mimi.

Na kuna hasidi wangapi ambao wamesongwa na chuki (balaa) zao wenyewe walizokuwanzao dhidi yangu, na wakakosa raha kwa sababu ya hasira zao kwangu. Wamenichapa kwa ukali wa ndimi zao, na kunichafua kwa kunisingizia (kunipchika) mimi aibu zao weo. Wameifanya heshima yangu kuwa shabaha ya mashambulizi yao, na (wakajitahidi) kunivika tabia mbaya ambazo daima zilikuwa ni tabia zao wao. Wamejaribu kunitia katika dhiki kwa hila zao, na kunilenga kwa njama zao ovu (halifu).

Hivyo basi (baada kukabiliwa na njama hizo), nilikuelekezea maombi yangu, Ewe Mola wangu, kwa lengo la kuomba msaada Wako, (nilifanya hivyo) nikiwa na imani thabiti juu ya kupata majibu ya haraka kutoka Kwako. (Na nilifanya hivyo) nikifamu fika kwamba; katu hatowezi kukumbwa na dhuluma, yule anayetafuta ulinzi chini ya kivuli cha himaya Yako, na wala hatakumbwa na hofu, yeyote yule anayekimbilio katika ngome ya ushindi Wako. (Nami baada ya kukimbilia kwenye mamlaka yako), umenikinga dhidi ya madhara yake (dhidi ya madhara ya adui zangu).

Na ni mawingu mangapi ya karaha kunikengeusha nayo (Na ni mawingu mangapi ya ya madhara ulionipambazulia), na (ni mawingu mangapi ya neema) ulinielekezea, na (ni makunjuo mangapi) ya rehema (Zako) ulionikunjulia, na (ni aina ngapi za afya) ulizonivika nazo, na (ni macho mangapi ya fitina (dhidi yangu) uliyonifumbia, na ni magubiko mangapi ya kero (dhidi yangu) uliyoniondolea.

Na ni matumaini mangapi mema uliyoyatimiza (Na ni dhana ngapi chanya ulizonitimizia), na ni hali ngapi za uhitaji ulizoziondoa, na ni maanguko ngapi (dhidi yangu) ulilolinyanyua (ulinishika mkono na kuninyanyua nikaweza kusimama), na ni aina ngapi za umasikini (zilizkuwa zikinikabili nawe) (Nawe) ulizigeuza (kuwa ni utajiri badala ya umaskini).

Yote hayo ni neema na fadhila zitokazi Kwako. Na katika yote hayo, mimi nilikuwa nimezama katika kukuasi. Uovu wangu haukukuzuia Wewe kuendelea kunifanyia hisani, wala hilo (wala hisani Zako juu yangu) hazikunizuia kufanya mambo yanayokukasirisha. (Bila shaka) Wewe haulizwi juu ya unachokifanya (juu ya maamuzi Yako).

Hakika Uliombwa nawe Ukatoa, na hata kabla hujaombwa Ulianza kutoa. Fadhila (hisani) Zako ziliombwa nawe hukuchoka kutoa (Nawe hukuwa mbahili katika kutoa hisani hizo). Ewe Bwana wangu, umekataa (kufanya jengine lolote lile), isipokuwa kutenda Hisani, kuneemesha, kutoa kwa wingi na kuneemesha kupita kifani. Nami nimekataa (kutende jengine lolote lile) isipokuwa kukiuka matakatifu Yako, kuvuka mipaka Yako na kusahau maonyo Yako. Basi, sifa zote njema ni Zako, Ewe Mungu wangu, Mwenye uwezo usioshindwa, na Mwenye upole usiye na haraka.

Hii ni nafasi (hali) ya yule aliyekiri wingi wa neema (Zako juu yake), kisha akazikabili kwa mapungufu (mbali mbali), na yeye mwenyewe ametoa ushuhuda dhidi ya nafsi yake juu (tendo lake la) upotezaji (wa haki zako).

Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika mimi ninajikurubisha Kwako kupitia hadhi ya juu ya Muhammadiyya (aliyonayo mtume Wako Muhammad), (pia ninajikurubisha Kwako kupitia hadhi) na nasaba tukufu na safi ya Ali (Kwa lulgha nyengine: Ninajikurubisha Kwako kupitia cheo cha nafasi ya Uimamu wa Ali). Na ninaelekea Kwako kupitia (watukufu) wawili hawa ili uniepushe na shari ya hili na lile (kadha wa kadha). Hakika jambo hilo halikukanzi ndani ya uwezo Wako, wala halikulemei katika nguvu Zako, Nawe ni Muweza juu ya kila kitu.

Hivyo basi, Ee Mola wangu, niruzuku kutoka katika hazina ya rehema yako na ufanisi wako usio na kikomo, kile kitakachokitumia kama nyenzo (ngazi) ya kupanda daraja hadi kufikia radhi Zako, na niweze kupata amani kwacho dhidi ya adhabu Yako, Ewe Mrehemevu kuliko warehemevu wote.

🌞
🔄
➖
➕

Rejea

  1. ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 28.
  2. ↑ Ansarian, Diyar Asheqan, 1373, juz. 7, uk. 503-515 ; Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 28-46.
    Sherh Farzahaye Duaye Chehelo Shish Sahife Az Site Irfan.
  3. ↑ Ansarian, Diyar Asheqan, 1373, juz. 7, uk. 497-515.
  4. ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 3, uk. 23-46.
  5. ↑ Fahri, Sherh wa Tafsir Sahifa Sajjadih, 1388, juz. 3, uk. 345-364.
  6. ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 6, uk. 199-252.
  7. ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 539-549.
  8. ↑ Darabi, Riyadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 575-588.
  9. ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 2, uk. 433-462.
  10. ↑ Faydh Kashani, Ta'baqat al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 91-92.
  11. ↑ Jazairi, Sharh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1402 AH, uk. 236-241.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Jazairi, Izu-Din, Sherh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Beirut, Dar al-Taaruf Lil-Matbuat, 1402 AH.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.