Kushukuru

Kutoka wikishia

Kushukuru (Kiarabu: الشُكر) ni kutoa shukurani na kuthamini kwa ulimi na kivitendo neema za Mwenyezi Mungu (swt). Wanazuoni na wasomi wa elimu ya irfan (maurafaa) wa Kiislamu wanasema kuwa, kushukuru kumegawanyika kayika makundi matatu: Kushukuru kwa ulimi, kwa moyo na kwa vitendo. Kushukuru kwa ulimi ni kukiri kwa maneno kuhusiana na neema, kushukuru kwa moyo ni kutambua neema za Mwenyezi Mungu na kushukuru kivitendo ni kuonyesha utiifu katika vitendo kuhusiana na neema za Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa Aya za Qur’ani, hatua ya mwanadamu ya kushukuru neema za Mwenyezi Mungu ni kwa manufaa yake mwenyewe na kwamba, kushukuru au kutoshukuru neema katu hakuna madhara yoyote yale kwa Mwenyezi Mungu; kwani Mola Muumba si mwenye kumhitajia mwanadamu wala amali zake. Kwa muktadha huo, kushukuru neema hupelekea kupatikana baraka na kuongezewa neema kwa mwenye kushukuru. Imamu Ali bin Abi Twalib (a.s) anakitambua kitendo cha kushukuru kwamba, ni ishara na alama ya imani, taqwa na chimbuko la baraka na kubakia neema.

Utambuzi wa Maana na Daraja Yake

Kushukuru maana yake ni kukumbuka na kutambua neema za Mwenyezi Mungu na hufanyika kwa kwa moyo, ulimi na kivitendo.[1]

Katika baadhi ya Aya za Qur’ani Tukufu kama:[2] «فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ» (Basi nikumbukeni nitakukumbukeni), na nishukuruni wala msinikufuru. Kushukuru neema kumekuja mkabala wa kukufuru neema. Na Aya nyingine:[3] «لِيَبْلُوَنِي أَأَشْكُرُ‌ أَمْ أَكْفُرُ‌» ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Kushukuru katika Aya zilizotangulia kuko mkabala wa kukufuru; kwani miongoni mwa maana za kukufuru ni kufunika na ni kana kwamba kafiri anafunika neema za Mwenyezi Mungu na Muumini anaziondolea pazia kwa shukrani zake na kuzikiri kwake. Maana ya kukiri neema pia imefichwa katika neno “shukr” (kushukuru) na kunaambatana na aina ya kufanya taadhima, kukiri na pia kukumbuka neema na kuidhihirisha, na kinyume chake ni kufr, ambayo ina maana ya kusahau na kufunika neema.[4] Katika hadithi mashuhuri ambayo Imamu Swadiq (a.s) amezungumzia askari wa akili na ujinga ameitaja shukr (kushukuru) kuwa ni katika askari wa akili na dhidi yake yaani kukufuru kuwa ni katika askari wa ujinga.[5]

Katika Qur’ani kushukuru kumetumiwa katika maudhuii tofauti tofauti; na miongoni mwa matumizi hayo ni kushukuru neema za kimaada,[6] kutoa shukurani kwa ajili ya dini na kumpwekesha Mwenyezi Mungu,[7] kushukuru kutokana na uwepo wa Mwenyezi Mungu na dini,[8] na kushukuru kwa ajili ya msahama na maghufira.[9]

Katika hadithi zilizopokewa kutoka kwa Maasumina pia, kumezungumziwa maana ya kushukuru pamoja na vielelezo vyake; Imamu Ali bin Abi Twalib (a.s) amebainisha kwamba, kushukuru ni katika alama na ishara za imani,[10] taqwa (uchaji Mungu),[11], sababu ya kutiwa majaribuni na katika mitihani,[12] pambo la nguvu na uwezo,[13] sababu ya kuongezewa[14] na kuhifadhiwa na kubakia neema. 15] Kadhalika imenukuliwa kutoka kwake akisema kuwa, Waislamu wanapaswa kuwa ni wenye kushukuru kwa hali yoyote ile.[16]

Matokeo ya Kushukuru

Kadhalika angalia: Aya ya 7 ya Surat Ibrahim

Kwa mujibu wa Aya za Qur’ani,[17] hatua ya mwanadamu ya kushukuru neema za Mwenyezi Mungu ni kwa manufaa yake mwenyewe na kwamba, kushukuru au kutoshukuru neema katu hakuna madhara yoyote yale kwa Mwenyezi Mungu; kwani Mola Muumba si mwenye kumhitajia mwanadamu wala amali zake. Kwa muktadha huo, kushukuru neema hupelekea kupatikana baraka na kuongezewa neema kwa mwenye kushukuru.[18] Kadhalika kushukuru ni sababu ya kuongozwa katika njia ya kweli na ya haki.[19] Mkabala wa hilo, yaani kutokushukuru huwa sababu ya mwanadamu kupata adhabu.[20]

Rejea

Vyanzo