Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Aya ya Tayammum

Kutoka wikishia

Aya ya Tayammum (Kiarabu: آية التيمم ) ni inayopatikana katika sehemu ya mwisho ya Aya ya 6 ya Surat al-Maa’idah na Aya ya 43 ya Surat An-Nisaa. Aya hii ni miongoni mwa Aya mama za kisheria (Ayaatul Ahkaam) zilizomo ndani ya Qur’ani Tukufu. Kwa mujibu wa mafundisho ya Aya hii, mafakihi wameafikia kuwa tayammum ni mbadala wa kisheria wenye kuchukua nafasi ya Udhu na Ghusl (josho la wajibu), katika mazingira ambayo maji hayawezi kupatikani, au matumizi yake yanaweza kusababisha madhara kiafya. Aidha, mafakihi wamefafanua vya kutosha juu ya utaratibu wa kutekeleza tayammum.

Tofauti za kitafsiri na uelewa wa baadhi ya maneno yaliyomo ndani ya Aya ya tayammum, zimepelekea kuzaliwa mitazamo tofauti ya kifiqhi miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu kuhusiana na namna sahihi ya kutekeleza tayammum, na maeneo yanayopaswa kupanguswa ndani ya kitendo cha tayammum. Kwa mfano, wengi miongoni mwa mafaqihi wa Kishia wa kutokea upande wamadhehebu ya Imamiyyah, wakitoa hukumu ya kupangusa katika tendo la tayammum, wanasema kwamba; kulingana maelezo ya Aya ya kutammam, haipaswi kwa mwenye kutayyamma kuupangusa uso wake mzima katika utekelezaji wake wa amali hiyo, bali yatosha kupangusa sehemu tu ya uso wake, ambayo ni paji la uso. Kinyume chake, mafaqihi wa madhehebu ya Ahlu al-Sunnah wanaiona Aya hiyo kuwa inawajibisha kuupangusa uso mzima bila ya kuacha kitu ndani yake.

Aisha kwa mujibu wa fatwa za wanazuoni wa Shia Imamiyyah, ni kwamba; kile kipengele kinachohusiana na kufuta mikono kilichoko ndani ya Aya husika, kinamtaka mwenye kutayammam kufuta viganja vya mikono yake kwa kupitisha kiganja cha mkono wake wa kushoto juu ya nyuma ya mkono wake wa kulia, huku akifuta kuanzia kwenye kifundo cha mkono huo hadi ncha za vidole. Kisha kuweka tena mkono wake wa kuli juu ya nyuma ya mkono wake wa kushoto na kufanya kama alivyofanya kwenye mkono wake wa kulia. Hata hivyo, baadhi ya mafaqihi wa Ahlu-Sunnah wanasema kuwa; ni wajibu kufuta kuanzia ncha za vidole hadi kwenye viwikoni (kwenye kisugudi).

Matini ya Aya

Mada ya kisheria inayobainisha na hukumu ya tayammum imekuja mara mbili ndani ya Qur’ani Tukufu. Mara ya kwanza, ni mwishoni mwa Aya ya 6 ya Surat al-Ma’ida, ambako kumefafanuliwa masharti na taratibu za kujitoharisha. Mara ya pili, mada hii imekuja mwishoni mwa Aya ya 43 ya Suratu al-Nisaa, ambako hukumu hiyo imetajwa tena kwa muktadha wa mazingira fulani yanayomzuia mja matumizi ya maji. Matini ya Aya hizo ni kama ifuatavyo:


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَى حَتَّى تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّى تَغْتَسِلُوا وَإِنْ كُنْتُمْ مَرْضَى أَوْ عَلَى سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِنْكُمْ مِنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا


Enyi mlioamani! Msikaribie Sala mkiwa katika hali ya ulevi (kulewa), kiasi cha kutoweza kubaini bayana matamshi yenu. Kadhalika, msingie (msimamishe) Sala mkiwa na hali ya janaba (unyama mkubwa wa kiibada) hadi pale mtakapofanya ghusli (kuoga), hadi mtakapokuwa na ufahamu kamili wa maneno mnayoyatamka. Na wala, msiikaribie Sala hali mkiwa katika na janaba, hadi mtakapojitoharisha kwa kuoga josho la janaba, isipokuwa kwa yule mpita njia tu (atakayengia msikitini kwa dharura. Kwa mfano labda alisahau kitu msikitini). Na endapo mtakuwa katika hali ya ugonjwa, au mpo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni, au mmegusana (mmeingiliana) na wanawake; kisha mkakosa maji ya kujitoharisha, basi fanyeni tayammum kwa kutumia kutumia sehemu ya tabaka la juu ya ardhi iliyo safi (ardhi safi/vumbi safi). Basi Jifuteni nyuso zenu na mikono yenu (kwa kutumia udongo huo). Kwa hakika, Mwenye Ezi Mungu daima ni Msamehevu na Mrehemevu.[1]

وَإِنْ كُنْتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا وَإِنْ كُنْتُمْ مَرْضَى أَوْ عَلَى سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِنْكُمْ مِنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ مِنْهُ مَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُمْ مِنْ حَرَجٍ وَلَكِنْ يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ.


Na ikiwa mpo katika hali ya janaba, basi jitohasheni. Lakini, iwapo mtakuwa ni wagonjwa, au mko safarini, au mmoja wenu ametoka chooni, au mmeingiliana na wanawake, kisha mkakosa maji, basi tayamamuni kwa kwa kutumia ardhi safi (vumbi safi). Hivyo basi futeni nyuso zenu na mikono yenu kwa kutumia ardhi hiyo. (Bila shak) Mwenye Ezi Mungu hataki kukutieni matatizoni (katika sheria hii). Bali, anataka kukutakaseni na kukukamilisheni neema Zake juu yenu, hwenenda awa ni wenye kushukuru.[2]


Nafasi ya Aya ya Tayammum

Aya ya tayammum ni miongoni mwa Ayaatul Ahkaam (Aya za Hukumu) zilizomo ndani ya Qur’ani Tukufu. Kwa kutegemea ushahidi wa Aya hii, wanazuoni wa sheria za Kiislamu wamewea kutoa fatwa juu ya uhalali wa tayammum kama mbadala wa Udhu na Ghusli (josho la wajibu).[3] Pia Aya hii ndiyo inayotumiwa na wanazuoni wa fiqhi kwa ajili ya kubainisha masharti na namna ya kutayammam kwa ajili ya kusimamisha Sala, pale ambapo watu watakosa maji ya kwa ajili Udhu au Ghusli.[4] Kwakua Aya hii ndiyo inaweka msingi wa kuruhusu uhalali wa tayammum kama mbadala wa Wudhu na Ghusli, hii ilipelekea Aya hii kujulikana kwa jina la Aya ya Rukhsa, ikimaanisha Aya inayotoa ruhusa ya kisheria.[5]

Vigezo vya Uhalali wa Tayammum

Mafaqihi (wanazuoni wa sheria ya Kiislamu), kwa kuzingatia Aya husika, wametaja na kuweka wazi hali zinazomruhusu mtu kufanya Tayamum badala ya Udhu na Ghusli. Hali hizo ni kama ifuatavyo:

  • Maradhi: Kwa mujibu wa kifungu kisemacho وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ (Na iwapo mtakuwa wagonjwa), kilichoko katika Aya husika, imefahamika kwamba; iwapo mukallaf (mtu aliye na jukumu la kisheria) atakuwa katika hali ya ugonjwa, kwa namna ambayo hataweza kutumia maji kwa sabubu ya madhara yanayoweza kusababishwa na maji hayo, hiyoitampa ruhusa ya kutayamma badala ya kutia Udhu na kukoga.[6]
  • Kukosekana kwa Maji: Kfifungu kisemacho فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً (Mkiwa hamkupata maji) kinaruhusu moja kwa moja kwamb; endapo mukallaf atakuwa katika hali hadath asghar (uchafu mdogo) au khadath akbar (uchafu mkubwa), kisha akawa hana maji ya kutosha kwa ajili ya Udhu na Ghusli (josho la wajibu), au pia akawa hana uwezo wa kuyafikia maji hayo, basi ataruhusiwa kufanya tayamum badala ya Udhu na Ghusli.[7]

Safari

Katika kufasiri kifungu cha Qur’ani kisemacho أَوْ عَلَیٰ سَفَرٍ (au mkiwa safarini), wanazuoni wa Fiqhi na Kigezo:Wafasiri wa Qur’ani, wanasema kwamba; safari kama safari, si sababu moja ya inayompelea mtu alazimike kutafuta Udhu au Ghusli. Bali sababu iliyopelekea kifungu hicho kutajwa katika Aya hiyo ni kwamba; mara nyingi safari huambatana na mazingira ya kukosa maji, au kuyapata kwa njia ya shida na mashaka, kiasi kwamba muislamu anaweza kuogopa na kuhisi kwamba, iwapo atayatumia maji hayo kwa Udhu au Ghusli, basi maisha yake yatakuwa hatari kutokana na kiu kali inayosababishwa na mashaka ya safari. Katika hali kama hizi, Sharia inamruhusu mja kufanya tayammum, kama mbadala wa Udhu au Ghusli.[8]

Tofauti za Kimitazamo Kuhusiana na Maana ya Maneno ya Aya

Kumekuwa na tafsiri mbalimbali za maneno fulani yaliyotumika katika Aya za Qur'ani, tofauti ambazo zimepelekea kuwepo kuwepo kwa fatawa tofauti miongoni mwa wanazuoni mbali mbali wa fani ya fiqhi. Maneno muhimu yenye khitilafu miongoni mwa wanazuoni wa fiqhi na wafasiri mbali mbali ni kama ifuatavyo:

«Neno Lamastum (لامَسْتُم)»

Neno (لامَسْتُم) (Lamastum) linalotokana na mzizi wa neno (لَمْس) (Lamsu) lenye maana ya kugusa: Kulingana na mafaqihi na wafasiri wa Qur'ani wa upande wa madhehebu ya Shia, neno hili halirejelei tu maana ya mguso wa kugusana kimwili mwanamke; bali ni lugha ya kimajazi inayomaanisha tendo la ndoa. Nalo ndilo tendo lenye kuwajibisha josho la kuoga janaba.[9] Baadhi ya Mafaqihi (wanazuoni wa sheria ya Kiislamu), wakiwemo Fadhil Miqdad katika Kanz al-Irfan na Rashid Ridha katika Tafsir al-Manar, wamemnasibishia Imam Shafi'i rai nadharia ya kifiqhi inayodai kwamba; miongoni mwa mambo yanayobatilisha Udhu, ni lile tendo la kugusana kimwili tu kati ya mwanamume na mwanamke Ghair-Mahram (asiye ruhusiwa kisheria kumgusa kabla ya ndoa).[10] Hoja hii ya kifiqhi imejengwa kupitia welewa wa wahusika wa fatwa hiyo, katika kuzifahamu na kuzifasiri Aya zilizokuja kufafanua hukumu na masharti yanayojuzisha tayammum. Ama Msimamo wa Malik ibn Anas, mmojawapo wa Maimamu wakuu wa Madhehebu Manne ya Fiqhi za Ahli-Sunnah unasema kwamba; mgusano wa kimwili baina ya mwanamke na mwanamme walioko nje ya ndoa unaopelekea kubatilika kwa Udhu, ni ule mgusano wenye kuambatana na hisia za matamanio ya kijinsia.[11]

«Neno Sa'id ( صَعِيد)»

Istilahi ya Neno ( صَعِيد) (Sa'id) imekuwa ndiyo kiini cha chimbuko la mijadala ya kifiqhi kuhusiana na uanishaji wa mipaka juu ya nyenzo zinazokubalika kisheria katika utekelezaji wa tayammum. Tofauti hizi hutokana na tafiti za kileksika na kisemantiki za neno hilo, lenye nafasi ya kiutaratibu katika kubainisha ardhi inayokubalika kutumika kama chombo cha utakaso mkavu (tayammum).[12] Kwa mujibu wa wanazuoni wa Kishia, leksimu (kipashio) “Sa‘id” inahusiana na kila kipengele (kitu) kinachobeba sifa za ardhi, kuanzia mawe, udongo mgumu hadi chembe za kokoto.[13] Kinyume chake, baadhi ya watafiti wa taaluma ya lugha, kama vile mfano Jawhari, wameonekana kulifinya na kulipa maana nyembamba mno neno hilo, ambapo wamelihusisha tu na udongo laini au vumbi. Hii ndiyo sababu ya kupatikana khitilafu katika utoaji wa fatwa ndani ya mada hii.[14]

Ufafanuzi wa Neno طَیِب (Tayyib) katika Kipengele cha Sa'idan Tayyiban"'

Baada ya kujadili maana ya neno "Sa'id", lenye maada ya tabaka la juu la ardhi, sasa tunaangazia neno طَیِب (Tayyib) lenye maana ya kitu bora au safi, lililoko katika Aya ya Qur'an inayoelekeza tayammum, neno ambalo limekuja kama ni sifa ya ardhi katika Aya hiyo. Kimsingi, wasomi wana mitazamo miwili mikuu kuhusiana na neno طَیِب (Tayyib):

  1. Tabataba'i (katika kitabu chake Al-Mizan) akitoa tafsiri ya neno hili anasema kwamba: Neno "Tayyib", ni sifa inamaanisha uasili wa ardhi. Hivyo basi ardhi yoyote ile, iwe udongo au jiwe, haipaswi kuwa imepoteza hali yake ya asili. Hii inamaanisha kwamba; haikubaliki mtu kutumia vifaa kama vile; jasi, chokaa, au vitu vingine vinavyofanana na hivyo ambavyo vimebadilishwa kutoka katika hali yake ya kiasili kwa kuokwa au kwa kupashwa moto.[15]
  2. Mtazamo wa pili unafasiri siya ya "Tayyib" kwa maana ya usafi. Wasomi hawa huamini kwamba neno "Tayyib" lililotumika katika Aya ya tayammum, limekuja likinamaanisha ardhi safi. Hivyo basi, wao wanaamini kwamba; ni lazima ardhi inayotumiwa kwa ajili ya tayammum iwe ni ardhi safi na isiwe na najisi ndani yake.[16]

Maana ya Tayammum (Utakaso Mkavu)

Makala Kuu: Kutayammam (Utakaso Mkavu)

Kuna tofauti za kimitazamo miongoni mwa wanazuoni kuhusiana na maana ya neno "tayammum" linapotumika katika Aya za Qur'an zilizotangulia. Tofauti hizi za kimitazamo zimekuja kutokana ufasiri wa neno hili, ambao wakati mwengine limeonekana kufasiriwa kilugha na wakati mwengine kiistilahi. Mitindo ya tafasiri mbili hizi ni kama ifuatavyo:

  1. Tafsiri ya Lugha (Maana ya Asili): Wako walioona neno tayammum linapaswa kufasiriwa kulingana na maana yake ya kiasili (leksika), ambapo neno hubeba maana ya kukusudia au nia.[17]
  2. Tafsiri ya Kisheria (Maana ya Shar'i): Wengine wanaamini kuwa; neno hili ni istilahi ya maalumu inayohusiana na dini/kisheria, yenye maana ya hatua maalum ya utakaso.[18] Na maana yake ni: kugusa (kugongesha) viganja vya mikono juu ya ardhi safi, kisha kupaka uso na sehemu ya nyuma ya mikono kwa kutumia viganja hivyo vilivyogusishwa (vilivyogongesha) kwenye ardhi hiyo.[19]

Jinsi ya Kutayammam (Kwa Mujibu wa Fiqhi ya Imamiyya)

Wanazuoni wa sheria za Kiislamu (mafiqihi), wakirejelea Aya ya Qur'an inayosema: فَامْسَحُوا بِوُجُوهِکمْ وَأَیدِیکم؛ (Panguseni nyuso zenu na mikono yenu), kila mmoja kulingana na madhehebu yake wameweza kubainisha hukumu mbali mbali kuhusiana na tayammum, ikiwemo; jinsi ya kufanya tayammum, viungo vya tayammum pamoja na mipaka unayohusiana na tayammum kwenye viungo hivyo.[20] Wanazuoni wengi wa kundi la Imamiyyah (miongoni mwa madhehebu ya Kishia) wanaamini kwamba; herufi 'Ba’' (ب) inayopatikana katika neno بِوُجُوهِکمْ / bi-wujūhikum (pa au penye nyuso zenu), ina maana ya "baadhi". Hivyo basi, wao huamini kuwa yatosha mwenye kutayammam kupangusa sehemu tu ya uso wake.[21] Aidha kwa kuzingatia mafundisho ya Sunna za bwana Mtume (s.a.w.w) na Maimamu Maasumu (a.s), Shia Imamiya wanasema kuwa; sehemu iliyokusudiwa hapo, ni sehemu ya paji la uso. Ama kwa upande kiwango kinachopaswa kupanguswa, wao wanaamini kwamb; ni wajibu (lazima) kupangusa paji la uso kwa kutumia mikono yote miwili, na kupangusa huku kunapaswa kuanza kutokea sehemu ya juu ya paji la uso na kwenda hadi kwenye nyusi na sehemu ya juu ya pua.[22] Baada ya kumaliza kupangusa paji la uso, kulingana na fiqhi ya Imamiya, ni wajibu kupangusa migongo ya viganja vya mikono miwili. Hili hufanyika kutoka kifundo cha mkono (kiganja) hadi mwishoni mwa ncha za vidole, kwa kutumia mkono mwingine (yaani, mkono wa kulia hupanguswa kwa kushoto, na kinyume chake).[23]

Kulinga na maelazo yanayonukuliwa kutoka kwa Muhammad Jawad Maghniyyah, ni kwamba; Madhehebu yote manne ya Ahlu-Sunnah pamoja na Sheik Saduq wa upande wa madhehebu ya Shia Imamiyyah wanatoa tafsiri moja kuhusu neno "Wujuh" (uso) lililokuja katika Aya ya Qur'ani فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ (Futeni Nyuso zenu). Wao wanasema kwamba; neno hio linamaanisha uso mzima, na si sehemu tu ya uso huo. Hivyo, inakuwa ni wajibu kwa mwenye kutayammam kupangusa uso mzima, ikijumuisha ndevu zilizopo katika maeneo husika ya uso huo.[24] Tukirudi kwenye neno أَيْدِ (Ayd) linalohusiana na kupangusa mikono katika tayammum, tutayakuta madhehebu ya Shafi'iyyah na Hanafiyyah yakiamini kwamba; neno hili linarejelea eneo la mikono linaloanzia Atraaf al-Asabi’i (ncha za vidole) hadi Mirfaq (kiwiko), kama ilivyo katika utekelezaji wa Udhu. Kwa hivyo, eneo hilo lote ndilo linapaswa kufutwa katika utekelezaji wa tayammum.[25] Mtazamo wa madhehebu ya Malikiyya na Hanbaliyya unasema kwamba; ni wajibu kufuta kuanzia ncha za vidole hadi kweny vifundoni mwa mkono), na ni Mustahab (Sunnah) kupangusa hadi viwikoni mwa mikono hiyo.[26]

Rejea

  1. ↑ Surat al-Nisaa, Aya ya 43.
  2. ↑ Surat al-Maida, ya 6.
  3. ↑ Fadhil Miqdad, Kanz al-Irfan Fi Fiqh al-Qur’an, 1373 S, juz. 1, uk. 27; Irwani, Durusu Tamhidiya Fi Tafsiri Ayaat al-Ahkam, 1428 AH, juz. 1, uk. 76.
  4. ↑ Fadhil Jawad, Masalik al-Afham ila Ayaat al-Ahkam, 1365 AH, juz. 1, uk. 66-67; Bahrani, Hadaik al-Nadhirah, 1363 AH, juz. 4, uk. 243-244.
  5. ↑ Suyuti, Al-Durr al-Manthur, Dar al-Fikr, juz. 3, uk. 26.
  6. ↑ Fakhr al-Razi, Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 11, uk. 309; Fadhil Jawad, Masalik al-Afham ila Ayaat al-Ahkam, 1365 AH, juz. 1, uk. 63.
  7. ↑ Fadhil Miqdad, Kanz al-Irfan, 1373 AH, juz. 1, uk. 26.
  8. ↑ Muhaqiq Ardabili, Zubdat al-Bayan, Al-Muktabat al-Murtadhawiyya li-Ihyaa’i al-Athar al-Ja’fariyya, uk. 19; Fakhr Razi, Tafsir al-Kabeer, 1420 AH, juz. 11, uk. 310; Tabataba'i, al-Mizan, 1363 AH, juz. 5, uk. 226.
  9. ↑ Fadhil Miqdad, Kanz al-Irfan, 1373 AH, juz. 1, uk. 25; Fadhil Jawad, Masalak al-Afham ila Ayaat al-Ahkam, 1365 AH, juz. 1, uk. 63.
  10. ↑ Fadhil Miqdad, Kanz al-Irfan, 1373 AH, juz. 1, uk. 25; Rashid Ridha, Tafsir al-Manar, 1990 AH, juz. 5, uk. 97.
  11. ↑ Alusi, Tafsir Ruh al-Ma'ani, 1415 AH, juz. 3, uk. 41; Fadhil Miqdad, Kanz al-Irfan, 1373 AH, juz. 1, uk. 25.
  12. ↑ Najafi, Jawahir al-Kalam, 1362 AH, juz. 5, uk. 120.
  13. ↑ Najafi, Jawahir al-Kalam, 1362 S, juz. 5, uk. 118; Sabzivari, Mahdhab al-Ahkam, Dar al-Tafsir, juz. 4, uk. 377.
  14. ↑ Jawahiri, Sihah al-Lugha, 1407 AH, chini ya neno "Sa'id".
  15. ↑ Tabataba'i, Al-Mizan Fi Tafsir al-Quran, 1417 AH, juz. 5, uk. 229.
  16. ↑ Muhaqiq Ardabili, Zubdat al-Bayan, Al-Muktabat al-Murtadhawiyya li-Ihya'i Athar al-Ja'fariyya, uk. 19; Fadhil Jawad, Masalak al-Afham ila Ayaat al-Ahkam, 1365 AH, juz. 1, uk. 66.
  17. ↑ Tazama Muhaqiq Ardabili, Zubdat al-Bayan, al-Muktabat al-Murtadhawiyya l-Iya al-Athar al-Ja'fariyya, uk. 19; Rashid Ridha, Tafsir al-Manar, 1990, juz. 5, uk. 100.
  18. ↑ Tabarsi, Majma' al-Bayan, 1415 AH, juz. 3, uk. 91; Bahrani, al-Hadaik al-Nadhira, 1363 AH, juz. 4, uk. 244.
  19. ↑ Amili, Madariq al-Ahkam, 1429 AH, juz. 2, uk. 175.
  20. ↑ Muhaqiq Ardabili, Zubdat Al-Bayan, Al-Muktabat al-Murtazawiyya Li-Ihya'i al-Athar al-Jaafari, uk. 19; Fakhr Razi, al-Tafsir al-Kabir, 1420 AH, juz. 11, uk. 313.
  21. ↑ Fadhil Miqdad, Kanz al-Irfan, 1373 S, juz. 1, uk.27; Fadhil Jawad, Masalak al-Afham ila Ayaat al-Ahkam, 1365, juz. 1, uk.66.
  22. ↑ Fadhil Miqdad, Kanzu al-Irfan, 1373 S, juz. 1, uk.27.
  23. ↑ Fadhil Miqdad, Kanzu al-Irfan, 1373 S, juz. 1, uk.27; Mughniyeh, Fiqh Ala al-Madhahib al-Khamsa, 1421 AH, uk. 71.
  24. ↑ Mughniyeh, Fiqh Ala al-Madhahib al-Khamsa, 1421 AH, uk. 70.
  25. ↑ Mughniyeh, Fiqh Ala al-Madhahib al-Khamsa, 1421 AH, uk. 70.
  26. ↑ Jaziri, Fiqh Ala al-Madhahib al-Arba, 1419 AH, Juz. 1, uk. 248; Mughniyeh, Fiqh Ala al-Madhahib al-Khamsa, 1421 AH, uk. 70.

Vyanzo

  • Alousi, Mahmoud bin Abdullah, Tafsir Ruh al-Ma'ani, Beirut, Dar al-Katb al-Alamiya, 1415 AH.
  • Irwani, Mohammad Baqir, masomo ya utangulizi katika tafsiri ya aya za Al-Ahkam, Qom, Dar al-Fiqh kwa uchapishaji na uchapishaji, chapa ya tatu, 1428 AH.
  • Bahrani, Youssef, Hadaeq al-Nadrah, Qom, Al-Fakr al-Islami Foundation, 1363.
  • Johari, Abu Nasr Ismail bin Hammad, Sahaha Taj al-Lagha na Sahaha al-Arabiyyah, Beirut, Dar al-Alam Lamlayin, chapa ya 4, 1407 AH.
  • Rashid Reza, Muhammad, Tafsir al-Manar, Misr, Al-Masriyya al-Al-Katab, 1990.
  • Sabzevari, Seyyed Abdul Ali, Mahezab Al-Ahkam, Qom, Dar al-Tafseer, Bita.
  • Siyuti, Jalaluddin, Alder al-Manthor, Beirut, Dar al-Fakr, Bita.
  • Tabatabaei, Sayyid Muhammad Hussein, Al-Mizan fi Tafsir al-Quran, Qom, Ismailiyan Publications, 1363 AH.
  • Tabarsi, Fadl ibn Hassan, Majma al-Bayan, Beirut, Al-Alamy Publications Foundation, 1415 AH.
  • Fadel Jawad, Jawad ibn Saeed, Masalak al-Afham ili Ayat al-Ahkam, Tehran, Mortazavi Publications, 1365 AH.
  • Fadel Miqdad, Miqdad ibn Abdullah, Kanz al-Irfan fi Fiqh al-Quran, Tehran, Mortazavi Publications, 1373 AH.
  • Fakhr Razi, Muhammad bin Omar, Tafsir al-Kabir, Beirut, Dar Ihya al-Turat al-Arab, 1420 AH.
  • Mohaqiq Ardabili, Ahmad bin Muhammad, Zubdat al-Bayan fi Akhmaan al-Quran, Tehran, Al-Muktabah al-Murtazaviya la Ihya al-Athar al-Jaafariyya, Beta.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Elimu ya Sheria juu ya Shule Tano za Fikra, Beirut, Dar Al-Tiyar al-Jadeed, 1421 AH.
  • Najafi, Muhammad Hassan, Vito vya Hotuba, Beirut, Dar Ihya al-Turaht al-Arabi 1983.