Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Allah

Kutoka wikishia

Allah (Kiarabu: اللّه); ni jina maalumu na maarufu zaidi la Mungu linalotumika katika dini ya Kiislamu. Kwa mujibu wa imani ya wanazuoni wa Kiislamu, Allah ni jina linalokusanya sifa zote kamilifu za Kiungu na ndilo Ismu al A'adham (Jina Kuu Zaidi). Kadhalika, wanazuoni hawa wanasema kuwa, jina hili lina nafasi ya juu zaidi katika Qur'ani na dua mbalimbali, na ndilo mhimili mkuu wa imani ya upweke wa Mungu, Shahada mbili, uliomo ndani ya Aya mbalimbali za Qur'ani. Neno Allah ni jina maalumulinalotumika kwa ajili ya Mungu tu, na wala halitumiwi kwa ajili ya kumwashiria mwengine yeyote yeyote yule asiyekuwa Yeye. Neno hili limetajwa zaidi ya mara 2000 katika Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya Ja'afar Subhani, ambaye ni mfasiri wa Qur'ani, ni kwamba; idadi kubwa ya wanahadithi na wafasiri wanaamini kuwa ,neno Allah limetokana na mzizi wa neno "Alaha" (اله) lenye maana ya "mwenye kustahiki kuabudiwa". Pamoja na hayo, kuna mitazamo mingine iliyotajwa kuhusiana na asili ya neno hili, ikiwa ni pamoja na maana ya kustaajabisha (tahayyur), kukimbilia msaada (faza'a), na kupata utulivu wa moyo.

Picha ya mchoro wa neno Allah iliyochorwa juu ya ukuta wa Haramu ya Imam Hussein (a.s)

Tukirudi katika irfani ya Kiislamu, tutalikuta jina Allah likiwa kileleni mwa mfumo (mlolongo) wa majina ya Mwenyezi Mungu, na majina mengine yote yanachimbuka kutoka kutoka katika kiini cha jina hili. Neno Allah lina matumizi mbalimbali katika utamaduni na jamii za Kiislamu. Miongoni mwa matumizi yake, ni kutumiwa kwenye sarafu za zama mbalimbali za Kiislamu pamoja na maeneo matakatifu, kama vile haramu na misikiti. Pia miongoni mwa matumizi yake mengine ni kuandikwa kwenye bendera na nembo za kitaifa za baadhi ya nchi za Kiislamu, kama vile Iran, Jamhuri ya Azerbaijan, na Iraq.

Nafasi ya Jina la Allah katika Utamaduni wa Kiislamu

"Allah" ni jina maalumu la Mwenyezi Mungu[1] na ni maarufu zaidi katika dini ya Kiislamu.[2] Wanazuoni wa Kiislamu wanalichukulia jina hili kuwa ndiyo mhimili mkuu wa upweke wa Mungu na Ikhlasi, na ndilo jilna lenye nafasi ya juu zaidi katika Qur'ani na dua mbalimbali.[3] Pia wanazuoni hawa wanasema kuwa, neno Allah lina maana na rejeo moja tu nalo ni Mwenyezi Mungu. Jina hili ndilo jina pekee linalokusanya sifa zote za ukamilifu wa Mwenyezi Mungu, na halitumiwi kwa mwengine yeyote yule asiyekuwa Mungu.[4] Hivyo basi, jina la Allah ndilo linaloshika mhimili mkuu katika mada zinazomuhusu Mwenyezi Mungu katika Kitabu kitakatifu cha Waislamu (Qur'ani) na Nahj al-Balaghah. Aidha imeelezwa kuwa, sifa zote za ukamilifu wa dhati ya Mungu zilizomo katika Qur'ani zinathibitishwa kupitia jina hili la Allah.[5]

Neno Allah ndilo mhimili wa kauli mbiu mbili kuu za Uislamu, yaani Shahada mbili; uwepo wa mungu yeyote asiyekuwa Allah unakanushwa kupitia shahada ya kwanza, na shahada ya pili ainatambulisha au inamtambua rasmi Mtume Muhammad (s.a.w.w.) kama mjumbe wa Allah.[6]

Neno Allah, likiambatana na majina mengine kama "Rab" (Mola) na "Ilah" (Mungu wa kuabudiwa), ndiyo majina yanayotumiwa zaidi kwa ajili ya Mungu katika Qur'ani.[7] Inaelezwa kwamba, neno Allah limekaririwa mara 2699 katika Qur'ani Tukufu,[8] mara 2702,[9] au mara 2807.[10]

Idadi kubwa ya wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kuwa, Allah ndilo Jina tukufu zaidi Ismu al A'adham (jinata tukufu zaidi).[11] Miongoni mwa sababu za jina hili kuwa ni jina tukufu zaidi, ni kwamba neno Allah ndilo msingi mkuu wa upweke wa Mungu, na asiyeamini, kwa kulitamka neno hili, mtu huvuka kutoka kwenye ukafiri na kuingia kwenye imani (Uislamu). Na iwapo mtu atatamka na kutaja jina jengine lisilikuwa hilo, kama vile "La ilaha illa al-Rahman" (Hapana mungu isipokuwa Mwingi wa Rehema), tamko hilo halitamtoa katika ukafiri na kuingia katika Uislamu.[12]

Kuna visawe mbalimbali vinavyotumika katika lugha mbalimbali kama mbadala wa neno Alllah. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili hutumika neno "Mungu", na katika lugha ya Kiajemi, neno Khoda ndilo linalotumika kama kisawe mbadala cha neno "Allah".[13] Aidha kuna visawe kadhaa vya jina hili vinavyopatikana ndani ya vitabu vya dini mbalimbali. Katika tafsiri za hivi karibuni za vitabu vitakatifu vya Wayahudi, Wakristo, na Wazoroasta, majina kama vile "Yehova", "Theos", na "Ahura Mazda" yanayoashiria Mungu, yametafsiriwa kama visawe vya"Allah" linalotumiwa na wazungumzaji wa lugha ya Kiarabu.[14] Neno Allah lilikuwa likitumiwa hata kabla ya ujio wa Uislamu. Aidha katika Sura ya 87 ya Surat al-Zukhruf na Sura ya 25 ya Surat Luqman, kuna ishara zinazoonesha matumizi ya neno hili kabla ya kuteremshwa kwa Qur'ani.[15]

Asili ya Neno na Maana Yake

Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa neno Allah ni la asili ya lugha ya Kiarabu,[16] ilhali wengine wanasema kuwa, asili yake ni ya Kiebrania au Kisuryani.[17] Kwa mujibu wa maoni ya baadhi ya wasomi, neno "Allah" asili yake ilikuwa ni "Al Ilah" (الإله), ambapo hamza ya pili iliondolewa kutokana na kutumika mara kwa mara na likasalia kuwa ni "Allah".[18] Wengine nao wanaamini kuwa neno Allah limetokana na mzizi wa neno "Laha" (لاه), ambapo herufi za "Al" (ال) zilipowekwa mwanzoni mwake, lilibadilika na likawa "Allah".[19] Kuna hitilafu za mitazamo kuhusu iwapo neno Allah limenyumbulika kutoka kwenye neno jengine au ni jina ghafi (lisilonyumbulika).[20] Kwa mujibu wa maelezo ya Fakhru al Razi, mafakihi wengi na wanazuoni wa Usuul al Fiqhi wanaamini kuwa jina hili halikunyumbulika kutoka kwenye neno jengine.[21] Wale wanaomini kuwa neno Allah limenyumbulika kutoka kwenye mzizi wa neno jengine, wanataja asili mbalimbali za mzizi wa jina hili.[22] miongoni mwa nadharia mbalimbali kuhusiana na neno hilo ni kama ifuatavyo:

Neno Allah likiwa limeandikwa kwenye minara ya Haramu ya Imam Ali (a.s)
  • Jina la Allah limenyumbulika kutoka kwenye mzizi wa neno "Alaha" (اله) au (Aliha), lenye maana ya "mwenye kustahiki kuabudiwa".[23] Kwa mujibu wa maelezo ya Ja'far Subhani, ambaye ni mfasiri wa Qur'ani, ni kwamba; idadi kubwa ya wanahadithi na wafasiri wamekubaliana na mtazamo huu.[24] Maana hii pia imepokewa katika hadithi mbalimbali.[25]
  • Kauli nyengine inasema kuwa; Limenyumbulika kutoka neno "Aliha" (أَلِهَ) au "Waliha" lenye maana ya "kustaajabu / kuchanganyikiwa" (tahayyur); kwa sababu akili za wanadamu zinashindwa kuifikia dhati Yake.[26]
  • Limenyumbulika kutoka kwenye mzizi wa neno "Alaha" lenye maana ya "kukimbilia msaada na kutegemea" (faza'a); kwa sababu viumbe humkimbilia na kumtegemea Yeye, pale wanapokabiliwa na shida na dhiki mbalimbali.[27][28]
  • Wengine wamesema neno hili limenyumbulika kutoka kwenye mziziz wa neno "Alaha" lenye maana ya "utulivu wa moyo"; kwa sababu kumkumbuka Allah kunaleta utulivu na amani moyoni.[29]
  • Pia kuna waliosema kuwa neno Allah limenyumbulika kutoka kwenye mzizi wa neno "Laha" (لاهَ) lenye maana ya "kufichika"; kwa sababu Mwenyezi Mungu amefichikana na akili, dhana, na fikra za viumbe.[30]

Allah katika Irfani ya Kiislamu

Kwa mujibu wa watafiti wa masuala ya kiiirfani, katika Irfani ya Kiislamu ni kwamba majina ya Mwenyezi Mungu yamepangwa kwa utaratibu maalumu, na jina linalokusanya sifa zote yaani Allah, ndilo lililoko kileleni mwa majina yote ya Mwenyezi Mungu. Kwa mtazamo wa wanazuoni hawa, Baada ya jina hili, yanafuata majina manne makuu nayo ni "al-Awwal" (yaani wa Kwanza, "al-Aakhiru" (wa Mwisho), "Dhahiru", (wa Dhahiri) na "al-Baatinu" (wa Siri). Baada majina hayo yanafuata Majina Saba Makuu (Asma al Sab'ah) ambayo yanachimbuka kutoka kwenye jina la Allah, na utaratibu huu unaendelea hadi kufikia majina madogo zaidi ya sifa Zake. Kwa hiyo, katika irfani, sifa na majina yote ya Mungu yanarejea kwenye jina hili kuu la Allah.[31]

Matumizi ya Neno Allah

Neno Allah limeandikwa kwenye bendera na ni nembo ya kitaifa ya Iran[32] na kwenye nembo ya kitaifa ya Jamhuri ya Azerbaijan.[33] Pia neno hiili limo katika bendera na nembo ya nchi ya Iraq, na ni neno linalotumiwa katika kauli mbiu ya "Allahu Akbar" (Allah ni Mkubwa Zaidi).[34] Neno Allah, likiwa peke ya au likiwa limeunganishwa na maneno mengine, lilikuwa ni miongoni mwa maandishi muhimu yaliyochorwa kwenye sarafu za tawala mbalimblai za Kiislamu zilizopita.[35] Neno hili pia limetumiwa kwa njia mbalimbali katika maeneo mengi matakatifu kama vile haramu takatifu na misikiti mbalimbali ulimwenguni. Kadhalika, waandishi na wataalamu wengi wa sanaa ya kaligrafia wamekuwa wakiandika neno hili kwa kutumia mitindo na aina mbalimbali za miandiko ya kaligrafia:

Rejea

  1. Fakhru al Razi, Al Tafsir al Kabir, Juz. 1, uk. 143; Tabataba'i, Al Mizan fi Tafsir al Qur'an, Juz. 1, uk. 18; Subhani, Manshure Javid, Juz. 2, uk. 119.
  2. Kaf'ami, Al Maqamu al Asna, uk. 25.
  3. Kaf'ami, Al Maqamu al Asna, uk. 25-26.
  4. Safi Gulpaygani, Al Ilahiyyat fi Nahj al Balaghah, uk. 36.
  5. Safi Gulpaygani, Al Ilahiyyat fi Nahj al Balaghah, uk. 33-36.
  6. Paketchi, «الله» (Allah), uk. 73.
  7. Misbah Yazdi, Khodaashinasi, uk. 58.
  8. Ruhani, Al Mu'ujam al Ihsai li Alfadhi al Qur'an al Karim, Juz. 2, uk. 244-262.
  9. Safi Gulpaygani, Al Ilahiyyat fi Nahj al Balaghah, uk. 34.
  10. Kashifi, Jawahir al Tafsir, uk. 357; Ashtiyani, Tafsire Sureye Fatihat al Kitab, uk. 63.
  11. Kashifi, Jawahir al Tafsir, uk. 357, 361; Kaf'ami, Al Maqam al Asna, uk. 26; Khomeini, Misbah al Hidayah, uk. 12-13; Ashtiyani, Tafsire Sureye Fatihat al Kitab, uk. 64.
  12. Kashifi, Jawahiru al Tafsir, uk. 361; Ashtiyani, Tafsire Sureye Fatihatu al Kitab, uk. 64.
  13. Jawadi Amoli, Tauhid dar Qur'an, uk. 228.
  14. Paketchi, «الله» (Allah), uk. 73.
  15. Tabataba'i, Al Mizan fi Tafsir al Qur'an, Juz. 1, uk. 18; Subhani, Manshure Javid, Juz. 2, uk. 116-117.
  16. Fakhru al Razi, Al Tafsir al Kabir, Juz. 1, uk. 148; Subhani, Manshure Javid, Juz. 2, uk. 116.
  17. Angalia: Fakhru al Razi, Al Tafsir al Kabir, Juz. 1, uk. 148; Subhani, Manshure Javid, Juz. 2, uk. 116.
  18. Angalia: Sheikh Saduq, Al Tawhid, uk. 195-196; Sheikh Tusi, Al Tabyan fi Tafsir al Qur'an, Juz. 1, uk. 27; Tabataba'i, Al Mizan fi Tafsir al Qur'an, Juz. 1, uk. 18; Subhani, Manshure Javid, Juz. 2, uk. 118.
  19. Sheikh Tusi, Al Tabyan fi Tafsir al Qur'an, Juz. 1, uk. 27; Tabrisi, Majma' al Bayan, Juz. 1, uk. 91.
  20. Subhani, Manshure Javid, Juz. 2, uk. 117.
  21. Fakhru al Razi, Al Tafsir al Kabir, Juz. 1, uk. 143.
  22. Angalia: Abu al Futuh al Razi, Raudhu al Janan, Juz. 1, uk. 55-57.
  23. Angalia: Sheikh Saduq, Al Tawhid, uk. 195; Sheikh Tusi, Al Tabyan fi Tafsir al Qur'an, Juz. 1, uk. 27; Tabrisi, Majma'a al Bayan, Juz. 1, uk. 91; Abu al Futuh al Razi, Raudhu al Janan, Juz. 1, uk. 57; Tabataba'i, Al Mizan fi Tafsir al Qur'an, Juz. 1, uk. 18.
  24. Subhani, Manshure Javid, Juz. 2, uk. 117.
  25. Angalia: Kulayni, Al Kafi, Juz. 1, uk. 87; Sheikh Saduq, Al Tawhid, uk. 221.
  26. Tabrisi, Majma' al Bayan, Juz. 1, uk. 91; Tabataba'i, Al Mizan fi Tafsir al Qur'an, Juz. 1, uk. 18.
  27. Tabrisi, Majma' al Bayan, Juz. 1, uk. 91; Subhani, Manshure Javid, Juz. 2, uk. 118.
  28. Abu al Futuh al Razi, Raudhu al Janan, Juz. 1, uk. 55-56.
  29. Tabrisi, Majma' al Bayan, Juz. 1, uk. 91; Subhani, Manshure Javid, Juz. 2, uk. 118.
  30. Tabrisi, Majma'a al Bayan, Juz. 1, uk. 91; Abu al Futuh al Razi, Raudhu al Janan, Juz. 1, uk. 56; Subhani, Manshure Javid, Juz. 2, uk. 118.
  31. Yazdanpanah, Mabani wa Usule Irfane Nazari, uk. 455-460; Amininejad na wengineo, Mabani wa Falsafeye Irfane Nazari, uk. 237-240.
  32. «طرح پرچم ایران؛ بازتاب گفتمان انقلابی و اسلامی», Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu (IRNA).
  33. «لفظ مقدس الله در مرکز آرم حکومتی جمهوری آذربایجان», Shirika la Habari la Aran.
  34. «پرچم عراق و سیر تحول آن», Iraqyar.
  35. Angalia: Sarafrazi, «Sha'air-e Shi'i bar Sekke-haye Islami ta Sheklgiri-ye Hokumat-e Safaviyan», uk. 9-11, 19, 22 na 23.

Vyanzo

  • Abu al Futuh al Razi, Hussein bin Ali. Raudhu al Janan wa Rauhu al Janan fi Tafsir al Qur'an. Uhakiki: Muhammad Mehdi Naseh na Muhammad Ja'far Yahaghi. Mashhad: Astan-e Quds-e Radhavi, 1408 H.
  • Amininejad, Ali na wengineo. Mabani wa Falsafeye Irfane Nazari. Qom: Taasisi ya Elimu na Utafiti ya Imam Khomeini, Chapisho la kwanza, 2011 M.
  • Ashtiyani, Jalal al Din. Tafsire Sureye Fatihat al Kitab. Qom: Ofisi ya Propaganda ya Kiislamu, 1998 M.
  • «لفظ مقدس الله در مرکز آرم حکومتی جمهوری آذربایجان» (Neno Takatifu la Allah Katikati ya Nembo ya Kiserikali ya Jamhuri ya Azerbaijan), Shirika la Habari la Aran. Tarehe ya kutembelewa: 29 Julai 2026 M.
  • «پرچم عراق و سیر تحول آن» (Bendera ya Iraq na Historia ya Mabadiliko Yake), Tovuti ya Iraqyar. Tarehe ya kuwekwa: 14 Novemba 2020 M., Tarehe ya kutembelewa: 29 Julai 2026 M.
  • Fakhr al Razi, Muhammad bin Umar. Al Tafsir al Kabir. Beirut: Dar Ihya al Turath al Arabi, Chapisho la tatu, 1420 H.
  • Jawadi Amoli, Abdullah. Tasnime. Qom: Kituo cha Uchapishaji cha Isra, Chapa ya tatu, 2002 M.
  • Jawadi Amoli, Abdullah. Tawhid dar Qur'an. Uhakiki: Haydar Ali Ayyubi. Qom: Kituo cha Kimataifa cha Uchapishaji cha Isra, 2016 M.
  • Kashifi, Mullah Hussein. Jawahir al Tafsir. Tehran: Kituo cha Utafiti cha Miras-e Maktub, 2000 M.
  • Kaf'ami, Ibrahim bin Ali. Al Maqam al Asna fi Tafsir al Asma al Husna. Uhakiki: Fars al Hassuun. Qom: Taasisi ya Qaim Al-e Muhammad, 1412 H.
  • Khomeini, Sayyid Ruhullah. Misbah al Hidayah ila al Khilafah wa al Wilayah. Tehran: Taasisi ya Uhifadhi na Uchapishaji wa Athari za Imam Khomeini, 2013 M.
  • Kulaini, Muhammad bin Ya'qub. Al Kafi. Tehran: Dar al Kutub al Islamiyyah, 1407 H.
  • Misbah Yazdi, Muhammad Taqi. Khodashinasi. Qom: Uchapishaji wa Taasisi ya Elimu na Utafiti ya Imam Khomeini, 2017 M.
  • Najafi, Muhammad Hassan. Jawahir al Kalam fi Sharh Shara'i' al Islam. Beirut: Dar Ihya al Turath al Arabi, Chapisho la saba, 1983 M.
  • Paketchi, Ahmad. «الله» (Allah). Ndani ya Dairat al Ma'arif al Bozorg al Islami, Juzuu. 10. Tehran: Kituo cha Ensaiklopidia Kuu ya Kiislamu, Chapisho la kwanza, 2001 M.
  • Ruhani, Mahmoud. Al Mu'jam al Ihsai li Alfaz al Qur'an al Karim. Mashhad: Astan-e Quds-e Radhavi, 1993 M. / 1414 H.
  • Sarafrazi, Abbas. «شعائر شیعی بر سکه‌های اسلامی تا شکل‌گیری حکومت صفویان» (Alama za Kishia kwenye Sarafu za Kiislamu hadi Kuanzishwa kwa Serikali ya Safavid). Ndani ya Shia Shenasi, Toleo la 51 (2015 M.).
  • Safi Gulpaygani, Lutfullah. Al Ilahiyyat fi Nahj al Balaghah. Qom: Bostan-e Kitab, 2007 M.
  • Sheikh Saduq, Muhammad bin Ali bin Babawayh. Al Tawhid. Qom: Jame'eh-ye Modarresin-e Howzeh-ye Ilmiyyeh-ye Qom, Chapisho la kwanza, 1398 H.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan. Al Tabyan fi Tafsir al Qur'an. Beirut: Dar Ihya al Turath al Arabi, Bila tarehe.
  • Subhani, Ja'far. Manshure Javid. Qom: Taasisi ya Imam Sadiq (a.s), 2011 M.
  • «طرح پرچم ایران؛ بازتاب گفتمان انقلابی و اسلامی» (Muundo wa Bendera ya Iran; Akisi ya Mazungumzo ya Mapinduzi na Kiislamu), Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu (IRNA). Tarehe ya kuwekwa: 15 Julai 2020 M., Tarehe ya kutembelewa: 29 Julai 2026 M.
  • Tabataba'i, Sayyid Muhammad Hussein. Al Mizan fi Tafsir al Qur'an. Beirut: Muassasat al A'lami li al Matbu'at, 1390 H.
  • Tabrisi, Fadhl bin al Hassan. Majma' al Bayan fi Tafsir al Qur'an. Tehran: Naser Khosrow, Chapisho la tatu, 1993 M.
  • Yazdanpanah, Sayyid Yadollah. Mabani wa Usule Irfane Nazari. Ngando ya Sayyid Ata Anzali. Qom: Taasisi ya Elimu na Utafiti ya Imam Khomeini, Chapisho la pili, 2010 M.
  • Yazdi, Muhammad Kazim. Al Urwat al Wuthqa ma'a al Ta'liqat. Qom: Madrasah Ali bin Abi Talib, 1428 H.