Malik bin Nuwaira

Kutoka wikishia

Malik bin Nuwaira (Aliyeuawa mwaka wa 11 Hijria):  alikuwa mmoja wa masahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliye uliwa kinyume na  sheria kupitia upanga wa Khalid bin Walid. Kifo cha Malik katika vita vya Riddah, kimekuwa ni miongoni mwa masuala yenye mvutano mkubwa wa kidini kati ya Waislamu wa Kishia na Kisunni. Waislamu wa Kishia hulitumia tukio hili katika kupinga nadharia ya uadilifu wa masahaba wote. Omar bin Khattab aliamini kwamba Khalid bin Walid alistahili kuadhibiwa kwa jinai ya kumuua Malik na kwa kosa la kulala na mke wake. Lilikuwa ni jambo la wazi mbele ya Omar kwamba; kulingana na sheria za Kiislamu, Khalid alistahili kupigwa mawe. Hata hivyo, Abu Bakar alimtetea Khalid kwa kusema kwamba; maamuzi ya Khalid ylitegemea fikra ya ijitihadi, na kwamba yeye alijitahi ambayo ni haki yake ya kisheria, na hivyo hakustahili kuadhibiwa.

Moja ya Hadithi zilizopokewa na Fadhil bin Shadhan, inasema kwamba; Mtume Muhammad (s.a.w.w), alimbashiria Pepo Malik bin Nuwaira, akisema kuwa, Nuwaira ni miongoni mwa watu wa Peponi, kisha pia alimuusia kushikamana na uongozi wa Imamu Ali (a.s), na kumtambua kama ni khalifa wake. Jambo ambalo linaonekana katika nyenendo za Malik bin Nuwaira, kwani alipokwena Madina baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), alionekena kumkosoa Abu Bakar kwa kutomkabidhi Imam Ali (a.s) uongozi, kama ilivyoagizwa na bwana Mtume (s.a.w.w). Kulingana na watafiti wa Kishia, Malik alikataa kuikabidhi zaka yake kwa serikali ya Abu Bakar, hii ni kwa sababu yeye hakuitambua kuwa ni serikali halali, jambo ambalo lilipelekea kifo chake. Baadhi ya waandishi wa Kisunni, ili kuhalalisha matendo ya Khalid bin Walid, wameamua kumtambulish Malik kama ni mtu aliye ritadi (aliye toka katika Uislamu). Hata hivyo, Waislamu wa Kishia na baadhi ya Masunni wameyakana madai haya dhidi ya Malik. Wamekuwa na msimamo huo wakisimamia hoja ya moni ya masahaba, kwa kuma maoni kadhaa masahaba yanayothibitisha Uislamu wake, na kwamba Abu Bakar alitoa fedha kufidia kifo chake.


Utambulisho na Hadhi ya Malik bin Nuwaira

Malik bin Nuwaira bin Jamra at-Tamimi ni mmoja wa masahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) naye alikuwa ni miongoni mwa wakuu (Arbabu) na viongozi wa zama za Ujahiliya na hata baada ya kudhihiri kwa Uislamu. [1] Malik alikuwa ni mshairi maarufu na aliye kuwa na diwani yake maalumu ya mashairi. [2] Malik yeye mwenyewe aliamua kwenda kwa bwana Mtume (s.a.w.w) na kusilimu. [3] Baadae bwana Mtume (s.a.w.w) alimteua kuwa ni mwakilishi wake amaye kazi yake ilikuwa ni kukusanya kutoka katika kabila lake na kuzifikisha kwa bana Mtume (s.a.w.w). [4]

Kwa mujibu wa Sheikh Abbas Qummi, ambaye ni miongoni mwa wahadithi mashuhuri wa Kishia wa karne ya kumi na nne Hijria, ni kwamba; Malik bin Nuwaira aliuawa kwa kutokana na mapenzi yake ya kina kwa Ahlul-Bait (a.s). [5] Kuna moja ya Riwaya zilizo simuliwa na Fadhil bin Shadhan, isemayo kwamba; Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimtambulisha Malik bin Nuwaira kuwa ni miongoni mwa watu wa Peponi. [6] Tukio hili lilitokea pale Malik alipo muomba bwana Mtume (s.a.w.w) amfundishe uhakika wa kiini cha imani, bwana Mtume naye (s.a.w.w) akamfundisha baadhi ya hukumu za kisheria na kumwongoza kumfuata Imamu Ali (a.s) kama ni khalifa wake. [7]

Kulingana na nukuu za Ibn Shadhan; baada ya kufariki wa bwana Mtume (s.a.w.w), Malik bin Nuwaira alikwenda Madina na alipogundua kuwa Abu Bakar ndiye aliye shikilia nafasi ya khalifa, alikabiliana naye kwa kumkosoa kwa kutomkabidhi Imamu Ali (a.s) uongozi kama alivyoagiza na Mtume (s.a.w.w). [8] Kufuatia malalamiko na ukosoaji wake huo, kwa amri ya Abu Bakar, (Qunfudh) na Khalid bin Walid, Malik alitolewa msikitini kwa nguvu. [9]

Kifo cha Malik bin Nuwaira ni mojawapo ya masuala yenye changamoto kubwa katika mijadala ya kidini kati ya Shia na Sunni. [10] Kuuliwa kwa Malik kupitia Khalid bin Walid, pamoja na kitendo cha Khalid kufanya mahusiano na mke wa Malik baada ya kifo chake, ni miongoni mwa matukio ya kashfa zaidi yanayohusiana na Vita vya Ridda. [11] Watafiti wa Kishia, wakitumia tukio hili la kihistoria, wanakosoa nadharia ya Sunni inayosema kuwa masahaba wote walikuwa ni watu waadilifu, na wanadai kwamba; nadharia hii ilianzishwa ili kutetea baadhi ya tabia na nyenendo ovyo za baadhi ya masahaba. [12] Kwa mujibu wa maelezo ya Maqdasi, mwanahistoria wa karne ya nne Hijria, ni kwamba; baada ya mvurugiko na mgawanyiko uliotokana na suala la Ukhalifa, mgawanyiko wa pili wa Waislamu ulijitokeza katika Vita vya Ridda; ingawa Abu Bakar aliamini kuwa ilipaswa Waislamu kupigana na watu wa Ridda, ila Waislamu wengine walipingana msimamo huo uliosimamiwa na Abu Bakar. [13]


Mauaji ya Malik katika Vita vya Ridda

Kifo cha Malik bin Nuwaira ni tukio lenye utata mkubwa katika historia ya Uislamu, hasa mbele ya wanahistoria wa Kishia. Wanahistoria hawa wanasisitiza na kushikilia msimamo wa kwamba; Malik bin Nuwaira aliuawa kwa sababu mwenendo mbovu wa kimaadili wa Khalid bin Walid. [14] Malik alikataa kutoa na kukabidhi Zaka yake serikalini mwa Abu Bakar na badala yake alikuwa akiigawa miongoni mwa watu wa kabila lake. [15] Inasemekana kuwa sababu ya kukataa kwake ilikuwa ni mashaka juu ya uhalali wa ukhalifa wa Abu Bakar na wasi wasi wa usahihi wa kuiweka zaka yake mikononi mwa serikali hiyo. [16]

Khalid bin Walid, kwa amri ya Abu Bakar, aliagizwa kukabiliana na uasi wa Malik na kabila lake. [17] Malik, alihudhurishwa mbele ya Khalid yeye pamoja na mkewe (Umm Tamim) ili kuthibitisha kwamba yeye si mritadi. Hata hivyo, Khalid alipomuona mke wa Malik ambaye alikuwa ni mzuri mwenye kupendeza, alichukua maamuzi ya kumuua Malik, kisha usiku huo huo alilala na mke wa huyo ambaye alikuwa bado yupo katika kipindi cha eda baada ya kuliwa kwa mumewe. [18] Kifo cha Malik kiliripotiwa kutokea mnamo mwaka wa 11 Hijria. [19]

Matendo haya kinyume na sheria za Kiislamu yaliyofanywa na Khalid yaliibua upinzani mkubwa kutoka miongoni mwa baadhi ya Masahaba kama vile Abu Qutada al-Ansari na Abdullah bin Omar. [20] Omar bin Khattab alimuomba Abu Bakar amvue Khalid madaraka ya uongozi alionao kutokana na makosa hayo. [21] Omar alisisitiza kuwa Khalid alistahili kisasi kwa kosa la kumuua Malik na pia anastahili kupigwa mawe kwa tendo la kulala na mke Malik kinyume na sheria. [22] Hata hivyo, Abu Bakar alimwondolea Khalid lawama na kumtetea, akisema kuwa alikuwa na sababu za kujitetea juu ya makosa yake, kwani matendo yake hayo aliyatenda kupitia msingi wa ijitihadi. [23] Kulingana na mwanahistoria wa Kimasri, Muhammad Hussein Haikal, ni kwamba; Maamuzi ya Abu Bakar yalitokana na mahitaji yake ya huduma za Khalid katika utawala wake, hivyo aliendelea kumtetea na kumtumia. [24] Lakini Omar hakusahau makosa yake, na baada ya kuwa Khalifa wa kwanza (Abu Bakar), Omara alichukua maamuzi ya alimvua Khalid uongozi wa jeshi. [25]


Jee Malik Mritadi au Musilamu

Waislamu wa Shia na baadhi ya Waislamu wa Sunni wameleta hoja mbalimbali zinazothibitisha Uislamu wa Malik bin Nuwayrah. Baadhi ya hoja hizo ni:

1.       Malik na wafuasi wake walikiri Uislamu wao na walikuwa wakisali kama Wailamu wengine.

2.       Masahaba kadhaa walitoa ushahidi wakithibithisa Uislamu wao.

3.       Abu Bakar alilipa fidia kwa familia ya Malik baada tukio la kuuawa kwake.

4.       Abu Bakar alitoa amri ya kumtaka Khalid bin Walid kuachana na mke wa Malik. [26]

Tukikiachana na yote hayo, bado miongoni mwa Waislamu wa madhehebu ya Kisunni kuna mitazamo tofauti kuhusaiana na Uislamu wa Malik. Baadhi yao wanamuarifisha Malik kama ni mtu aliye kengeuka na kutoka nje ya Uislamu (mritadi). [27] Mwanahistoria maarufu wa Kiislamu, Muhammad Hussein Haikal, alijaribu kutetea vitendo vya Khalid bin Walid kwa kusema kwamba; ingawa kulala na mwanamke aliyekuwa katika eda, ni kinyume na sheria za Kiislamu, ila sheria hiyo haipaswi kutumika dhidi ya watu wenye vipaji maalum kama Khalid, ambaye alikuwa na msaada mkubwa kwa utawala wa Abu Bakar. [28] Haikal pia alieleza kwamba, kwa kuzingatia huduma nyingi alizozitoa Khalid katika kuusaidia utawala wa Kiislamu, utagundua kwamba; mauaji ya Malik na kitendo chake cha kulala na mke wa Malik ni jambo dogo mno ikilinganishwa na huduma alizozitoa. [29]

Allama Amini [30] na Sharfuddin, [31] wanazuoni maarufu wa Kishia, baada ya kunukuu tukio la mauaji ya Malik bin Nuwaira, walikosoa vya kutosha utetezi wa Waislamu wa Kisunni wenye nia ya kufinika fedheha na aibu zaKhalid bin Walid kuhusiana na mauaji hayo. Abbas Mahmoud Al-Aqqad, mwandishi wa Kimisri, alikiri ya kwamba; ingawa kuna tofauti za riwaya kuhusiana  mauaji ya Malik, ila ukweni ni kwamba mauaji hayo hayakuwa na msingi wala ulazima wowote ule wa kutendeka kwake, na ni jambo la kusikitisha kwamba tukio hilo lilitokea ndani ya nyenendo za maisha ya Khalid. [32]