Kuzaa watoto

Kutoka wikishia

Kuzaa watoto ni jambo ambalo limezingatiwa na Qur’an na hadithi za Maasumina kuwa, zuri na la kupendeza. Dua ya Nabii Ibrahim (a.s) na Zakaria (a.s) ya kutaka kuruzukiwa mtoto katika umri wa uzee wao na habari njema ya Mwenyezi Mungu ya kujibiwa maombi yao inachukuliwa kuwa ni dalili ya umuhimu wa suala hili. Pia, katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), imetajwa kwamba atajifakharisha kwa wingi wa Ummah wake Siku ya Kiyama.

Matokeo yasiyoweza kufidika yameorodheshwa kuhusiana na kupunguza kuzaa, ambayo ni pamoja na kupunguza ukuaji wa uchumi na nguvu kazi na matatizo ya kiutamaduni na kisiasa. Wasiwasi na mahangakaiko ya kiuchumi na kielimu sambamba na mabadiliko ya mtindo wa maisha ya watu pia yamezingatiwa kuwa moja ya vikwazo muhimu vya kuchukua hatua ya kuzaa. Wapinzani wa hili wanasema kwamba katika utamaduni wa kidini, riziki ya watoto imehakikishwa na kudhaminiwa na Mwenyezi Mungu. Pia wanaamini kwamba, ikiwa idadi ya watoto ni tatizo katika nyanja hii, familia zenye mtoto mmoja zilipaswa kulea watoto bora zaidi. Lakini hali haiko hivyo.

Kufuatia ongezeko la idadi ya watu wa Iran katika miaka ya 60 Hijria Shamsia, maafisa wa nchi hiyo waligeukia sera za udhibiti wa idadi ya watu; lakini Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Iran mwaka 1391 Hijria Shamsia, aliona kuwa, kuendelea kwa sera hii kuanzia katikati ya muongo wa 70 na kuendelea ni kosa na hivyo akasisitiza ulazima wa watu kuzaa watoto. Mnamo tarehe 24 Mehr 1400 Hijria Shamsia, Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran) nalo pia liliidhinisha sheria ya kusaidia familia na na kufanya idadi ya watu kuwa kijana.

Nafasi

Katika Qur’ani Tukufu mtoto ametajwa kwa sifa na ibara mbalimbali kama neema [1], pambo la maisha, [2] nuru ya jicho [3] na sababu ya msaada wa Mwenyezi Mungu. Sifa hizi kuhusiana na mtoto ni ithbati tosha juu ya kuwa zuri na jambo la kupendeza suala la kuzaa na kuwa na watoto kwa mtazamo wa Qur’ani. [5] Kadhalika dua ya Nabii Ibrahim (a.s) na [6] Nabii Zakaria (a.s) [7] za kumuomba Mwenyezi Mungu awaruzuku watoto tena katika umri na kipindi cha uzee na bishara ya Mwenyezi Mungu kwao ya kujibu dua zao [8] ni nukta nyingine inayoonyesha umuhimu wa maudhui ya kuzaa na kuwa na watoto kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu. [9]

Katika hadithi pia, kuna riwaya nyingi zilizopokewa kutoka kwa Maasumina (a.s) ambazo zinabainisha kuwa zuri na linalofaa suala la kuzaa watoto na kuongeza idadi ya familia. [10] Katika kitabu cha al-Kafi moja ya vitabu vya hadithi vyenye itibari kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia kuna hadithi mbalimbali zilizonukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) ambazo zinasisitiza juu ya suala la ndoa na kuzaa na amebainisha kwamba, Oaneni mzaane ili mpate kuwa wengi, kwani mimi nitajifaharisha kwa watu wa umma zingine Siku ya Kiyama. [11] Katika hadithi nyingine ambayo sanadi na mapokezi yake yamekubaliwa, [12] Mtume ameagizia na kusisitiza wazi juu ya kuzaa watoto wengi. [13]

Matokeo ya kupunguza uzazi

Katika baadhi ya tafiti, "kuzeeka kwa idadi ya watu" ndio matokeo makuu na mabaya ya kupungua kwa uzazi, na inasemekana kuwa tukio hili litakuwa na matokeo yasiyoweza kufidika ambapo miongoni mwayo ni: . Matatizo ya kiuchumi: Kupungua kwa uzalishaji na ukuaji wa uchumi, gharama kubwa za bima, utekelezaji wa mipango ya msaada kwa wastaafu, ambayo yatasababisha nchi kukumbwa na mgogoro wa kiuchumi. . Tatizo la nguvukazi: Kwa kupungua kwa nguvukazi, ili kuzuia kufungwa kwa viwanda na hata kwa nafasi na vyeo muhimu, itakuwa lazima wageni lazima watumike. . Hatari za kisiasa na kiusalama: Mabadiliko katika muundo wa idadi ya watu wa jamii kutapelekea kupungua kwa vijana wa kutetea usalama na mamlaka ya nchi. [14]

Matatizo na wasiwasi wa kuzaa

Matatizo na vikwazo vingi vimeorodheshwa na kutajwa kuwa ndivyo vinavyosababisha watu wajizuie kuzaa. [15] Baadhi ya matatizo haya ni:

Matatizo ya kiuchumi

Hofu ya kushindwa kudhamini mahitaji ya kifedha kwa watoto na gharama zao, umekuwa moja ya wasiwasi wa mara kwa mara wa wazazi kuhusu kupata watoto. [16] Kwa maana kwamba, watu wana wasiwasi kwamba, wakizaa watashindwa kuwalisha, kuwavisha na kuwasomesha watoto kutokana na hali ya ugumu wa maisha waliyonayo. Hii ni katika hali ambayo, katika utamaduni wa Kiislamu, riziki ya watoto imehakikishwa na kudhaminiwa na Mwenyezi Mungu. [17] Katika Qur’an, Mwenyezi Mungu anawahutubu watu katika zama za ujahilia ambao walikuwa wakiwauwa watoto wao kwa hofu ya umasikini na kutokuwa nacho na kitendo kinahesabiwa kuwa ni dhambi kubwa. Mwenyezi Mungu anasema: Wala msiwauwe wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni hatia kubwa. [18] Kadhalika imetajwa katika kitabu cha Kafi kwamba, mmoja wa masahaba wa Imam Kadhim (a.s.) aliuliza mtazamo wa Imamu katika barua aliyomuandikia kuhusu kujizuia kupata watoto kutokana na ugumu wa malezi na ukosefu wa fedha. Imam akajibu: “Tafuteni mtoto (zaeni); kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye anayewaruzuku. [19]

Wasiwasi wa malezi

Wengine wanaona kuwa idadi ya watoto kuwa wengi ni kikwazo cha kuwapa malezi sahihi na kwa sababu hiyo hawataki kuzaa watoto wengi. [20] Katika kujibu hili, imeelezwa kuwa: Mosi: Kwa kuzingatia baadhi ya Aya za Qur’ani, [21] suala la malezi na kuwaongoza watu liko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Pili: Ikiwa ni kweli suala la malezi ni mojawapo ya shida kuu katika suala hili, basi familia za mtoto mmoja zilipaswa kulea watoto bora. Tatu: Ikiwa mhimili wa malezi ya watoto utakuwa ni huba na Wilaya (uongozi) wa Ahlu al-Bayt (as), basi wasiwasi mwingi katika suala la malezi utatoweka. [22]

Mabadiliko ya mtindo wa maisha

Miongoni mwa vikwazo katika njia ya kupata watoto, inatajwa kuwa ni mabadiliko katika mtindo wa maisha na hivyo kupigania ustawi na ubinafsi wa baadhi ya familia; [23] yaani, ubinafsi wa baadhi ya wazazi na kutokuwa na moyo wa kujitolea umewafanya wapuuze upweke wa mtoto wao na kuzingatia masuala yao ya ustawi; kwa sababu wanaona kwamba, kuzaa na kuwa na mtoto mwingine ni sababu ya kukosekana utulivu katika starehe zao; [24] hii ni katika hali ambayo katika mtindo wa maisha ya Kiislamu, ustawi na starehe hazitambuliwi kuwa ndio lengo kuu la maisha, na kila moja ya ustawi na taabu huchukuliwa kuwa ni ya kutamanika na ya kufaa ikiwa matokeo yake yatakuwa ni kwa ajili ya kumtumikia Mwenyezi Mungu. [25]

Sera za uzazi nchini Iran Kuanzia mwaka 1355 hadi 1357 Hijria Shamsia idadi ya watu nchini Iran iliongezeka maradufu. [26] Kwa kuibuka kwa matatizo katika sekta ya elimu, afya na makazi na kwa kutabiri kwamba miaka ya 80 itakuwa muongo wa ndoa na uzazi kwa vijana, viongozi wa Iran waligeukia kwa dhati sera za kudhibiti idadi ya watu. [27]. Lakini mwaka 1391; Ayatullah Khamenei, aliona kuwa, kuendelea kwa sera hii kuanzia katika katikati ya muongo wa 70 na kuendelea ni kosa na hivyo akasisitiza ulazima wa watu kuzaa watoto. [28] Mnamo tarehe 24 Mehr 1400 Hijria Shamsia, Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran) nayo pia iliidhinisha sheria ya kusaidia familia na na kufanya idadi ya watu kuwa kijana. [29] Katika sheria hii, kumezingatiwa mambo kama utoaji mikopo na ardhi bure kwa watu wanaozaa watoto. [30]

Monografia

. Risalat Nikahiyah, Kahesh Jami’yat dharbei sahamgin bar Paykar Muslimin, mwandishi: Sayyid Muhammad Hussein Tehrani. [31]