Kusema Uwongo
Uwongo (Kiarabu: الكذب) ni kusema maneno yaendayo kinyume na uhalisia wa jambo lilivyo, tendo ambalo halikubaliki wala kupendeza mbele ya jamii, pia tendo kidini, huhisabiwa kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa. Qur'an na Hadithi, na inachukuliwa kama ufunguo wa maovu yote na muharibifu wa imani. Khulka hii ya kusema uwongo, imekemewa vikali ndani ya Qur’ani na Hadithi na kuhisabiwa kuwa ndio funguo ya maovu. Qur’ani na Hadithi zimelichukulia tendo hili kuwa; ni adui atokomezaye imani. Kusema uwongo ni haramu, ila imeruhusiwa kufanya hivyo katika baadhi ya nyakati maalumu wa kama vile; kusuluhisha mizozo ilioko baina ya watu, na kulinda na kuhami roho au mali, iwe ni yako au ya mtu mwengine.
Kuna matokeo na madhara kadhaa yaliolezwa katika Hadithi, yanayo sababishwa na usemaji uwongo ambayo huwasibu watu ulimwenguni humu hadi siku ya Kiama (Akhera), ikiwa ni pamoja na kupoteza uaminifu na heshima mbele ya watu, umaskini, adhabu ya Mungu, kupoteza imani, na kulaaniwa na malaika.
Choyo, ubakhili, imani dhaifu, ni miongoni mwa sababu zilizotajwa kama ndio chanzo na motisha unaopelekea kusema uwongo. Kuelewa athari na matokeo ya kusema uwongo, pamoja na kuzingatia Aya na Hadithi zinazokemea hilo, ni miongoni mwa tiba na suluhisho la kukabiliana na usemaji uwongo.
Ufafanuzi wa dhana
Uwongo ni tendo liendalo kinyume na maadili na maana yake ni kusema kitu kinyume na ukweli ulivyo [1] au kunukuu maneno na kuyanasibisha kwa mtu ambaye hakuyasema maneno hayo. [2] Uwongo ni kinyume cha ukweli na uaminifu, na mtu asemaye uwongo huitwa mwongo. [3]
Nafasi ya uwongo
Uwongo ni mojawapo ya maovu yalio katika orodha ya makossa makuu ya kimaadili [4] na ni mojawapo ya dhambi mbaya zaidi, [5] ambapo katika baadhi ya Hadithi, imetambuliwa kuwa ndio ufunguo wa dhambi zote. [6] Kulingana na maoni ya Mulla Ahmad Naraghi ni kwamba; kuna marejeo mengi katika Aya na Hadithi yanazokemea uwongo na udanganyifu. [7] Pia katika vitabu vya Hadithi [8] na maadili, kuna milango pekee inayojadili masuala ya uwongo. Kwa mfano, katika kitabu cha Al-Kafi, sura izungumziayo uwongo ina Hadithi 22 zinazokemea usemaji uwongo. [9] Katika Hadithi mashuhuri ya Imamu Swadiq (a.s) inayo zungumzia “Jeshi Liungalo Mkono Akili na Jeshi Liungalo Mkono Ujinga”, Imamu (a.s) ameusishwa na usema kweli na jeshi akili na akauhusisha usemaji uwongo jeshi la ujinga [10]. Katika Quran, mwongo ameksbiliwa na laana na ghadhabu za Mwenye Ezi Mungu. [11] Uwongo pia ni miongoni mwa maudhi muhimi zijadiliwazo katika vitabu vya maadili, na kutafitiwa kama ni mojawapo ya maovu ya kimaadili ndani ya jamii. [12]
Pia uwongo umeelezwa na kutafitiwa katika sura za saumu, hija, biashara, na kiapo [13] katika vitabu vya sharia (fiqhi). Kwa mfano, kusema uwongo ni haramu katika ibada za Hija, hukumu hii imezungumziwa katika masuala misingi ya ibada ya Hija. [14] Pia, kumsingizia Mwenye Ezi Mungu na Mtume (s.a.w.w) ni mojawapo ya mambo yanayobatilisha saumu. Hukumu hii nayo imejadiliwa katika misingi ya hukumu za saumu na mashatri yake. [15]
Je, uwongo ni miongoni mwa dhambi kuu?
Katika baadhi ya Hadithi, uwongo umeelezwa na kuzingatiwa kama ni mojawapo ya dhambi kuu. [16] Hiyo ndio sababu iliyo mfanya Shahid Thani kuingiza uwongo katika orodha ya dhambi kuu zisababishazo kumtoa mtu katika sifa uadilifu. [17] Hata hivyo, Sheikh Ansari, akitegemea Hadithi nyingine [18], ametaraji kuwepo uwezekano ya kwamba; Kusema uwongo kunaweza kuhisabiwa kuwa ni miongoni mwa dhambi kuu iwapo tu uwongo huo utasababisha maafa. [19]
Pia, katika baadhi ya Hadithi, suala la kumsingizia uwongo Mwenye Ezi Mungu na Mtume (s.a.w.w) limezingatiwa kuwa ni mojawapo ya dhambi kuu. [20] Baadhi ya wanazuoni kwa kuzingatia Hadithi hizo, wamesema kwamba dhambi kubwa ya uwongo inahusiana moja kwa moja na suala la kumsingizia uwongo Mungu na Mtume wake, au kwamba Hadithi hizi zinaonyesha uzito wa dhambi hiyo katika katika suala hili. [21]
Sababu na motisha unaopelekea kusema uwongo
Kuna motisha na sababu tofauti zilizotajwa katika kusema uwongo; kulingana na moja ya Hadithi, chanzo cha uwongo kinachukuliwa kuwa ni udhaifu na udhalili wa nafsi. [22]. Pia, sababu kama vile; udhaifu wa imani, vishawishi vya shetani, ubakhili na choyo ni miongoni mwa sababu zingine za mtu kusema uwongo, huku suala la utashi wa kufikia mali na cheo vikiwa ni mojawapo ya motisha wa kusema uwongo. [23]
Matokeo na athari za kusema uwongo
Baadhi ya matokeo ya kusema uwongo ni pamoja na:
- Kupoteza uaminifu: Imamu Ali (a.s) amenukuliwa akisisitiza kuepuka urafiki na mtu mwenye kusema uwongo, kwa sababu yeye huendelea kusena Uwongo kufikia kwamba hata ukweli wake pia huwa hakuna anaye uamini. [24]
- Kupoteza imani: Kulingana na Hadithi kutoka kwa Imamu Baqir (a.s) ni kwamba; kusema uwongo huvunja nyumba ya imani. [25]
- Adhabu ya Mungu: Imenukuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), ya kwamba; ni vyema kuepuka kusema uwongo, kwani uwongo ni uovu na dhulma, na mwongo na mtenda dhulma makazi yao ni motoni. [26]
- Kulaaniwa na Malaika: Kulingana na Hadithi kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) ni kwamba; Pale muumini asemapo uwongo bila ya dharura maalumu, humlaaniwa na malaika sabini elfu, na harufu mbaya hutoka moyoni mwake hadi kuifikia arshi (ya Mwenye Ezi Mungu), na Mwenyezi Mungu humwandikia dhambi za uzinifu sabini, ambapo dogo la dhambi hizo ni uzinifu wa mtu kuzini na mama yake. [27]
Aidha matokeo mengine ya kusema uwongo yalioelezwa katika Hadithi ni; fedheha, [28] umaskini, [29] na kupoteza kumbukumbu. [30] Kulingana na kauli ya Mulla Ahmad Naraghi katika kitabu chake Ma'araju al-Sa'adah, ni kwamba; kusema uwongo humdhalilisha na humshusha mtu na ni sababu zinazopelekea mtu kufedheheka na kuchukiza duniani na Akhera. [31]
Njia na mbinu za kutibu usemaji uwongo
Mulla Ahmad Naraghi anaamini kuwa ili kurekebisha tabia ya kusema uwongo, hatua kadhaa lazima zichukuliwe ili mtu aweze kuwa mwaminifu. Hatua hizo ni pamoja na:
- Kuzingatia Aya na Hadithi zinazokemea kusema uwongo.
Kuzingatia matokeo ya kidunia na ya akhera ya kusema uwongo, kama vile adhabu katika maisha ya baadaye na kupoteza heshima na uaminifu katika ulimwengu huu.
- Kufikiria kwa makini athari na faida za kusema kweli.
- Kufikiria kabla ya kuzungumza.
- Kuepuka kuwa karibu na waongo na watenda dhambi. [32]
Kwa mujibu wa maoni ya Naser Makarim Shirazi, mmoja wa viongozi wa kidini na wafasiri wa Qur'ani, katika kitabu chake Maadili katika Qur'ani (اخلاق در قرآن), ni kwamba; uongo unapaswa kutibiwa kwa kurekebisha mizizi ya kusema uwongo. Kwa mfano, ikiwa sababu ya kusema uwongo ni udhaifu wa imani, basi inapaswa kuimarisha imani, na ikiwa ni ubakhili na husuda, basi inapaswa kutatuliwa tatizo hilo. Pia, ni muhimu kuwaepuka watu wasemao uwongo au mazingira yanayotia motisha wa kusema uwongo. [33]
Uwongo unaojuzu
Kusema uwongo ni haramu. [34] Hata hivyo, katika hali ambayo uwongo huo utakuwa nahudumia na kudhamini faida muhimu, katika hali kama hiyo uwongo huzingatiwa kuwa ni halali au hata ni wajibu. [35] Mahala ambapo uwongo huwa ni halali ni kama ifwatavyo:
- Katika ya dharura: Kusema uwongo katika hali ya dharura (kulazimishwa au kulazimika) ni halali, kama vile kusema uwongo kwa nia ya kuokoa maisha yako, mali, au maisha na mali za matu wengine zilioko hatarini. [36]
- Kurekebisha mahusiano (kusuluhisha): Ni halali kusema uwongo kwa lengo la kurekebisha na kusuluhisha kati ya watu wliogombana . [38]
- Vitani dhidi ya adui: Kulingana na baadhi ya Hadithi, ni halali kusema uwongo vitani ili kupotosha maadui. [39]
Kutoa ahadi za uwongo kwa mke na watoto
Kulingana na baadhi ya Hadithi, ni halali kumpa mke ahadi za uwongo. [40] Kwa hivyo, katika vitabu vya maadili, suala la kumpa mkea na watoto ahadi za uwongo limevuliwa na kuwekwa nje ya huku za haramu. [41] Walakini, wanazuoni wa madhehebu ya Shia hawafikirii kuwa kumdanganya mke ni jambo la halali. [42] Pia imesemwa kwamba; Hadithi hizi hazilingani na Aya zipingazo suala la uvunjaji wa ahadi. [43] Suala hili linapingana na Hadithi zinazokataza kutoa ahadi bila ya kuwa na nia ya kuitekeleza. [44] Baadhi pia wanaamini kwamba; kuzifanyia kazi Hadithi hizo, na kuwaamili watu wa familia yako kulingana na maudhui ya Hadithi kama hizo, kunachangia katika kusababisha malezi mabaya ya maadili na kuwahamasisha watoto kusema uwongo na kuvunja ahadi zao. [45]
Rejea
Madhui zinazo fungamana
Vyanzo
- Anṣārī, Murtaḍā. Al-Makāsib. [n.p]: Turāth al-Shaykh al-Aʿẓam, [n.d].
- Īrwānī, Jawād. "Aṣl-i ṣidāqat dar Qurʾān wa taḥlīl-i mawārid-i jawāz-i kidhb". Āmūza-hā-yi Qurʾānī 13 (1390).
- Khomeinī,, Sayyid Rūḥ Allāh. Taḥrīr al-wasīla. Tehran: Muʾassisah-yi Tanẓīm wa Nashr-i Āthār-i Imām Khomeinī, 1379 Sh.
- Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī & Muḥammad Ākhūndī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
- Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Muʾassisat al-Wafāʾ, 1403 AH.
- Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Akhlāq dar Qurān. Qom: Madrasat al-Imām ʿAlī b. Abī Ṭālib (a), 1377 Sh.
- Muṣṭafawī, Ḥasan. Al-Tahqīq fī kalimāt al-Qur'ān al-karīm. Tehran: Wizārat-i Farhang wa Irshād-i Islāmī, 1368 Sh
- Narāqī, Aḥmad b. Muḥammad Mahdī. Miʿrāj al-saʿādāt. Qom: Muʾassisat Intishārāt-i Hijrat, [n.d].
- Narāqī, Mahdī b. Abī Dhar. Jāmiʿ al-saʿādāt. Edited by Muḥammad Kalāntar. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1967.
- Nūrī, Mīrzā Ḥusayn al-. Mustadrak al-wasāʾil wa musṭanbit al-wasā'il. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1408 AH.
- Qummī, Shaykh ʿAbbās. Safīnat al-biḥār wa madīnat al-ḥikam wa l-āthār. Tehran: Farāhānī, 1363 SH.
- Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Tehran: Nashr-i Ṣadūq, 1367 Sh.
- Shahīd al-Thānī, Zayn al-Dīn b. ʿAlī. Al-Rawḍa al-bahiyya fī sharḥ al-lumʿat al-Dimashqiyya. Edited by Muḥammad Kalāntar. 1398 AH.
- Shaʿrānī, Abu l-Ḥassan. Nathr-i ṭūba. Tehran: Islāmīyya, [n.d].
- Yazdī, Sayyid Muḥammad Kāẓim al-. Al-ʿUrwat al-wuthqā. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1420 AH.