Kuamka kabla ya alfajiri

Kutoka wikishia

Kuamka kabla ya alfajiri (Kiarabu: القيام بالسحر) katika fasihi ya Kiislamu maana yake ni kuwa macho kabla ya adhana ya alfajiri ambapo inaelezwa kuwa, miongoni mwa faida zake ni kusamehewa madhambi na kujibiwa dua. Kwa mujibu wa hadithi mbalimbali, Maasumina (a.s) walikuwa wakiamka na kubakia macho kabla ya adhana ya alfajiri kwa ajili ya kusali Sala ya usiku na kusoma dua Sahar (dua ya daku) katika mwezi wa Ramadhani ni miongoni mwa amali ambazo zimekokotezwa na kuusiwa wakati wa kuwa macho kabla ya adhana ya alfajiri.

Katika baadhi ya nchi ni ada na mazoezi kupiga madufu na ngoma, sambamba na kusoma kaswida za kuamsha watu kula daku katika masiku ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Maana na Utambuzi

Kuamka kutoka usingizini kabla ya adhana ni kuwa macho wakati kuchomoza jua na adhana ya alfajiri [1] na kwa mujibu wa baadhi ya hadithi maana yake ni kabla ya kuchomoza alfajiri ya kweli (adhana ya alfajiri). [2] Neno Sahar katika kamusi mbalimbali limeelezwa kuwa lina maana ya ((mwisho wa usiku)), [4] ((kabla ya kuchomoza alfajiri)), [5] ((muda mchache kabla ya asubuhi)) [6] na kipindi ambacho giza la usiku linapochanganyika na mwanga wa mchana". [7]

Neno Sahar limetumika katika Aya isemayo: ((وَالْمُسْتَغْفِرِینَ بِالْأَسْحَارِ ; na wanao omba maghafira kabla ya alfajiri)). Surat al-Imran- 17. Fakhruddin Turayhi (aliaga dunia 1087), mtambuzi wa lugha wa Kishia amesema ina maana ya, muda mchache kabla ya alfajiri. [8]

Nafasi

Maudhui ya Sahar (kabla ya alfajiri) imejadiliwa katika vitabu vya hadithi katika milango inayohusiana na Saumu [9] na Sheikh Kulayni (aliaga dunia 329 Hijiria) msomi na mtaalamu wa elimu ya hadithi wa Kishia ameleta hadithi kuhusiana na Sahar katika mlango wa "Auqat va Hallat ke dar an omidi ast dua mustjaba shavad" (nyakati na hali ambazo kuna matumaini ya dua kujibiwa). [10] Katika vitabu vya Fiqhi pia Sahar (kabla ya alfajiri) imejadiliwa katika mlango wa Saumu [11] na nyakati za Sala za sunna. [12]

Wataalamu wa elimu ya Irfan wameelezea katika athari zao suala la kuamka kabla ya alfajiri [13] na kumeashiriwa hilo katika mashairi ya Kifarsi kama ya Hafez [14], Malik al-Shu'araa Bahar [15] na mashairi ya wanazuoni na wasomi kama Mahdi Ilahi Qumshei [16].

Kuamka Kabla ya Alfajiri Maasumina (a.s)

Kwa mujibu hadithi mbalimbali, Ahlul-Bayt (a.s) walikuwa wakiamka kabla ya alfajiri na walikuwa wakijishughuilisha na kuomba dua na kunong'ona na Mwenyezi Mungu. [18] Kadhalika kwa mujibu wa hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia, moja ya nyakati ambazo Mitume walikuwa wakizichagua kwa ajili ya dua na kunong'ona na Mwenyezi Mungu ulikuwa ni wakati wa kabla ya alfajiri. [19]

Faida

Katika hadithi kumelezwa faida mbalimbali za kuamka kabla ya alfajiri na baadhi yake ni kusamehewa madhambi [20] na kujibiwa dua. [21] Kwa mujibu wa hadithi wakati watoto wa Nabii Ya'qub walipomtaka baba yao awaombee msahama kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kosa walilokuwa wamefanya katika tukio la Yusuf, Nabii Ya'qub alichelewesha hilo mpaka wakati wa kabla ya kuchomoza jua (kabla ya alfajiri), kwani dua na kuomba msamaha katika wakati huu hutakabaliwa. [22]

Katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) amenukuliwa akieleza kwamba, kuomba maghufira watu kadhaa wakati wa kabla ya alfajiri, huwa kizingiti cha kushushwa adhabu, [23] na kwa mujibu wa hadithi nyingine, riziki hugawanywa wakati wa Sahar (kabla ya kuingia alfajiri). [24]

Amali

Imeusiwa na kutiiliwa mkazo katika hadithi mbalimbali juu ya kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu wakati wa Sahar (kabla ya kuingia alfajiri). [25] Kupiga mswaki [26] na kusali Sala ya usiku, ni miongoni mwa amali na matendo yaliyousiwa na kukokotezwa kufanywa katika wakati huu wa kabla ya kuchomoza alfajiri. [27]

Kwa mujibu wa hadithi, ni mustahabu kusoma Dua Sahar katika mwezi wa Ramadhani [28] na kula daku kwa ajili ya wanaofunga saumu wakati wa kabla ya kuingia alfajiri. [29]

Ada na Mazoea

Ada ya kusoma kaswida za kuamsha watu kula daku katika mwezi wa Ramadhani ilikuweko nchini Iran na hilo hufanyika kabla ya kuingia alfajiri. [30. Inaelezwa kuwa, ada hii imeenea pia baina ya Waislamu wa India. [31] Ada ya kupiga ngoma na madufu kwa ajili ya kuwaamsha watu kula daku katika mwezi wa Ramadhani imezoeleza katika nchi kama Syria na hata katika nchi za Afrika Mashariki. Nchi Uturuki watu husoma mashairi kwa namna ya nyimbo wakati wa kuwaamsha watu kwa ajili ya kula daku katika mwezi wa Ramadhani.

Vyanzo

  • Attributed to Imam Sadegh (a). Miṣbāḥ al- sharīʿa. Beirut: Aʿlamī, 1400 AH.
  • Farāhīdī, Khalīl b. Aḥmad. Kitāb al-ʿayn. Qom: Dār al-Hijra, 1409 AH.
  • Ḥāʾirī Ṭabaṭabaʾī, Sayyid ʿAlī b. Muḥammad. Rīyāḍ al-masāʾil fī taḥqīq al-aḥkām bi-dalāʾil. Edited by Muḥammad Bahramand/Muḥsin Qadīrī. 1st edition. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1418 AH.
  • Ḥasanzāda, Āmulī, Ḥasan. Ilāhīnama. [n.p] Nashr-i Alif Lām Mīm, 1381 sh.
  • Ibn Sīdah, ʿAlī b. Ismaʿīl. Al-Muḥkam wa l-muhīt al-aʿzam. Second edition. Beirut: Dar al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1421 AH.
  • Ibn Fāris. Muʿjam maqāyīs al-lugha. Qom: Maktab al-Aʿlām al-Islāmī, 1404 AH.
  • Ilāhī Qumshiʾī, Muḥyi al-DDīn Mahdī. Majmūʿa diwān-i ilāhī. Tehran: Kitābfurūshī-yi barādarān-i ʿlamī, 1366 sh.
  • Jāwīd, Hūshang. Mūsīqī-i ramaḍān dar Iran. Tehran: Sūra-i Meihr, 1383 sh.
  • Jawharī, Ismāʾīl b. Ḥammād al-. Tāj al-Lugha wa ṣiḥāh al-ʾarabīyya. Beirut: Dār al-ʾIlm li-l-Malāyīn, 1376 AH.
  • Kūfī Ahwāzī, Ḥusayn b. Saʿīd al-. Al-Zuhd. Edited by Ghulām Riḍā ʿIrfānīyān. Qom: Al-maṭbaʿa al-ʿlmiya, 1402 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1429 AH.
  • Malik al-Shuʿarā-yi Bahār. Muḥammad Taqī. Dīwān-i ashʿār-i Malik al-Shuʿarā-yi Bahār. Tehran: Āzād Mihr, 1382 sh.
  • ManṣūrManṣūr-i Lārījānī, Ismāʿīl. Sīmāyi saḥar khīzān dar nahj al-balāgha. Tehran: Āya, 1387 sh.
  • Qummī, ʿAlī b. Ibrāhīm al-. Tafsīr al-Qummī. Qom: Dār al-Kitāb, 1404 AH.
  • Rāghib al-Iṣfahānī, Ḥusayn b. Muḥammad al-. Mufradāt alfāẓ al-Qurʾān. Edited by Ṣafwān ʿAdnān Dāwūdī. Beirut: Dār al-Qalam, 1412 AH.
  • https://hajj.ir/fa Ramaḍan wa Zībāīī Tafāwut-i Āʾīnhā dar kishwarhāy-i jahān(persian).
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Thawāb al-aʿmāl wa ʿiqāb al-aʿmāl. Qom: Dār al-Sharīf al-Raḍī, 1406 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Faḍāʾil al-ashhur al-thalātha. Edited by Ghulām Riḍā Irfānīyān Yazdī. 1st edition. Qom: Kitābfurūshī-yi Dāwarī, 1396 AH.
  • Shah ābādī, Muḥammad ʿAlī. Rashaḥāt ul-biḥār. Tehran: Pazhūhishkada-yi Farhang wa Andīsha-yi Islāmī, 1386 sh.
  • Ṭurayḥī, Fakhr al-Dīn b. Muḥammad al-. Majmaʿ al-baḥrayn. Edited by Sayyid Aḥmad Ḥusaynī. Tehran: al-Maktaba al-Murtaḍawīyya, 1375 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥamamd b. al-Ḥasan al-. Miṣbāḥ al-mutahajjid wa silāḥ al-mutaʿabbid, Beirut: Muʾassisat Fiqh al-Shīʿa, 1411 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Istibṣār fīmā ikhtalafa min al-akhbār. Edited by Sayyid Ḥasan al-Khirsān. 1st edition. Tehran: Dar al-Kutub al-Islāmiyya, 1390 AH.