Nenda kwa yaliyomo

Kifo kwa Amerika

Kutoka wikishia

Kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika" (Kifarsi: Marg bar Amrika), imekuwa ni nembo muhimu ya harakati za Kiislamu nchini Iran pamoja na baadhi ya nchi fulani duniani, hasa katika kupinga sera za serikali ya Marekani. Kauli mbiu hii, iliyozaliwa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979, inaonekana kama ni alama ya kupinga ukoloni, ubeberu, na uingiliaji kati wa Marekani katika masuala ya ndani ya mataifa mengine duniani, hasa mataifa ya Kiislamu.

Kwa mtazamo wa baadhi ya watu, kauli mbiu hii ni mwendelezo wa mapambano ya kiitikadi yanayoungwa mkono na Aya za Qur'ani zinazohimiza kupinga ukafiri na ushirikina. Wengine huichukulia kama dhihirisho la dhana ya kidini ya Tabarri (kujitenga na kutoshirikiana na maadui wa Uislamu), ambayo ni sehemu muhimu ya itikadi za Kiislamu. Kiongozi Mkuu wa Kidini wa Iran, Ayatullahi Ali Khamenei, akiielezea kauli mbiu hii amesema kwamba; kauli hii ina mantiki pana nadni yake na ni kauli eyendayo na akili salama ya wanadamu. Yeye anasema kwamba; kauli hii ni sawa na wito wa kujilinda na maovu ya kila aina, ikiwemo nguvu za kishetani.

Hata hivyo, kauli mbiu hii imezua mjadala ndani ya jamii ya Iran. Baadhi ya harakati za kisiasa nchini humo zimeikosoa na kuunga mkono juhudi za kuitoa kwenye sekta za mawasiliano na mahusiano ya serikali. Wao wanasema kwamba; hata mwanzilishi wa mapinduzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (Imamu Ruhollah Khomeini), alikubaliana na kuondolewa kwa kauli mbiu hii kutoka kwenye vyombo vya habari vya serikali wakati wa uhai wake. Kwa upande mwingine, wafuasi wa kauli mbiu hii wanadai kwamba; madai hayo hayana msingi, huku wakisisitiza kuwa uamuzi wa mwisho kuhusiana na kauli mbiu hiyo unapaswa kubaki mikononi mwa Kiongozi Mkuu wa Kidini (Walii faqihi), ambaye kwa sasa ni Ayatullahi Sayyid Ali Khamenei.

Nafasi ya Kauli Mbiu ya "Kifo kwa Amerika"

Kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika" imeelezwa kuwa ni kiashiro cha Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, chenye malengo na madhumuni ya kupinga ukoloni. [1] Wengine wanaiona kama kauli mbiu hii kuwa ndiyo nguzo na msingi mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, [2] na wala haijawekewa muda wala mipaka ya zama maalum katika kuifanyia kazi kauli hiyo muhimu. [3] Mohammad-Taqi Misbah Yazdi, mujitahidi na mwanafalsafa wa Kishia, anaamini kwamba watu wa Iran wanaiona kauli mbiu hii kuwa ni sawa na takbira zinazopigwa baada ya sala za jamaa. [4]

Kwa mujibu wa maoni ya Ayatollah Khamenei, kiongozi wa pili wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika" ni kauli mbiu yenye mantiki inayosapotiwa na misingi mikuu ya kifikra na kiakili, kwani kauli hii mbiu inamaanisha kifo juu ya sera za kibeberu za Marekani [5] na kifo juu ya viongozi wa Marekani katika zama zote. [6] Yeye amesema kwamba; kauli mbiu hii ni kama kauli maarufu ya kujikinga na kuwa tayari kila wakati dhidi ya Shetani, na anaamini kwamba kauli mbiu hii inawaweka watu tayari katika kukabiliana na tamaa za wabeberu wa kimataifa. [7]


Vielelezo vya Kidini Kuhusiana na Kauli Mbiu Hii

Baadhi ya vielelezo kutoka katika Qur’ani vinavyoweza kutumika kama ni msingi wa kauli mbiu hii ya “Kifo kwa Amerika” ni Aya ya 8 ya Suratu Muhammad, Aya ya 4 ya Suratu Buruj, Aya ya 19 ya Suratu Mudath-thir na Aya ya 10 ya Suratu Dhariyaat. Watafiti mbali mbali wanaamini kwamba; Aya hizi ni zinahusiana na laana ya kuwatikia mauti baadhi ya makafiri pamoja na baadhi ya washirikina. Hii ni kwa kutokana na kwamba; Aya hizi zimetumia neno “Qutila «قُتِلَ»”, lenye maana ya “Wameangamizwa au Kifo Kiwe Juu Yao”. [8] Pia kuna baadhi wanoamini kwamba; kauli mbiu hii ya “Kifo kwa Amerika”, inawezekana kuhisabiwa ni moja matawi ya dini (Furu’u Al-Diin), na ni moja amali ya kutokubaliana na maadui wa dini (Tabarriy). [9]


Nafasi ya Kauli Mbiu ya "Kifo kwa Amerika"

Mbali na Iran, kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika" pia kauli mbiu hii inaonekana kuienea na kutumika katika baadhi ya nchi nyengine za Asia, Ulaya, Afrika, na Amerika ya Kusini. [10] Ayatullah Khamenei ameeleza kwamba; jambo hili limekua ni kizingiti kikubwa kwa Marekani [11] na ni ishara ya mabadiliko yasio epukika katika ngazi ya kimataifa. [12] Kwa mfano, Sayyid Hussein Al-Huthi, mwanzilishi na kiongozi wa kwanza wa harakati za Ansarullah ya Yemen, katika hotuba yake yenye kichwa kisemacho "Mayowe dhidi ya Wabeberu", alitangaza kauli mbiu zisemazo: "Allahu Akbar, Kifo kwa Amerika, Kifo kwa Israel, Laana kwa Wayahudi, na Ushindi kwa Uislamu" kuwa ni tungo ya kauli mbiu rasmi ya Waislamu wa eneo hilo. [13]

Upinzani dhidi ya Kauli Mbiu ya "Kifo kwa Amerika"

Kuna baadhi ya watu nchini Iran, wanaotaka kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika" iondolewe kutoka kwenye siasa za Iran. Kwa mfano, Mohammad-Taqi Rahbar, ambaye ni mmoja wa wanafunzi wa kidini na mwanaharakati wa kisiasa, anasema kwamba; kauli mbiu hii inaweza kuondolewa kwa kuanzisha uhusiano wa kirafiki na Marekani. [14] Sadiq Zibakalam, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Tehran, anasema kwamba; kushikilia kauli mbiu hii kunapelekea gharama na hasara kubwa kwa Iran. [15] Wengine wamehusisha suala la kushindwa kwa Iran na kutengwa katika uwanja wa kimataifa na kauli mbiu hii, kauli ambayo imesababisha kujiondoa kwa Marekani kutoka kwenye meza ya majadiliano ya nyuklia (JCPOA). Majadiliano ambayo yaliukuwa yakifanyika kwa nia ya kutafuta muwafata juu ya mpago wa nyuklia wa Iran. [16] Akbar Hashemi Rafsanjani, aliyekuwa kiongozi wa kidini na mwanasiasa, naye pia katika kumbukumbu zake alisema kuwa; Imamu Khomeini, kiongozi wa kwanza wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alikubaliana na kuondolewa kwa kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika" kutoka kwenye vyombo vya habari vya serikali ya Iran. [17]

Kwa upande mwingine, baadhi ya watu kama vile; Sayyid Ahmad Khatami, Imamu wa Ijumaa wa Tehran, wanasema kuwa, kuondolewa kwa kauli mbiu hii ni jukumu la Kiongozi Mkuu wa Kidini (ambaye kwa hivi sasa na Ayatullahi Sayyid Ali Khamaenei). [18] Ayatullahi Sayyid Ali Khamenei, katika kujibu swali kuhusu iwapo kauli mbiu hii inasababisha uadui wa Marekani dhidi ya Iran, anasema kwamba; wabeberu wa kidunia wanapinga na wako dhidi ya kuibuka kwa harakati za kudai haki na kutafuta maendeleo ya kisayansi. Mabeberu hao hawaridhii kuona mataifa yalio nje ya mamlaka yao yanapata maendeleo, hivyo kauli mbiu hii ni kisingizio tu cha kuficha makucha yao. [19] Yeye ameongeza akisema kuwa; Uadui wa Marekani ulianza tokea tarehe 19 Agosti 1953, wakati ambapo hakuna mtu nchini Iran aliyekuwa akitumia kauli mbiu hii ya "Kifo kwa Amerika". [20] Sayyid Ali Khamenei anaamini kuwa; Kwa kuwa Marekani bado inaendelea na "shari", "kuingilia kati mabo ya ndani", na "ukhabithi wake", basi kauli mbiu hii ya "Kifo kwa Amerika" nayo itabaki na haitatoweka kwenye vinywa vya watu wa Iran. [21]



Historia

Kuna ripoti mbalimbali kuhusiana na asili na chimbuko la kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika". Wengine wanaamini kwamba; kwa mara ya kwanza kabisa kauli mbiu hii ilitolewa na wanafunzi na wapinzani wa Shah wa Iran, wakati wa safari yake kwenda Marekani, iliyojiri mnamo tarehe 14 Novemba mwaka 1977. [22] Kulingana na nyaraka zilizopatikana baada ya harakati za uvamizi wa ubalozi wa Marekani huko Tehran, yaonekana kwamba; kauli mbiu hii ilitumiwa na watu walioandamana katika harakati hizo, ambapo waliandika kauli mbiu hii juu ya kuta za ubalozi huo. Tendo amabalo lilifanyika wakati wa maandamano hayo ya msimu wa vuli wa mwaka 1978. [23] Wengine pia wamehusisha matumizi ya kauli mbiu hii na maandamano ya wanafunzi yaliofanyika mnamo tarehe 4 Novemba 1978. [24]


Katika Vyombo vya Habari na Sanaa Mbali Mbali

Katika miaka ya baadae, baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Kuliamka sera maalumu za kuonesha uhalifu wa Marekani. Sera hizi zilianza kufanyika kupitia tamsha maalumu lenye mbao kadhaa nadi yake, ikiwa ni pamoja na; maonyesho, makongamano, mashindano na uzalishaji wa kazi za sanaa zilizobeba kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika". Hatimae sera hizi zilikuwa na kupata umaafu na mwishowe kuwa ni miongoni mwa matukio muhimu ya kitaifa na kimataifa nchini Iran. Kwa mfano, Tamasha la "Kifo kwa Amerika" hufanyika kila baada ya miaka kadhaa, likiwaweka pamoja wasanii kutoka nchi mbalimbali duniani. Wasanii ambao huonesha sanaa zao kwa mfumo wa; picha, michoro ya hati maalumu, katunu, filamu za hikaya, klipu, nyimbo, na mashairi. [25]

Aidha tamashi hili huhamasikwa kupitia mashindano Mashindano ya "Typografia ya kauli mbiu ya “Kifo kwa Amerika", [26] maonyesho ya mfululizo wa mabango yenye ibara ya kauili mbiu ya "Kifo kwa Amerika", yanayojiri katika viwanja vya vyuo vikuu [27], na pia tamasha la sanaa la kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika". Harakati hizi hufanyika mbele ya wageni na kutumbuizwa na baadhi ya wasanii (waimbaji) maarufu duniani wanaopinga vitendo vya ubeberu. [28]

Katika hafla ya sita ya hitimisho ya Tamasha la Filamu la Ammar, kulizindulia zawadi maalum ya mosaiki yenye kauli mbui ya “Kifo kwa Amerika". Zawadi hii, ni  zawadi inayotolewa kila mwaka kwa na kukabidhiwa yule mwenye kazi inayopinga zaidi ubeberu wa Marekani. Kwa mara ya kwanza kwa Mehdi Naqavian, mkurugenzi wa filamu ya hikaya ya "Ndugu" inayozungumzia athari za uchaguzi wa urais wa kumi nchini Iran, ndiye aliye fanikiwa kupokea zawadi hii katika hitimisho hili la sita la Tamasha la Filamu la Ammar. [29]


Sanaa za Picha

Mosaiki za Sakafu ya Uwanja wa Msikiti wa Khuzan katika Mji wa Khomein zenye Kauli Mbiu ya "Kifo kwa Amerika" kwa hati (font) za za Kufi [30]

Kuchoma Bendera ya Marekani huko New York wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya George Floyd [31]

Kibonzo (kikatuni) cha kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika", dhidi ya kauli ya Trump inayodai kwamba hakusikia sauti isemayo "Kifo kwa Amerika" kutoka kwa watu wa Iran [32]

Picha ya kitabu kiitwacho “Chera Marq bar Amrika Jahan-Khoor” (Kwa Nini Kifo kwa Amerika, Mtafunaji wa Ulimwengu)", kilichoandikwa na Ali Shoaibi. [33]