Khalilullah (Lakabu)

Kutoka wikishia

Khalilullah (Kifarsi: خلیل‌الله (لقب)) Ni ibara ya Kiarabu iliojengeka kupitia maneno mawili “Khalilu na Allah”. Katika lugha ya Kiarabu neno “Khalilu” humaaanisha rafiki kipenzi, na neno “Alla” lina maana ya Mungu. Kwa hiyo neno “Khalilullah” lina maana ya “rafiki kipenzi wa Mwenye Ezi Mungu”, [1] nalo ni lakabu maalum ya Nabii Ibrahim (a.s). [2] Imeelezwa ya kwamba; nafasi ya kuwa Khalilullah ni nafasi na sifa kubwa mno, na ni makhususi kwa Nabii Ibrahim (a.s), [3] ambayo ni nafasi ya juu zaidi kuliko hata nafasi ya unabii na utume. [4] Katika moja ya Hadithi kutoka kwa Imam Sadiq (a.s), imeelezwa kuwa; kwanza kabisa Menye Ezi Mungu alimchagua Ibrahim kama mja (abd) wake, kisha kama nabii, baadae kama mtume, na hatimaye kama rafiki (khalil). [5]

Aya ya 125 ya Suratu An-Nisa inasema: “واتَّخَذَ اللَّهُ إِبْراهیمَ خَلیلاً Na Allah alimchagua Ibrahim kuwa ni rafiki yake (kipenzi)". [6] Neno " واتَّخَذَwattakadha" limetafsiriwa kwa maana ya kuchagua au kuteua. [7] Mwanzoni mwa aya hii, Mwenye Ezi Mungu amewataka watu kufuata dini ya Ibrahim [8], kisha ili kuwashawishi wengine kumfuata Ibrahim, Aya hii mwaishoni mwake inamalizi kwa kusema; Na Mwenye Ezi Mungu alimchagua Ibrahim kama rafiki kipenzi. [9] Zamakhshari, mwanazuoni na mfasiri wa Kisunni, amelifasiri neno rafiki kama ni fumbo linalomaanisha kuchaguliwa pamoja na kule Ibrahim kuwa na sifa maalum zipatikanazo kati ya marafiki wawili. [10]

Pia Hadithi zimemtaja Ibrahim kama ni Khalilullah. [11] Hata Nabii Ibrahim (a.s) naye pia alijitaja kama Khalilullah. [12] Waislamu wa mji wa Al-Khalil ulioko Palestina iliyokaliwa kimabavu, ambayo ndio nchi aliyokuwa akiishi Ibrahim (a.s) [13], waliuita mji huo kwa jina la Al-Khalil, jina ambalo limetokana na Aya ya 125 ya Suratu An-Nisa. [14] Ingawa lakabu hii imekuwa ni sifa maalum kwa Nabii Ibrahim, ila pia kuna baadhi ya Hadithi na dua zilizotumia wasifu huo katika kumsifu bwana Mtume (s.a.w.w), [15] Imam Ali pamoja [16] na Imam Hussein (a.s) [17].

Pia katika fasihi ya Kiajemi, Nabii Ibrahim (a.s) anajulikana kama ni Khalil. Mulla Ahmad Naraqi katika mathnawi Ta'qdis aliandika:

Allah Mwingi wa Utukufu alimteua na kumuita kuwa Khalil wake.

Hadhi ya urafiki ilimfikia kutoka kwa Mola, na hivyo akapewa lakabu ya Khalilullah. [18]

Mshairi mwingine aliandika akisema:

Msingi wa Nyumba ya Kaaba uliwekwa na Khalilullah (Ibrahim),

Lakini Ali alizaliwa ndani ya Kaaba, na mwenye nyumba akawa amejitokeza. [19]

Hadithi zimeelezea sababu mbalimbali zilizo mfanya Mwenye Ezi Mungu amchague Ibrahim na kumweka kwenye nafasi hii. [20] Katika kitabu cha Al-‘Ilalu Al-Sharaa’i'i, kuna sehemu yenye kichwa cha habari kisemacho "Sababu zilizomfanya Mwenye Ezi Mungu amchague Ibrahim kuwa ni rafiki yake kipenzi". [19] Kuna Hadithi nyingi zilizotajwa juu ya Nabii Ibrahim (a.s) katika sehemu hiyo. [21] Kwa mujibu wa Hadithi, nafasi ya Khalilullah kwa Ibrahim inatokana na kusujudu sana, kuwapa chakula wahitaji, kusali usiku, kutowakataa masikini, ukarimu kwa wageni [22], na kutoomba chochote kutoka kwa yeyote yule isipokuwa kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu mwenyewe.[23] Wafasiri wengine wamesema; kuacha kuabudu sanamu na kumwabudu Mungu ndio msingi wa yeye kupata sifa hiyo. [24]

Maana ya Khalil

Kuna maana mbili zinazoweza kupatikana kuhusiana na neno Khalil:

Khalil kwa maana ya rafiki kipenzi; Kiasilia neno Khalil linatokana na al-khullah lenye maana ya rafiki. [25] Maana hii inapatika katika tafsiri ya; “Tafsiri ya Majma'u al-Bayan”, ambayo ni tafsiri ya Kishia iliyoandikwa katika karne ya sita. [25] Mfasiri wa Kishia, aitwaye Makarem Shirazi, pia ameihisabu maana kuhusiana na Nabii Ibrahim hii kuwa ni sahihi. [27] Wafasiri wengine pia wanakubaliana na maana hii. [28]

Khalil kwa maana ya umaskini; Pia yawezekana kuwa neno Khalil linatokana na neno al-khallah lenye a maana ya umaskini. [29] Baadhi pia wanaamini kuwa; Neno Khalil kwa Nabii Ibrahim lina maana ya kuwa maskini na mwenye uhitaji mbele ya Mungu. [30] Allama Tabatabai anaamini kuwa jina Khalil lina maana ya umaskini, hii ni kwa mujibu wa Hadithi isemayo kuwa; Ibrahimu aliitwa Khalil kwa sababu ya kutoomba chochote kutoka kwa yeyote yule isipokuwa Mungu pekek. Kwa maoni yake, maana sahihi ya Khalilullah ni kule mtu kutomlalamikia yeyote yule kuhisiana na mahitaji yake isipokuwa Mwenye Ezi Mungu peke yake na kuto omba msaada kutoka kwa mtu yeyote yule isipokuwa Mungu peke yake. [31]

Rejea

Vyanzo