Kanuni ya Soko la Waislamu

Kutoka wikishia

Kanuni ya Soko la Waislamu (Kiarabu: قاعدة سوق المسلمين) ni sheria na kanuni ya kifikihi ambayo kwa mujibu wake inajuzu kuuza na kununua katika soko la Waislamu ngozi na nyama za wanyama waliochinjwa na mnyama huyo anahukumiwa kuwa ni tohara na hakuna haja ya kufanya uchunguzi kuhusiana na uhalali wa nyama hiyo. Mafakihi wakitumia ijmaa (itifaki ya wanazuoni), mbinu na mtindo wa kivitendo wa Waislamu na hadithi wametumia kanuni hiyo kama hoja. Kwa mujibu wa mtazamo na nadharia ya Maulamaa wa elimu ya Usul, endapo ushahidi au habari ya muadilifu itakapogongana na kanuni ya soko la Waislamu, kanuni hii haitafanya kazi na kwa msingi huo mnyama huyo atahisabiwa kuwa hajachinjwa kihalali, na hivyo nyama na ngozi yake si halali.

Muhtawa wa Kanuni

Soko la Waislamu au gulio la Waislamu ni kanuni ya kifikihi ambayo kwa mujibu wake inajuzu kuuza na kununua nyama na viungo vya mnyama ambaye nyama yake ni halali kuliwa katika soko la Waislamu na hakuna haja ya kufanya uchunguzi na utafiti kuhusiana na uhalali na utohara wake.[1] Makusudio ya soko la Waislamu ni soko ambalo wauzaji wengi au wote ni Waislamu.[2]

Nafasi na Umuhimu

Kanuni ya soko la Waislamu imejadiliwa katika vitabu kwa anuani ya kanuni ya kifikihi.[3] Kadhalika katika elimu ya Usul hujadiliwa kwa sura tofauti kama moja ya hoja za kuthibitishia jambo.[4] Mafakihi hutumia kanuni hii kwa ajili ya kunyambua hukumu za kisheria katika baadhi ya milango ya fikihi kama Sala, biashara, vyakula, vinyaji, uwindaji na vichinjwa.[5]

Kwa mujibu wa baadhi ya mafakihi, kutokana na kuwa sahihi baadhi ya miamala kama kuuza na kununua wanyama, nyama, ngozi na viungo vyake na kadhalika kula nyama zao kunategemea kanuni hii, endapo kanuni hii itakuwa haina hoja, muamala huu utakabiliwa na matatizo na kwa msingi huo, kila Muislamu anapaswa kuchinja mnyama mwenyewe jambo ambalo litaleta shida na kuvuruga mfumo wa Kiislamu na matokeo yake ni kukosekana ukuaji wa soko lao.[6] Kwa mujibu wa kanuni hii ni halali kununua na kuuza nyama na viungo (pamba, ngozi n.k)[7] vya wanyama ambao nyama zao ni halali kuliwa katika nchi za Kiislamu na hukumu yake ni kuwa tohara.[8]

Nafasi ya Kanuni Mkabala na Hoja Zingine

Endapo kanuni ya soko la Waislamu itagongana na moja ya misingi ya kivitendo, kanuni ya soko la Waislamu itatangulizwa kutokana na kuwa ni hoja;[9] kwa sababu msingi wa kutumia misingi ya kivitendo (Usul Amali) ni shaka na kwa kuweko hoja, shaka haina nafasi;[10] lakini kama itagongana na hoja zingine kama hoja ya wazi na habari ya muadilifu (kwa mujibu wa hoja zake katika maudhui) hoja hiyo itatangulizwa mbele ya kanuni ya soko la Waislamu.[11]

Nyaraka

Mafakihi wakitumia hoja mbalimbali kama ijmaa, hadithi na mbinu za mtindo wa kivitendo wa Waislamu wameitaja kanuni ya soko la Waislamu kuwa ni hoja.

  • Ijmaa: Kwa mujibu wa ijmaa ya mafakihi wa Kishia ni kuwa, soko la Waislamu ni hoja na ina dalili na hoja juu ya uhalali na utoharifu wa nyama na viungo vya mnyama vilivyonunuliwa katika soko la Waislamu.[12] Baadhi ya wengine wamesema, ijmaa ni ushahidi ambao hauna hoja.[13]
  • Mtindo wa kivitendo wa Waislamu: Sira ya Waislamu na mtindo wao tangu zama za Maimamu (a.s) kuhusiana na kununua nyama na viungo vya mnyama ambaye nyama yake ni halali kutokana katika soko la Waislamu ilikuwa ni kufanya hivyo pasi na kufanya uchunguzi kuhusiana na namna mnyama huyo alivyochinjwa.[14]
  • Hadithi: Hurr Amil katika kitabu chake cha Wasail al-Shia’h, ametaja hadithi nyingi katika milango tofauti ya tohara, uwindaji, vichinjwa, vyakula, vinywaji na biashara[15] ambapo vinaashiria hoja ya kanuni hii.[16]

Kutabikisha

Makusudio ya Waislamu katika kanuni hii ni maana yake jumla na sio maalumu kwa Shia Imamiyyah bali inajumuisha pia makundi mengine ya Kiislamu.[17] Kadhalika makusudio ya soko la Waislamu ni gulio na maeneo katika ardhi za Kiislamu na sio lazima wakazi wake wote wawe ni Waislamu bali makusudio ni kwamba, akthari ya wakazi wake wawe ni Waislamu.[18]

Kwa mujibu wa Shahid Thani, kama wakazi wake watakuwa sawa kwa sawa baina ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu, au wasiokuwa Waislamu wakawa ni wengi, kanuni ya soko la Waislamu hapa haitafanya kazi; isipokuwa kama nyama itachukuliwa kutoka mikononi mwa Waislamu. Kadhalika yeye anaamini kwamba, katika kuthibiti soko la Waislamu, sio lazima mtawala awe ni Muislamu.[19] Lakini Ayatullah Boroujerdi anasema kuwa, kuwa mtawala ni Muislamu kunathibiti soko la Waislamu. Ikiwa mtawala ni Muislamu basi soko litakuwa ni soko la Waislamu hata kama akthari ya watu wa soko sio Waislamu.[20]

Katika kitabu chake cha Riyadh al-Masail, Sayyid Ali Tabatabai yeye anaona kuwa, kigezo cha kufahamu soko la Waislamu ni ada na mazoea katika jamii na anaamini kwamba, soko la Waislamu ni mahali ambapo wakazi wake wengi au wote ni Waislamu.[21]

Rejea

  1. Musawi Bajnurdi, Al-Qawaida al-Fiqihiyyah, 1377 S, juz. 4, uk. 160; Burujurdi, Tibiyan al-Salat, 1426 AH, juz. 4, uk. 17.
  2. Muasase Dairat al-Ma'arif al-Fiqh al-Islami,Farhang Fiqh Mutabaq Madhhab Ahlul-Bayt (a.s), 1387 S, juz. 2, uk. 43.
  3. Tazama: Bajnurdi, Al-Qawaida al-Fiqihiyyah, 1377 S, juz. 4, uk. 155; Irawani, Darus Tamhidiyyah Fi al-Qawaida al-Fiqihiyyah, 1432 AH, juz. 2, uk. 77.
  4. Tazama: Sheikh Ansari, Faraid al-Usul, 1428 AH, juz. 3, uk. 20.
  5. Tazama: Muhaqiq Hilli, al-Muutabar, 1407 AH, juz. 2, uk. 78; Najafi, Jawahir al- Kalam, 1432 AH, juz. 12, uk. 233.
  6. Saifi Mazandarani, Mbani al-Fiqh al-Faal, 1425 AH, juz. 1, uk. 181; Irawani, Darus Tamhidiyyah Fi al-Qawaida al-Fiqhiyyah, 1432 AH, juz. 2, uk. 77.
  7. Ridhai-Nasab, Yazdan-Bakhsh, «Barresi Mabani wa Huquq Qaide Suuq al-Muslimiin», uk. 85.
  8. Ansari, «Barresi Qaide Suuq al-Muslimiin wa Miizan Hujiyyat An», uk. 7.
  9. Musawi Bajnurdi, al-Qawaida al-Fiqihiyya, 1377 S, juz. 4, uk. 169.
  10. Saifi Mazandarani, Mabani al-Fiqh al-Faal, 1425 AH, juz. 1, uk. 197
  11. Saifi Mazandarani, Mabani al-Fiqh al-Faal, 1425 AH, juz. 1, uk. 197
  12. Saifi Mazandarani, Mabani al-Fiqh al-Faal, 1425 AH, juz. 1, uk. 185
  13. Saifi Mazandarani, Mabani al-Fiqh al-Faal, 1425 AH, juz. 1, uk. 185
  14. Musawi Bajnurdi, al-Qawaida al-Fiqihiyya, 1377 S, juz. 4, uk. 155.
  15. Hurr Amili, Wasail al-Shia, 1414 AH, juz. 24, uk. 70 na juz. 27, uk. 292 na juz. 3, uk. 490 na juz. 4, uk. 455.
  16. Makarim Shirazi, Al-Qawaida al-Fiqihiyyah, 1370 S, juz. 2, uk. 108-111.
  17. Irawani, Darus Tamhidiyyah Fi al-Qawaida al-Fiqhiyyah, 1432 AH, juz. 2, uk. 87.
  18. Jawahiri, Buhuthi Fi al-Fiqhi al-Muasir, 1419 AH, juz. 2, uk. 259.
  19. Shahid Thani, Hashiyeh Shara'i al-Islam, 1380 S, juz. 1, uk. 119.
  20. Burujurdi, Tibiyan al-Salat, 1426 AH, juz. 4, uk. 19-20.
  21. Tabatabai, Riyadh al-Masail, 1412 AH, juz. 12, uk. 118.

Vyanzo

  • Ansari, Adham, «Barresi Qaide Suuq al-Muslimiin wa Miizan Hujiyyat An», Dar Mahename Kanun, Tehran, Nashr Kanun Sardaftaran, No. 67, Bahmman 1385 S.
  • Irawani, Muhammad Baqir, Darus al-Mahidiyyah fi al-Qasas al-Fiqhiyyah, Qom, Darus Tamhidiyyah Fi al-Qawaida al-Fiqhiyyah, Qom, Dar al-Fiqh lil-matbuat wa Nashr, Chapa ya tano, 1432 AH.
  • Burujurdi, Sayyid Hussein, Tibiyan al-Salat, Qom, Ganj Irfan lil-matbuat wa Nashr, chapa ya kwanza, 1426 AH.
  • Jawahiri, Hassan, Durus Fi al-Fiqhi al-Muasir, Dar al-Dhahair, Beirut, chapa ya kwanza, 1419 AH.
  • Hurr Amili, Muhammad bin Hassan, Wasail al-Shi'a, Qom, Muasase Ahlul-bayt, 1414 AH.
  • Ridhai-Nasab, Ansiyeh na Haniyeh Yazdanbakhsh, «Barresi Mabani wa Huquq Qaide Suuq al-Muslimiin», Dar Fasil-name Takhasusi Fiqhi wa Huquqi Arshian Fars, Shiraz, Mwaka wa kwanza, Toleo la nne, Zamistun 1401 S.
  • Saifi Mazandarani, Ali Akbar, Mabani al-Fiqh al-Faal Fi al-Qaqida al-Fiqihiyyah al-Islamiyyah, Qom, Daftar Intisharat Islami, Chapa ya kwanza, 1425 AH.
  • Shahid Thani, Zainu-Din Bin Ali, Hashiyeh Shara'i al-Islam, Qom, Intisharat Bustan Kitab, 1380 S.
  • Sheikh Ansari, Murtadha, Faraid al-Usul, Qom, Majmau al-Fikr al-Islami, chapa ya 9, 1428 AH.
  • Tabatabai, Sayyid Ali, Riyadh al-Masail, Qom, Muasase Intisharat Islami, chapa ya kwanza, 1412 AH.
  • Muasase Dairat al-Ma'arif al-Fiqhi al-Islami, Farhang Fiqhi Mutabiq Madhhab Ahlul-bayt (a.s), Qom, intisharat Muasase Dairat al-Ma'arif al-Fiqh al-Islami, 1387 S.
  • Muhaqiq Hilli, Najmuddin Jafar bin Al-Hassan, al-Muutabar Fi Sharh al-Mukhtasar, Qom, Intisharat Muasase Sayyid Shuhada, Chapa ya kwanza, 1407 AH.
  • Makarim Shirazi, Nassir, Al-Qawaida al-Fiqihiyyah, Qom, Madrase Imam Ali bin Abi Talib (a.s), Chapa ya tatu, 1370 S.
  • MusaWi Bajnurdi, Sayyid Hassan, Al-Qawaida al-Fiqihiyyah, Qom, Nashr al-Hadi, 1377 S.
  • Najafi, Muhammad Hassan, Jawahir al-Kalam Fi Sharh Shara'i al-Islam, Qom, Muasase Nashr Islami, 1432 AH.