Nenda kwa yaliyomo

Abdus Salih

Kutoka wikishia

Abdu Salih (Kiarabu: العبد الصالح). Ibara ya Abdu Salih inasimama kwa maana ya mtumishi mwema (mja mwema), ambayo hutumiwa katika Qur'ani kama ni istilahi kuelezea baadhi ya watu maalumu. Vyanzo vya pande zote mbili Shia na Sunni vimemtambua Imamu Kadhim (a.s) kwa jina na lakabu ya Abdu Salih, kutokana na wingi wa ibada zake katika kumwabudu Mola wake.

Neno hili limekuwa likitumiwa kwa mtindo wa wingi katika Qur'an (ibaaduka as-saaliheen).[1] Qur'an inawataja nabii Nuh na Lut kuwa ni watumishi wema wa Mwenyezi Mungu (‘Ibadu al-salihina).[2] Kulingana na Riwaya, Dhul-Qarnayn pia amepewa jina la Abdu Salih.[3]

Kwa mujibu wa vyanzo vya Shia na Sunni, Imamu Kadhim (a.s) amepewa cheo cha Abdu Salih kutokana na wingi wa ibada zake.[4]

Katika moja ya nukuu za riwaya zitokazo kwake, pia ndani yake ametambuliwa kwa jina hili.[5]

Katika ibara za maandiko ya [[ziara (sala na salamu) ya Abbas], iliyosimuliwa na Imamu Swadiq (a.s) pia yeye (Abass) ametambuliwa kama ni Abdu Salih.[6] Vivyo hivyo, katika ziara ya Muslim bin Aqil[7] na Hani bin Urwa,[8] wote wawili wametambuliwa kwa jina la Abdu Salih ndani ya ziara hiyo.

Katika salamu itolewayo mwishoni mwa kila sala, pia salamu hizo huelekezwa kwa waja wema wa Mwenyezi Mungu (ibaadullahi as-saaliheen).[9]

Rejea

  1. Qurʾan, 17:19.
  2. Qurʾan, 66:10.
  3. Majlisī, Biḥār al-anwār, juz. 12, uk. 199; ʿAyyāshī, Tafsīr al-ʿAyyāshī, juz. 2, uk. 343.
  4. Baghdādī, Tārīkh Baghdād, 1417 H, juz. 13, uk. 29; Yaʿqūbī, Tārīkh al-Yaʿqūbī, juz. 2, uk. 414.
  5. Tazama: Kulaynī, al-Kāfī, juz. 1, uk. 177, 539; juz. 3, uk. 59, 109; juz. 4, uk. 72, 412.
  6. Ibn Qūlawayh, Kāmil al-zīyārāt, uk. 257; Majlisī, Biḥār al-anwār, 1403 H, juz. 98, puk. 277
  7. Ibn Mashhadī, al-Mazār al-kabīr, uk; Majlisī, Biḥār al-anwār, juz. 97, uk. 428. 178.
  8. Ibn Mashhadī, al-Mazār al-kabīr, uk; Majlisī, Biḥār al-anwār, juz. 97, uk. 428. 178.
  9. Imamu Khomeini na wengineo, Risale Tawdhih al-masail (marajiu), Daftar Intisharat Islami, juz. 1, uk. 598.

Vyanzo

  • ʿAyyāshī, Muḥammad b. Masʿūd al-. Tafsīr al-ʿAyyāshī. Edited by Rasūlī Maḥallātī. Tehran: al-Maṭbaʿa al-ʿIlmīyya, 1380 Sh.
  • Ibn Mashhadī. Al-Mazār al-kabīr. Edited by Jawād Qayyūmī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1419 AH.
  • Ibn Qūlawayh, Jaʿfar b. Muḥammad. Kāmil al-zīyārāt. Edited by ʿAbd al-Ḥusayn Amīnī. Najaf: Dār al-Murtaḍawīyya, 1356 Sh.
  • Khaṭīb al-Baghdādī, Aḥmad b. ʿAlī. Tārīkh Baghdād. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1417 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī & Muḥammad Ākhūndī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Yaʿqūbī, Aḥmad b. Yaʿqūb al-. Tārīkh al-Yaʿqūbī. Beirut: Dār al-Ṣādir, [n.d].