Sadiq (Lakabu)

Kutoka wikishia
Makala hii inahusu jina la Imam Sadiq (AS). Ili kujifunza kuhusu haiba ya Imam (a.s.), tazama utangulizi wa Imamu Swadiq (a.s)

Sadiq ni cheo mashuhuri zaidi cha Imamu Swadiq (a.s)[1] Cheo hiki amepewa Imamu wa sita wa Mashia kwa sababu ya ukweli wake wa maneno na vitendo.[2] [2] hivyo basi aliitwa swadiq kwa sababu katika maisha yake hakuwahi kusikika akisema uongo [3] [3] Kwa mujibu wa riwaya kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s.), Imamu wa sita aliitwa Sadiq ili kumtofautisha na Jafar mwongo [4] [4] Kwa mujibu wa riwaya iliyotajwa kutoka kwa Ali Ibn Al-Hussein, Imamu wa nne wa Mashia aliulizwa : kwa nini watu wa mbinguni wanamwita Imamu wa Sita Sadiq, na hali ya kuwa nyinyi nyote (maimamu maasumu) ni waaminifu na wakweli? Akajibu: Baba yangu amepokea kutoka kwa babu yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW), kwamba anapozaliwa mwanangu “Ja’far bin Muhammad bin Ali bin Husein” muite Sadiq. Kwa sababu mtoto wake wa tano ataitwa Jafar na atadai uimamu kwa uwongo, naye ni Jafar, mwongo mbele ya Mwenyezi Mungu na atamzulia uongo Mwenyezi Mungu.[5] [5] Baadhi pia wamesema Imamu Sadiq (AS) alipewa jina la utani la Sadiq ili kuepuka kushiriki katika maasi na harakati za kimapinduzi za zama zake; Kwa sababu wakati huo, mtu aliyekusanya watu karibu naye na kuwachochea waasi dhi ya serikali aliitwa mwongo.[6] [6]

REJEA

1. Majlisi, Jalau Al-Ayoun, 2002, uk.869.

2. Mudhaffar, Al-Imam al-Sadiq, 1421 AH, juzuu ya 2, uk.190.

3. Majlisi, Bihar al-Anwar, 1363, juzuu ya 47, uk.33.

4. Qomi, Muntaha al-Amal, 1379, juzuu ya 2, uk.1336.

5. Qomi, Muntaha al-Amal, 1379, juzuu ya 2, uk.1336.

6. Paktachi, "Jafar Sadiq (AS), Imam", uk.181.

VYANZO

  • Paktachi, Ahmad, "Ja'far Sadiq (a.s.), Imam", Tehran, Encyclopedia ya Kiislamu, Juzuu 18, Kituo cha Encyclopedia ya Kiislamu, 1389.
  • Qomi, Sheikh Abbas, Muntaha al-Amal fi Tawarikh al-Nabi wa al-Al, Qom, Dilil Ma, 1379.
  • Majlisi, Muhammad Baqir, Bihar al-Anwar, Tehran, Islamia, 1363.
  • Majlisi, Muhammad Baqir, Jalau Al-Ayoun, Qom, Surur, 2002.
  • Mudhaffar, Muhammad Hussein, Imam al-Sadiq (a.s.), Qom, jamiatu Al- Madrasin, 1421 AH.
  1. Majlisi, Jalau Al-Ayoun, 2002, uk.869.
  2. Mudhaffar, Al-Imam al-Sadiq, 1421 AH, juzuu ya 2, uk.190.
  3. Majlisi, Bihar al-Anwar, 1363, juzuu ya 47, uk.33.
  4. Qomi, Muntaha al-Amal, 1379, juzuu ya 2, uk.1336.
  5. Qomi, Muntaha al-Amal, 1379, juzuu ya 2, uk.1336.
  6. Paktachi, "Jafar Sadiq (AS), Imam", uk.181.