Hotuba ya Imamu Hussein siku ya Ashura

Kutoka wikishia
Maombolezo ya Muharram

Hotuba ya Imamu Hussein (a.s) (Kiarabu: خطبة الإمام الحسين (ع) يوم عاشوراء) katika siku ya Ashura inaashiriwa matamshi aliyoyatoa Imamu Hussein (a.s) katika siku ya Ashura mwaka 61 Hijiria ambayo aliyatoa alipokuwa akilihutubu jeshi la Omar bin Sa'd. Katika hotuba hiyo, Imamu Hussein alijitambulisha kisha akabainisha kwamba, sababu ya kuja kwake Iraq ni kuitikia mwito wa watu wa al-Kufa. Katika hotuba hiyo Imamu Hussein alitaja baadhi ya majina ya waandishi wa barua waliokuwa katika jeshi la Omar bin Saad, akawakumbusha mwaliko wao na akasisitizia suala la kukataa kwake madhila na kutotoa baia na kiapo cha utii kwa Yazid bin Mu'awiyah.

Kwa mujibu wa ripoti ya Abu Mikhnaf, mwandishi wa historia ya tukio la Karbala, waandishi wa barua walikana mwito na mwaliko wao. Kadhalika Shimr bin Dhil-Jawshan alikata hotuba ya Imamu Hussein (a.s). Muhammad Hadi Yusufi Gharawi msomi na mwanahistoria anasema, kitendo hicho cha Shimr kilikuwa na lengo la kuzuia kuathirika askari wa jeshi la Omar bin Sa'd.

Umuhimu na nafasi

Khutba ya Imamu Hussein (a.s) ni maneno ya Imamu wa tatu wa Waislamu wa Kishia, ambayo aliyatoa siku ya Ashura katika mwaka wa 61 Hijiria mbele ya askari wa Omar bin Sa'd, wale askari wa Ubaidullah bin Ziyad, gavana wa Yazid bin Muawiyah huko al-Kufa, ambao walitumwa Karbala kupigana na Imamu Hussein (a.s) Maneno haya yamesimuliwa kwa nukuu tofauti katika vyanzo vya Shia na Sunni. [1]

Maudhui ya hotuba

Imamu Hussein (a.s) aliwataka askari wa Omar bin Saad wasikilize maneno yake na wasiharakishe vitani, ili aweze kuwanasihi. Pia aliwataka wampe nafasi ya kueleza sababu ya kuja kwake Kufa, ili wasiwe ni wenye kukosea na kuchanganya mambo. [2]

Aliendelea kujitambulisha na akataja na kuashiria nasaba yake kwa Imamu Ali (a.s), Mtume (s.a.w.w), Hamza bin Abdul Muttalib na Jafar bin Abi Talib. [3] Vile vile alitaja maneno ya Mtume (s.a.w.w) kuhusu yeye na ndugu yake Imamu Hassan (a.s) kwamba "hawa wawili ni mabwana wa mabarobaro wa peponi" na akawaambia ikiwa hawakubali maneno yake basi wawarejee maswahaba kama Jabir bin. Abdullah al-Ansari, Abu Saeed al-Khudhri, Sahl bin Sa'd Saedi, Zayd bin Arqam na Anas bin Malik ambao walikuwa wangali hai. [4] Kisha huku akiashiria kuwa yeye ni mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), akawauliza askari wa Ibn Saad, “Je, nimemuua yeyote kati yenu, au nimeharibu mali ya mtu yeyote, au nimemjeruhi yeyote?” [5]

Baada ya hayo, aliwahutubu Shabath bin Rab’i, Hajjar bin Abjar, Qays bin Ash’ath na Yazid bin Harith miongoni mwa waandishi wa barua za watu wa Kufa, akisema, “Je, si ninyi mlioniandikia barua na kuniita nije katikak mji wa Kufa?” [6 Akaendelea na maneno yake kwa kusoma Aya isemayo:إِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَ رَبِّكُمْ أَنْ تَرْجُمُونِ ; Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe” [7] ambayo inaashiria kisa cha Nabii Mussa mkabala wa vitimbi vya Firauni na akasoma pia Aya isemayo: أعوذ بِرَبِّي وَ رَبِّكُمْ مِنْ كُلِّ مُتَكَبِّرٍ لا يُؤْمِنُ بِيَوْمِ الْحِسابِ ; "Mimi najikinga kwa Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi anilinde na kila mwenye jeuri asiye iamini Siku ya Hisabu, [8] na akahitimisha hotuba yake hiyo kwa Aya hizo. [9]

Radiamali

Kwa mujibu wa Abu Mikhnaf, wakati Imamu Hussein (a.s) alipowataka askari wa Ibn Sa'd wasikilize maneno yake ili kueleza sababu ya kuja kwake al-Kufa, baadhi ya wanawake na watoto walianza kulia. Imamu Hussein (a.s) alimtaka Hadhrat Abbas na Ali Akbar kuwanyamazisha, na akasema maneno yake ambayo ni mashuhuri sana: سَكِّتَاهُن‏ فَلَعَمْرِي لَيَكْثُرَنَّ بُكَاؤُهُنَّ ; Naapa kwa Mwenyezi Mungu, bado wana vilio vingi mbele yao. [10]

Pia, baada ya hapo Imamu Hussein (a.s) aliwataka askari wa Ibn Sa'd kuwarejea masahaba ambao wangali hai iwapo hawakubaliani na maneno yake. Shimr bin Dhil al-Jawshan alipaza sauti na kusema: Huyu anamuabudu Mwenyezi Mungu katika maneno tu na hajui anasema nini? Maneno ya Shimr yalifuatiwa na radimali ya Habib bin Mudhahir ambaye alimwambia Shimr, moyo wako umepigwa muhuri. [11] Kwa mujibu wa Muhammad Hadi Yusufi Gharawi, mtafiti wa historia ya Kiislamu, kukatizwa kwa hotuba ya Imamu Husein na Shim ilikuwa ni kuzuia hotuba yake isije kuathiri jeshi la Ibn Sa'd. [12]

Waandishi wa barua wakakana kwamba, walitoa mwaliko kwa Imamu Hussein (a.s). [13] Baada ya hotuba ya Imamu Hussein (a.s) Qays bin Ash’ath alisema: Kwa nini humpi baia binamu yako (Yazid)? Imamu Hussein akasema: Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitaweka mkono wangu katika mikono yenu kama watu walio madhalili na sitakimbia kama watumwa." [14]

Hotuba ya Imamu Hussein

أَيُّهَا النَّاسُ اسْمَعُوا قَوْلِي وَ لَا تَعْجَلُوا حَتَّى أَعِظَكُمْ بِمَا يَحِقُّ لَكُمْ عَلَيَّ وَ حَتَّى أُعْذِرَ إِلَيْكُمْ فَإِنْ أَعْطَيْتُمُونِي النَّصَفَ كُنْتُمْ بِذَلِكَ أَسْعَدَ وَ إِنْ لَمْ تُعْطُونِي النَّصَفَ مِنْ أَنْفُسِكُمْ فَأَجْمِعُوا رَأْيَكُمْ ثُمَّ لا يَكُنْ أَمْرُكُمْ عَلَيْكُمْ غُمَّةً ثُمَّ اقْضُوا إِلَيَّ وَ لا تُنْظِرُونِ إِنَّ وَلِيِّيَ اللَّهُ الَّذِي نَزَّلَ الْكِتابَ وَ هُوَ يَتَوَلَّى الصَّالِحِينَ


“Enyi Watu! Nisikilizeni, na msikimbilie vita na umwagaji damu ili niweze kukunasihini kwa yale mnayostahiki juu yangu, ambayo ni kukupeni mawaidha na ushauri, na ili niweze kueleza sababu iliyonifanya nije katika nchi hii, iwapo mtasikiliza maneno yangu na kukubali udhuru wangu, na kuingia pamoja nami kupitia mlango wa haki na uadilifu, basi ni wazi kwamba mtakuwa mmeipata njia ya Saada na Mafanikio, na hamtakuwa tena na sababu ya kupigana vita dhidi yangu, lakini ikiwa hamtakubali udhuru wangu (na maonyo yangu) na mkakataa kuingia pamoja nami kupitia mlango wa Haki na Uadilifu, basi mnaweza kuungana mkono na kutekeleza uamuzi wenu mbaya (wa kunishambulia) pasina kuchelewa, lakini (mtambue kwamba) katika hali hii, jambo hili halina shaka tena kwenu, na Mwenye kunihami ni Mwenyezi Mungu aliyeiteremsha Qur’an, na ni Mwenye kuwahami (kuwasaidia) na kuwasimamia watu wema”.

ثُمَّ حَمِدَ اللهَ وَ أَثْنَى عَلَيْهِ وَ ذَكَرَ اللهَ بِمَا هُوَ أَهْلُهُ وَ صَلَّى عَلَى النَّبِيِّ (ص) وَ عَلَى مَلَائِكَةِ اللهِ وَ أَنْبِيَائِهِ فَلَمْ يُسْمَعْ مُتَكَلِّمٌ قَطُّ قَبْلَهُ وَ لَا بَعْدَهُ أَبْلَغُ فِي مَنْطِقٍ مِنْهُ ثُمَّ قَالَ أَمَّا بَعْدُ فَانْسُبُونِي فَانْظُرُوا مَنْ أَنَا ثُمَّ ارْجِعُوا إِلَى أَنْفُسِكُمْ وَ عَاتِبُوهَا فَانْظُرُوا هَلْ يَصْلُحُ لَكُمْ قَتْلِي وَ انْتِهَاكُ حُرْمَتِي أَ لَسْتُ ابْنَ بِنْتِ نَبِيِّكُمْ وَ ابْنَ وَصِيِّهِ وَ ابْنِ عَمِّهِ وَ أَوَّلِ الْمُؤْمِنِينَ الْمُصَدِّقِ لِرَسُولِ اللهِ بِمَا جَاءَ بِهِ مِنْ عِنْدِ رَبِّهِ أَ وَ لَيْسَ حَمْزَةُ سَيِّدُ الشُّهَدَاءِ عَمِّي أَ وَ لَيْسَ جَعْفَرٌ الطَّيَّارُ فِي الْجَنَّةِ بِجِنَاحَيْنِ عَمِّي


Kisha akamhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu na kumtaja Mwenyezi Mungu kwa yale anayostahiki, na akamswalia Mtume Muhammad (s.a.w.w), na Malaika wa Mwenyezi Mugu na Manabii wake. Hawakuwahi kumsikia (mzungumzaji au) msemaji kabla yake au baada yake ambaye alikuwa ni mfasaha zaidi katika mantiki kuliko yeye. Kisha akasema: “Ama baada (ya kumhimidi Mwenyezi Mungu na kumtakia Sala na Salamu Mtume wake: Enyi watu! Niambieni Mimi ni nani? Kisha rudini kwenye nafsi zenu na zikemeeni (na mjihukumu wenyewe), Kisha tizameni, Je, inafaa kwenu nyinyi kuniua na kukiuka heshima yangu?! Je! mimi si mtoto wa binti ya Nabii wenu?! Je! mimi si mtoto wa walii na binamu ya Nabii wenu?! Je, mimi si mtoto wa yule aliyeamini kabla ya Waislamu wote?! Na zaidi ya yote, akamsadikisha Mtume wa Mwenyezi Mungu na kuukubali ujumbe aliokuja nao kutoka kwa Mola wake?! Je, Hamza Sayyid al-Shuhada sio ami yangu?! Je, Jafar al-Tayar - Mwenye kupaa kwa mabawa mawili Peponi – sioaAmi yangu?! Je, hamkusikia maneno ya Mtume (s.a.w.w) kuhusu mimi na ndugu yangu aliposema: Hawa wawili ni mabwana wa vijana wa Peponi”?!


أَ وَ لَمْ يَبْلُغْكُمْ مَا قَالَ رَسُولُ اللهِ لِي وَ لِأَخِي هَذَانِ سَيِّدَا شَبَابِ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَإِنْ صَدَّقْتُمُونِي بِمَا أَقُولُ وَ هُوَ الْحَقُّ وَ اللهِ مَا تَعَمَّدْتُ كَذِباً مُنْذُ عَلِمْتُ أَنَّ اللهَ يَمْقُتُ عَلَيْهِ أَهْلَهُ وَ إِنْ كَذَّبْتُمُونِي فَإِنَّ فِيكُمْ مَنْ لَوْ سَأَلْتُمُوهُ عَنْ ذَلِكَ أَخْبَرَكُمْ سَلُوا جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللهِ الْأَنْصَارِيَّ وَ أَبَا سَعِيدٍ الْخُدْرِيَّ وَ سَهْلَ بْنَ سَعْدٍ السَّاعِدِيَّ وَ زَيْدَ بْنَ أَرْقَمَ وَ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ يُخْبِرُوكُمْ أَنَّهُمْ سَمِعُوا هَذِهِ الْمَقَالَةَ مِنْ رَسُولِ اللهِ ص لِي‏ وَ لِأَخِي أَ مَا فِي هَذَا حَاجِزٌ لَكُمْ عَنْ سَفْكِ دَمِي


“Ikiwa mtasadikisha na kukubali maneno yangu haya ninayo yasema, basi kwa hakika hayo yote ni ya kweli na hakuna sehemu ndani yake yanapopingana hata kidogo, kwa sababu sijawahi kusema uwongo katika maisha yangu yote, tangu siku hiyo nilipotambua kwamba, Mwenyezi Mungu anawakasirikia na kuwachukia waongo na uongo unawarudia na kuwadhuru wao wenyewe”. “Na ikiwa hamuamini niliyoyasema (na mkanikadhibisha), basi kwa hakika baadhi ya Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) wangali hai, mnaweza kuwauliza. Waulizeni akina: Jabir bin Abdullah al-Ansari, Abu Saeed Khudhri, Sahl bin Saad Al-Saedi, Zaid bin Arqam, na Anas bin Malik. Watu hawa watakujulisheni kwani wamesikia maneno yote kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuhusu mimi na ndugu yangu, na tambueni kuwa sentensi hii moja inaweza kukuzuieni kuniua na kuimwaga damu yangu”.


فَقَالَ لَهُ شِمْرُ بْنُ ذِي الْجَوْشَنِ هُوَ يَعْبُدُ اللهَ عَلى‏ حَرْفٍ إِنْ كَانَ يَدْرِي مَا تَقَوَّلَ فَقَالَ لَهُ حَبِيبُ بْنُ مُظَاهِرٍ وَ اللَهِ إِنِّي لَأَرَاكَ تَعْبُدُ اللهَ عَلَى سَبْعِينَ حَرْفاً وَ أَنَا أَشْهَدُ أَنَّكَ صَادِقٌ مَا تَدْرِي مَا يَقُولُ قَدْ طَبَعَ اللهُ عَلَى قَلْبِكَ ثُمَّ قَالَ لَهُمُ الْحُسَيْنُ ع فَإِنْ كُنْتُمْ فِي شَكٍّ مِنْ هَذَا أَ فَتَشُكُّونَ أَنِّي ابْنُ بِنْتِ نَبِيِّكُمْ فَوَ اللهِ مَا بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَ الْمَغْرِبِ ابْنُ بِنْتِ نَبِيٍّ غَيْرِي فِيكُمْ وَ لَا فِي غَيْرِكُمْ وَيْحَكُمْ أَ تَطْلُبُونِّي بِقَتِيلٍ مِنْكُمْ قَتَلْتُهُ أَوْ مَالٍ لَكُمُ اسْتَهْلَكْتُهُ أَوْ بِقِصَاصِ جِرَاحَةٍ فَأَخَذُوا لَا يُكَلِّمُونَهُ فَنَادَى يَا شَبَثَ بْنَ رِبْعِيٍّ يَا حَجَّارَ بْنَ أَبْجَرَ يَا قَيْسَ بْنَ الْأَشْعَثِ يَا يَزِيدَ بْنَ الْحَارِثِ أَ لَمْ تَكْتُبُوا إِلَيَّ أَنْ قَدْ أَيْنَعَتِ الثِّمَارُ وَ اخْضَرَّ الْجَنَابُ وَ إِنَّمَا تَقْدَمُ عَلَى جُنْدٍ لَكَ مُجَنَّدٍ

Wakati huo, Shimr bin Dhil - Jawshan alitambua kwamba maneno ya Imamu Hussein (a.s) yanaweza kuwa na ufanisi na kubadilisha ari ya jeshi lake na kuwazuia kupigana dhidi yake, kwa hiyo akaamua kufanya jambo fulani ili aweze kuikatisha hotuba ya Imamu Hussein (a.s). Na hapo ndipo alipopiga kelele kwa sauti kubwa na kusema: “(Huyu Hussein) Anamwabudu Mungu kwa neno moja na hata hajui anasema nini?!” Habib bin Mudhahir alimjibu Shimr na kumwambia: “Naapa kwa Mungu! Kwa hakika mimi naona kuwa wewe unamuabudu Mwenyezi Mungu kwa maneno sabini, na ninashuhudia kwamba unasema ukweli kwamba huelewi anachokisema - Imamu Hussein (a.s) -, Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameupiga muhuri moyo wako”. Baada ya Habib bin Mudhahir kumjibu Shimr, Imamu Hussein (a.s) aliendelea na hotuba yake na kusema: “Ikiwa mna shaka na maneno ya Mtume (s.a.w.w) kuhusu mimi na ndugu yangu, je pia mnatilia shaka kuwa mimi ni mtoto wa binti wa Mtume wenu?! Naapa kwa Mwenyezi Mungu! Katika dunia yote iwe Mashariki au Magharibi, hakuna miongoni mwenu wala miongoni mwa wasio kuwa nyingi, Mtoto wa Nabii wenu asiyekuwa Mimi, Ole wenu! Je, nimemuua mtu miongoni mwenu kwamba, mnataka kuniua ili kulipiza kisasi?! Je, nimeharibu mali ya mtu yeyote? Au nimemsababishia mtu jeraha ambalo kwa hilo mnataka kulipiza kisasi”? Walikaa kimya mbele ya hotuba ya Imamu Huusein (a.s) na hakuna mtu yeyote aliyekuwa na jibu la kumjibu. Akanadi Imamu Hussein (a.s) akisema: “Ewe Shabath bin Rib'i! Na Ewe Hajjar bin Abjar, na Ewe Qays bin Ash'ath, na Ewe Zayd bin Harith! Je, sio nyinyi mlioniandikia barua ya mwaliko mkisema: matunda yetu yameiva, na miti yetu ni ya kijani kibichi na iliyokomaa. Utawasili al-Kufa na kukuta jeshi lililo na vifaa na ambalo liko tayari katika khidma! (Tunakusubiri, na katika kukusubiri tunahesabu dakika)?!”. (Watu hawa hawakuwa na jibu kwa maneno haya ya Imamu Hussein (a.s) isipokuwa kukanusha, “فقالو: لم نفعل” na ndipo waliposema: “Hatujakuandikia barua kama hiyo”! Imamu (a.s) ambaye alikabiliana na kukanusha kwao na akasema kwa mshangao mkubwa: (سبحان لله، بلى ولله لقد فعلتم عجبا!) Mnawezaje kukataa hilo, Wallahi, mliniandikia barua hiyo”).


فَقَالَ لَهُ قَيْسُ بْنُ الْأَشْعَثِ مَا نَدْرِي مَا تَقُولُ وَ لَكِنِ انْزِلْ عَلَى حُكْمِ بَنِي عَمِّكَ فَإِنَّهُمْ لَمْ يُرُوكَ إِلَّا مَا تُحِبُّ فَقَالَ لَهُ الْحُسَيْنُ لَا وَ اللهِ لَا أُعْطِيكُمْ بِيَدِي إِعْطَاءَ الذَّلِيلِ وَ لَا أَفِرُّ فِرَارَ الْعَبِيدِ ثُمَّ نَادَى يَا عِبَادَ اللهِ إِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَ رَبِّكُمْ أَنْ تَرْجُمُونِ أَعُوذُ بِرَبِّي وَ رَبِّكُمْ مِنْ كُلِّ مُتَكَبِّرٍ لا يُؤْمِنُ بِيَوْمِ الْحِسابِ.[۱۵[


Qais bin Al-Ash’ath (kwa upande wake) akamwambia Imamu Hussein (a.s): “Hatujui unachokisema, lakini ni kwa nini (usishuke na) kujisalimisha (kwa kutoa kiapo na bai’) kwa binamu yako?), kwa hakika atakutendea upendavyo, na hatakuletea usumbufu hata kidogo". Imamu Hussein (a.s) akamwambia: "Hapana, Wallah! sitakupeni mkono wangu (kwa kutoa bai’a na kujisalimisha kwenu) kama afanyavyo mtu dhalili! na wala sitakimbia kutoka katika uwanja wa vita na adui kama wakimbiavyo watumwa”. Kisha Imamu Hussein(a.s) akanukuu Aya Tukufu ya Qur'an inayosimulia kisa cha Nabii Musa (a.s) katika kukabiliana na ukaidi wa Mafir’auni. Akanadi kwa kusema: “Enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Najikinga kwa Mola wangu na Mola wenu ili msinirujumu (kutokana na kukataa kwenu kukubali maneno yangu). Najikinga kwa Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi kutokana na kila mwenye kiburi na muasi asiyeamini (Siku ya Hesabu) Siku ya Kiyama”. [16]

Hotuba ya pili

Allama Majlisi amenukuu katika kitabu chake cha Bihar al-Anwar akinukuu kutoka katika kitabu cha Manaqib cha Ibn Shahrashub hotuba nyingine ya Imamu Hussein kwa jeshi la Omar bin Sa’d katika siku ya Ashura. [17] Hotuba hii ya Imamu Hussein ilitokana na kutonyamaza askari wa Omar bin Sa’d na kutokuwa tayari kusikiliza maneno yake. Imamu Hussein alisema: Nyinyi hamsikilizi maneno yangu kwa sababu matumbo yenu yamejaa mali ya haramu na mioyo yenu imepigwa muhuri wa ukatili na roho mbaya. [18]