Nenda kwa yaliyomo

Fatima binti ya Imamu Hassan (a.s)

Kutoka wikishia
Angalia hapa kwa ajili ya matumizi mengine ya Fatima ili kuondoa utata.

Fatima binti ya Imamu Hassan (a.s) (Kiarabu: فاطمة بنت الحسن (ع)) ni mke wa Imamu Sajjad (a.s) na mama wa Imamu Muhammad Baqir (a.s). Fatima ni katika wapokezi wa hadithi na Imam Swadiq (a.s) amesema kuhusiana naye kwamba: Alikuwa mmoja wa wanawake waumini, mchaji Mungu, mkarimu, mtu wa mambo ya kheri na Mwenyezi Mungu anawapenda watu wanofanya mambo ya kheri. Fatima alikuweko katika tukio la Karbala na alichukuliwa mateka baada ya tukio hilo.

Utambulisho

Fatima Ummu Abdallah, [1] baba yake ni Imam Hassan (a.s) na mama yake ni Ummu Is’haq binti ya Talha bin Ubaydullah al-Taymi, [2]. Kuniya zake zingine ni Ummu Muhammad, [3] au Ummu Abduh. [4] Jabir anasema katika riwaya moja kwamba, ameona majina ya mama wa Maimamu katika Sahifa ya Fatima. Katika hadithi hii, yeye anamtambua Ummu Abdallah binti wa Imamu Hassan bin Ali bin Abi Talib kuwa ni mama wa Imamu Baqir (a.s). [5]

Yeye ni katika wapokezi wa hadithi na katika vitabu vya hadithi kumenukuliwa hadithi kutoka kwa Fatima bin al-Hassan kutoka kwa baba yake Imam Hassan (a.s). [6] Imam Sadiq (a.s) amesema kuhusiana na daraja yake kwamba: Alikuwa mmoja wa wanawake waumini, mchaji Mungu, mkarimu, mtu wa mambo ya kheri na Mwenyezi Mungu anawapenda watu wanofanya mambo ya kheri. [7] Katika vyanzo vya historia hakujaelezwa mwaka alioaga dunia wala sehemu aliyozikwa.

Kufunga ndoa

Fatima Ummu Abdallah alifunga ndoa na Imamu Sajjad (a.s) ambaye ni binamu yake na hii ilikuwa ndoa ya kwanza baina ya watu wa familia ya Alawi (watu kutoka katika ukoo wa Ali bin Abi Talib (a.s). [7] Imenukuliwa katika Nasikh al-Tawarikh: Fatima ni mke pekee wa daima wa ndoa ya daima wa Imamu Sajjad (a.s). [9] Kuolewa Fatima na Ali bin al-Hussein (a.s) kulipelekea kizazi chao kutoka upande wa Imamu Baqir (a.s) na kuendelea iwe ni kupitia mama wa Imamu Hassan Mujtaba (a.s) na kwa upande baba iwe ni kupitia kwa Imamu Hussein (a.s). Ndoa hii ilipelekea Imamu Baqir (a.s) apewe lakabu ya Hashimi baina ya Hashimiyyun, Alawi baina ya Aalwiyyun au Fatimi baina ya Fatimiyyun. [10]

Matunda ya ndoa hii yalikuwa kuzaliwa mtoto mwingine kwa jina la Abdallah, [11] ambaye kutokana na uzuri na ujamali pamoja na ung’avu aliokuwa nao alipewa lakabu ya Bahir yenye maana ya kung’ara. [12] Abdallah alikuwa ni mkubwa kwa Imamu Muhammad Baqir (a.s) na alikuwa msimamizi wa wakfu za Mtume (s.a.w.w) na Imamu Ali (a.s). [13]

Kuweko katika tukio la Karbala

Fatima bint al-Hassan alikuweko katika tukio la Karbala na alichukuliwa mateka pamoja na manusura wengine wa familia ya Imamu Hussein (a.s). [14]

Rejea

Vyanzo

  • Amīn, al-Sayyid Muḥsin al-. Aʿyān al-Shīʿa. Edited by Ḥasan Amīn. Beirut: Dār al-Tʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, [n.d].
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Tahdhīb al-tahdhīb. Beirut: Dār Ṣādir, [n.d].
  • Ibn ʿAsākir, ʿAlī b. al-Ḥasan. Tārīkh madīnat Dimashq. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Fikr, 1415 AH.
  • Khoei, Sayyid Abū l-Qāsim al-. Muʿjam rijāl al-ḥadīth. Najaf: Muʾassisat al-Khoei al-Islāmīyya, [n.d].
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Uṣūl al-Kāfī. Tarjuma-yi Ḥasan Ḥasanzāda Amulī. Qom: Qāʾim Āl-i Muḥammad, 1387 Sh.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār al-jāmiʿa li-durar akhbār al-aʾimmat al-aṭhār. Edited by a group of authors. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿala l-ʿibād. Edited by Muʾassisat Āl al-Bayt. Qom: al-Muʾtamar al-ʿĀlamīyya li-alfīya al-Shaykh al-Mufīd, 1372 Sh.
  • Qummī, Shaykh ʿAbbās. Muntahā l-āmāl. Qom: Muʾassisat Intishārāt-i Hijrat, [n.d].