Fatuma binti Ali (a.s)

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Fatima binti Ali)

Fatma binti Ali (a.s) (Kiarabu: فاطمة بنت علي بن أبي طالب) (aliaga dunia 117 Hijiria) alikuwa mmoja wa mateka wa Karbala na mmoja wa wapokezi wa hadithi. Muhammad bin Abi Said bin Aqil mume wa Fatma aliuawa shahidi katika tukio la Karbala. Fatma binti Ali alikuweko katika tukio la Karabala na baada ya kuuawa shahidi Imamu Hussein (a.s) alichukuliwa mateka pamoja na manusura wengine wa kafila na msafara wa Imamu Hussein (a.s).

Fatma amepokea na kusimulia hadithi kutoka kwa baba yake, Asma bint Umais, Umama binti Abi al-A's, Ummu al-Hassan binti ya Imamu Ali, Imamu Hassan na wengineo. Kadhalika Harith bin Ka'ab al-Kufi, Abdul-Rahman bin Abi Naim al-Bajali, 'Ubayd Allah b. Bashir al-Ju'fi, Musa al-Juhani, Abu Basir wamenukuu riwaya na hadithi kutoka kwake. Hadithi zilizonukuliwa kutoka kwake maudhui zake ni za kiitikadi, kifiq'h na kiakhlaq (kimaadili).

Fatma bint Imam Ali (a.s) amenukuu hadithi ya Manzila na Radd al-Shamsh. Abu Mikhnaf amenukuu tukio la Karbala kutoka kwa Fatma bint Ali kupitia kwa mtu mmoja.

Nasaba

Fatma ni binti wa Ali bin Abi Talib na mama yake ni Ummu Walad. [1] Aliolewa na Muhammad bin Abi Said bin Aqil na akamzalia binti aliyeitwa Hamida. [2]

Muhammad bin Abi Said, mume wa Fatma aliuawa shahidi katika tukio la Karbala [3] na Fatma akaolewa na Said bin Aswad bin Abi al-Bahtari [4] na akamzalia Barzah na Khalid. [5] Baada ya Said, Fatma alikuja kuolewa na Mundhir bin Ubayda bin Zubayr [6] na akazaa naye watoto wawili ambao ni Othman na Kabra. [7] Fatma baada ya Mundhir alikuwa hai [8] na aliaga dunia mwaka 117 Hijiria. [9]

Hadithi

Fatma amepokea na kusimulia hadithi kutoka kwa baba yake, [10] Asma bint Umais, [11] Umama binti Abi al-A's, [12] Ummu al-Hassan binti ya Imamu Ali, [13] Imamu Hassan [14] na wengineo. Kadhalika Harith bin Ka'ab al-Kufi, Abdul-Rahman bin Abi Naim al-Bajali, 'Ubayd Allah b. Bashir al-Ju'fi, [15] Mussa al-Juhani, [16] Issa bin Othman, [17] Abu Basir [18] na kadhalika wamenukuu riwaya na hadithi kutoka kwake. Hadithi zilizonukuliwa kutoka kwake aghalabu maudhui zake ni za kiitikadi, [19] kifiq'h [20] na kiakhlaq (kimaadili). [21]

Fatma bint Imam Ali (a.s) amenukuu hadithi ya Radd al-Shamsh [22] na Manzila. [23] Inaelezwa kuwa, Nasai na Ibn Majah wamenukuu hadithi kutoka kwake. [24]

Tukio la Karbala

Fatma alikuwepo katika tukio la Karbala na alipelekwa Damascus pamoja na Zainab (a.s) na mateka wengine [25] Katika kikao cha Yazid, mtu mmoja kutoka kwa watu wa Syria alimwomba Yazid bin Muawiyah ampatie Fatma ili amfanye kanizi wake. Ombi hilo lilikabiliwa na jibu kali kutoka kwa Bibi Zaynab (a.s). [26] Abu Mikhnaf aliripoti tukio hili kutoka kwa Fatma lakini kupitia kwa Harith bin Ka'b. [27]

Pia, Fatma amezungumzia kuhusu kutendewa mema na Nu'man bin Bashir katika njia ya kutoka Damascus kwenda Madina na mateka wa Karbala. Wakati msafara wa mateka wa Karbala ulipofika Madina, Fatma binti Ali, alimwambia dada yake Zainab: Mtu huyu wa Sham (Nu'man bin Bashir) alikuwa na wema na muamala mzuri kwetu sisi, je, unataka tumpe kitu? Zainab akasema: "Wallahi! hatuna cha kumpa isipokuwa mapambo yetu." Kisha wale wawili wakatuma bangili zao na vikuku vya miguu kwa Nu'mani na kumwomba msamaha. Lakini Nu'mani hakukubali, akasema:

Lau niliyoyafanya yangekuwa kwa ajili ya dunia, mapambo yenu na kidogo zaidi hayo yangenifurahisha, lakini Wallahi sikufanya haya isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na ukaribu wenu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.[28]

Mahalati katika kitabu cha Riyahin al-Sharia ameelezea kushangazwa kwake juu ya kutokuwa mashuhuuri Bwana huyu katika vitabu vya Rijaal vya Kishia. [29]

Rejea

Vyanzo

  • Abū Mikhnaf. Waqʿat al-ṭaff. Third edition. Qom: Daftar al-Nashr al-Islāmī, 1417 AH.
  • Barqī, Aḥmad b. Muḥammad al-. Rijāl. Tehran: Intishārāt-i Dānishgāh-i Tehran, 1383 Sh.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Wasāʾil al-Shīʿa. Qom: Muʾassiast Āl al-Bayt, 1409 AH.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Beirut: Dār al-Jail, 1412 AH.
  • Ibn al-Jawzī, ʿAbd al-Raḥmān b. ʿAlī. Al-Muntaẓam fī tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Qādir ʿAṭāʾ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1412 AH.
  • Ibn Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Al-Kāmil fī al-Tārīkh. Beirut: Dār al-Ṣādir, 1385 AH.
  • Ibn Athīr, ʿAlī b. Muḥammad. Usd al-ghāba fī maʿrifat al-ṣaḥāba. Beirut: Dār al-Fikr, 1409 AH.
  • Ibn Ḥabīb al-Baghdādī. Al-Muḥabbar. Edited by Ilse Lichtenstaedter. Beirut: Dār al-Āfāq al-Jadīda, [n.d].
  • Ibn Ḥazm. Jumhurat ansāb al-ʿarab. Edited by Lujnat min al-ʿUlamā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1403 AH.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad b. Manīʿ al-Baṣrī. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Qādir ʿAṭāʾ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1990.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1365 Sh.
  • Maḥallātī, Dhabīḥ Allāh. Rayāḥīn al-sharīʿa. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, [n.d].
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Second edition. Beirut: Muʾassisat al-Wafāʾ, 1404 AH.
  • Maqrizī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Imtāʿ al-asmāʾ. Edited by Muḥammad ʿAbd al-Ḥamīd al-Namīsī. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1420 AH.
  • Nūrī, Mīrzā Ḥusayn al-. Mustadrak al-wasāʾil. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1408 AH.
  • Ṣāliḥī al-Shāmī, Muḥammad b. Yūsuf al-. Subul al-hudā wa al-rashād fī sīrat khayr al-ʿibād. Edited by ʿĀdil Aḥmad ʿAbd al-Mawjūd. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1414 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abū l-Faḍl Ibrāhīm. Beirut: Dār al-Turāth, 1387 AH.