Nenda kwa yaliyomo

Asma bint Umais

Kutoka wikishia
Maqam Asma bint Umais katika Babu Aswaghir huko Syria

Asma bint Umais (Kiarabu: أسماء بنت عميس) (ambaye alifariki baada ya mwaka wa 38 Hijiria), alikuwa ni mmoja wa masahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Naye ndiye aliyemsaidia Imam Ali (a.s) kuiosha maiti ya bibi Fatima (a.s). Asma hapo mwanzo alikuwa ni mke wa bwana Jafar bin Abi Talib, na baada ya Jafar kufa shahidi, aliolewa na Abu Bakr bin Abi Quhafa. Baada ya kufariki Abu Bakar, bibi Asma aliolewa na Imam Ali (a.s). Watoto aliowazaa bibi Asma ni; Abdullah bin Jafar (mume wa bibi Zainab (a.s)) na Muhammad bin Abi Bakar ambaye baadae alikuwa ni wakala wa Imam Ali (a.s) huko Misri.

Kwa mujibu matakwa ya wosia wa bibi Fatimah (a.s), bibi Asma pamoja na Imam Ali (a.s), ndiwo waliochukuwa jukumu la kuuosha mwili wa bibi Fatimah (a.s). Pia yeye ndiye aliyetengeneza la bibi Fatimah (a.s), likiwa ndio jenela kwanza katika Uislamu. Alitengeneza jeneza hilo ili kuuhifadhi mwili bibi Fatimah usionekane. Pia kwa mujibu wa riwaya, yeye ndiye aliyekuwa karibu ya Fatimah akiwa dakika zake za mwisho za maisha yake. Naye ndiye aliyeripoti na kunukuu jinsi ya Hassan na Hussein (a.s) pamoja na baba yao Ali (a.s) walivyokabiliana na mwili wa Fatima (a.s). Asma alikuwa mmoja wa Waislamu wa mwanzo walikuwemo katika harakati za kuhama. Yeye akiwa pamona na mumewe Jafar alihamia Habasha (Ethiopia) na baadae kuhamia Madina. Bibi Asma amenukuu na kusimulia Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w).

Wasifu wa maisha yake

Asma alikuwa ni binti wa Umais bin Ma'ad. Kabila la baba la ni Bani Khath-am, mama yake ni Hind bint Aoun.[1] Dada zake ni:

  • Salma bint Umais ambaye alikuwa ni mke wa bwana Hamza bin Abdul Muttalib.
  • Dada yake wa pili kwa upande wa mama yake, ni Maimuna aliyekuwa mke wa bwana Mtume (s.a.w.w).[2]

Asma aliolewa na Ja’afar ambaye ni ndugu wa Ali bin Abi Talib (a.s), yeye alikuwa ni miongoni mwa watu wa mwanzo waliosilimu, yasemekana kuwa yeye alisilimu kabla ya Mtume (s.a.w.w), kuweka kuweka nanga kwenye nyumba ya bwana Arqam.[3] Mnamo mwaka wa tano Hijiria, Asma[4] yeye pamoja na mumewe walifunga safari ya kuhamia Habasha (Ethiopia),[5] na mnamo mwaka saba Hijiria alihamia Madina. [6] Baada ya mumewe kufa shahidi mnamo mwaka wa nane Hijiria, katika mapambano ya vita Mu-utah,[7] bibi Asma aliolewa na Abu Bakar, na baada ya hapo akaolewa na Imam Ali (a.s).[8] baadhi ya riwaya kutoka Imam Sadiq (a.s), zimemhisabu bibi Asma kuwa ni miongoni mwa wanawake wa Peponi.[9]

Uhusiano baina ya bibi Asma na bibi Fatima (a.s)

kwa mujibu wa wosia wa fatimah (a.s), bibi Asma akifungamana na bwana Ali bin Abi Talib ndiye aliyeukosha mwili wa Fatimah (a.s).[10] kulingana na riwaya za upande wa madhehebu ya shia, ni kwamba; jeneza la kwanza kabisa katika uislamu lilikuwa na jeneza lilitengenezwa na bibi asma kwa ajili ya mwili wa bibi fatimah (a.s). imeelezwa ya kwamba pale fatimah (a.s) alipokuwa mgonjwa, alimuomba bibi Asma pindi atakapofariki dunia, asiuweke mwili wake juu ya jeneza lisislo na hifadhi, kwa hiyo Asma akamtengenezea jeneza lenye hifadhi kamili linalofanana na jeneza aliloliona huko Habasha. na Fatimah (a.s) alifurahi sana baada ya kuliona jeneza hilo.[11] [angalizo 1] pia, kwa mujibu wa maelezo ya riwaya, yeye ndiye alikuwa pembeni mwa Fatimah (a.s) katika saa za mwisho za maisha yake. pia bibi Asma ndiye aliyeripoti jinsi Hassan na Hussein (a.s) na baba yao Ali (a.s) walivyokabiliana na mwili wa Fatimah (a.s).[12] vilele harakati za maombolezo ya kifo cha Fatimah (a.s), zimenukuliwa kupitia riwaya na nukukuu za bibi Asma.[13]

Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya ni kwamba; Bibi Asma pia alishiriki kwenye sherehe ya ndoa baina ya Imam Ali na bibi Fatima (a.s).[14] Pia kulingana na baadhi ya riwaya, bibi Asma alikuwa ndiye mkunga wa bibi Fatima (a.s) katika nyakati za kujifungua.[15] Kwa jinsi maelezo ya bwana Ali Ibn Isa Arbili mwanazuoni wa Kishia wa fani ya akida (mwanatheolojia) wa karne ya 7 Hijiria, anamesema kwamba; yaonekana kuwa kumetokea makosa katika kurekodi hadithi zinazohusiana na bibi Asma, yaani kuna mchanganyo ulifanyika baina ya Asma binti Yazid Ansari na Asma binti Umays, kwa sababu ndoa ya Fatima ilikuwa imefanyika mwaka wa 2 au 3 wa mwandamo, hali ya kwamba, Asma binti Umays hadi kutekwa kwa Khabar (mwaka 7 wa mwandamo) bado alikuwa yupo Habasha.[16] Arbili pia anaona kwamba kulitokea makosa kati ya Asma na Salma bint Umays, ambaye ni mke wa Hamza. Makosa hayo yalitokea kwa sababu Asma alikuwa ni maarufu zaidi kuliko Salma, ndiyo maana simulizi za riwaya hizo zikanasibishwa kwake, au labda mmoja kati ya wasimulizi alikosea katika kunukuu riwaya hizo, na wengine wakamfuata katika nukuu hizo[17][Maelezo 2]

Pia Asma alikuwa pembeni mwa Mtume (s.a.w.w), pale Mtume (s.a.w.w) alipokuwa akivuta pumzi zake za mwisho.[18]

Kunukuu hadithi

Asma amesimulia Hadithi kadhaa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w)[19] Pia, wanawe ambao ni Abdullah, Saeed bin Musayyib, Urwa bin Zubair na wengineo wamenukuu kutoka kwake.[20]Fatimah binti ya Ali (a.s), amenukuu kutoka kwake mbili maarufu ambazo ni Hadithi ya Manzlah[21] na Hadithi ya Raddul Shams.[22]

Ahmed bin Abi Yaqub, mwanahistoria wa karne ya tatu, ameashiria kuwepo kwa kitabu cha Asma ambacho kilikuwa na nukuu za maneno ya Mtume (s.a.w.w) ndani yake.[23]

Watoto wake

Watoto aliowazaa Asma ni; Abdullah, Muhammad na Aoun kupitia mumewe Jafar bin Abi Talib.[24] Kwa upande mwengine, alimzaa Muhammad bin Abi Bakr kupitia mumewe Abu Bakar,[25] ambaye alikuwa wakala wa Imam Ali (a.s) huko Misri.[26] Kwa upande wa Imamu Ali (a.s) alipata mtoto aliyejulikana kwa jina la Yahya[27] ambaye alifariki udogoni.[28]

Kifo chake

Ibn Kathir ambaye ni mwanahistoria wa Damascus wa karne ya 8 Hijiria, ameorodhesha tukio la kifo cha bib Asma katika orodha ya matukio ya mwaka wa 38 Hijiria.[29] Ila baadhi ya vyanzo vya historia, vimeelezea kuwa, kifo chake kilitokea baada ya kifo cha Imam Ali (a.s) kilichotokea mnamo mwaka wa 40 Hijiria.[30] kuna Kaburi fulani linalohusishwa naye katika mava ya Babu Al-Saghir ilioko huko Damascus.[31]

Rejea

  1. Ibn Kalbi, Nasab Ma'ad Waliyaman Al-Kabir, 1408 AH, juz. 1, uk. 356-358.
  2. Ibn Kalbi, Nasab Ma'ad Waliyaman Al-Kabir, 1408 AH, juz. 1, uk. 356-358.
  3. Ibn Saad, Tabaqat Al-Kubari, 1410 AH, juz. 8, uk. 219.
  4. Maqrizi, Amtaul-asmai, 1420 AH, juz. 9, uk. 116.
  5. Ibn Hisham, Al-Sirah al-Nabawiyyah, Dar al-Maarifah, juz. 1, uk. 323.
  6. Ibn Abd al-Barr, al-Istiyab, 1412 AH, juz. 1, uk. 242.
  7. Ibn Saad, Tabaqat Al-Kubari, 1410 AH, juz. 8, uk. 219.
  8. Ibn Abd al-Barr, al-Estiyab, 1412 AH, juz. 3, uk. 1784-1785.
  9. Sheikh Sadouq, Al-Khiswal, 1362 S, juz. 2, uk. 363.
  10. Balazri, Ansab al-Ashraf, 1959 AH, juz. 1, uk. 405.
  11. Erbali, Kashf al-Ghumah, 1381 H, juz. 1, uk. 503.
  12. Erbali, Kashf al-Ghumah, 1381 H, juz. 1, uk. 500-501.
  13. Tazama: «روضه و توسل بسیار جانسوز_ویژه فاطمیه»، Payghah khaymeghah.
  14. Tazama: Ganji Shafi'i, Kifayyah al-Talib, Dar Ihya Tarath Ahl al-Bayt, uk. 306; Erbali, Kashf al-Ghumah, 1381 H, juz. 1, uk. 365-366.
  15. Erbali, Kashf al-Ghumah, 1381 H, juz. 1, uk. 551.
  16. Erbali, Kashf al-Ghumah, 1381 H, juz. 1, uk. 373.
  17. Erbali, Kashf al-Ghumah, 1381 H, juz. 1, uk. 366-367.
  18. Balazri, Ansab al-Ashraf, 1959 AH, juz. 1, uk. 545.
  19. Hamidi, Al-MUs'nad, 1996, juz. 1, uk. 328; Waqidi, al-Maghazi, 1409 H, juz. 2, uk. 766.
  20. Dhahabi, Sir ila'am al-Nabilah, 1427 H, juz. 3, uk. 519.
  21. Ibn Abd al-Barr, al-Estiyab, 1412 H, juz. 3, uk. 1097.
  22. Huru Amili,Ith'bat al-hudaa, 1425 H, juz. 1, uk. 414.
  23. Yaqoubi, Tarikh Al-Yaqoubi, Dar Sadir, juz. 2, uk. 101.
  24. Ibn Saad, Tabaqat Al-Kubari, 1410 H, Juz. 8, uk. 219.
  25. Ibn Abd al-Barr, al-Estiyab, 1412 H, uk. 1784-1785.
  26. Tabari, Tarikh al-Umam wal-Muluk, 1387 H, juz. 4, uk. 555-556.
  27. Ibn Abd al-Barr, al-Estiyab, 1412 H, uk. 1784-1785.
  28. Abulfaraj Esfahani, Maqatil al-Talibiin, Dar al-Maarifah, uk. 37.
  29. Ibn Kathir, al-Bidaya wa al-Nahiya, 1407 H, juz. 7, uk. 318.
  30. Ibn Hajr Asqlani,Taqrib al-Tahdhib, 1406 H, uk. 743.
  31. Qaidan, Amakin ziyaratii siyahatii Syria 1387 S, uk. 105.

Vyanzo

  • Abū l-Faraj al-Iṣfahānī, ʿAlī b. al-Ḥusayn. Maqātil al-ṭālibīyyīn. Edited by Sayyid Aḥmad al-Ṣaqar. [n.p]. 1959 CE.
  • Āmilī, Muḥammad b. Ḥasan. Ithbāt al-hudāt bi l-nuṣūṣ wa al-muʿjizāt. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī, 1425 AH.
  • Amīn, al-Sayyid Muḥsin al-. Aʿyān al-Shīʿa. Edited by Ḥasan Amīn. Beirut: Dār al-Tʿāruf li-l-Maṭbūʿāt, 1403 AH.
  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Muḥammad Ḥamīd Allāh. Cairo: 1959.
  • Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Siyar aʿlām al-nubalāʾ. Edited by Shuʿayb al-Arnaʾūt. Beirut: 1404 AH.
  • Encyclopedia of Islam. New Edition. Leiden, 1956
  • Ḥākim al-Nayshābūrī. Muḥammad b. ʿAbd Allāh al-. Al-Mustadrak ʿala l-ṣaḥīḥayn. Hyderabad Deccan: 1341 AH.
  • Ḥamīdī, ʿAbd Allāh. Al-Musnad. Edited by Ḥabīb al-Raḥman Aʿzamī. Hyderabad Deccan: 1380-1382 AH.
  • Ibn Isḥāq, Muḥammad. Al-Sīyar wa al-maghāzī. Edited by Suhayl Zukār. 1st edition. Beirut: Dār al-Fikr, 1978.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Taqrīb al-tahdhīb. Edited by ʿAbd al-Wahhāb ʿAbd al-Laṭīf. Beirut: 1395 AH.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad. Al-Ṭabaqāt al-kubrā. Beirut: Dār al-Ṣādir, [n.d].
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Beirut: Dār al-Jail, 1412 AH.
  • Ibn Kalbī, Hisham b. Muḥammad. Nasab al-muʿid wa Yaman al-kabīr. Edited by Ḥasan Nājī. Beirut: ʿĀlam al-Kutub, 1408 AH.
  • Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Tabriz: 1381 AH.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Cairo: 1380 AH.
  • Ibn Qutayba al-Dīnawarī, ʿAbd Allāh b. Muslim . Al-Maʿārif. Edited by Tharwat ʿAkkāsha. Cairo: 1388 AH/1969 CE.
  • Ibn Hishām, ʿAbd al-Malik. Al-Sīra al-nabawīyya. Edited by Muṣṭafā al-Saqā. Cairo: 1355 AH/1936.
  • Ganjī al-Shāfiʿī, Muḥammad b. Yūsuf al-. Kifāyat al-ṭālib. Edited by Muḥammad Hādī Amīnī. Tehran: 1404 AH.
  • Kashshī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Ikhtīyār maʿrifat al-rijāl known as Rijāl al-Kashshī. Edited by Ḥasan Muṣṭafawī. Mashhad: 1348 Sh.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Muʾassisa al-Wafaʾ, 1403 AH.
  • Mizzī, Yūsuf b. ʿAbd al-Raḥmān al-. Tuḥfat al-ashrāf. Mumbai: 1400 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Khiṣāl. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: 1362 Sh.
  • Ṣafdī, Khalīl b. Ībak. Al-Wāfī bi l-Wafīyāt. Edited by Fānās. Beirut: 1401 AH/1981.
  • Qummī, Shaykh ʿAbbās. Muntahā al-āmāl. Aʿlām al-Tuqā, Summer 1382 Sh. [n.p].
  • Wāqidī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Al-Maghāzī. Edited by Marsden Jones. London: 1996 CE.
  • Yaʿqūbī, Aḥmad b. Abī Yaʿqūb al-. Tārīkh al-Yaʿqūbī. Beirut: Dār Ṣādir, [n.p].