Aya ya Maharimu

Kutoka wikishia
Aya ya 23 ya Surat al-Nisaa

Makala hii inahusianan na Aya ya maharimu katika Qur'ani. Ili kufahamu mafuhumu na maana ya kuwa haramu angalia makala ya maharimu.


Aya ya maharimu (Kiarabu: آية المحارم) ni Aya ya 23 ya Surat al-Nisaa ambayo inawatambulisha ndugu na watu wa nasaba ambao ni haramu kuoana nao. Katika Aya hii kumetambulishwa kundi la wanawake wa aina saba ambao kutokana na uhusiano wa nasaba, wanawake wa aina mbili ambao kutokana na kuchangia ziwa, na wanawake wa aina nne ambao kutokana na ndoa au uhusiano usio wa nasaba, ni haramu kuwaoa. Katika Aya ya 31 ya Surat al-Nur mashuhuri kama Aya ya Hijabu pia wametajwa na kuarifishwa baadhi ya maharimu.


Maandishi na tarjuma ya aya

Ni aya ya 23 ya surat al-Nisaa ambayo imetaja makundi ya wanawake ambao ni haramu kuwaoa.


حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ مِنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُمْ مِنْ نِسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُمْ بِهِنَّ فَإِنْ لَمْ تَكُونُوا دَخَلْتُمْ بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَنْ تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ إِنَّ اللَّهَ كَانَ غَفُورًا رَحِيمًا

Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipokuwa yale yaliyokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
(Quran: 4: 23)

Sababu ya kushuka aya hii

Sheikh Tusi anasema katika tafsiri yake ya Qur'an ya al-Tibyan Fi Tafsiri al-Qur'an sehemu ya Aya ya 23 ya Surat al-Nisaa inayosema: (وَحَلائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلابِكُمْ;Pia mmeharimishwa wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu), ya kwamba, katika zama na kipindi ambacho Mtume(s.a.w.w) alikuwa amemuoa Zaynab bint Jahash mke wa Zayd bin Haritha (mtoto wake wa kupanga) baada ya mwanawe huyo kuuawa katika vita vya Mutah, na washirikina wakaanza kusema na kunong'ona kuhusiana na hilo. [1]

Imekuja katika tafsiri Nemooneh ya kwamba, hatua ya Mtume ya kumuoa Zaynab binti Jahash ililenga kuondoa ada ya zama za ujahilia ambapo sheria zote za watoto halisi wa mtu zilikuwa zikitabikishwa (zikitekelezwa) pia kwa mtoto wa kupanga na kumuoa mke wa mtoto wa kupanga baada ya kufariki kwake dunia au kumpa talaka lilihesabiwa kuwa jambo baya na lisilopendeza. [2]

Maharimu

Makala asili: Maharimu na Maharimu wa kunyonya(Ridhwa'ah)

Kwa hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameharamisha kuoa aina kadhaa za wanawake. Na uharamu wao uko mafungu mawili: Fungu la Kwanza: Ni la uharamu wa milele, kwa maana ya kuwa hakuna mabadiliko; kama vile mtoto, dada, shangazi n.k. Fungu la Pili: Ni lile la uharamu wa muda; kama vile mke wa mtu mwengine ambapo akiachika mtu anaweza kumuoa n.k. Maharimu ni watu ambao kutokana na kuwa na uhusiano wa kindugu wanaweza kuangaliana na kudhirisha mapambo baina yao lakini ni haramu kuoana. [3] Aya ya maharimu inabainisha watu wenye uhusiano wa kinasaba (wa damu), wa sababu(usio wa nasaba) nyingine na wa kunyonya (ziwa moja) ambapo ni haramu kuoana nao. [4]

  • Uhusiano wa Nasaba (damu): Ni aina ya uhusiano wa kizazi baina ya watu. [5] Wanazuoni wa fikihi wakitegemea Aya hii wanasema kuwa, ni haramu kuoana aina saba ya wanaume na aina saba ya wanawake. [6] Kwa maana kwamba, kuna aina saba ya wanaume na aina saba ya wanawake ambao hawawezi kuoana, kwani kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu ni haramu.
  • Mama na bibi (nyanya); wa upande wa baba na wa upande wa mama. [7]
  • Binti na binti wa mtoto. [8]
  • Dada. [9]
  • Mtoto wa kaka (binti wa kaka), watoto, wajukuu na vitukuu, vilembwe na vinying'inya na kuendelea chini zaidi. [10]
  • Mtoto wa dada (binti wa dada) watoto, wajukuu na vitukuu, vilembwe na vinying'inya na kuendelea chini zaidi. [11]
  • Mama mdogo na mama wadogo wa baba na mama. [12]
  • Shangazi na mashangazi wa baba na mama. [13
  • Ridhwa'ah (kunyonya ziwa moja): Uharamu kutokana na kunyonya ziwa moja. Nasaba hii inapatikana kwa watoto wawili kunyonya ziwa na mwanamke ambaye si mama yake. Hivyo mtoto huyu ambaye amenyonya ziwa la mwanamke ambaye sio mama yake na mtoto ambaye amenyonya ziwa hilo hilo lakini yeye ni mama yake, wawili hawa wanakuwa maharimu kutokana na kuchangia ziwa kwa maana kwamba, hawawezi kuoana. [14] Katika Aya hii kumeashiriwa kuwa haramu kumuoa mama na madada wa kunyonya ziwa moja. [15] Wanazuoni wa fikihi wakitegemea hadithi kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) inayosema: Kila kile ambacho ni haramu kutokana na nasaba ni haramu pia kutokana na kuchangia ziwa." [16] Wanawake wote ambao wanaume wanameharamishiwa kuoana nao kutokana na nasaba, wanawake ambao ni maharimu kutokana na kunyonya ziwa moja nao pia ni haramu kuoana nao. [17]
  • Uhusiano usio wa nasaba: Maharimu wa uhusiano usio wa nasaba hujitokeza baada ya mke na mume kufunga ndoa ambapo, baadhi ya watu katika familia zao huwa haramu kuoana na baadhi ya ndugu za mume na mke ambao hawa wanatambuliwa kama maharimu wa uhusiano usio wa damu (nasaba). [18] Aya ya maharimu imeashiria aina nne ya wanawake wa aina hii ambao ni: Mama mkwe (mama wa mke) na kwenda juu, binti wa mke ambaye amefunga naye ndoa na akamuingilia, mke wa mtoto na kukusanya baina ya madada wawili. [19]

Nukta za kitafsiri

Kwa mujibu wa baadhi ya wafasiri, sehemu ya Aya inayosema: (وَأَن تَجْمَعُواْ بَيْنَ الأُخْتَيْنِ إِلاَّ مَا قَدْ سَلَفَ; Na (ni haramu) kuwaoa pamoja dada wawili isipo kuwa yale yaliyo kwisha pita), inaashiria nukta hii kwamba, kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja katika zama za ujahilia lilikuwa jambo la kawaida na watu ambao waliwahi kuwa na ndoa kama hii huko nyuma hawana makosa wala adhabu, lakini wanapaswa kumchagua mmoja kati ya dada hao wawili na kumuacha wa pili. [20]

Aya yenye kuhusiana

Makala asili: Aya ya Hijabu

Aya ya 31 ya Surat al-Nur ambayo ni mashuhuri kwa Aya ya Hijabu nayo sambamba na kubainisha baadhi ya maagizo kwa wanawake imewataja baadhii ya maharimu.


وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ… وَلا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلاَّ لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاء بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاء بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَى عَوْرَاتِ النِّسَاء وَلا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Na waambie Waumini wanawake… wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa
(Quran: 24: 31)