Aya ya Jilbab

Kutoka wikishia

Aya ya Jilbab (Kiarabu: آية الجلباب) Ni Aya ya 59 ya Surat al-Ahzab ambayo inawataka wanawake wajiteremshie Jilbab zao ili wasiudhiwe na wanaume. Katika Aya hii limetumika neno “Jalabib” ambalo ni wingi wa Jilbab. Jilbab inaelezwa maana yake ni nguo ambayo ni kubwa zaidi kuliko mtandio (kitambaa cha kichwa).

Fadhl bin Hassan Tabrasi, mmoja wa wafasiri wa Kishia anaamini kuwa, Aya hii ni makhsusi kwa wanawake huru ambao kwa kuvaa hijabu watofautishwe na wajakazi na mtu asiwaudhi na kuwafanyia ubaya na wengine wanaamini kwamba, Aya hii inajumuisha wanawake wote na inatawaka wanawake wote wafanye mambo kwa unyenyekevu na kwa kujistiri ili wasalimike na dhana mbaya na mtu asiwaudhi.

Sayyid Hussein Burujerdi mmoja wa Marajii Taqlidi na Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai, mmoja wa wafasiri wa Qur’an tukufu wa Kishia wanaamini kwamba, kwa mujibu wa Aya ya Jalbab, wanawake wanapaswa kujifunika nyuso zao. Mkabala na wao, Sheikh Ja’afr Sobhani na Sheikh Murtadha Mutahhari wanapinga hilo na wametosheka na mtazamo wa kufunika nywele tu.

Utambulisho, Andiko la Aya na Tarjumi

Aya ya 59 ya Surat al-Ahzab ambayo ndani yake kumezungumziwa aina ya hijabu inajulikana kwa jina la Aya ya Jalbab/Jilbab. [1]

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَن يُعْرَفْنَ فَلا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا


Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie jalbab zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.



(Quran: 33: 59)


Sababu ya Kushuka

Kwa mujibu wa yale yaliyoandikwa katika tafsiri ya Qumi ni kwamba, sababu ya kushuka ni kwamba, katika zama za Mtume (s.a.w.w) wanawake walipokuwa wakienda msikitini kwa ajili ya Swala ya Jamaa, baadhi ya vijana wa kiume walikuwa wakiketi katika njia wanayopita na kuwajumu na kuwafanyia maudhi. [2]

Maana ya Jilbab

Neno “Jalabib” ni wingi wa “Jilbab”. Raghib Isfahani ameandika, jilbab huitwa shati na mtandio; [3] lakini imekuja katika Maj’maa al-Bahrain kwamba: Jilbab ni vazi ambalo ni kubwa zaidi ya mtandio na dogo kuliko juba na joho na huvaliwa na wanawake na hufunika kuanzia kichwani mpaka katika vifua vyao. [4] Mustafa, mtambuzi wa maneno na islahi za Qur’an yeye anaamini kwamba, jilbab ni kitu kinachofunika nguo na kusitiri mwili na nguo kwa pamoja na ni chadori (juba la Kiirani) na juba ambalo linafunika mwili mzima wa mwanamke na huvaliwa juu ya nguo. [5]

Makusudio ya Kutambulika ni Nini?

Fadhl bin Hassan Tabarsi, mfasiri wa Qur’an wa Kishia wa karne ya sita Hijiria ametoa tafsiri ya maana mbili katika tafsiri yake ya Maj’maa al-Bayan kuhusiana na sehemu ya Aya ya Jilbab inayosema: (ذَلِكَ أَدْنَى أَن يُعْرَفْنَ فَلا يُؤْذَيْنَ ; Hivyo ni karibu zaidi kuweza kujulikana wasiudhiwe).

Wafasiri wengine waliofasiri Aya hii wamechagua moja kati ya tafsiri mbili hizi za Tabarsi:

  • Kwa mujibu wa tafsiri ya kwanza ambayo ni mtazamo wa Tabarsi: Makusudio ya kutambulika katika Aya hiyo ni kufahamika na kujulikana kuwa wao ni wanawake huru na sio wajakazi (watumwa wa kike) na kwa msingi huo wasihujumiwe; Kwani katika zama hizo, baadhi ya waliokuwa wakiwaudhi na kuwashambulia wanawake walikuwa wakifanya hivyo kwa wanawake wasio huru. Kadhalika baadhi ya wanafiki walikuwa wakiwahujumu wanawake huru na walipokuwa wakishtakiwa kwa kitendo hicho, walikuwa wakisema kuwa, “tulidhani ni (makanizi) wajakazi”. Kwa kitendo hicho, wanafiki wakawa wamepokonywa kisingizio chao. [6]
  • Tafsiri ya pili ambayo Tabrasi ameinasibisha kwa Abu Ali Habbani (mwana nadharia na mwanatheolojia wa Kimu’tazila (aliaga dunia 303 Hijria), anasema, makusudio ya kujulikana ni kwamba, ifahamike na kutambulika kwamba, wanawake hao ni watu wa kuvaa na kujisitiri kwa hijabu, ni wasafi na wenye heshima zao, ili wanaume mafasiki na wachafu wasiwafuate; kwani watu mafasiki wanapoona mwanamke amejistiri vizuri kwa vazi la heshima na ni mwenye kujiheshiu huwa hawamvamii na kumfanyia maudhi. [7] Allama Tabatabai na Murtadha Mutahhari wamechukua mtazamo huu. [8]

Matumizi ya Kifiq’h

Aya ya Jilbab imetumiwa pia katika mijadala na maudhui ya Kifiq’h. [9] Kwa mujibu wa Murtadha Mutahhari, wafasiri kama Zamakhshari na Fakhrurazi wamesema, maana ya Aya hii ni kwamba, ni wajibu kwa wanawake kufunika nyuso zao. [10] Allama Tabatabai pia ana mtazamo na uwelewa kama huu. [11] Kwa mujibu wa Shekhe Ja’afar Sobhani na Ayatullah Burujerdi nao wana mtazamo huu huu na wametumia hoja hii kwamba, kuteremsha jilbab ambako kumeamrishwa katika Aya hii, kiulazima ni kufunikwa sura yote. [12]

Murtadha Mutahhari na Ja’afar Sobani wamekataa ujengeaji hoja huo; kwa mujibu wa Mutahhari ni kwamba, Aya hii haibainishi mipaka ya vazi, bali inabainisha kwamba, wanawake Waislamu wafanye mambo kwa kujiheshimu na kwa unyenyekevu na kwamba, mavazi yao yasiwe na upande wa mapambo ya kidhahiri tu. Ameandika: “wasiudhiwe”, inaunga mkono mtazamo huu. [13] Ja’afar Sobhani pia akitumia ibara hii hii kama hoja ameandika, lengo la kuteremshia jilbab ni wanawake huru wafahamike na kutofautishwa na makanizi (wajakazi) na hivyo wasiudhiwe, lengo hili linapatikana kwa kufunika nywele. Kwa msingi huo, kufunika uso na sura sio lazima. [14]

Rejea

Vyanzo

  • Makarim Shirazi, Nashir, Kitab al-Nikah. Riset: Muhammad Ridha Hamidi dan Mas'ud Makarim, Qom: Madrasah Imam Ali bin Abi Thalib, cet. 1, 1424 HS
  • Muthahari, Murtadhawi, Majmueye Atsar, Teheran: Penerbit Sadra, 1390 S
  • Qomi, Ali bin Ibrahim, Tafsir al-Qomi, Riset dan editor: Thayib Musawi Jazairi. Qom: Dar al-Kitab, cet. 3, 1404 HS
  • Ragib Isfahabi, Husain bin Muhammad, Mufradat fi Gharib al-Quran, Riset: Shafwan Adnan Dawudi, Damaskus/Beirut: Cet. 1, 1412 HS
  • Subhani, Ja'far, Nidham al-Nikah fi al-Shariah al-Islamiah al-Ghara. Qom: Yayasan Imam Shadiq, 1375 S
  • Shubairi Zanjani, Sayyid Musa. Kitab al-Nikah, Qom: Yayasan Pazuhasyiye Ra'ye Pardaz, cet, 1, 1419 HS
  • Tabrasi, Fadhl bin Hassan, Majma' al-Bayan fi Tafsir al-Quran, Teheran: Nashir Khusru, cet. 3, 1372 S
  • Tabatabai, Sayyid Muhammad Hussein, al-Mizan fi Tafsir al-Quran, Qom: kantor Penerbit Islami, cet. 5, 1417 HS
  • Tarihi Fakhruddin, Majma' al-Bahrain, Riset: Saysid Ahmad Husseini, Teheran: Toko buku Murtadhawi, cet. 3, 1375 S
  • Tim Peneliti, Farhang Nameh Ulum-e Qurani, Qom: Lembaga Penelitian Ulum va Farhangg-e Islami, cet. 1, 1394 S