Nenda kwa yaliyomo

Aya ya Amman Yujiibu

Kutoka wikishia
Aya ya Amman Yujiibu

Aya ya Amman Yujiibu (Kiarabu: آية أمن يجيب) Ni sehemu ya Aya ya 62 ya Surat An-Naml inayo eleza ya kwamba; Mwenye Ezi Mungu ndiye msikivu pekee wa maombi anayetatua matatizo ya binadamu. Ibara ya Aya hiyo ni kama ifuatavyo: «اَمَّن یُّجیبُ المُضطَرَّ اِذا دَعاهُ وَ یَکشِفُ السُّوءَ؛ ; Je, yupo yule anayejibu kilio cha mwenye dhiki anapomwomba na kuyaondoa maovu; au kwa lugha nyengine: [Ni nani] anayemuitikia mwenye shida anapomwomba na kumwondolea matatizo yake?»

Kwa ujumla katika mila za Waislamu wengi, Aya hii hujulikana kwa jina la ‘Amman Yujiibu’. Pia Aya hii inashauriwa kusomwe wakati wa taabu na matatizo mabali mbali. Pia amali maalumu inayoitwa ‘Khatmu Amaan’ ambayo ni miongoni mwa mila zilizo enea miongoni mwa jamii za Waislamu wa Kishia. Kulingana na baadhi ya wafasiri wa Qur’ani, ibari hii inahisiana na dhana ya Tawhidi, ambapo Mwenye Ezi Mungu ndani ya ibara hii anawauliza washirikina; Je, yupo mbora anayejibu kilio cha mwenye dhiki kuliko Mungu Mwenyewe? Au je, yupo miongoni mwa miungu yenu anaye weza kufanya chochote katika suala hilo?

Kwa msingi wa baadhi ya Hadithi na maoni ya mafasiri wa Kishia kuhusiana na Aya hii ni kwamba: Aya hii inahusiana na Imamu Mahdi (a.s), ambayo ilishuka kuhusiana naye, na maana ya neno «mudhtarr» ni yeye (a.s). Lakini kuna kundi jengine la wafasiri waliosema kwamba; Imam Mahdi (a.s) ni mojawapo ya wahusika wa Aya hiyo, na kiuhalisia Aya inawahusu watu wote wenye dhiki, amabayo imekuja kuwaahidi kuwa maombi yao yatasikilizwa.

Nafasi ya Aya Hii Katika Mila na Tamaduni za Wanajamii

Kauli isemayo: «اَمَّن یُّجیبُ المُضطَرَّ اِذا دَعاهُ وَ یَکشِفُ السُّوءَ ; Je, ni nani anaye mjibu mwombaji mwenye dhiki na kumwondolea shida (zake hizo)?» Inapatikana katika Aya ya 62 ya Surat An-Naml. Katika lugha ya kawaida maneno haya hufasiriwa kama ni dua. Pia kuna amali maalumu iitwayo “Khatmu Amman Yujib” ni moja amali ya kawaida. [1] Bila shaka Aya yenyewe haina mtindo wa kidua, bali wanoitumia Aya hii kama ni dua, hushauriwa kuisoma kama ilivyo ‘Ya Man Yujibu Al-Mudhtarra Idhaa Da’ahu «یا مَنْ یجیبُ الْمُضْطَرَّ إِذا دَعاهُ» [2] au ‘Ya Man Yujibu Duaa Al-Mudhtarri «يَا مَنْ يُجِيبُ دُعَاءَ الْمُضْطَرِّ». [3]

Mirza Jawad Malaki Tabrizi amewashauri watu ambao wamepitiwa na mwezi wa Ramadhani bila ya kufanikiwa kupata mabadiliko katika hali zao, watafute msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia Aya hii, kwa ajili ya kupunguza ugumu na kujiboresha. [4]

Uhusiano Wake na Tauhidi

Katika Aya ya Amman yujiibu (اَمَّن یُّجیب): Mungu anatambuliwa kuwa ndiye chanzo pekee cha kuitikia maombi na kuondoa matatizo ya mwanadamu, jambo ambalo limepelekea dhana hii kuhusishwa moja kwa moja na dhana ya Tawhidi. [5] Kulingana na maoni ya Ayatullahi Makarim Shirazi, ni kwamba; Mungu katika Aya hii pamoja na Aya kadhaa zinazoanzia na «اَمَّنْ» ambayo ni ibara ya swali, ni dalili na ithibati za wazi za Tawhidi zlizokuja kwa njia ya maswali na kuwahukumu washirikina. [6] Hili ni swali la tatu kati ya maswali matano ambayo Mungu anawauliza washirikina, ambapo anawauliza ikiwa je, yule anayejibu maombi ya mwenye shida ni bora? Au miungu yenu ambao haina uwezo wa chochote? [7]

Nani Mhusika wa Neno Mudhtarru (مُضطَر)?

Katika maelezo ya baadhi ya Hadithi za Kishia kuhusiana na madhumuni ya neno Mudhtarru (مُضطَر) (mwenye shida), imeelezwa ya kwamba; Imamu Mahdi (a.s) ndiye Mudhtaruu aliye kusudiwa katika Aya hiyo. Kwa mfano, katika moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) iliyoorodheshwa katika kitabu cha tafsiri ya Qummiy, imesemekana kuwa; Aya ya 62 ya Suratu an-Naml inamzungumzia Qa’im Aalu Muhammad (a.s), ambaye ndiy mudhtarru halisi. Hadithi hiyo imeendelea kusema kwamba; Wakati ambao yeye atachukua hatua ya kusali na kuomba dua akiwa eneo la Maqamu Ibrahim, Mwenye Ezi Mungu atamjibu dua yake na baada ya yeye “kuondolewa ubaya unaomkabili” na (kupata ufumbuzi wa matatizo), hapo basi yeye atawekwa kuwa ni Khalifa wa ardhini humu. [8]

Nu’umani (aliyefariki mwaka 360 Hijiria) katika chake Al-Ghaibah, katika tafsiri ya Aya ya ‘Amma Yujibu”, ananukuu Hadithi kupitia kwa Muhammad bin Muslim kutoka kwa Imamu Baqir (a.s) akisema kuwa; Aya ya 62 ya Suratu An-Naml, imeshuka ikimzungumzia Imamu Mahdi (a.s) ambaye ataungwa mkono na Jibril pamoja na wafuasi wake 313, baada ya kudhihiri kwake huko Makka. [9]

Kulingana na maoni ya Sharif Lahiji (aliyefariki mwishoni mwa karne ya kumi na moja Hijria), ni kwamba; Kulingana na Hadithi kutoka kwa Imamu Sadiq na Imam Baqir (a.s), Aya hii imeteremshwa kuhusiana na Qa’im Aal Muhammad (a.s) (Imamu Mahdi). [10] Pia katika sehemu ya dua ya Nudba, Imam Mahdi (a.s) ameitwa kuwa ni mtu aliye katika hali ya dharura (Mudhtarru), ambaye dua zake ni zenye kujibiwa, ambapo mojo ya kipengele cha dua hiyo kinasema: «أَيْنَ الْمُضْطَرُّ الَّذِي يُجابُ إِذا دَعا؟ ; Yuwapi yule aliye katika hali ya dharura ambaye hujibiwa aombapo maombi yake?» [11]

Allama Tabatabai (aliyeaga dunia mwaka 1360 Shamsia), na Makarim Shirazi wamesema kwamba; kule Hadithi kuashisria suala la Imamu katika kubainisha sababu ya kushuka kwa Aya hii, kuna nia ya kutoa baadhi ya mifano hai ya wahusika wa Aya hii, na haina ya kumhusisha Imamu Mahdi peke yake kuhusiana na sababu za kushuka kwake, bali yeye ni kama moja ya mifano tu. Wafasiri hawa wanaenedelea kwa kusema kwamba; Aya hii watu wote wenye shida bila ya kukoma katika kiwango cha fulani. [12] Ali bin Ibrahim pia ana maoni ya kwamba; tafsiri hizo zilizo tolewa kuhusiana na Aya hii kupitia Hadithi hizo, ni maana ya batini ya Aya hiyo. [13]

Uhusiano kati ya Dharura (Kutokuwa na Hila) na Majibu ya Maombi

Baadhi ya wanazuoni wa Kishia kama vile Fadhlu bin Hassan Tabrisi (aliyefariki mwaka 548 Hijiria), Fathallah Kashani (aliyefariki mwaka 988 Hijiria) na Makarim Shirazi wameeleza katika tafsiri ya Aya ya 62 ya Surah An-Naml, wamesema kwamba; Mwenyezi Mungu anajibu maombi ya kila mtu; lakini kwa kuwa maombi ya mwenye dhiki ni yenye nguvu zaidi na yenye unyenyekevu zaidi, hii imepelekea kuwepo kwa haja na kukatikiwa na sababu za uokozi, ni sharti la kujibiwa kwa dua ya mwombaji. [14] Muhammad Sabziwari (aliyefariki 1368 Hijiria) na Allama Tabatabai pia wameeleza kuwa; haja na dharura iliyo ashiriwa katika Aya hiyo, ni ishara ya haja halisi inayo mfunganisha mja na Mola wake. [15] Kulingana na nadharia za wafasiri wa Kishia; Yule mwenye dhiki na dharura kali aliye tajwa katika Aya «Amejibu nani» , ni yule mtu ambaye mwenye dhiki juu ya jambo fulani, ambaye hana mashiko mengine yoyote anayotegemea isipokua kinga ya Mwenyezi Mungu peke yake. [16] Tha’alabi, [17] Zamakhshari, [18] Fakhru al-Razi, [19] na Baydhawi [20] ni miongoni mwa wanazuoni wa kutoka upande wa madhehebu ya Sunni waliokubaliana na maana hii ya Mudhtarru aliye tajwa ndani ya Aya hiyo.

Je, Kila Mwenye Shida Hujibiwa Maombi Yake?

Kwa mtazamo wa baadhi ya wanazuoni wa Kishia kama vile Fat’hullah Kashani, ni kwamba; neno Mudhtarru (مضطر) katika Aya hii hailiwaingizi watu wote katika mhimili wake; hii ni kwa sababu ya kwamba, kuna watu wengi walio katika hali ngumu ambao Mwenyezi Mungu hajajibu maombi yao kwa sababu hilo ni bora kwao, yaani kutojibu dua zoa ndio kheri kwao. [21] Zamakhshari, [22] Fakhru al-Razi, [23] Baidhawi, [24] na Alusi [25] ni miongoni mwa wanazuoni wa Kisunni wanakubaliana na maoni haya. Kulingana maoni ya Sharif Lahiji, ni kwamba; kiuhalisia maombi ya wote walio katika hali ngumu hujibiwa maombo yao, na ikiwa maombi ya mtu fulani hayakujibiwa, hiyo ni kwa sababu yay eye kuwa bado hajafikia kile kiwango cha kudharurika kisawasawa. [26]

Rejea

Vyanzo