Nenda kwa yaliyomo

Aya ya 216 katika Suratu Al-Baqarah

Kutoka wikishia

Aya ya 216 katika Suratu Al-Baqarah: ni Aya iliyokuja kuainisha na kufafanua wajibu wa Jihadi kwa Waislamu. Wachambuzi na wafasiri wa maandiko matakatifu ya Qur’ani, wanaeleza wakisema kuwa; wajibu huu unaoelezewa ndani ya Aya hii, ni Wajibu Kifai (wajibu wa kutosheleza). Kwa mujibu wa maoni ya wachambuzi na wafasiri mbali mbali mbali, ni kwamba; Aya hii imekuja kutoa hukumu hii ya jihadi, kutokana na utambuzi finyi alionao mwanadamu, kwa mara nyingi mwanadamu huchukulia baadhi ya masuala kuwa ni yenye madhara na yasio na faida maishani mwake; ilhali masuala hayo yana kheri na manufaa makubwa mno, na ni masuala msingi ndani ya maisha yake. Kinyume chake, mara kwa mara mwanadamu huyu huonekana kuvutiwa na masuala mengine; wakati ambapo, kiuhalisia, masuala hayo huwa ndiyo chanzo cha madhara na shari mbali mbali zinayomsibu mwanadamu.


Wafasiri wa Qur'ani, wakitegemea maudhui ya Aya hii, wamesema kwamba; ingawaje vita vya Jihadi vina ugumu na wala havipendezi mbele ya wengi miongoni mwa Waislamu, ila utekelezaji wa ibada hii huleta matokeo kadhaa mazuri yanayofidia usumbufu unaosababishwa na vita hivi. Ufafanuzi mwingine uliotolewa kuhusiana na Aya hii ni kwamba; kutokana na elimu ya binadamu kuwa na mipaka maalumu katika utambuzi wa mambo mbali mbali, hivyo basi elimu hii ya kibinadamu haitoshelezi katika kuandaa mfumo na mustakbali bora wa maisha ya mwanadamu. Hivyo basi, mwanadamu hana budi kuegemea ile elimu kamilifu isiyo na mipaka itokayo kwa Mola wake.


Wajibu wa Pamoja wa Jihadi kwa Waislamu (Faradhi ya Kifaya)

Aya ya 216 ya Suratu Al-Baqarah ni Aya maalumu inayojadili dhana ya Jihadi na hadhi yake, pamoja na kuelezea wajibu wake wa pamoja kijamii (wajibu kifaya) unaowakabili Waislamu wote. [1] Aidha, kuna Riwaya madhubuti ilioko ndani ya kitabu kiitwacho Da'a'im al-Islam, iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Ali (a.s), yenye kuthibitisha wajibu huo kifaya kwa Waislamu. [2] Makarem Shirazi ambaye ni mwanazuoni na mfasiri mashuhuri wa Kishia, anatoa hoja isemayo kwamba; Aya hii, ni mwendelezo wa Aya ya 215 ya Suratu Al-Baqarah nayo ni Aya inahusiana umuhnimu wa kutoaji wa mali kwa ajili ya Allah, Aya hii ni Aya yenye kutoa msisitizo mkubwa juu ya kujitolea muhanga katika njia ya Mwenye Ezi Mungu. [3] Tafsiri nyengine ya Qur’ani iitwayo Anware-Darakhshan inafafanua ikisema kwamba; Aya hii ilikuwa ikiwa ni karipio kwa kundi la wale Waislamu waliohoji uhalali wa amri ya Jihadi kutokana na mashaka yaliyomo ndani yake, ambao walikuwa wameghafilika kwamba; Mwenye Ezi Mungu alitoa amri hiyo kwa kuzingatia maslahi ya umma na ili kuondosha vizingiti vinavyokuwa vikikwamisha ustawi na ueneaji wa Uislamu. [4]

Vilevile, kwa mujibu wa wafasiri hawa wa Qur’ani ni kwamba; Aya ya 216 ya Suratu Al-Baqarah inakusudia kutoa mwangaza juu ya ukweli wa kwamba; mwanadamu ni mchanga mno kielimu, na kutokana na ufahamu wake mdogo kuhusiana na uhalisia wa maisha ulivyo, hilo hufanya afanye makosa katika kuchambua mambo mbali mbali yaliomo maishani mwake likiwemo suala la Jihadi katika njia ya Mwenye Ezi Mungu. Hiyo ndiyo sababu hasa ianyomfanya yeye, mabaya ayahisabu kuwa ni mema kwake, na kinyume chake, yale lilio mema kwake huchukulia kuwa ni mambo mabaya na hatari dhidi yake. [5] Fadhlu bin Hassan al-Tabarsi, mmoja wa wafasiri wa Qur'an, ameandika akisema kwamba; Hakuna hata mmoja mweye imani ya Ata'a bin Abi Rabah, ambaye aliamini kuwa wajibu wa Jihadi katika Aya hii unawahusu Masahaba peke yao. Kwani wafasiri wengine wote wanakubaliana (wana ijmai) kwamba Aya hii inawalenga Waislamu wote kwa jumla. [6]

Aya ya 216 Kama Ilivyokuja Katika Qur’ani

﴿كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَكُمْ وَعَسَى أَنْ تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ وَعَسَى أَنْ تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَكُمْ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ٢١٦﴾

Mmefaradhishiwa (jukumu la) kupigana vita vya Jihadi, hali ya kuwa ni jambo linalokukereni. Hata hivyo, yawezekana mkakichukia kitu fulani ilhali ndicho chenye maslahi kwenu, na yawezekana mkakipenda kitu fulani ilhali ndicho chenye madhara kwenu. Na Mwenye Ezi Mungu ndiye Mjuzi (wa yote), na ninyi si wenye ujuzi (juu ya uhalisia wa mambo ulivyo).


Kwa Nini Vita Havikuwa ni Jambo Linalowapendweza Waislamu?

Kuna mitazamo miwili mikuu miongoni mwa wafasiri kuhusiana na swali hili. Mtazamo wa kwanza, unaowakilishwa na wanazuoni kadhaa wakuu, akiwemo Allamah Tabataba'i, Jawadi Amuli na Sayyid Muhammad Hussein Fadhluallah, nao ule mtazamo usemao kwamba; Waislamu waliona vita kuwa jambo gumu, hii ni kutokana na asili yake ya ukatili na umwagaji damu uliomo ndani yake. Kwa mujibu wao, Waislamu walikubali kubeba jukumu hili la kupigana Jihadi kwa lengo la kutafuta radhi za Mungu tu. [7]

Kwa upande wa pili, mwanazuoni Muhammad Jawad Mughniyah anatoa hoja tofauti kuhusiana na hili.  Yeye akitoa maoni yake anasema; Tukitazama mwenendo mzima wa Masahaba wa Mtume (s.a.w.w), tunaona kuwa; Jihadi haikuwa ngumu kwao; kinyume chake, wao walionekana kuitafuta kwa shauku kubwa mno. Hata waliona kuwa watakula hasara mno, iwapo wao hatopata taufiki ya kufa shahidi vitani. Kwa mtazamo wa Mughniyah, sababu ya Waislamu kutopenda vita haikuwa ni kutokana na ugumu wake, bali ilikuwa ni hofu ya kushindwa kutokana na uchache wao wa idadi na udhaifu wa vifaa vya kijeshi walivyokuwa navyo ikilinganishwa na maadui zao. [8]

Dhana ya Utegemezi wa Maarifa na Vitendo vya Binadamu kwenye Mielekeo ya Nafsi

Ufasiri chambuzi wa Aya wa 216 cha Surah Al-Baqarah unaibua hoja na madai ya kisaikolojia na kitheolojia yasemayo kwamba; mara nyingi maarifa (ilm) na vitendo (amal) vya binadamu hupotoshwa na mielkeo ya nafsi (tamayyulaat nafsani). Aya husika inasema: "...na yawezekana mkachukia kitu (fulani) ilhali ni bora kwenu, na yawezekana (pia) mkapenda kitu (fulani) ilhali ni kiovu (shari) kwenu..."

Katika tafsiri yake, msomi na mfasiri maarufu ajulikanaye kwa jina la Mohammad-Ali Rezai Esfahani, anajenga hoja isemayo kwamba; kikawaida binadamu huelekea kujenga misingi yake ya epistemolojia (nadharia ya maarifa) pamoja na nyenendo za maadili yake juu ya matamanio ya nafsi yake, jambo ambalo linakosolewa vikali na Aya hii. Ili kuthibisha na kuimarisha hoja yake hiyo, anatoa mifano akisema kwamba: Binadamu huvutiwa na mambo mbali mbali, kama vile; uvivu, starehe (hedonism), vyakula haramu pamoja na vitendo vya dhambi, ambavyo kimsingi ni shari (uovu) kwake. Kinyume chake, hukwepa mambo yenye kheri naye, kama vile dawa uchungu zenye ponyo ndani yake alizoamrishwa na dokta wake kuzitumia kwa ajili ya tiba ya maradhi fulani. [9]

Kadhalika, Tafsir Rahnama inaimarisha mtazamo huu kwa kusema; Vigezo vya kimaadili vya "kheri" na "shari" havifungamani na hisia za ridhaa au karaha za kibinadamu. Kwa hiyo, hisia za binadamu hazipaswi kuwa ni kigezo cha msukumo wa utekelezaji au uachaji wa sheria za Mungu. [10]


Dhana ya Kutegemea Ujuzi wa Mungu Katika Kuelewa Maslahi ya Mwanadamu

Kifungu cha mwisho cha aya ya 216 ya Surah Al-Baqarah, “Wallāhu yalamu wa-antum lā talamūn” ("Na Mwenyezi Mungu anajua, nanyi hamjui"), kimekuwa msingi wa mijadala ya kiteolojia na kifalsafa. Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah anasema kuwa; Aya hii inasisitiza ulazima wa muumini kuwa na imani na yakini thabiti (iṭmi'nān) juu ya sheria za Mwenye Ezi Mungu. Hoja yake imejengwa juu ya dhana isemayo kwamba; Ujuzi wa Mwenye Ezi Mungu ni kamilifu wenye kujumuisha mambo yote ya dhahiri pamoja na batini. Naye hupanga sheria zake kupitia elimu Yake hiyo isio na mipaka. Hivyo, ufuasi wa sheria zake ndio njia pekee ya kupata maslahi na kuepukana madhara mbali mbali. [11]

Makarem Shirazi anastawisha wigo wa hoja hii, akisema kwamba; Aya hii imekuja kutufafanuli msingi ya kiepistemolojia ya kwamba: Mwanadamu hapaswi kufungamanisha hatima za majaaliwa yake kwenye maarifa yake finyu. Hivyo basi, ni lazima ufahamu wa mwnadamu kufunganishwa na elimu ya Mwenye Ezi Mungu isio na ukomo, hasa katika nyanja za sheria. [13] Mtazamo huu unaungwa mkono na wafasiri wengine kadhaa wanaoamini kwamba; utambuzi wenye ukomo wa maarifa ya binadamu ndiwo unaojenga sifa ya unyenyekevuna utiifu mbele ya mamlaka ya Mwenye Ezi Mungu.

Sheikh Tusi kwa upande wake ametumia kifungu cha mwisho cha Aya hii ya 216, kisemacho; “Wallāhu yalamu wa-antum lā talamūn” ("Na Mwenyezi Mungu anajua, nanyi hamjui"), katika kukanusha itikadi ya mfungiko na uainikaji wa majaaliwa (determinism/fatalism) ya mwanadamu. Yeye anasema kwamba; Amri ya Jihadi ilitolewa kwa msingi wa ujuzi wa Mwenye Ezi Mungu kulingana na maslahi ya Jihadi kwa mwanadamu, jambo linalothibitisha kuwepo kwa hiari katika uwajibikaji wa mwanadamu. Ama Hashemi Rafsanjani emetumia Aya hii katika kutoa maoni yake juu ya mwelekeo wa kisiasa-kisheria. Yeye anasema kwamba; Aya hii imekuja kutupua kigezo kuwa mtunga sheria (legislator), kianachutufahamisha kwamba, mtunga sheria anapaswa kuwa na ufahamu wa kina juu ya maslahi na madhara halisi ya mambo mbali mbali, ili asije kuhadaika na sura ya nje ya nyenendo na matukio ya kijamii yalivyo. [15]