Nenda kwa yaliyomo

Al-Takattuf

Kutoka wikishia

Al-takattuf katika Sala (Kiarabu: التكتف في الصلاة ), ni neno la Kiarabu linalo maanisha kitendo cha kusali huku mikono ikiwa imefungwa, kwa njia ambayo kiganja cha mkono wa kulia kinakaa juu ya mgongo wa mkono wa kushoto huku mikono yote miwili ikiwa iko juu ya kitovu au kwenye kifua.

Wanazuoni wa Shia wanachukulia suala la kufunga mikono katika Sala kuwa ni haramu, na wanaamini ya kwamba kitendo hichi kinabatilisha Sala. Ili kuthibitisha nadharia yao, Mashia wanarejelea hadithi ambazo zinaripoti kwamba Mtume alisali bila kufunga mikono katika Sala yake. Pia kuna Hadithi kutoka upande wa Ahlul-Bayt (a.s) ambazo zinakataza kufungu mikono katika Sala. Wanazuoni wa Shia wanaruhusu suala la kufunga mikono katika Sala katika hali za taqiyyah tu.

Kwa maoni ya wanazuoni wengi wa Sunni, kufunga mikono katika sala ni mustahabbu (ni sunna). Baadhi yao wanaamini ni wajibu na pia kuna wanao amini kuwa ni makruhu miongoni mwa wanazuoni hao wa Kisunni. Kuna tofauti ya maoni kati ya wanazuoni wa Sunni kuhusu jinsi ya kufunga mikono katika sala, mahali pa kuweka mikono na wakati wa kufunga mikono katika sala.

Wanazuoni wa Sunni katika kuthibitisha nadharia yao, wanategemea baadhi ya Hadithi zisemazo kuwa ni halali kufunga mikono katika sala. Ila Mashia wanaamini kwamba; baadhi ya Hadithi hizi zina kasoro katika chanzo cha nukuu zake na baadhi nyingine zina kasoro katika maudhui yake.

Maana ya Al-takattuf na nafasi kwa Shia na Sunni

Maana ya neno al-takattuf (التکتف): Ni kuweka mikono juu ya kifua au tumbo wakati wa kuswali, katika hali ambayo, kiganja cha mkono wa kulia huwekwa juu ya mgongo wa mkono wa kushoto [1] Kitendo hiki hujulikana kwa majina tofauti, kama vile: al-takattuf التکتف, [2] Takfir, [3] Qabdhu [4] na Wadh’u. [5] Kinyume cha neno al-takattuf ni Esdal au Saddle, ambalo linamaanisha kuachilia mikono. [6]

Al-takattuf ni mojawapo ya masuala yenye utata kati ya madhehebu ya Shia na madhehebu mengine.[7] Wengi wa Sunni wana lihisabu tendo la Al-takattuf kuwa mojawapo ya matendo ya nidhamu zinazopendekezwa kwenye amali ya sala. [8]

Jinsi ya kufunga mikono

Ainiy, mmoja wa mafaqihi wa Kisunni, amelifafanua tendo la kufunga mikono kuwa ni; kuweka kiganja cha mkono wa kulia nyuma ya kifundo cha mkono wa kushoto, ili kifundo cha mkono wa kushoto kiwe ndani ya kiganja cha mkono wa kulia; Lakini baadhi ya wanazuoni wengine wa Kisunni wamechagua kuweka kiganja cha kulia juu ya vifundo vya mkono wa kulia, yaani sehemu inayo anzwa kuosha wakatia wa kutia udhu. [9] Wengine wamesema: kiganja cha mkono wa kulia kiwekwe nyuma ya kiganja cha kushoto, ili kidole gumba na kidole kidogo cha mkono wa kushoto viwe ndani ya himaya ya kiganja cha mkono wa kulia. [10]

Wapi pahala pa kuwekwa mikono katika kufunga sala?

Aina za ufungaji wa mikono katika madhehebu tofauti

Wafuasi wa madhehebu ya Sunni hawakuwafikiana kinadharia kuhusu mahali ambapo mikono hupaswa kuwekwa wakati wa kufunga sala. Baadhi yao wamehukumu mikono kuwekwa chini ya kitovu [11] na wengine wanafikiri inapaswa kuwekwa kifuani au chini yake. [12] Hanafi na Hambali wanahukumu mikono kuweka chini ya kitovu, na kusema kwamba; hiyo ndio Sunna juu ya amali hiyo. Shafi'i yeye ameona kuweka mikono chini ya kifua ndio Sunna. [13] Bin Bazi, mmoja wa wanazuoni wa Kiwahhabi, anaamini kuwa mikono inapaswa kuwekwa kifuani. [14]

Baadhi pia wamesema kuwa wanaume wanapaswa kuweka mikono chini ya kitovu na wanawake juu ya kifua. [15]

Mahali pa kuwekwa mikono wakati wa kufunga sala

Ainiy, mwanachuoni wa Kisunni, anasema kwamba Abu Hanifah na Abu Yusuf wanalichukulia suala la kufunga mikono kuwa ni Sunna katika kisimamo cha sala, na baadhi ya wengine wanaona kuwa ni Sunna wakati wa kusoma Surat al-Fatiha pamoja na Sura tu. Kwa mtazamo wa Ainiy, kufunga mikono ni Sunna wakati wa kusimama kwenye kisimamo ambacho ndani yake mna utajo (dhikri) za Sunna ambazo zimetajwa katika Hadithi kama vile kismamo baada ya takbiratu al-Ihram na kisimamo baada ya kutoka katika rukuu. Kwa kauli yake ni kwamba, kundi la wanazuoni wa Kisunni, kwa lengo la kuwapinga Shia, wamelipa umuhimu suala la kufunga mikono katika aina zote za visimamo vya ndani ya sala, na wakalihisabu kuwa ni tendo la Sunnah. [16] Kwa hiyo, kuna tofauti kuhusu juu ya kufunga mikono baada ya kurukuu, wakati wa kunuti, katika sala ya maiti na baina ya takbira za Sala ya Idi. [17]

Imeripotiwa kwamba Hanafi na Shafi'i wanalihisabu suala la kufunga mikono juu ya kifua baada ya kurudi kutoka rukuu, kuwa ni uzushi. Ibn Hambal, kiongozi wa madhehebu ya Hambali, pia amenukuliwa kwa maoni tofauti kuhusiana na jambo hili, mojawapo ni kwamba; muumini yupo uhuru juu ya kufunga au kuto funga mikono katika sala. [18]

Hukumu za kifiqi kulingana na madhehebu ya Shia

Kulingana na maoni maarufu miongoni mwa wanazuoni wa Shia ni kwamba, haijuzu kufunga mikono katika ibada ya sala, na kufanya hivyo ni haramu na hupelekea kubatilika kwa sala. [19] Sayyid Murtadha [20] na Sheikh Tusi wamedai kuwa kuna ittifaki ya wanazuoni juu ya hukumu hii. [21] Baadhi ya wanazuoni wa Shia wametona huku tu ya kuharamisha amali hiyo, na sio kwamba jambao linaloweza kupelekea sala ya mja kubatilika.[22][23] Muhammad Hassan Najafi katika kitabu chake Jawaahirul Kalaam amesema kuwa Abu Saleh Halabi anachukulia suala la kufunga mikono kuwa ni makruh (lisilopekezwa) na kuiachia wazi mikono hiyo ni mustahabbu (Sunna). [24]

Hoja za wanazuoni wa Shia juu ya hukumu hii ni Hadithi ambazo zimemnukuu Mtume akisali bila kufunga mikono. [25] Miongoni mwazo ni Hadithi ambayo Abu Hamid Saadi ameinukuu na kuelezea namna ya Mtume (s.a.w.w) alivyo kuwa akisali, ambapo ndani yake hakuzungumzia suala la kufunga mikono. [26] Pia kuna Hadithi kutoka kwa Maimamu wa Shia ambazo zimenukuliwa wakikataza kufunga mikono katika sala. [27] Imenukuliwa kutoka kwa Imam Ali (a.s) na Imam Baqir (a.s) [28] kwamba; kufuna mikono ni desturi ya Wamajusi. [29] Sahibu al-Jawahiri anaamini kuwa desturi hii ilienezwa na Omar bin Khattab ambayo iliigwa kutoka kwa mateka wa Kiajemi. [30]

Hukumu ya kugunga mikono katika hali ya taqiyya

Mafuqaha wa Shia kama vile Shahidi Thani na Sheikh Murtadha Ansari, wameona kuwa kufunga mikono huruhusiwa katika hali ya taqiyyah tu, katika hali hiyo jambo hili huwa ni halali bali ni wajibu. [31] Hata hivyo, Ayatullah Khamenei, mmoja wa mafaqihi wa zama hizi (wa karne ya kumi na tano Hijiria), amesema kuwa kufunga mikono si jambo linaloingia katika taqiyyah, kwani katika zama za hivi sasa hakuna anaye bughudhiwa kwa kuto funga mikono, kwa kufunga mikono itakuwa ni halali tu katika hali ya dharura. [32]

Hukumu ya kifiqhi kwa mujibu wa madhebebu ya Ahlus-Sunnah

Wanazuoni wa Ahlu-Sunnah wanachukulia suala la kufunga mikono kuwa ni ishara ya unyenyekevu, kujisalimisha, na kumheshimu Mwenye Ezi Mungu. [33] Walakini, kuna tofauti za maoni kuhusu hukumu ya kifiqhi juu ya amali hii ya kufunga mikono:

  • Mustahabbu: Kwa mujibu wa mafaqihi wa Ahlus-Sunnah kama Abu Hanifa, Shafi'i, Ibnu Hambal, na wengi wa wanazuoni wa Ahlus-Sunnah, ni kwamba; kufunga mikono ni amali ya mustahabbu. [34]
  • Mustahabbu (Sunna) ya hiari: Auzai (aliye zaliwa mwaka 707 na kufariki 774 Miladia) [35] na Ibnu Abdu al-Barr (aliye ishi kati yam waka 368 na 463 Hjiria) waliamini kuwa; kufunga mikono ni Sunna ya hiari. [36]
  • Wajibu: Al-Albani (aliye ishi kati ya mwaka 1333 na 1420 Miladia) na Shawkani (aliye ishi kati ya mwaka 1173 na 1250 Miladia) wanaamini kuwa tufunga mikoni ni jambo la wajibu katika sala. [37]
  • Makruhu (lisilopendekezwa): Kwa mujibu wa maelezo ya Qurtubi (mfasiri wa madhehebu ya Maliki), ni kwamba; Malik bin Anas anaamini kuwa kufunga mikono ni makruh katika sala za faradhi, na ni mustahabb katika sala za sunna. [38]Imesemekana kuwa Abdullah bin Zubeir na Hassan Basri pia nao walikuwa na imani kama hiyo. [39]
  • Baadhi ya faqihi wa Ahlus-Sunnah wanachukulia kufunga mikono kuwa ni maalum katika hali ambayo mja atakuwa amechoka kutokana na kusimama kwa muda mrefu. [40]

Hati na vielelezo vya Sunni kuhusu kufunga mikono

Masunni wametaja Hadithi kadhaa katika kuthibitisha madai yao juu ya Imani ya amali hii ya kufunga mikono katika ibada ya sala. Baadhi ya Hadithi hizo ni: [41]

  • Hadithi ya Sahlu bin Saad: Katika Hadithi hii, imeelezwa kwamba; watu walikuwa wakipewa maagizo ya kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto wakati wa sala. [42]
  • Hadithi ya Wail bin Hujur: Wail anasimulia kuwa Mtume (s.a.w.w) baada ya takbiratu al-Ihramu, alikuwa akitoa mikono yake kutoka kwenye mikono ya nguo zake na kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto. [43]
  • Hadithi ya Abdullah bin Mas'ud: Katika Hadithi hii imeelezwa kwamba; Ibn Mas'ud alikuwa akiiweka mkono wake wa kushoto juu ya mkono wake wa kulia wakati wa sala, na Mtume (s.a.w.w) alipomwona akauchukua mkono wake wa kulia na kuuweka juu ya mkono wake wa kushoto. [44]
  • Hadithi ya Ibn Abbas: Ibn Abbas ananukuu kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) kwamba Mitume waliamuriwa kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto wakati wa sala zao. [45]
  • Hadithi iliyosimuliwa na Imam Ali (a.s): Kulingana na hadithi hii, moja ya sunna za sala ni kuweka mikono chini ya kitovu. [46]

Ukosoaji kutoka kwa Mashia

Mashia wanaamini kuwa kuna mashaka katika baadhi ya Hadithi hizi ambazo ndio tegemeo la madhehebu ya Sunni; kwa sababu ndani yake kuna wapokezi ambao hawaminiki, ambao hata kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wa Ahlul-Sunnah pia si wenye kukubalika. [47] Baadhi ya wanazuoni wa Kisunni pia kulingana maelezo ya Hadithi hizo, hawafikii natija ya kwamba: kufunga mikono ni jambo la wajibu au ni sunna. [48]

Monografia (seti ya arodha ya vitabu vilivo andikwa kuhusiana na maudhui hii)

Baadhi ya vitabu vinavyo tafiti na kukosoa suala la kufunga mikono ni kama ifuatavyo:

  • Al-Irsal wa al-Takfir bayna al-Sunnah wa al-Bid'ah الاِرسالُ و التَّکفیر بینَ السُّنةِ و البِدعَه: kazi ya Najmuddin Tabasi, ambayo ni sehemu ya mkusanyo kutoka katika kitabu chake kiitwacho “Baina ya Sunnah wa al-Bid’ah, ambamo ndani yake mmetafitiwa masuala yenye mgongano kati ya Shia na Sunni, kama vile ndoa ya muda (mut’a). [49] Mkusanyo huu umewekwa katika mfumo wa kitabu, kilicho itwa; “Diraasaatu al-Fiqhiyyah fii Masaaili Khilafiyyah . [50]
  • Tawdih al-Maqal fi al-Damm wa al-Irsal توضیحُ المَقال فی الضَّمّ و الاِرسال: cha Muhammad Yahya Salim Azan, kilicho chapwa na Daru al-turath al-Yemeniy mjini Sana'a. [51]
  • Al-Qawl al-Fasl fi Ta'id al-Sunnah al-Sadl القولُ الفَصل فی تأییدِ سُنَّةِ السَّدْل: cha Muhammad ‘Aabid, Kitabu hichi kiliandikwa kwa nia ya ukosoaji dhidi ya amali ya kufunga mikono katika sala na kwa lengo la kuthibitisha ukweli juu ya kuachia mikono katika sala, kwa mujibu wa madhehebu ya Malik bin Anas. [52]
  • Risalah Mukhtasarah fi al-Sadl رسالةٌ مُختَصَرةٍ فی السَّدْل: cha Abdulhamid Mubarak Al-Sheikh. [53]
  • Risalah fi Hukm Sadl al-Yadayn fi al-Salah 'ala Madhhab al-Imam Malik رسالةٌ فی حکم سَدْلِ الیَدَین فی الصَّلاة علی مذهبِ الامام مالک: cha Muhammad bin Muhammad al-Maghribi, anaye julikana kwa jina Shinqiti. Kitabu hichi kimechapwa na Dar al-Fadhilah. [54]
  • Al-Qabdhu fi al-Salah القَبضُ فی الصَّلاه: kilicho chapwa na The World Ahlul Bayt Assembly ambacho ni sehemu ya kitabu kiitwacho "Fi Rahab Ahlul Bayt . [55]

Maudhui zinazo fungamana


Rejea

  1. Najafi, Jawaharlal Kalam, 1362, juzuu ya 11, uk.15; Zaheili, Fiqh al-Islami na Adelta, Dar al-Fikr, juzuu ya 2, uk.873.
  2. Ibn Arabi, al-Futuhat al-Makiyya, Dar al-Sadr, juzuu ya 1, uk. 419.
  3. Najafi, Jawaharlal Kalam, 1362, juzuu ya 11, uk.15.
  4. Tabasi, Mafunzo ya Kisheria katika Masuala ya Khilafah, 1387, juzuu ya 1, uk.195.
  5. Mughniyeh, Fiqh Ali al-Mahabh al-Khamsa, 1421 AH, juzuu ya 1, uk.110.
  6. Mubarakfouri, Tohfat al-Ahuzi, 1410 AH, juzuu ya 2, uk.73;
  7. Kundi la waandishi, katika Rahab Ahl al-Bayt, 1426 AH, juz.21, uk.11.
  8. Ibn Jabrin, Ufafanuzi wa Umada al-Ahkam, juzuu ya 13, uk. 47.
  9. Aini, al-Banayyah Sharh al-Hudaiyah, 142 AH, juz.2, uk.181.
  10. Aini, al-Banayyah Sharh al-Hudaya, 1420 AH, juzuu ya 2, uk.181.
  11. Banbaz, mkusanyo wa fatwa na makala mbalimbali, mkuu wa Idara ya Utafiti wa Kisayansi na Fata katika Ufalme wa Saudi Arabia, juzuu ya 29, uk.240.
  12. Aini, al-Banayyah Sharh al-Hudaiyah, 1420 AH, juz.2, uk. 181.
  13. Al-Tayar na wengineo, Fiqh Al-Misr, 1433 AH, Juz.1, uk.283.
  14. Benbaz, mkusanyo wa fatwa na makala mbalimbali, mkuu wa Idara ya Utafiti wa Kisayansi na Al-Iftaa katika Ufalme wa Saudi Arabia, juzuu ya 29, uk. 240.
  15. Hanafi Razi, Tohfat al-Maluk, 1417 AH, uk. 69.
  16. Aini, al-Banayyah Sharh al-Hudaiyah, 1420 AH, juz.2, uk.183.
  17. Aini, al-Banayyah Sharh al-Hudaiyah, 1420 AH, juz.2, uk.183.
  18. Atiyah, Sharah Balogh al-Maram, juzuu ya 61, uk. 6.
  19. Kundi la waandishi, katika Rahab Ahl al-Bayt, 1426 AH, juz.21, uk.12.
  20. Sayed Mortaza, Rasaila al-Sharif al-Mortaza, 1421 AH, juz.1, uk. 219.
  21. Sheikh Tusi, al-Khalaf, 1407 AH, juzuu ya 1, uk.322
  22. Mughniyeh, Fiqh Ali al-Mahabh al-Khamsa, 1421 AH, juzuu ya 1, uk.111.
  23. Mughniyeh, Fiqh Ali al-Mahabh al-Khamsa, 1421 AH, juzuu ya 1, uk.111.
  24. Najafi, Jawaharlal Kalam, 1362, juzuu ya 11, uk.15.
  25. Mkusanyiko wa waandishi, katika Rahab Ahl al-Bayt, 1426 AH, juz.21, uk.22.
  26. Tirmidhi, Al-Jamae al-Sahih, Dar al-Hadith, juzuu ya 2, uk.84.
  27. Hamiri, Qarb al-Asnad, 1413 AH, uk. Sheikh Tusi, Tahzeeb al-Ahkam, 1407 AH, juzuu ya 2, uk. 84.
  28. Sheikh Sadouq, Al-Khasal, 1362, juzuu ya 2, uk.622.
  29. Har Ameli, Wasal al-Shia, 1409 AH, juzuu ya 7, uk. 265.
  30. Najafi, Jawaharlal Kalam, 1362, juzuu ya 11, uk.19.
  31. Shahid Thani, Roz al-Janan, juzuu ya 2, uk. 423; Sabzevari, Mehzb al-Ahkam, 2008, juzuu ya 2, uk.391; Sheikh Ansari, Rasail al-Faqih, 1414 AH, juzuu ya 1, uk. 96.
  32. Khamenei, Ajuba al-Astaftaat, 2008, juzuu ya 1, uk.160.
  33. Aini, al-Banayyah Sharh al-Hudaiyah, 1420 AH, juz.2, uk.183.
  34. Aini, al-Banayyah Sharh al-Hudaiyah, 1420 AH, juz.2, uk.180.
  35. Aini, al-Banayyah Sharh al-Hudaiyah, 1420 AH, juz.2, uk.180.
  36. Sarawi, Al-Qatuf al-Daniyeh, 1997, juzuu ya 2, uk.37.
  37. Awaisheh, Al-Masua'a al-Fiqhiyyah al-Misrah, 1423 AH, juz.2, uk.9; Shukani, Nil al-Awtar, 1413 AH, juz.2, uk 217.
  38. Qurtubi, Mwanzo wa Al-Mutajtahid na Mwisho wa Al-Maqtasad, 1425 AH, Juzuu ya 1, uk 146.
  39. Navi, al-Majmoj Sharh al-Muhdez, Dar al-Fikr, juzuu ya 3, uk. 311.
  40. Aini, al-Banayyah Sharh al-Hudaiyah, 1420 AH, juzuu ya 2, uk.181.
  41. Kundi la waandishi, katika Rahab Ahl al-Bayt, 1426 AH, juz.21, uk.15.
  42. Bukhari, Sahih al-Bukhari, 1311 AH, juzuu ya 1, uk.148.
  43. Nishaburi, Sahih Muslim, 1374 AH, juzuu ya 1, uk.301; Mulla Heravi, Marqat al-Janan fi Sharh Mishkah al-Masabih, 1422 AH, juz.2, uk. 657.
  44. Abu Daoud, Sunan Abi Daoud, Saida, juzuu ya 1, uk.200.
  45. Tabrani, Al-Mu'jam al-Kabir, Cairo, juzuu ya 11, uk. 199.
  46. Dar al-Qutni, Sunan al-Dar al-Qutni, 1424 AH, juzuu ya 2, uk. 34.
  47. Mkusanyiko wa waandishi, katika Rahab Ahl al-Bayt, 1426 AH, juz.21, uk.21.
  48. Mkusanyiko wa waandishi, Fai Rahab Ahl al-Bayt, 1426 AH, Juz. 21, uk. 16, 19; Sobhani, Al-Itsam Balkitab na Al-Sunnah, 1375, uk 67.
  49. «إرسال التکفیر بین السنة و البدعة - نسخه متنی»، کتابخانه دیجیتال تبیان.
  50. «دراسات فقهیه فی مسائل خلافیه»، کتابخوان قائمیه.
  51. «توضيح المقال في الضم والارسال»، وبگاه دار المقتبس.
  52. «القول الفصل في تأييد سنة السدل على مذهب مالك بن أنس»، وبگاه کتابخانه عین الجامعه.
  53. «رسالة مختصرة في السدل»، وبگاه کتابخانه عین الجامعه.
  54. «رسالة في حكم سدل اليدين في الصلاة على مذهب الأمام مالك بالشنقيطي»، وبگاه آرشیو اینترنت.
  55. «فی رحاب أهل البیت علیهم السلام - ۲۱ - القبض فی الصلاة التکتف»، وبگاه مجمع جهانی اهل‌بیت.

Vyanzo

  • Abu Daawuud, Suleiman bin Ash'ath, Sunan Abi Dawood, Saida, Al-Maktaba al-Asriya,[n.d].
  • Ibn Jabrin, Abdullah bin Abd al-Rahman, Sharh Imaada al-Ahkam, Bija, Bina, [n.d].
  • Ibn Hajr Asqlani, Ahmed Bin Ali, Tahdhib al-Dhadib, Beirut, Dar al-Sadr, [n.d].
  • Ibn Arabi, Mohi al-Din, al-Futuhat al-Makiyya, Beirut, Dar al-Sadr, [n.d].
  • «إرسال التکفیر بین السنة و البدعة - نسخه متنی»، کتابخانه دیجیتال تبیان، تاریخ بازدید: ۱۸ خرداد ۱۴۰۲ش.
  • Bukhari, Muhammad bin Ismail, Sahih al-Bukhari, Bulaq, al-Mutababa al-Kubari al-Amiriyah, 1311 AH.
  • Binbaz, Abdulaziz bin Abdullah, mkusanyiko wa fatwa na makala mbalimbali, Bijab, Mkuu wa Idara ya Utafiti wa Kisayansi na Al-Ifata katika Ufalme wa Saudi Arabia, [n.d].
  • Tirmidhi, Muhammad bin Isa, al-Jamae al-Sahih, Cairo, Dar al-Hadith, [n.d].
  • «توضيح المقال في الضم والارسال»، وبگاه دار المقتبس، تاریخ بازدید: ۵ تیر ۱۴۰۲ش.
  • Dar al-Qutni, Ali bin Omar, Sunan al-Dar al-Qutni, iliyotafitiwa na Shi'ab al-Arnauut, Beirut, Al-Rasalah Foundation, chapa ya kwanza, 1424 AH.
  • Jaziri, Abdur Rahman bin Muhammad, Fiqh Ali al-Mahabh al-Arba, Beirut, Dar al-Kitab al-Ulamiya, chapa ya pili, 1424 AH.
  • Kundi la waandishi, Fi Rahab Ahl al-Bayt, Qom, Al-Majma Al-Alami Lahl al-Bayt, chapa ya pili, 1426 AH.
  • Hamiri, Abdullah bin Jafar, Qorb al-Asnad, Qom, taasisi ya Al-Al-Bayt, chapa ya kwanza, 1413 AH.
  • Hanafi Razi, Muhammad bin Abi Bakr, Tohfa al-Maluk, Beirut, Dar al-Bashair al-Islamiyya, chapa ya kwanza, 1417 AH.
  • Khamenei, Majibu ya Maswali, iliyotafsiriwa na Ahmad Reza Hosseini, Tehran, Islamic Propaganda Organization, toleo la 51, 2008.
  • «دراسات فقیه فی مسائل خلافیه»، کتابخوان قائمیه، تاریخ بازدید: ۱۸ خرداد ۱۴۰۲ش.
  • «رسالة فی حکم سدل اليدين في الصلاة على مذهب الامام مالك بالشنقیطی»، وبگاه آرشیو اینترنت، تاریخ بازدید: ۵ تیر ۱۴۰۲ش.
  • Sobhani, Jafar, Al-Itsam katika Kitabu cha Vitabu na Sunnah, Tehran, Al-Thaqafa na Al-Islamiyyah, 1375.
  • Sabzevari, Seyyed Abdul Ali, Mahdez al-Ahkam fi bayan halal va haram, Qom, Dar al-Tafseer, toleo la kwanza, 2008.
  • Seyyed Mortaza, Ali bin Hossein, Rasaila al-Sharif al-Mortaza, Qom, Ayatollah Murashi Najafi Maktaba ya Umma, 1421 AH.
  • Shukani, Muhammad bin Ali, Nile al-Awtar, Misri, Dar al-Hadith, chapa ya kwanza, 1413 AH.
  • Shahidi Thani, Zain al-Din bin Ali, Ruz al-Jinan fi Sharh Irshad al-Azhan, Qom, Shule ya Mafunzo ya Kiislamu, chapa ya kwanza, 1422 AH.
  • Sheikh Ansari, Morteza, Rasail Faqhieh, Qom, Sheikh Ansari World Congress, 1414 AH.
  • Har Amili, Muhammad bin Hasan, Wasal al-Shia, Qom, Taasisi ya Al-Al-Bayt, chapa ya kwanza, 1409 AH.
  • Sheikh Sadouq, Muhammad bin Ali, al-Khasal, utafiti wa Ali Akbar Ghafari, Qom, Jamia Modaresin, chapa ya kwanza, 1362.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, Al-Khalaf, Qom, Al-Nashar al-Islami Foundation, 1407 AH.
  • Sheikh Sadouq, Muhammad bin Ali, al-Khasal, utafiti wa Ali Akbar Ghafari, Qom, Jamia Modaresin, chapa ya kwanza, 1362.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, Al-Khalaf, Qom, Al-Nashar al-Islami Foundation, 1407 AH.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hasan, Tahzeeb al-Ahkam, Tehran, Darul Kitab al-Islamiya, chapa ya 4, 1407 AH.
  • Tabarani, Suleiman bin Ahmad, Al-Mu'jam al-Kabir, Cairo, Skuli ya Ibn Taymiyyah, chapa ya pili, beta.
  • Tabasi, Najmuddin, Masomo ya Kisheria katika Masuala ya Khilafah, Qom, Taasisi ya Bostan Kitab, toleo la pili, 1387.
  • Tayar, Abdullah bin Muhammad, na wengineo, Fiqh Al-Misr, Riyadh, Madar Al-Watan Publishing House, chapa ya pili, 1433 AH.
  • Atiyeh, Ibn Mohammad Salem, maelezo ya ukomavu wa al-Maram, bija, bina, bita.
  • Awaisheh, Hossein bin Audeh, Al-Musua'a al-Fiqhiyyah al-Misrah fifiqh al-kitab na sunnah al-mutahrah, Dar Ibn Hazm, Beirut, chapa ya kwanza, 1423 AH.
  • Aini, Mahmoud bin Ahmad, al-Banayyah Sharh al-Hudayeh, Beirut, Dar al-Katb al-Alamiya, chapa ya kwanza, 1420 AH.
  • Qurtubi, Muhammad bin Ahmad, Mwanzo wa Al-Mujtahd na Mwisho wa Al-Maqtasad, Cairo, Dar al-Hadith, 1425 AH.
  • «فی رحاب أهل البیت علیهم السلام - ۲۱ - القبض فی الصلاة التکتف»، وبگاه مجمع جهانی اهل‌بیت، تاریخ بازدید: ۳ تیر ۱۴۰۲ش.
  • «القول الفصل في تأييد سنة السدل على مذهب مالك بن أنس»، وبگاه کتابخانه عین الجامعه، تاریخ بازدید: ۵ تیر ۱۴۰۲ش.
  • Mubarakfouri, Muhammad bin Abdul Rahim, Tohfa Al-Ahuzi, Beirut, Dar al-Kitab Al-Alamiya, chapa ya kwanza, 1410 AH.
  • Mughniyeh, Mohammad Javad, Fiqh Ali al-Mahabh al-Khamsa, Beirut, Dar al-Tayar al-Jadid, 1421 AH.
  • Najafi, Mohammad Hassan, Javaher Al-Kalam, Beirut, Ufufuo wa Urithi wa Kiarabu, toleo la 7, 1362.
  • Nawi, Yahya bin Sharaf, al-Majmoj Sharh al-Mahzab, Beirut, Dar al-Fikr, Bita.
  • Nishabouri, Muslim, Sahih Muslim, Cairo, Isa Al-Babi Al-Halabi na Washirika, 1374 AH.