Nenda kwa yaliyomo

Al-Sirah al-Mutashari’ah

Kutoka wikishia

Sirah al-Mutashari'ah (Kiarabu: السيرة المتشرعة) ni makubaliano ya kivitendo ya wafuasi wote au wafuasi wengi wa dini au madhehebu kuhusiana na amali maalumu. Kwa maneno mengine ni kuwa, ni kitendo na amali ya Waislamu kwa sababu wao ni Waislamu na wanashikamana na hukumu za Sharia. Sirah Mutashari’ah ni moja ya masuala ambayo yanajadiliwa katika elimu ya Usul al-Fiqih. Suala la kuwa hoja Khabar Wahid na hoja ya dhahir ni miongoni mwa mambo ya kimsingi na muhimu ambayo yanatumika katika mchakato wa kunyambua hukumu za sheria kwa ajili ya kuthibitisha sirah Mutashari’ah. Kadhalika mafakihi wakiwa na lengo la kuthibitisha baadhi ya masuala ya fikihi wametumia Sirah Mutashari’ah.

Kwa mujibu wa baadhi ya Usuliyuun ni kuwa Sirah Mutashari’ah ambayo ilikuweko katika zama za Imamu Maasumu na yeye mwenyewe alikuwa mmoja wa watekelezaji wake ni hoja. Kadhalika ni sira ambayo haikufanywa na Maasumu, bali iliwekwa wazi mbele ya macho yake na kuisikia na wakati huo huo hakuikataza, hivyo ni hoja. Kundi la Usuliyyun wamezichukulia aina hizi za sira kuwa ni mithili ya makubaliano.

Usuliyyun wanasema kuwa Sirah Mutashari’ah kimsingi inaonyesha tu uhalali wa kitendo na kutoharamishwa kwake au uhalali wa kuacha kitendo na kutokuwa kwake wajibu na haithibitishi kanuni kama wajibu, mustahabu, uharamu na makuruhu.

Utambuzi wa Maana na Nafasi Yake

Sirah Mutashari'ah ni makubaliano ya kivitendo ya wafuasi wote au wafuasi wengi wa dini au madhehebu kuhusiana na amali maalumu.[1] Kwa maneno menghine ni kuwa, ni mtindo endelevu wa amali baina ya wafuasi wa dini au madhehebu maalumu juu ya kufanya amali au kuiacha..[2] Kwa mujibu wa fasili na maana iliyotolewa na Mirzai Naini ni kwamba: Sirah Mutashariah ni amali na kitendo cha Waislamu kwa sababu wao ni Waislamu na wanashikamana na hukumu za Sharia.[3]

Katika Fikihi na Usul kumetumiwa mno kama hoja Sira Mutashari’ah[4] na mjadala wa hoja yake unahesabiwa kuwa miongoni mwa masuala ya elimu ya Usul al-Fiqh na hilo limejadiliwa katika baadhi ya athari za Usul.[5]

Wamesema kuhusiana na wigo mpana wa kuwa dalili Sirah Mutashari’ah kwamba, kimsingi inaonyesha tu uhalali wa kitendo na kutoharamishwa kwake au uhalali wa kuacha kitendo na kutokuwa kwake wajibu na haithibitishi kanuni kama wajibu, mustahabu, uharamu na chukizo.[6]

Tofauti ya Sirah Mutashari’ah na Sirah Uqalaa

Makala Kuu: Sirah Uqalaa

Sirah Mutashari’ah ni maalumu zaidi ya Sirah Uqalaa na yenyewe kimsingi ni Sira ya Waislamu au wafuasi dini au madhehebu fulani juu ya kufanya au kuacha kufanya jambo fulani wote au wafuasi wengi wa dini au madhehebu kuhusiana na amali maalumu[7] katika hali ambayo, Sirah Uqalaa ni msingi na makubaliano ya wote au akthari ya uqalaa (wenye akili) juu ya kufanya au kuacha kufanya jambo.[8] Kuhusiana na tofauti ya mawili haya katika hoja na itibari pia imeelezwa kwamba, kama Sirah Mutashari’ah itathibiti yenyewe huwa ni dalili ya hukumu ya kisheria; lakini Sirah Uqalaa sio hoja; isipokuwa kwa taqrir na kuungwa mkono na Maasumu au iwe haijapingwa na yeye.[9]

Inaelezwa kwamba, Sirah Mutasharia’h ina ustahiki wa kuzuia Sirah Uqalaa kuwa na taathira katika kuthibitisha hukumu ya sheria; lakini Sira Uqalaa haina ustahiki huo kuhusiana na Sirah Mutashari’ah.[10]

Uhusiano wa Sirah Mutashari’ah na Ijmaa

Usuliyuun wanasema kuwa, Sirah Mutashari’ah ni aina fulani ya Ijmaa (makubaliano).[11] Muhammad Ridha Muzaffar, mmoja wa wanazuoni wa Kishia anasema kuwa, Sirah Mutashari’ah ni aina ya juu kabisa ya Ijmaa; kwa sababu ni makubaliano (Ijmaa) ya kivitendo ya Maulamaa na wasiokuwa wao juu ya kufanya au kuacha kufanya jambo katika hali ambayo katika aina zingine za Ijmaa (makubaliano) ni ya kimatamko na ni maalumu tu kwa wazanazuoni.[12]

Mgawanyiko wa Sirah Mutashari’ah na Hoja Yake

Katika elimu ya Usul Fiqih, kumetajwa mgawanyiko na aina za Sirah Mutashari’ah ambazo ni:

  • Sira ambazo bila shaka zilikuwako katika zama za Maasum na Maasumu mwenyewe alikuwa mmoja wa watekelezaji wake;[13] kama sira ya Waislamu ya kuwa na imani na kufanyia kazi hadithi ambazo zilikuwa zikinukuliwa na watu ambao ni thiqa (wa kuaminika na walikuwa kiunganishi baina ya Maasumu na watu wengine.[14] Usuliyyun wanasema kuwa, hakuna shaka aina hii ya sira ni hoja na yenyewe ni dalili ya hukumu ya sheria.[15]
  • Sira ambazo zilikuwako katika zama za Maasum na Maasumu mwenyewe hakuwa mmoja wa watekelezaji wake, lakini aliziunga mkono na kuzithibitisha na alikuwa akikubaliana nazo.[16] Aina hii ya sira imetambuliwa kuwa ni hoja.[17]
  • Sirah Mustahadatha au sira ambayo tuna yakini kwamba, imepatikana baada ya zama za Maasumu(as) na ina mafungamano na zama zake pia;[18] Usuliyuun wanasema aina hii ya sira amayo haisadifiani na zama za maasumu (as) ba ina ridhaa na saini (uthibitisho) na kuungwa mkono na Maasumu, haina hoja na kwa mtazamo wao haikubaliki.[19]
  • Sira ambayo tuna sgaka kwamba, kwamba, ina mafungamano na zama za maasumu (as) na aliisikia au alioona au la.[20]Baadhi ya Usuliyyun hawajaitambua aina hii ya sira kuwa ni hoja.[21]

Matumizi yake Katika Masuala ya Fikihi

Baadhi ya matumizi ya Sira Mutashari’ah katika masuala ya kifikihi ni:

  • Kwa mtazamo wa wanazauoni wa fikihi ni kuwa, Sirah Mutashari’ah imesimama juu ya ukweli kwamba ikiwa mtu atapata kitu miongoni mwa mali inayohamishika na inayoruhusiwa (mubaha), anakuwa mmiliki wake. Sirah hii iliwekwa wazi mbele ya Maasumu (a.s) na aliisikia na hapakuwa na katazo kuhusu hilo.[22]
  • Kuhusiana na kuleta umiliki katika Baiu muataat (muamala na biashara ambayo ndani yake muuzaji na mnunuzi wanafanya hivyo pasina ya aqd mahususi). Imamu Khomeini anasema. Sira Mutashari’ah kuanzia kwa wanazuoni na waja wema mpaka kwa wasiokuwa wao ilikuwa namna hii kwamba, wakati walipokuwa wakinunua sokoni mkate au nyama na kadhalika bila ya ijab na qabul (matamko ya muamala) msingi wao haukuwa juu ya ibaha (kuruhusiwa) bali ulikuwa juu ya umiliki.[23]
  • Moja ya aina za mutaharat kwa mtazamo wa mafakihi ni kuondoa najisi kutoka katika mwili wa mnyama..[24] Agha Ridha Hamedani anasema, moja ya hoja za fat’wa hii ni sira na msingi wa mutashari’ah (mtunga sheria) katika kuamiliana na wanyama ambapo licha ya kuwa alikuwa akifahamu kwamba, miili yao wakati wa kuzaliwa ilikuwa na damu ya kuzaliwa, lakini baada tu ya kuondolewa najisi, anawahesabu kuwa ni toraha na wasafi.[25]
  • Ja’afar Subhani anasema kuwa, moja ya hoja za wenye mtazamo wa kujuzu kubakia kumkalidi (kumfuata) Marjaa Taklidi aliyefariki ni Sirah Mutashari’ah[26] na amesema kuwa, Sira Mutashari’ah katika nchi zote hususan katika nchi zenye njia dhaifu za mawasiliano iliegemezwa juu ya kuwa walipokuwa wakimkalidi mujtahid enzi za uhai wake pia walimfuata baada ya kufa kwake mpaka walipopata mfano wake au bora kuliko huyo.[27]

Matumizi Yake Katika Masuala ya Usulul Fiq’h

Katika elimu ya Usul Fiq’h Sira Mutashariu’ah inatumika kama hoja kwa ajili ya kuthibitisha masuala mawili nmiongoni mwa masuala ya kimsingi ya elimu hiyo yaani kuthibitisha hoja ya Khabaa WahId na kuthibitisha Hujiyat Dhawahir.[28]

Kwa mfano, wamesema kuwa sira  ya Waislamu na wanazuoni wa kidini katika zama zote na hata zama za Mtume (s.a.w.w) na Maimamu maasumu (a.s) na miongoni mwa maswahaba wao iliegemezwa katika kuamini habari ya mtu muaminifu (thiqqah) na hakujaja katazo kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na Maimamu Maasumina (a.s) kuhusiana na hilo.[29] Pia, wamesema kuhusiana na Hujiyat Dhawahir kuwa sira ya Waislamu wote na hata masahaba wa Maimamu (a.s) yalitokana na ukweli kwamba wao walikuwa wakiamini na kutegemea maneno ya dhahiri kwa ajili kufikia maana yake na hakuna uthibitisho wa kuweko katazo kuhusiana na hilo.[30]

Msuala Yanayo Fungamana

Rejea

  1. Jam'ii Az Navisandegane, al-Faiq fi al-Usul, uk. 131, 1444 H.
  2. Jam'ii Az Navisandegane, Farhangnameh Usul Fiqh, uk. 496, 1389 S.
  3. Kadhemi Khurasani, Fawaid al-Usul, juz. 3, uk.192.
  4. Jam'ii Az Navisandegane, al-Faiq fi al-Usul, uk. 131, 1444 H.
  5. Tazama: Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 155, 1405 H; Hashimi Shahrudi, Buhuth fi Ilm al-Usul, juz. 4, uk. 233, 1417 H; Saifi Mazandarani, Badayi' al-Buhuth fi Ilm al-Usul, juz. 9, uk. 267, 1429 H.
  6. Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 158, 1405 H.
  7. Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 155, 1405 H.
  8. Saifi Mazandarani, Badayi' al-Buhuth fi Ilm al-Usul, juz. 9, uk. 268, 1429 H.
  9. Tazama: Isfahani, Hashiah al-Makasib, juz. 1, uk. 104, 1418 H.
  10. Saifi Mazandarani, Badayi' al-Buhuth fi Ilm al-Usul, juz. 9, uk. 273, 1429 H.
  11. Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 155, 1405 H.
  12. Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 155, 1405 H.
  13. Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 155, 1405 H.
  14. Sheikh Ansari, Faraid al-Usul, juz. 1, uk. 343.
  15. Kadhemi Khurasani, Fawaid al-Usul, juz. 3, uk. 192; Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 155, 1405 H; Hashimi Shahrudi, Buhuth fi Ilm al-Usul, juz. 4, uk. 247, 1417 H.
  16. Sheikh Ansari, Faraid al-Usul, juz. 2, uk. 55.
  17. Sheikh Ansari, Faraid al-Usul, juz. 2, uk. 55; Kadhemi Khurasani, Fawaid al-Usul, juz. 3, uk. 192; Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 155, 1405 H.
  18. Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 155, 1405 H.
  19. Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 155, 1405 H.
  20. Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 155, 1405 H.
  21. Mudhaffar, Usul al-Fiqh, juz. 2, uk. 156, 1405 H.
  22. Hashimi Shahrudi, Buhuth fi Ilm al-Usul, juz. 4, uk. 236, 1417 H.
  23. Imam Khomeini, Kitab al-Bai', juz. 1, uk. 55, 1410 H.
  24. Tazama: Tabatabai Yazdi, al-Urwah al-Wuthqa, juz. 1, uk. 287, 1417 H.
  25. Hamadani, Mishbah al-Faqih, juz. 1, uk. 363, 1417 H.
  26. Subhani, al-Mabsut fi Ilm al-Usul, juz. 4, uk. 701, 1432 H.
  27. Subhani, al-Mabsut fi Ilm al-Usul, juz. 4, uk. 702, 1432 H.
  28. Tazama: Sheikh Ansari, Faraid al-Usul, juz. 1, uk. 343; Hashimi Shahrudi, Buhuth fi Ilm al-Usul, juz. 4, uk. 249, 1417 H.
  29. Sheikh Ansari, Faraid al-Usul, juz. 1, uk. 343; Hashimi Shahrudi, Buhuth fi Ilm al-Usul, juz. 4, uk. 421, 1417 H.
  30. Hashimi Shahrudi, Buhuth fi Ilm al-Usul, juz. 4, uk. 249, 1417 H.

Vyanzo

  • Isfahani, Muhammad Hussein. Hashiah al-Makasib. Qom: Dar al-Mustafa li Ihya al-Turath, juz. 1, 1418 H.
  • Imam Khomeini, Sayid Ruhullah. Kitab al-Bai'. Qom: Nashr Ismailiyan, 1410 H.
  • Jami'i az navisandegane, al-Faiq fi al-Usul. Qom: Muasasah al-Nashr li al-Hauzat al-Ilmiah, 1444 H.
  • Jami'i az navisandegane, Farhangnameh Usul. Qom: Pajuheshgah Ulum va Farhang-e Islami, 1389 S.
  • Subhani, Ja'far. al-Mabsut fi Usul al-Fiqh. Qom: Muasasah Imam Sadiq (as), juz. 1, 1431 H.
  • Saifi Mazandarani, Ali Akbar. Badayi' al-Buhuth fi Ilm al-Usul. Qom: Muasasah al-Nashr al-Islami, juz. 3, 1436 H.
  • Sheikh Ansari, Murtadha. Faraid al-Usul. Qom: Majma' al-Fikr al-Islami, 1419 H.
  • Tabatabai Yazdi, Sayid Muhammad Kadhim. al-Urwah al-Wuthqa. Qom: Muasasah al-Nashr al-Islami, juz. 1, 1417 H.
  • Kadhemi Khurasani, Muhammad Ali. Farid al-Usul. Qom: Muasasah al-Nashr al-Islami, 1376 S.
  • Mudhafar, Muhammad Ridha. Usul al-Fiqh. Qom: Nashr Danesh Islami, 1405 H.
  • Hashimi Shahrudi, Sayid Mahmud. Buhuth fi Ilm al-Usul (Taqrirat Dars Usul Sayid Muhammad Baqir Sadr). Qom: Markaz al-Ghadir li al-Dirasat al-Islamiah, juz. 2, 1417 H.
  • Hamadani, Ridha. Misbah al-Faqih. Qom: Al-Muassah al-Ja'fariyah li Ihya al-Turath, 1376 S.