Al-Jihad al-Ibtidai’

Kutoka wikishia

Al-Jihad al-Ibtidai’ (Kiarabu: الجهاد الابتدائي) maana yake ni Waislamu kuanzisha vita (vya jihadi) dhidi ya washirikina na makafiri kwa lengo la kupanua Uislamu na kuhakikisha imani na itikadi ya Tawhidi na uadilifu vinatawala katika jamii. Akthari ya wanazuoni wa fiq’hi (mafakihi) wa Kishia wanatambua kuwa, kuweko Imamu Maasumu, nguvu ya kutosha ya Waislamu kwa ajili ya jihadi na kuwalingania Uislamu makafiri kabla ya kuanza vita, ni miongoni mwa masharti ya al-Jihad al-Ibtidai’; hata hivyo baadhi ya mafakihi akiwemo Sheikh Mufid (336 au 338-413 Hijiria), Sayyid Abul-Qassim Khui, Sayyid Ali Khamenei, Husseini-Ali Montazeri na Muhammad Muumin wao hawaoni kama uwepo wa Imamu ni sharti la kuwa wajibu Waislamu kuanzisha vita dhidi ya makarifi (al-Jihad al-Ibtida’i).

Baadhi ya mafakihi na watafiti wa vita vya zama za Bwana Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) vilikuwa kwa ajili ya kujihami, mkabala na wao Muhammad Taqi Misbah Yazdi anasema kuwa, kuviita vita vyote vya Uislamu kuwa ni vya kujihami kunazingatiwa kuwa ni matokeo ya kuwekwa katika mfumo wa viwango na thamani zinazokubalika na kutawala hivi sasa katika nchi nyingi za ulimwengu.

Wanazuoni wa Kishia katika kujibu tuhuma ya mgongano wa al-Jihad al-Ibtidai’ na uhuru wa imani na Aya ya La Ikrah Fi al-Din, wamesema wazi na bayana kwamba; kupitia Aya za jihadi haiwezekani kuchukua mafuhumu na uelewa ya kwamba, inapasa kuwalazimisha makafiri na washirikina kuukubali Uislamu. Kwa sababu makusudio ya al-Jihad al-Ibtida’i ni kuwasaidia wanaodhulumiwa, kupiga vita ukandamizaji na kuweka na kuandaa mazingira ya kuchagua dini kwa uhuru.

Utambuzi wa maana

Al-Jihad al-Ibtidai’ maana yake ni Waislamu kuanzisha vita dhidi ya washirikina na makafiri kwa lengo la kuwalingania Uislamu, Tawhidi na uadilifu. Katika vita hivyo Waislamu ndio wa kwanza kuanzisha vita. [1] Ayatullah Montazeri (mmoja wa Marajii Taqlidi) anasema kuwa, Waislamu kuanzisha vita maana yake ni kuwapatia watu wa mila zingine dini ya Uislamu na thamani zake; ambapo hufuatilia suala la kutokomeza dhulma, utawala wa dhalimu na kuandaa uwanja na mazingira ya kuhakikisha dini ya Mwenyezi Mungu inatawala kwa hiari na kwa chaguo la watu (na sio kwa kulazimishwa). [2]

Nafasi na umuhimu

Muhammad Taqi Misbah Yazdi (1313-1399 Hijiria Shamsia), mmoja wa wanazuoni wa elimu ya fikihi wa Kishia anasema kuwa, al-Jihad al-Ibtidai’ ni “katika dharura na mambo ya lazima ya fiq’h ya Kiislamu” na anaamini kwamba, wanazuoni wa fiq’h wa Kishia na Kisuni wameafikiana katika kuwa halali jambo hili. [3] Baadhi ya wanasema kuwa, kwa mujibu wa raia mashuhuri ya mafakihi, al-Jihad al-Ibtidai’ ni wajibu kifai [4] na akthari ya wanazuoni wa Kishia hususan mafakihi wa karne za mwanzo za Hijiria wanaamini kwamba, kuanzisha vita vya jihadi na watu hawa ni wajibu; makafiri, kundi miongoni mwa Ahlul-Kitab (kama Mayahudi, Wakristo na Wazortoshti) ambao hawakubali kutoa jizia (fidia) na kuishi kwa mujibu wa sheria za utawala wa Kiislamu. [5]

Hussein-Ali Montazeri [6] na Nassir Makarim Shirazi (alizaliwa 1305 Hijiria Shamsia) [7] miongoni mwa mafakihi wa Kishia na Neematullah Salihi Najafabadi (1302- 1385 Hijiria Shamsia), [8] wamevitaja vita vya jihadi mwanzoni mwa Uislamu kwamba; vilikuwa vya kujihami, na vilikuwa vikipiganwa kwa minajili ya kuwaokoa wanaodhulumiwa na kuondoa vizingiti vya tablighi ya Uislamu. mkabala na wao Muhammad Taqi Misbah Yazdi (1313-1399 Hijiria Shamsia) anasema kuwa, hatua ya wanazuoni wa Kiislamu ya kuviita vita vyote vya Uislamu kuwa ni vya kujihami kulitokana na fremu za vigezo na thamani zinazokubalika na kutawala hivi sasa katika nchi nyingi za ulimwenguni (uliberali, kupigania uhuru) na hivyo kulihalalisha hilo. [9]

Masharti ya al-Jihad al-Ibtidai

Kwa mujibu wa nadharia mashuhuri za Maulamaa wa Kishia, kuanzisha vita Waislamu dhidi ya makafiri (al-Jihad al-Ibtidai’) kuna masharti matatu:

  1. Kuwepo Maasumu: Kwa muktadha huo haijuzu kuanzisha jihadi katika zama za ghaiba.
  2. Nguvu za kutosha za Waislamu kwa ajili ya kuanzisha jihadi.
  3. Kuwalingania makafiri Uislamu na kutimiza hoja kabla ya kuanza vita vyenyewe. [10]

Kuwepo Imamu Maasumu na kutoa idhini yeye au naibu wake maalumu, [11] kwa mujibu wa kauli mashuhuri ya mafakihi wa Kishia akiwemo Sheikh Tusi (385-460 Hijiria), [12] Kadhi Ibn Barraj (takribani 400-481 Hijiria), [13] Ibn Idris, (takribani 543-598 Hijiria) [14] Muhaqqiq Hilli (602-676 Hijiria), [15] Allama Hilli (648-726 Hijiria), [16] Shahid Thani (911-955 au 965 Hijiria) [17] na Sahib al-Jawahir (1202-1266 Hijiria), [18] ni sharti la kuanzisha vita vya jihadi Waislamu [19] na haijumuishi manaibu wote kiujumla (mafakihi). [20]

Pamoja na hayo, baadhi ya mafakihi kama Sheikh Mufid, [21] Abu Salah Halabi (374-447 Hijiria), [22] na Salar Deylami (aliaga dunia: 448 Hijiria), [23] hawatambui kama uwepo wa Imamu Maasumu ni sharti la kuanzisha jihadi na kwa muktadha huo wanaamini kwamba, inajuzu kuanzisha vita hivyo katika zama za ghaiba. [24] Baadhi ya mafakihi wa zama hizi kama Sayyid Abul Qassim Khui (1278-1371 Hijiria Shamsia) [25], Sayyid Ali Khamenei (alizaliwa 1318 Hijiria Shamsia), [26] Hussein-Ali Montazeri (1301-1388 Hijiria Shamsia), [27] na Muhammad Muumin (1316-1397 Hijiria Shamsia), wanasema kuwa, sharti la uwepo wa Imamu Maasumu haiwezekani kulithibitisha kwa mujibu wa Aya za Qur’ani na hadithi za Maasumina na hivyo wanaamini kwamba, jihadi ambayo Waislamu ndio wanaoanzisha vita (al-Jihad al-Ibtidai’) ni wajibu katika zama ghaiba ya Maasumu pia kwa sharti la kutimia masharti; [28] na kwa mujibu wa baadhi neno “Imamu Muadilifu” lililokuja katika hadithi za jihadi halina maana ya Imamu Maasumu. [29]

Kupingana na uhuru wa itikadi

Makala asili: Uhuru wa itikadi na Aya ya La ikrah fi ddin

Kwa mujibu wa itikadi ya baadhi al-Jihad al-Ibtidai’ hupelekea kueneza Uislamu kupitia kutisha na kulazimisha watu itikadi na hilo linapingana na Aya ya: ((لاَ إِكْراهَ فی الدِّينِ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَیِّ ; Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu)). [30] Kwa mujibu wa itikadi yao Aya hii inapinga kulazimisha watu katika dini. [31] Katika kujibu shubha hii, Maulamaa wa Kishia wamekuwa na utendaji tofauti kama vile:

  1. Aya zote za jihadi katika Qur’an iwe ni kwa njia ya moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, zina sharti na qayyid hii kwamba, jihadi inapaswa khwa kwa ajili ya kuwasaidia wanaodhulumiwa, kupambana na ukandamizaji na kuandaa mazingira ya kuchagua dini kwa uhuru kamili na sio kwa ajili ya kutwisha na kulazimisha dini. Baadhi wakiwa na utendaji huu, wamevitambua vita vyote vya jihadi kwamba, ni vya kujihami na kujitetea. [32]
  2. Hakuna Aya yoyote miongoni mwa Aya za jihadi ambayo imewajibisha jihadi kwa Waislamu kwamba, wapigane vita na washirikina na wawalazimishe kuukubali Uislamu na kama wasipokubali basi wawaue. [33] Fauka ya hayo, Ayatullha Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran anaamini kuwa, haiwezekani kueneza masuala ya itikadi kwa kutumia nguvu na mabavu. [34]
  3. Muhammad Taqi Misbah Yazdi (1313-1399 Hijiria Shamsia) anaamini kuwa, kuhalalishwa “al-Jihad al-Ibtidai” katika Uislamu, [35] lengo lake ni kutambua haki, kumuabudu Mwenyezi Mungu na kutawala dini ya Mwenyezi Mungu. Na sio kwa ajili ya kutaka madaraka, mamlaka na uongozi na sio kwa ajili ya maslahi ya kiuchumi na kimaada ya kila jamii; [36] kwani kuabudiwa Mwenyezi Mungu katika pembe zote za dunia kunahesabiwa kuwa ni katika haki Zake ili kupitia kuanzisha jihadi (ambayo kwa namna fulani ni kutetea na kuhami Tawhidi) kutokomezwe shirki, ukafiri, dhulma na ufisadi wa washirikina na makafiri na hivyo kuifanya Tawhidi itawale duniani. Sio kwa maana hii kwamba, watu wote katika dunia walazimishwe kuwa Waislamu. [37] Ayatullah Montazeri anasema, maana hii inaafikiana na Aya ya 256 ya Surat al-Baqarah. [38].

Monografia

  • Jihad Ebtidai dar sunat va sire nabavi; mwandishi Muhammad Murvarid. Mwandishi wa kitabu hiki sambamba na kubainisha mafuhumu na maana ya jihadi na aina zake anaamini kwamba, Jihad Ibtidai’ licha ya tofauti iliyonayo na jihadi ya kujihami; katika sira na mwenendo wa Mtume (s.a.w.w) ilikuwa na vigezo vya jihadi ya kujihami na kwa lengo la kuleta usalama. [39]
  • Jihad Ebtidai dar Qur’an Karim; mwandishi Muhammad Javad Fadhil Lankarani. Mwandishi wa kitabu hiki amechukua mkondo na utendaji wa kifiq’h na kitafsiri ambapo amezifanyia utafiti Aya ambazo zinazungumzia kuanzisha jihadi na makafiri na washirikina na kisha anatoa majibu ya shubha (utata) za watu ambao wanasema kuwa, baadhi ya aya za Qur’an zinakinzana na uhalili wa kuanzisha jihadi. [40]

Rejea

Vyanzo

  • Alquran
  • Abus Shalah Halabi, Taqi bin Najm, Al-Kāfī Fī al-Fiqh. Riset Ridha Ustadi, Isfahan: Perpustakaan Amirul Mu'minin Ali (a.s) al-'Ammah.
  • Adrikni, Muhammad Jawad, Abul Qasim Muqimi Haji, Jihad, Salah satu makalah dalam Andisye Name-e Enqelab-e Eslami, Tehran: Yayasan Pazuhesyi-e Farhanggi-e Enqelab-e Eslami, 1398 HS/2020.
  • Allamah Hilli, Hasan bin Yusuf, Tadzkirah al-Fuqahā', Qom: Yayasan Āl al-Bait (a.s) Li Ihya' at-Turats, 1414 H.
  • Amid Zanjani, Abbas Ali, Feqh-e Sehasi, Tehran: Amir Kabir, 1377 HS/1999.
  • Anshari (Khalife Shushtari), Muhammad Ali. Al-Mausū'ah al-Fiqhiyyah al-Muyassarah, Qom: Majma' al-Fikr al-Islami, 1415 H.
  • Bahrami, Qudartullah. Nizam-e Sehasi-e Ejtema'i-e Eslami, Qom: Sepah-e Pasdaran-e Enqelab-e Eslami, 1380 HS/2002.
  • Ibn Idris Hilli, Muhammad bin Manshur, As-Sarā'ir al-Hāwī Li Tahrīr al-Fatāwā, Qom: Hahasan an-Nashr al-Islami, 1410 H.
  • Jihad-e Ebteda'i Dar Qur'ān-e Karīm, Site Fazellankarani. Diakses tanggal 20 Desember 2022.
  • Jihad-e Ebteda'i Dar Sunnat Wa Sire-e Nabawi, Site Islamic-rf, Diakses tanggal 20 Desember 2022.
  • Jihad-e Ebteda'i, Site Makarem, Diakses tanggal 13 Juli 2017.
  • Jawid, Muhammad Jawad, Ali Muhammad Dust, Huquq-e Bashar-e Mu'asher Wa Jihad-e Ebteda'i Dar Eslam-e Mu'asher, Jurnal Pazuhesh Name-e Huquq-e Eslami. Tahun 11. Vol. 2, 1389 HS/2011.
  • Kamyab, Hussein, Ahmad Qudsi. Barresi-e Shubhe-e Jahad-e Ebteda'i Dar Tafsir-e Āye-e لا إكراه في الدين, Majalah Muthale'at-e Tafsiri, Vol: 11, 1391 HS/2013.
  • Khamene'i, Sayyid Ali, Muthabeq Ba Fatawa-e Hazrat-e Ayatullah Khamene'i. Tehran: Hahasan Pazuheshi-e Farhangg-e Enqelab-e Eslami, 1398 HS/2020.
  • Khu'i, Sayyid Abul Qasim, Minhāj ash-Shālihīn, Qom: Madinah al-'Ilm, 1410 H.
  • Mishbah Yazdi, Muhammad Taqi, Akhlaq Dar Qur'ān, Qom: Entesharat-e Muassese-e Amuzeshi Wa Pazuhesyi-e Emam Khomeini, 1391 HS/2013.
  • Mishbah Yazdi, Muhammad Taqi, Jang Wa Jahad Dar Qur'ān, Qom: Entesyarat-e Muassese-e Amuzeshi Wa Pazuheshi-e Emam Khomeini, 1383 HS/2005.
  • Muhaqqiq Hilli, Ja'far bin Hassan, Sharā'i' al-Islām Fī Masā'il al-Halāl Wa al-Harām. Qom: Esma'ilihan, 1408 H.
  • Mu'min, Muhammad, Jihad-e Ebteda'i Dar Ashr-e Gheibat, Majalah Feqh-e Ahl-e Beit, Vol: 26, 1380 HS/2002.
  • Muntazeri, Hussein Ali. Dirāsāt Fī Wilāyah al-Faqīh Wa Fiqh ad-Daulah al-Islāmiyyah, Qom: Al-Markaz al-'Alami Li ad-Dirasat al-Islamiyyah, 1409 H.
  • Muntazeri, Hussein Ali, Mujazatha-e Eslami Wa Huquq-e Bashar. Qom, 1429 H.
  • Muntazeri, Hussein Ali, Pasokh Be Porseshha'i Peiromun-e Mujazatha-e Eslami Wa Huquq-e Bashar, Qom: Orghan-e Danesh, 1387 HS/2009.
  • Qadhi Ibn Barraj, Abdul Aziz, Al-Muhaddzab, Qom: Hahasan an-Nashr al-Islami, 1406 H.
  • Salar Dailami, Hamzah bin Abdul Aziz, Al-Marāsim Fī Fiqh al-Imāmī, Riset Mahmud Bustani, Qom: Manshurat al-Haramain, 1404 H.
  • Shahib Jawahir, Muhammad Hassan, Jawāhir al-Kalām Fī Sharh Sharā'i' al-Islām, Beirut: Dar Ihya' at-Turath al-'Arabi, 1404 H.
  • Shahib Najaf Abadi, Ni'matullah. Jahad Dar Eslam. Tehran: Nasyr-e Nei, 1386 HS/2008.
  • Sharami, Saifullah, Adalat Nezad, Sa'id. Jahad. Jurnal Daneshname-e Jahan-e Eslam. Tehran: Bunyad-e Dayirah al-Ma'arif-e Eslami, 1386 HS/2008.
  • Shahid Thani, Zainuddin bin Ali, Ar-Raudhah al-Bahiyyah Fī Sharh al-Lum'ah ad-Damishqiyyah, Riset Kalantar, Qom: Perpustakaan ad-Dawari, 1410 H.
  • Sheikh Mufid, Muhammad bin Muhammad, Al-Muqni'ah, Qom: Yayasan an-Nashr al-Islami, 1410 H.
  • Sheikh Tusi, Muhammad bin Hassan, Al-Mabsūth Fī Fiqh al-Imāmiyyah, Tehran: Perpustakaan al-Murtadhawiyyah Li Ihya' al-Āthar al-Ja'fariyyah, 1387 H.