Nenda kwa yaliyomo

Al-Ash'ath bin Qays al-Kindi

Kutoka wikishia

Al-Ash'ath bin Qays al-Kindi (Kiarabu: الأشعَث بن قَيس الكِندي) (aliaga dunia 40 H) alikuwa mmoja wa makamanda wa jeshi la Imamu Ali (a.s) katika Vita vya Siffin ambaye aliunga mkono maamuzi ya Abu Musa Ash’ari na akazuia kuendelea kwa vita na Mu’awiya bin Abi Sufyan. Ash'ath alikuwa na mchango katika kusimama vita vya Siffin na katika suala la usuluhishi na upatanishi, alimpinga Abdullah bin Abbas kama hakimu kwa niaba ya Imamu Ali (a.s) na Wairaqi na akapendekeza Abu Musa Ash'ari apewe jukumu hilo. Baada ya vita vya Nahrwan, pale Imam Ali (a.s) alipotaka kupigana na Muawiya, Ash’ath alimpinga kwa kisingizio cha kuchoka na vita, jambo ambalo lilidhoofisha hamasa ya askari na kusababisha Imam Ali (a.s) aachane na uamuzi wa kupigana na Mu'awiyah.

Kwa mujibu wa ripoti za kihistoria, Ash'ath alifahamu kuhusu mpango wa kuuawa shahidi Imam Ali (a.s) na kwa mujibu riwaya kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), pia alikuwa na nafasi katika kifo cha Imamu Ali (a.s). Alikuwa mzee na kiongozi wa kabila la Kinda na wakala wa Othman bin Affan na Imam Ali (a.s) huko Azerbaijan.

Muhammad na Qays, ambao walihusika katika kifo cha kishahidi cha Imamu Hussein (a.s) na Ja'dah, mke wa Imamu Hassan (a.s), ambaye alimuua Shahidi Imamu Hassan kwa kuchochewa na Muawiyah, alikuwa ni mmoja wa watoto wa Ash'ath bin Qays.

Maisha

Ash'ath bin Qays alitoka katika kabila la Kinda na mzaliwa wa Hadhamout Yemen. [2] Baadhi ya wanahistoria wamempa jina la Ma'dikarib, jina lake la utani la Ash'ath likimaanisha nywele zilizovurugika (ambayo ina maana pia ya mtu mwenye tabia mbaya) na lakabu yake ni Abu Muhammad. [3] Mwaka wa 10 Hijria [4] alikwenda Madina kwa Mtume (s.a.w.w) akiwa ameafuatana na baadhi ya watu wa kabila lake na akasilimu. [5] Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana anahesabiwa kuwa miongoni mwa masahaba wa Bwana Mtume (s.a.w.w) na wasifu wake umebainishwa na kutajwa katika vyanzo na vitabu vilivyoandikwa kuwazungumzia masahaba wa Mtume (s.a.w.w). [6] Kadhalika katika vyanzo na vitabu vya Ahlu-Sunna kikiwemo kitabu cha Sahih Bukhari [7] na Sahih Muslim kuna hadithi zake alizopokea kutoka kwa Mtume (s.a.w.w). [8]

Ash'ath alikataa kutoa kiapo cha utii kwa Abu Bakr baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w). [9] Abu Bakr alituma askari Yemen kumkamata mateka Ash'ath na kumpeleka Madina. Baada ya hapo, Abu Bakr alimwachilia Ash'ath na akamuoa dada yake Umm Far'wah. [10]

Wakati wa ukhalifa wa Omar bin Khattab, Ash'ath alishiriki katika vita vya Yarmouk, kutekwa na kukombolewa Iraq [11] na vita vya Qadisiyah [12] na kukaa Kufa. [13] Aidha alikuwa wakala wa Othman bin Affan huko Azerbaijan [14] na alibakia katika nafasi hiyo pia katika zama za ukhalifa wa Imamu Ali (a.s). [15] Kwa mujibu wa Ibn Habib, mwanahistoria wa karne ya tatu, Ash'ath alikuwepo katika jeshi la Imam Ali (a.s) katika Vita vya Jamal [16], lakini barua ya Imamu Ali (a.s) kwake, inaonyesha kwamba hakuwepo katika Vita vya Jamal. [17]

Ash'ath alikufa akiwa na umri wa miaka 63. [18] Kifo chake kilirekodiwa katika mwaka wa 40 [19] au 42 Hijria. [20] Abu Na'im anaandika katika Ma'rifat al-Sahaba kwamba, Ash'ath alikuwa hai kwa usiku arubaini baada ya kuuawa shahidi Imam Ali (a.s.) na baada ya kifo chake, Imamu Hassan (a.s), ambaye alikuwa mkwe wake, alimswalia Sala ya maiti. [21]

Mchango Wake katika Kusimama Vita vya Siffin

Ash'ath alikuwa katika jeshi la Imamu Ali (a.s) katika vita vya Siffin na alikuwa mkuu wa jeshi la makabila ya Kinda na Rabi'ah. [23] Kwa mujibu wa riwaya ya Nasr bin Muzahim, Imam Ali (a.s.) alichukua uongozi wa makabila haya kutoka kwake na akaukabidhi kwa Hassan bin Makhduj, lakini baadhi ya masahaba wa Yemen wa Imamu Ali (a.s) hawakuiona hatua hiyo kama yenye maslahi na yenye kufaa. Matokeo yake, kukaibuka tofauti katika jeshi la Imamu Ali (a.s). Mu'awiyah alijaribu kumvutia Ash'ath, lakini Imamu Ali (a.s) alimpa uongozi wa mrengo wa kulia wa jeshi. [24] Wakati jeshi la Mu'awiya lilipolifungia maji ya Mto Furat jeshi la Imamu Ali (a.s), Ash'ath aliliondoa eneo hilo toka katika udhibiti wa jeshi la Sham [25]

Makala kuu: Barua ya Imamu Ali kwenda kwa Ash'ath bin Qays

Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, Ash'ath hakuona kuwa ni vyema kuendeleza vita dhidi ya Lailat al-Harir, (moja ya usiku ambao kulijiri mapigano makali baina ya jeshi la Muawiya na Imamu Ali) wakati idadi kubwa ya watu waliuawa na ushindi wa jeshi la Imam Ali ulikuwa karibu, [26] aliona kuwa, sio kwa maslahi kuendelea na vita. [27] Baada ya Muawiya kupata habari za msimamo wa Ash'ath alitoa amri ya kutundikwa Qur'ani juu ya mikuki na kutaka maamuzi na usuluhishi wa Qur’an wakisema kuwa, la Hukma illa Lilahi yaani Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu [28] Baada ya jeshi la Mu'awiya kutundika Qur'ani juu ya mikuki, Ash'ath alimpinga Imam Ali (a.s) [29] na kumtaka akubali mwito la takwa la kutolewa uamuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu.[30] Inasemekana kwamba Ash'ath kabla ya vita vya Siffin, alipopokea barua kutoka kwa Imamu Ali (a.s.), alikuwa na nia ya kujiunga na Muawiya, lakini masahaba wake walimzuia asifanye hivyo. [31]

Kuunga Mkono Maamuzi ya Abu Mussa ash'ari

Katika vita vya Siffin, Ash'ath alipenda maoni ya Mu'awiya kuhusu kuweka hakimu mmoja kutoka Syria na mwingine kutoka Iraq. [32] Alimpinga Abdullah bin Abbas kama hakimu kwa niaba ya Imamu Ali (a.s) na Wairaqi, na mwenyewe alipendekeza Abu Musa Ash'ari .[33] Kwa mujibu wa Yaqoubi, mwanahistoria wa karne ya 3 Hijria, wakati wa kuandika mkataba wa amani, wawakilishi wa majeshi hayo mawili walitofautiana juu ya cheo cha Amirul-Mu'minin kwa ajili ya Imam Ali (a.s) na Ash'ath alitaka kifutwe kwenye mkataba wa amani. [34]

Ash'ath aliamini kwamba kabla ya kuanza tena vita na Mu'awiyah, anapaswa kupigana na Makhawariji wa Nahrwan, [35] lakini baada ya vita vya Nahrawan, Imam Ali (a.s) alipowaita washirika wake kupigana na Mu'awiyah, alitoa kisingizio cha kuchoka na vita na hivyo hawezi kuendelea na vita. Maneno yake yalikuwa na athari kwa jeshi la Imam Ali (a.s) na kwa sababu hiyo, Imam Ali (a.s) aliacha kupigana na Mu'awiyah na akaenda Kufa. [36]

Kuwa Pamoja na Muljam katika Kuumuua Imamu Ali (a.s)

Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, Ash'ath alikuwa anafahamu kuhusu mpango wa kuuawa shahidi Imamu Ali (a.s). Kwa mujibu wa riwaya ya Yaqoubi, Ibn Muljam alipokwenda Kufa kutoka Misri kwa ajili ya kumuua Imamu Ali (a.s), alikaa katika nyumba ya Ash'ath kwa muda wa mwezi mmoja na alikuwa akitayarisha upanga wake. [37] Kwa mujibu wa ripoti, Ash'ath alimtaka Ibn Muljam achukue hatua ya kumuua Imamu Ali (a.s) kabla ya kupambazuka asubuhi ili asifedheheshwe na watu. [38] Baada ya pigo la Ibn Muljam, Ash'ath alimtuma mwanawe Qays ili akafahamu hali ya Imamu Ali (a.s) na kumjuza. [39] Hata hivyo, kuna riwaya kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) ambayo inaonyesha mchango wa Ash'tah katika kuuawa shahidi Imamu Ali (a.s). [40] pamoja na hayo, kuna ripoti ya kihistrora ya kwamba Ash'ath alipofahamu nia ya Ibn Muljam Muradi, alimfahamisha Imamu Ali (a.s). [41] Kama ilivyoelezwa katika vyanzo vya kihistoria, Ash'ath alimtishia kifo Imam Ali (a.s) [42] Inasemekana kwamba Imamu Ali (a.s) hakuwa akimuamini [43] na alimlaani na kumwita kuwa ni mtu mnafiki. [44]. Kwa mujibu wa Murtaza Mutahhari katika kitabu Dastan Rastan, Ash'ath alikuwa mtu mwenye tabia mbaya ambaye hakupenda njia na mbinu ya Ali na alikuwa na uhusiano wa siri na Mu'awiyah. [45] Aidha anamtambua Ash'ath kama mwanamfalme ambaye alikuwa akipingana na Imamu Ali (a.s) kwa taasubi zilezile za kikaumu na hivyo akamgeuka. [46]

Watoto

Baadhi ya watoto na wajukuu wa Ash'ath ni:

Rejea

Vyanzo