wikishia:Featured articles/2024

Kutoka wikishia

Kuonekana Mwenyezi Mungu (Kiarabu: رؤية الله) ni maudhui ya kiteolojia (kiitikadi) nayo ni kuhusiana na uwezekano wa kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho. Wasomi wa elimu ya teolojia wa madhehebu ya Shia Imamiyyah na wale wa kundi la Mu’tazila wanaamini kwamba, Mwenyezi haonekani kwa macho hapa duniani wala kesho akhera. Mtazamo wao ni kwamba; kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho kunalazimu Muumba huyo awe na mwili na umbo, na inafahamika kwa kawaida ya kwamba kila chenye mwili au kiwiliwili kina sehemu maalumu, na kuamini hivyo ni kumwekea mipaka Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa ni kinyume na hivyo kwa mujibu wa mantiki na mafundisho ya Uislamu. Hata hivyo mkabala na wao, madhehebu mengi ya kiteolojia ya Ahlu-Sunna kama Ash’ari, Ahlul-Hadithi, al-Mujassamiya, al-Karamiyyah na Salafiyah yenyewe yanaamini kwamba, kuna uwezekano wa kumuona Mwenyezi Mungu.

Read more ...