Zuhair bin Sulaim al-Azdi

Kutoka wikishia
Makaburi ya halaiki ya mashahidi wa Karbala katika haram ya Imam Hussein (a.s)

Zuhair bin Sulaim al-Azdi (Kiarabu: زهير بن سليم الأزدي) ni katika mashahidii wa Karbala katika siku ya Ashura mwaka 61 Hijiria. [1] Yeye ametambuliwa kuwa ni katika masahaba wa Imamu Ali (a.s). [2]

Mamaqani (aliaga dunia: 1351 Hijiria) anasema katika kitabu chake cha Tanqih al-Maqal ni kwamba, kwa mujibu wa ripoti za waandishi wa historia, aliingia Karbala akiwa pamoja na jeshi la Omar bin S'ad, lakini usiku wa Ashura alipofahamu kuhusu uamuzi wa jeshi la Omar bin Sa'ad wa kumuua Imamu Hussein (a.s) aliachana na jeshi hilo na kujiunga na Imamu Hussein (a.s). Zuhair aliuawa shahidi siku ya Ashura katika shambulio la kwanza. [3] Maudhui hii imekuja pia katika kitabu cha Ibsar al-Ain cha Muhammad Samawi (aliyeaga dunia: 1371 HijIria). [4] Katika Ziyarat al-Shuhadaa Zuhair anasalimiwa kwa ibara ya: ((السَّلَامُ عَلَى زُهَيْرِ بْنِ سُلَيْمٍ الْأَزْدِی ; Amani (ya Mwenyezi Mungu) iwe juu ya Zuhair bin Sulaim al-Azdi)). [5]

Zuhair alikuweko katika vita vya Qadisiyyah na alimuua mmoja wa makamanda wa jeshi la Iran aliyejulikana kwa jina la Nakharjan au Nakhir Khan. [6]

Yeye ni kaka wa Mikhnaf bin Sulaim al-Azdi, sahaba wa Mtume (s.a.w.w) na aliyekuwa mmoja wa makamanda wa jeshi la Imamu Ali (a.s). [7]

Katika vyanzo vya historia kumetajwa majina ya watu kama Abdallah bin Zuhair bin Sulaim kuwa ni mmoja wa makamanda wa jeshi la Omar bin Sa'ad katika tukio la Karbala [8] na kutambuliwa kama mtoto wa Zuhair. [9]