Yawm al-Hussein (ada ya kidini)
Wakati wa Kufanyika | Masiku ya Muharram na Safar |
---|---|
Mahali pa Kufanyika | Misikitini, Vyuoni, Husseiniyyah n.k |
Wenevu Kijiografia | Iran, India, Pakistan, Uingereza, Marekani |
Asili Kihistoria | Kufa Kishujaa kwa Imamu Hussein (a.s) katika Tukio la Karbala |
Nyenzo na Nembo | Uvaaji wa Nguo Nyeusi |
Siku ya Hussein (Kiarabu: یوم الحُسَین), (Kingereza: Hussein Day) ni jina la majimui na mkusanyiko wa ada za kidini za Waislamu wa madhehebu ya Shia ulimwenguni ambayo kikawaida hufanyika kwa ajili ya kukumbuka kifo na kuuawa shahidi Imamu Hussein (a.s). Ada na kawaida hii ya kidini hufanyika katika mataifa mbalimbali duniani na katika kumbukumbu hii hutolewa hotuba mbalimbali kuhusiana na shakhsia ya Imamu Hussein bin Ali (a.s), mashahidi wa Karbala na maana ya kufa shahidi. [1]
Katika baadhi ya hadithi pia tukio la Karbala limetajwa kwa jina la Yawm al-Hussein (Siku ya Hussein). [2] Katika miji ya Iran kama vile Isfahan na Boroujerd pia hufanyika mikusanyiko alasiri ya siku ya Ashura (siku ya kumi ya mwezi Muharram) kwa jina la Yawm-ul-Hussein. [3] Katika jiji la Bengaluru (Bangalore), India pia mkusanyiko wenye jina hili hufanyika kila mwaka wakati wa siku za maombolezo ya Muharram na Safar (Mfuunguo Nne na Mfunguo Tano). Katika hafla hii, wazungumzaji kutoka dini na madhehebu mbalimbali hutoa hotuba kwa lugha za Kiarabu, Kiurdu na Kiingereza kuhusu Imam Hussein (a.s). [4] Waandaaji wa kongamano hili hutangaza wito wa kueneza usawa na kulaani vitendo vya unyanyasaji na dhulma dhidi ya Waislamu na wafuasi wa dini nyinginezo. [5] Pia, wakati wa hafla hii, bendera za maombolezo huwasilishwa kwa taasisi mbalimbali za India na kutundikwa katika baadhi ya miji ya nchi hiyo. [6]
Kila mwaka katika kumi la tatu la mwezi Muharram, Jumuiya ya Wanafunzi wa Imamiya nchini Pakistan huandaa kongamano linaloitwa «Siku ya Hussein» katika vyuo vikuu vya Pakistan. [7] Kuna ripoti za upinzani wa serikali za mitaa za Pakistan dhidi ya kongamano hilo. [8] Hata hivyo kupitia baadhi ya ripoti inafahamika kwamba, maadhimisho ya kuzaliwa kwa Imamu Hussein (a.s) nchini Pakistan pia huitwa Siku ya Hussein.[9]
Hafla ya «Siku ya Hussein» (Hussein Day) pia hufanyika mjini New York. Mashia wa Marekani huandamana kila mwaka siku ya Jumapili iliyo karibu zaidi na Ashura na kuwapa wageni matawi ya maua na vipeperushi vinavyoelezea tukio la Karbala. [10] Pia kuna ripoti za siku hii nchini Uingereza. Mnamo mwaka wa 2013, jumuiya ya Shia ya Wessex ilifanya mkutano uliohudhuriwa na Wakristo, Wayahudi na madhehebu mengine za Kiislamu nchini Uingereza katika Kituo cha Al-Mahdi nchini Uingereza. [11] Jumuiya ya Ahlul-Bayt huko Scotland mnamo tarehe 12 Oktoba kila mwaka huendesha majimui ya mihadhara iitwayo «Siku ya Hussein» ikiwa na maudhui ya kuuawa shahidi Imamu Hussein (a.s), maana ya kufa shahidi na kupigania uadilifu. [12]
Maktaba ya Picha
-
Hussein Day katika Mji wa New York-Marekani.
-
Hussein Day katika Salt Lake City nchini Marekani.
-
Mkutano wa Siku ya Hussein Borujourd.
-
Maadhimisho ya Hussein Day huko Isfahan-Iran.
-
Mkutano wa Hussein Day, Chuo Kikuu cha Karachi, Pakistan.
-
Mkutano wa Hussein Day huko Wessex-Uingereza.
-
Maadhimisho ya Siku ya Husayn huko Scotland.
-
Mkutano wa Siku ya Hussein huko Bangalore-India.