Vita vya Mtume (s.a.w.w)

Kutoka wikishia

Vita vya Bwana Mtume (s.a.w.w) (Kiarabu: حروب النبي) ni vile vita vilivyofanyika baada ya Hijra ya Bwana Mtume (s.a.w.w) kutoka Makka na kuhamia Madina, vita ambavyo vilifanyika kwa lengo la kulinda jamii ya Kiislamu na kuanzisha dola ya Kiislamu. Kulingana na baadhi ya wanazuoni, vita vyote hivi vilifanyika kutokana na ukiukaji wa mapatano na makubaliano uliofanya na Wapagani (Makafiri) au kutokana harakati zao za kijeshi dhidi ya Waislamu. Kwa hivyo, madai ya Wamagharibi kwamba malengo ya vita yalikuwa ni kwa ajili ya kufikia matakwa ya kidunia, hayawezi kuwa ni sahihi na ni kinyume na nukuu na taarifa za kihistoria zilivyo.

Vita vyote ambavyo Bwana Mtume (s.a.w.w) alishiriki ndani yake, huitwa Ghazwa, na vita vyote vile ambavyo hakushiriki ndani yake, huitwa Sariyyyah. Katika taarifa za kihistoria, kuna karibu ya vita 80 vilivyorikodiwa ambavyo Bwana Mtume (s.a.w.w) alishiriki ndani yake, kati ya jumla hiyo karibu vita 30 vilipelekea mapigano mukhtasari ya kijeshi na vita vitano tu kati ya idadi hiyo vilipelekea mapigano makali ya kijeshi. Jumla ya idadi ya waliouawa imekadiriwa -kutoka kwa Waislamu na wasio Waislamu- katika vita vyote vya Mtume (s.a.w.w) ni kati ya watu 900 hadi 1600.

Qur'ani Tukufu imeashiria baadhi ya vita alivyo pigana bwana Mtume (s.a.w.w), pia Qur’ani imetaja imetaja kwa majina baadhi ya vita hivyo. Kulingana na maelezo ya wafasiri, ni kwamba; Kwa mara ya kwanza kabisa Waislamu walipewa ruhusa ya kupigana, ima kupia Aya ya 39 Surat al-Hajj au Aya ya 190 Surat Al-Baqara. Kulingana na Qur'ani, Mwenyezi Mungu aliwasaidia Waislamu katika vita kupitia nyenzo kadhaa ambazo ni; kikundi cha Malaika, kujenga khofu kwenye nyoyo za maadui, pamoja na kushusha utulivu katika nyoyo za Waumini.

Bwana Mtume katika vita vyake alionekana alionekana kuzingatia na kuchunga kanuni za kijeshi na yeye mwenye ndiye aliye kuwa akiongozi mkuu katika vita hivyo ambavyo vilikuwa na jukumu la kuleta matunda ya baadae. Aliheshimu haki za binadamu katika vita na alionya vikali dhidi ya kuwaua wanawake, watoto na wazee. Kusikiliza ushauri wa masahaba, kuepuka mauaji ya halaiki na kuteua mrithi huko Madina ni miongoni mwa nyenendo nyingine za kivita za bwana Mtume (s.a.w.w).

Bwana Mtume (s.a.w.w) alitumia mikakati na mbinu mbalimbali katika usimamizi wake wa vita, miongoni mwayo kama vile; mkakati wa kuakisi sura kanganyifu kutoka katika jesi la Waislamu, ili kufisidi njama za maadui, pamoja na kutumia vita vya kisaikolojia. Bwana Mtume (a.s.ew.w) aliwapanga askari wake katika vikosi vitano: kikosi cha mbele (washambulizi), kikosi cha kati, kikosi cha mrengo wa kulia, kikosi cha mrengo wa kushoto na kikosi saidizi. Hakuna Muislamu aliyelazimishwa kushiriki katika vita; pia walemavu na watu wadogo walizuiliwa kushiriki vitani.

Wanawake wengine kama vile Fatima Zahra (a.s), Ummu Aiman, Ummu Atiyyah na Ummu Ammarah walishiriki vitani kama walivyo shiriki wanaume, ambapo wa walijishughulisha na matibabu ya majeruhi, kuwaletea maji wapiganaji, kuandaa chakula, kukusanya pamoja na kuhifadhi mishale.

Malengo ya vita vya bwana Mtume

Bwana Mtume (s.a.w.w) alipigana vita dhidi ya maudi zake ili kueneza dini ya Kiislamu na kuanzisha dola ya Kiislamu. [1] Madui hasa wa Mtume kwa wakati huo walikuwa ni Wayahudi, Washirikina na Waroma. [2] Yeye alipambana na madui hao kwa wao walikuwa ni kizuizi cha kusimamisha dola ya Kiislamu [3] Kusitisha uvamizi wa wapagani na kuondoa fitina pia ilikuwa ni miongoni mwa malengo ya Mtume (s.a.w.w) katika vita. [4] Kabla ya bwana Mtume (s.a.w.w) kutangaza vita dhidi maadui zake, kwanza kabisa aliwashauri maadui hao kukubaliana na dini ya Kiislamu la si hivyo yeye atakuwa hana budi kukabiliana nao kwa vita. [5] Inasemekana kwamba kwa kuzingatia malengo ya kiungu, bwana Mtume (s.a.w.w) katika fasihi yake ya kidini alitumia ibara ya jihadi katika njia ya Mungu badala ya kutumia neno "vita" katika vita vyake. [6] Kulingana na baadhi ya watafiti,ni kwamba; bwana Mtume (s.a.w.w) katika vita vyake, mwanzo kabisa alikuwa akifafanua sababu, malengo, na kanuni za vita mbele ya jeshi la Kiislamu na baada ya hapo, hulifuma jeshi lenye nguvu na kuliongoza kulekea mapambanoni. [7]

Hata hivyo, watafiti wengi wa masuala ya Kiislamu wa Kimagharibi wamejaribu kuvisifu vita vya bwan Mtume (s.a.w.w), kuwa vita vilivyo kuwa na malengo ya kidunia na nia ya kushikilia utawala wa kisiasa na kiuchumi. [8] Bila shaka, wao hawana maoni yanayowiana katika kufafanua malengo ya vita vya bwana Mtume (s.a.w.w), kuna waliotaja malengo mengine kama vile; kupata ngawira na kujipatia riziki na maisha bora, tamaa ya madaraka, na kulipiza kisasi dhidi ya wapinzani wao. [9] Baadhi ya watafiti wameona madai haya kuwa siyo sahihi, na wanaamini kwamba nyaraka za kihistoria zinakanusha madai haya. [10] Pia, baadhi ya watafitii wa Kimagharibi wanaamini kwamba; Mtume (s.a.w.w) aliweza kuepuka vita kadri iwezekanavyo na alipigana pale tu ilipokuwa ni lazima, kwa ajili ya kulinda maslahi ua Uislamu na Waislamu. [11]

Vita asli (Ghazwa) na vita vya kimukhtasari (Sariyyah)

Makala asili: Ghazwa na Sariyyah

Katika vitabu vya historia ya Kiisalmu, vita vya Mtume (s.a.w.w.) viligawanywa katika makundi mawili: ghazwa na sariyyah. Ghazwa; ni vita ambavyo bwana Mtume (s.a.w.w) alishiriki na kuviongoza moja kwa moja yaya mwenyewe. [12] Sariya (vita mukhtasari); ni vita ambavyo bwana Mtume (s.a.w.w) hakushiriki ndani ya hivyo yeye mwenyewe, bali aliwatuma wanajeshi chini ya uongozi wa mtu mwingine. [13] Hata hivyo, baadhi ya wanazuoni wanaamini kwamba ufafanuzi huu kuhusiana na aina mbili hizi za vita si sahihi. Wao wanaamini kwamba ghazwa ni vita ambavyo vilifanyika kwa uwazi, na kwa idadi kubwa ya wanajeshi, na kwa mpangilio wa kijeshi, na sariya ni vita ambavyo vilifanyika kwa siri, kwa idadi ndogo ya jeshi, na bila mpangilio maalumu wa kijeshi. [14] Hata hivyo Maelezo haya mawili hayapingana na yaliopita kabla yake, juu ya mifano hai ya ghazwa na sariyyah, kwani bwana Mtume (s.a.w.w). Kwa mujibu wa ufafanuzi wa mwisho uliotolewa kuhusiana navita vya sariyyha (vita mukhtasari), ni kwamba; bwana Mtume (s.a.w.w) hakuwa akishiriki katika vita vilivyokuwa na operesheni ndogo zilizofanywa na idadi ndogo ya wanajeshi, kama vile operesheni za kushambulia kiuchokozi au kwa nia uchunguzi na upelelezi. [15]

Takwimu

Katika taarifa za kihistoria, kuna vita takriban 80 vilivyorekodiwa ambavyo viliongozwa na kupiganwa na bwana Mtume mwenyewe. [16] Kulingana na Hadithi iliyomo katika kitabu cha Tadhkiratu al-Khawas cha Imamu Hadi, idadi ya vita alivyo shiriki bwan Mtume (s.a.w.w), ni jumla ya vita 82. [17] Katika idadi hiyo ya vita vya ghazwa na sariya, takriban ni vita 30 tu vilipelekea mapambano ya kijeshi, na vita vingine vyote vilimalizika bila mapigano. [18] Pia, katika vita ambavyo vilipelekea mapigano ya kijeshi, ni vita vitano tu vilivyo kuwa muhimu ambavyo vilikuwa na mapigano makali. [19] Wanahistoria, kwa kuzingatia maelezo mbalimbali ya kihistoria, wamekadiria kuwa jumla ya waliouawa -wakiwemo Waislamu na wasio Waislamu- katika vita vyote vya Mtume (s.a.w.w.) ni kati ya watu 900 hadi 1600, [20] na jumla ya mashahidi wa Kiislamu walikuwa ni 317. [21]

Vita vya bwana Mtume katika Qur'ani

Aya ya 123 ya Surat Al-Imran, ambamo ndani yake jina la Vita vya Badr limetajwa.

Kuna idadi kadhaa ya Aya za Qur’ani zilizozungumzia vita alivyo pigana bwana Mtume (a.s.w.w), baadhi ya Aya zilizoelezea vita hivyo ni; Al-Baqarah, Al-'Imran, An-Nisa', Al-Ma'idah, Al-Anfal, At-Tawbah, Al-Ahzab, Al-Fatḥ, Al-Hashr, As-Saff, na Al-'Adiyāt. [22] Hata hivyo, ni majina ya vita vitatu tu, yaani Badr, Khandaq, na Hunain, yaliotajwa waziwazi katika Qur'ani. [26] Kwa mujibu wa maelezo ya Sheikh Tusi, mwandishi wa Tafsir al-Tibyani fi Tafsiri al-Qur’ani, ni kwamba; amri ya kwanza iliyo waamrisha au kuwapa idhini Waislamu kuingia vitani ilikuja baada ya kushuka kwa Aya ya 39 ya Suratu Al-Hajj. [27] Hata hivyo, kwa maoni ya Allama Tabatabai, mwandishi wa Tafsir al-Mizan, amri hii ilitolewa baada ya kushuka kwa Aya ya 190 ya Suratu Al-Baqarah. [28]

Misaada ya ghaibu

Katika baadhi ya vita, Mungu alimsaidia Mtume kwa msaada wa kiungu:

  • Katika vita vya Badr, kulingana na Aya ya 9 hadi 11 ya Suratu Al-Anfal, Mwenye Ezi Mungu aliwasaidia Waislamu kwa kuwapelekea Malaika. Mwenye Ezi Mungu pia aliingiza hofu nyoyoni mwa maadui zao na kuwafanya Waislamu wapate usingizi wa utulivu ili waweze kupumzika vya kutosha na hatimaye kuwashinda maadui zao. [29]
  • Katika vita vya Uhud, kulingana na Aya ya 151 ya Surat Al-'Imran, ingawa washirikina walishinda vita hivyo kwa kutumia fursa ya kosa la kundi fulani la Waislamu, na kama Mweye Ezi Mungu asengetia khofu vifuani mwao, basi wangeweza kuvamia mji wa Madina na kuung’oa Uislamu, ila kutokana na khofu walighairi njiana na kuamua kurudi Makka. [30]
  • Katika vita vya Ahzab, kulingana na Aya ya 9 ya Surat Al-Ahzab, makafiri wa Makka na makabila ya jirani waliungana pamoja ili kuuvamia mji wa Madina, kumuua Mtume, na kuung’oa Uislamu. Hata hivyo, Mwenye Ezi Mungu Mungu aliwasaidia Waislamu kwa kuwapelekea jeshi lisiloonekana, upepo, pamoja na dhoruba. [31]
  • Katika vita vya Hunain, kulingana na Aya ya 26 ya Surat At-Tawbah, kundi fulani la jeshi la Waislamu lilijivuna na hatimae makafiri walishinda katika vita hivyo mwanzoni. Hata hivyo, Mungu aliwashushia waumini hao amani na utulivu ili waweze kujiandaa tena kwa vita, na hatimaye kuwashinda maadui zao. [32]

Je, Vita vya bwana Mtume, ni jihadi ya kujilinda au ya kuanzisha vita?

Kwa maoni ya baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu, bwana Mtume (s.a.w.w) hakuwahi kuanzisha vita, na vita vyote vilivyo piganwa na bwana Mtume (s.a.w.w) ima vilisababishwa na kule makafiri kukiuka mapatano na kuharibu mikataba ya amni au harakati zao za kijeshi zilizokuwa zikihatarisha amani. [33] Pia, kwa maoni ya mwanazuoni maarufu wa Kishia; Muhammad Taqi Misbah Yazdi, ni kwamba; jihadi anzilishi ni moja ya mifano ya vita vya kujilinda, kwa sababu kama ilivyokuwa ni wajibu kuilinda roho na ardhi za Waislamu, basi pia ni wajibu kuilinda dini na haki ya Mwenye Ezi Mungu. [34]

Nyenendo na silka za Mtume katika vita

Mtume (s.a.w.w) alizingatia na kuchunga kanuni za kijeshi katika vita. [35] Alikuwa akitilia maanani mno nidhamu ya wanajeshi, na katika uongozi wake, hakuna mtu aliyeruhusiwa kuacha mahali pa kazi yake. [36] Mtume (s.a.w.w) aliongoza vita vyote vikubwa na vyenye hatima kwa Uislamu na Waislamu, navyo ni kama vile; Badr, Uhud na Khandaq, katika vita hivi yeye mwenyewe ndiye aliye kuwa jemedari ndani yake. [37] Kulingana na nukuu zilizokuja katika Nahjul Balagha; siku zote bwana Mtume (s.a.w.w), alikuwa ni mtu wa mstari wa mbele kabisa wa vita, na pale Waislamu walipotikisika kutokana na mawimbi makali ya kivita, walikuwa walikimbilia kwa bwana Mtume (s.a.w.w), ili kujilinda na mawibi hayo. [38] Bwana Mtume (s.a.w.w) alizingatia sana umuhimu wa kupata taarifa za adui [39] na alikuwa akiwatuma wapelelezi kwenda katika jeshi la maadui zao na kukusanya taarifa muhimu kutoka kwao, na akahakikisha kuwa siri za jeshi la upande wa Waislamu hazivuji na wala hazijulikani. [40] Mambo yafuatayo yameorodheshwa na kutajwa kuwa ni miongoni mwa mbinu za bwana Mtume katika vita:

  • Kuheshimu haki za binadamu: Kulingana na baadhi ya watafiti, bwana Mtume (s.a.w.w), alijitahidi katika vita vyake kupunguza vifo na upharibifu wa mali. [41] Alikataza kuua kwa mfumo wa mateso ya kukatkat amiili maadui zao, kukata miti na kuua wanawake, watoto na wazee. [42] hata wanawake na watoto pia walishiriki katika vita dhidi ya Waislamu, pia aliamuru kuto waua kwa kadri iwezekanavyo. [43] Kulingana na baadhi ya watafiti, kwa mara ya kwanza kabisa duniani, kanuni zinayohusiana na wafungwa wa uraiani wasio husika na jeshi, ziliandikwa katika dini ya Kiislamu. [44]
  • Diplomasi hai (endelevu) katika vita: Mtume ili kupata mafanikio zaidi, pamoja na vita, alizingatia pia kudumisha diplomasia hai; kwa hiyo, alitiana mikataba ya kisiasa na makundi yasiofungamana na upande wowote, ili kuzuia makundi hayo kujiunga na kujiunga na maadui wakuu wa Uislamu, mikataba ambayo iliwaruhusu Wialamu kuweza kufaidika na nguvu uwezo wa vikundi katika kukidhi mahitaji yao. [45] Bwana Mtume (s.a.w.w) alifanya mazungumzo na maadui zake, na pale alipoona kuwa; mazungumzo ya amani na suluhu ni yenye manufaa kwa upande wa Waislamu, aliamua kutia saini mkataba wa amani na adui zake ili kufikia malengo yake, na vinginevyo aliamua kuachana na mazungumzo hayo. [46]
  • Kuunda baraza la vita: [47] Kuunda kwa baraza la vita ni miongoni kwa mikakati ya bwana Mtume (s.a.w.w), mfano wake ni kuundwa kwa baraza la ndani la vita, lililokuwa likishughulikia mapambano ya ndani ya mji, au lile baraza la nje la vita lililoundwa katika vita vya Uhud, [48] au lile baraza lililompa bwana Mtume shauri wa kuchimba handaki katika vita vya Handaki. [49]
  • Kumteua makamu wa kushika na fasi yake huko Madina: Bwana Mtume (s.a.w.w) kila wakati na katika kila vita, alikuwa akimteua makamu wa kushika nafasi huko Madina kabla yeye kuondoka na kuelekea vitani. [50]
  • Usamehevu na ukarimu: Katika ukombozi wa mji wa Makka, aliwapa msamaha viongozi wa Quraishi, wakati wao hapo awali walipokuwa na nguvu, walimtoa bwana Mtume kutoka katika mji wake (wa Makka) na kuwaua jamaa na wafuasi wake bila ya huruma. [51]
  • Kuepuka mauaji ya halaiki: Bwana Mtume alikataza kutokomeza miji kwa kutumia sumu. [52]

Washiriki wa vita

Mtume hakulazimisha Muislamu yeyote kushiriki vitani. [53] Ingawa alinunua silaha kutoka kwa wasio Waislamu, ila hakutumia nguvu kazi yao. [54] Inasemekana kuwa watoto wenye umri wa chini wa miaka 15 hawakuruhisiwa kushiriki vitani, hii inamaanisha kwamba wanajeshi wote wa Kiislamu walikuwa na umri wa miaka 15 na kuendelea. [55] Kiuhalisia, bwana Mtume (s.a.w.w) hakuwaruhusu watu walio chini ya umri wa miaka 15 kushiriki vita. [56] Pale vita vilipokuwa havihitaji watu wengi, bwana Mtume (s.a.w.w) hakutangaza hakutangaza mbiu ya mgambo kwa jamii nzima. Hata hivyo, katika hali ambayo jeshi la Kiislamu lilihitaji nguvu zaidi, alitoa wito wa kuwaita watu wote wenye uwezo (isipokuwa walemavu) kupigana vita. [57] Ila bwana Mtume (s.a.w.w), hakuwahi kumlazimisha mtu yeyote kupigana vita. [58] Pia, bwana Mtume (s.a.w.w) aliwazuia wale watu waio kuwa na uwezo wa kupigana kushiriki vitani. [59] Kulingana na Mkataba wa Baiatu al-Harbu (Baiatu al-‘Aqabah), Waislamu wa mji wa Madina walikubali na kutia siani ya kwambaa; ulinzi wa kuyalinda maisha ya bwana Mtume huko Madina ni jukumu la watu wa Madina. Kwa mujibu wa mkataba huo, watu wa Madina hawakuwa na jukumu la kumlinda bwana Mtume (s.a.w.w), endapo yeye atapigana vita hali akiwa nje ya mji huo. [60] Kwa msingi huu, hadi vita vya Badri, askari wote wa bwana Mtume (s.a.w.w) walikuwa ni askari wailotoka upande wa Answari. Hata hivyo, baada ya kuanza vita vya Badri, Muhajirina nao walianza kushiriki katika vita kwa hiari zao wenyewe. [61]

Uwepo wa wanawake vitani

Wanawake pia walishiriki katika vita vya bwana Mtume kama walivyoshiriki wanaume vitani humo. 62] Miongoni mwa Michango wa wanawake katika vya bwana Mtume (s.a.w.w), kama vile:

  • Kutibu majeraha ya askari waliojeruhiwa
  • Kusambaza maji kwa askari
  • Kutayarisha chakula
  • Kukusanya na kuhifadhi mishale na silaha nyingine
  • Kusafirisha Majeruhi na waliouawa hadi mijini [63]

Baadhi ya wanawake, kama vile Kaabiyyah bint Saad na Rafidah Ansariyyah, pia walikuwa na mahema maalum ambayo majeruhi na wagonjwa wangepelekwa mahemani humo ili kutibiwa. [64]

Katika vita vya Khaibar, kulikuwa na wanawake sita katika jeshi la Mtume. [65] Katika vita vya Uhud, kulikuwa na wanawake 14 ambao walioshiriki katika vita hivyo, wakitibu majeraha ya askari na kuwapa maji na chakula. [66] Baadhi ya wanawake hawa ni pamoja na Fatima Zahra (a.s), Aisha, na Umm Ayman. [67] Fatima Zahra (a.s) katika vita vya Uhud, akisaidiwa na Imam Ali (a.s), alifunga vidonda vya bwana Mtume (s.a.w.w). [68] Ummu Ayman alishiriki katika vita vya Uhud na Khaibar. [69] Ummu Atiyah alishiriki katika vita vingi. [70] Kulingana na ripoti iliyoripotiwa kutoka kwake, yeye alishiriki katika vita saba. [71] Rabi'u bint Mu'awwadh pia alikuwa ni miongoni mwa wanawake walioandamana na Mtume katika vita. [72] Umm Ammarah pia alishiriki katika vita mbalimbali, kama vile Uhud, Khaibar, na Hunain. [73] Ambapo alipigana akiwa pamoja na wanaume vitani humo. Umm Ammarah alijeruhiwa katika vita mbalimbali, pia katika vita vya Uhud, pale bwana Mtume (s.a.w.w) alipowashambuliwa na washirikina alisimama kidete na kumlinda bwana Mtume (s.a.w.w) kwa upanga wake. [74]

Mbinu za kivita za Mtume (s.a.w.w)

Picha ya jinsi Jeshi la Ulinzi wa Waislamu lilivyoandaliwa

Katika baadhi ya vita bwana Mtume (s.a.w.w), kama vile vita vya Khaibar, [76] alitumia mbinu za jemedari "khumais" katika kuliandaa jeshi lake. [77] Katika mbinu hizi, wanajeshi walipangana katika vikundi vitano: kikosi cha mbele, kikosi cha kati, kikosi cha kulia, kikosi cha kushoto, na kikosi cha nyuma. [78] Moja ya mbinu za bwana Mtume (s.a.w.w) katika vita, ilikuwa ni kuvianzisha vita ndani ya ardhi ya madui zake, alifanya hivyo ili kuhakikisha kwamba hasara zote za vita zinawasibu maadui zake. [79] Katika baadhi ya matukio, jeshi la Waislamu lilisafiri kwa njia zisizojulikana ili kuzuia vikosi vya ujasusi vya maadui kuto kujua malengo na njama zao. [80] Katika baadhi ya matukio, bwana Mtume (s.a.w.w), baada ya kusikia habari za kukusanyika kwa maadui kwa nia ya kushambulia Waislamu, alianzisha mashambulizi ya kushtukizia (ya ghafla na yasio tarajiwa) dhidi ya maadui zake, ili kuwaangamiza na kuzuia kutokea vita kubwa zaidi, ambavyo pia vingeliweza kusababisha hasara kubwa zaidi. [81]

Taktiki danganyifu pia ilikuwa ni mojawapo ya njia nyingine za bwana Mtume (s.a.w.w) katika vita. [82] Katika vita vya Khaibar, Mtume kwanza kabisa aliliongoza jeshi lake kuelekea Ghatfan, kisha akatuma kikundi kidogo cha wanajeshi kuwaelekea maadui zao, ila yeye mwenyewe akiongozana na vikosi vyake kuu, alibadilisha mwelekeo wake na kuelekea Khaibar. Kwa njia hii, watu wa Ghatfan na Khaibar wote wakashtukiziwa ghafla bila ya kutarajia, jambo lilipelekea wao kutoweza kukutana na kuunganisha nguvu zao dhidi ya Wiaslamu. [83] Pia katika baadhi ya vita, bwana Mtume (s.a.w.w) alitumia vita vya kisaikolojia ili kuwashinda maadui zake. [84] Kwa mfano, katika vita vya Hamra al-Asad, Waislamu ulipokuwa ukiingia usiku, walikuwa wakiwasha moto katika sehemu 500 tofauti, ili kuwatia khofu maadui zao kupitia moto huo. [85] Vivyo hivyo, katika ushindi wa ukombozi wa mji Makka, Abbas bin Abdul Muttalib, kwa amri ya bwana Mtume (a.s.w.w), alimchukua Abu Sufyan hadi mwanzo wa bonde linaloishia mji wa Makka, ili aone umati mkubwa wa Waislamu kutokea bondeni hapo [86] na afute kichwa mwake wazo la kupambana na Waislamu, jambalo lilipelekea ukakamilika ukombozi wa mji wa Makka bila vita. [87] Katika vita mbalimbali bwana Mtume (a.s.w.w) alionekana kutumia mbinu za kushtukizia na kughafilisha. Kwa mfano, alishtusha Bani Qurayzah wakati wa mapigano kupitia mbinu za kuwavamia kwa uvamizi wa kushtukizia. Kupitia mbinu hiyo hiyo bwana Mtume aliweza kuwashinda watu mji Khaibar na Ahzabu (Vita vya Khandaq) walipokuwa mapambanoni mwao. [88]

Rasilimali na vifaa vya kivita

Baada ya serikali ya Kiislamu kuimarika, bwana Mtume (s.a.w.w) alichukua jukumu la kusimamia rasilimali na vifaa vya kivita. Hata hivyo, katika miaka ya kwanza ya uhamiaji wa bwana Mtume (s.a.w.w), kutoka Makka kwenda Madina, rasilimali na vifaa vinavyohitajika kwa vita vilitolewa na washiriki wa vita, matajiri pamoja na watu wengine wa kawaida. [89] Kwa mfano, bwana Mtume (s.a.w.w), alimwambia Saad bin Zaid aende pamoja na wafungwa wa Bani Qurayzah hadi Najd, ili kununua farasi na silaha kwa ajili ya jeshi la Kiislamu. [90] Pia katika vita vya Tabuk, baadhi ya masahaba walimwomba bwana Mtume (s.a.w.w) awape usafiri na vifaa vya kivita ili wasikose fadhila ya jihadi, na kwa upande wake bwana Mtume (s.a.w.w) aliamuru ombi lao kutimizwa. [91]

Bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa na mikataba na makabila mbalimbali iliyomruhusu kununua silaha na mahitaji mengine ya kijeshi kutoka kwao. [92] Pia, katika baadhi ya matukio, bwana Mtume (s.a.w.w), aliwakodia wanajeshi wake vifaa vinavyohitajika kutoka kwa makabila fulani. [93] Waislamu walitumia silaha bora zaidi katika baadhi ya vita vyao, kama vile manjaniki (chombo cha kupopolea) [94] na dabbabah (aina ya gari la vita ambalo lilitumika kuharibu kuta za ngome). [95] [96]