Upwekeshaji Katika Ngazi Ibada
Upwekeshaji Katika Ngazi Ibada (Tawhid Abadi): Ni hali ya kufanya ibada huku mwenye kuabudu akiwa anaabudu kwa kuielekeza ibada yake kwa Mungu Mmoja tu ambaye ni Alla, huku akiwa akiwa na imani ya kwamba; anayestahili kuabudiwa isipokuwa Alla peke yakee. Mafundisho haya ya msingi ni nguzo kuu katika dini zote za mbinguni, na ndio msingi wa wito wa mitume wote waliokuja duniani humu. Hili ni fundisho linalokubaliwa na Waislamu wote, ambalo limetiliwa mkazomno katika mafundisho ya Kiislamu. Wanazuoni wa fani ya theolojia na tafsir,i wanasema kwamba; Aya nyingi za Qur'ani Tukufu zinaashiria umuhimu wa upwekeshaji katika ngazi ya ibada. Kauli maarufu ya La ilaha illa Allah inafasiriwa kama tamko linaloelekeza moja kwa moja kwenye dhana hii muhimu ya upwekeshaji katika ngazi hii ya ibada. Kuna hoja kadha wa kadha (nyingi) zilizowasilishwa kwa ajili ya kuthibitisha upwekeshaji wa Mwenye Ezi Mungu katika ngazi ya ibada. Miongoni hoja na ithibati juu mada hii, ni hoja ya kuwepo kwa fungamano lazimifu (linalolazimiana) kati ya mja na Mola wake. Watoaji wa hoja hii wanasema kwamba; kuna mafungamano kadhaa lazimifu yaliopo baina ya Allan a mja wake, ikiwa ni pamoja na; fungamano lazimifu la kiuja (hali ya mtu kuwa ni mja) na Uungu (himaya ya ulezi wa Mungu), hali inayo jenga hisia ya udhaifu wa mlelewa (hisia ya kutaka kutumika na kutoa huduma ya shukurani). Mafungamano mengine ni fungamano la mmiliki na mmilikiwa na fungamano ya uhai na mauti. Kulingana na hoja na ithibati hizi; ibada imstahichia yule tu mwenye mamlaka kamili juu ya uhai na mauti ambaye ndiye mshika hatamu asili wa kila kitu kilichomo ulimwenguni. Kwa mujibu wa makubaliano ya Waislamu wote duniani ni kwamba; ni haramu na ni shirki kumuabudu kitu au mtu yeyote yule isipokua Mungu, na shirk ni dhambi kubwa inayo mtoa mtu katika imani ya Uislamu. Hata hivyo, kuna tofauti za kifikra miongoni mwa Waislamu juu ya baadhi ya matendo. kwa mfano, Waislamu wa dhehebu la Kiwahabi, wanayahisabu baadhi ya matendo kuwa ni ushirikina, ikiwemo; tawassul (kuomba msaada kupitia watu wema), tabaruku (kutafuta baraka), kuzuru makaburi, pamoja na kuomba msaada na uombezi kwa asiye kuwa Mungu. Kwa upande mwingine, wapinzani wao wanasisitiza ya kwamba; matendo haya ni shirk pale tu yanapofanywa kwa imani ya kumshirikisha mwingine na uungu au ulezi wa Mungu; vinginevyo, matendo haya hayapingani na dhana ya upwekesha Mungu katika ngazi ya ibada.
Umuhimu na Nafasi ya Upwekesha Mungu Katika Ngazi ya Ibada upwekesha Mungu katika ngazi ya ibada, ni moja wapo ya misingi muhimu katika dini za mbinguni. Imani hii ndiyo msingi asili wa ujumbe wa mitume wote waliokuja duniani humu. Kuna Aya nyingi katika zinazo lingania msingi huu. Mwenye Ezi Mungu ameshusha Aya kadhaa zinazo lingania msingi huo, miongoni mwazo ni Aya ya 36 ya Suratu An-Nahl, na Aya ya 25 ya Suratu Al-Anbiyaa, Aya hiz zinaelezea kwa uwazi kabisa juu ya dhana hii. [1] Wanazuoni wa elimu ya theolojia wanasisitiza kwamba; Waislamu na wengine wote na wale wote wenye kuamini juu ya Uungu wa Mungu Mmoja, wanakubaliana juu ya umuhimu wa kumwabudu Mungu pekee. [2] Na kama kuna khitilafu fulani kati yao, basi khitilafu hizo zitakuwa zinahusiana na tafsiri ya ibada na mifano yake hai. [3] Kwa mujibu wa Aya za Qur'ani na ripoti za kihistoria, ni kwamba; upotofu mkubwa zaidi uliodhihri katika kaumu mbali mbali kuhusiana na uwanja wa tawhidi, ulidhihiri kwenye itikadi ya upwekeshaji katika ngazi ya ibada. [4] Kulingana na maoni ya Allama Majlisi, washirikina wa Kikureishi walikubaliana na Waislamu juu ya imani ya umpweke wa Mungu kwenye ngazi ya uumbaji na upweke wake katika ngazi ya Uungu wake, inayojulikana kama “Tawhidu fi Al-khaaliqiyya” na “Tawhidu fi Al-rububiyya”. Hata hivyo, walitofautiana kimsingi kuhusiana na dhana ya upweke wa Mungu katika ngazi ya ibada, ambao ni “Tawhidu fi Al-ibada”. Hii inamaanisha kwamba ingawa walikubali kuwa Mungu ndiye Muumba pekee wa ulimwengu na Msimamizi wa kila kitu, ila walikuwa na mitazamo tofauti kuhusu ni nani anayestahili kuabudiwa pekee. Kwao, ibada ingeweza kuelekezwa kwa viumbe vingine, tofauti na mafundisho ya Waislamu yanayosisitiza kwamba ibada inapaswa kumwendea Mungu pekee. [5] Baadhi ya watu wanaona kwamba upwekeshaji katika ngazi ya ibada (Tawhidi fil Ibada) ni suala la msingi zaidi, ambalo hatime limechochea Waislamu wa madhehebu ya Kiwahabi kuchukua msimamo mkali dhidi ya Waislamu wengine, wakiwemo Shia na Sunni. Kwa mtazamo wa Mawahabi, ibada safi inapaswa kuelekezwa kwa Mungu pekee. Wao wanapinga baadhi ya matendo yafanywayo na Waislamu wengine, na kuvihisabu kama ni vya ushirikina. Miongoni mwa vitendo vipingwavyo na Mawahabi ni kama vile; kuomba msaada kutoka kwa asiyekuwa Mungu, kuomba shufaa kutoka kwa mawalii.., pamoja na kuzuru makaburi, kwao wao matendo haya ni aina za ushirikina na kinyume na tawhidi. Msimamo huu umesababisha migogoro na tofauti za kimtazamo kati ya Mawahabi na Waislamu wengine, ambao wana tafsiri tofauti kuhusiana na maana ya ibada na namna inavyopaswa kutekelezwa. [6] Imeelezwa kwamba Aya nyingi za Qur'ani ni zinaelezea wazi kabisa umuhimu wa upwekeshaji Mungu katika ngazi ya ibada (Tawhidu fi Al-ibada), ikisisitiza kwamba ibada sahihi na halisi ni ile inayoelekezwa kwa Mungu Mmoja peke yake. Miongoni mwa Aya zinazozungumzia hili, ni Aya ya 51 na 64 za Suratu Al-Imran, Aya ya 102 ya Suratu Al-An'am, Aya ya 36 ya Surau An-Nahl, Aya ya 25 ya Suratu Al-Anbiyaa, na Aya ya 61 ya Suratu Ya-Sin. [7] Neno “La ilaha illa Allah” pia linaeleweka kama ni kauli safi inayothibitisha upweke wa Alla katika ngazi ya ibada, ikimaanisha kwamba hakuna anayestahili kuabudiwa isipokuwa Mungu Mmoja tu naye ni Alla. Aya hizi na kauli hii zinaunda msingi mkuu wa mafundisho ya Kiislamu unaolenga kuhakikisha kuwa ibada zote zinabaki kuwa safi na kuelekezwa kwa Muumba Mmoja peke yake, bila ya ushirikina au ushirikishwaji wa wengine katika ibada. [8] Matokeo mabaya ya kumwabudu asiyekuwa Mungu yameakisiwa na Aya mbalimbali za Qur'ani. Miongoni mwa matokeo yaliyo akisiwa ndai ya Aya hizo ni; kufutwa na kubatilika matendo mema, kupotea njia, kuwa na bahati mbaya, kupata hasara kubwa Siku ya Kiyama, sambamba na kukumbana na hasira za Mwenye Ezi Mungu. [9] Haya ni maonyo makali yawekayo wazi athari za kufanya ibada kwa kumshirikisha mwengine au kitu chengine tofauti na Mungu Mmoja. Katika amri ya pili kati ya zile kumi za Nabii Musa (a.s), waumini wameelekezwa kwa msisitizo mkubwa juu ya kutomwabudu asiyekuwa Mungu, na hili limejenga msingi mkuu juu ya umuhimu wa upwekeshaji Mungu katika ngazi ya ibada (Tawhidu fi Al-iibada). [10] Amri ya Mungu kwa Musa, inasisitiza kwamba ibada zote zinapaswa kuelekezwa kwa Mungu Mmoja pekee, ikibainisha uzito wa dhambi ya ushirikina na umuhimu wa kuwa na ibada safi katika kumtii Muumba. Sisitizo hili la tawhidi katika ibada limekuwa kiini cha mafundisho ya manabii wa dini zote za kimbinguni, likionesha kuwa ni jambo la msingi ambalo waumini wanapaswa kulidumisha kwa bidii zao zote. Maelezo ya Ali Rabani Golpaigani, mtafiti wa theolojia ya Kishia, yanasema kwamba; kutokana na uwazi wa suala la upwekeshaji katika ngazi hii ya ibada (Tawhidu fi Al-iibada) na kutokuwepo kwa tofauti miongoni mwa Waislamu kuhusu hili, suala hili halikujadiliwa sana katika vitabu mbali mbali vya kale vya theolojia. Badala yake, lilijadiliwa zaidi katika vitabu vya maadili. Hata hivyo, umuhimu na ulazima wa kujadili suala hili uliongezeka baada ya kuibuka kwa Ibn Taymiyyah, ambaye alikuja na mawazo mapy mapya kuhusiana na uwanja wa upwekeshaji katika ngazi ya ibada pamoja na masuala yanayo husiana na mambo ya shirk. [11]
Welewa wa Dhana ya Upwekeshaji Katika Ngazi ya Ibada Upwekeshaji Katika Ngazi ya Ibada (Tawhidu fi Al-iibada), unahusisha moja kwa moja imani ya isemayo kwamba; Hakuna anayestahili kuabudiwa ispokuwa Alla peke yake, na wala hakuna mwingine uabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye tu. [12] Muhammad Taqi Misbah Yazdi akifafanua ngazi hii ya upwkeshaji yuasema kwamba; upwekeshaji katika ngazi ya ibada unahusiana na vitendo vya mwanadamu, kwa maana ya kwamba ibada zote zinapaswa kuelekezwa kwa Alla. [13] Kwa maoni yake, ibara ya “La ilaha illa Allah” inathibitisha upweke wa uungu pamoja na upwekeshaji katika ngazi ya ibada, ikionesha kwamba; Mungu ndiye pekee anayestahili kuabudiwa. [14] Hata hivyo, kuna tofauti za mitazamo kuhusiana na uhusiano kati ya upwekeshaji katika ngazi ya ibada na upweke katika ngazi ya Uungu. Baadhi ya wanazuoni Kishia, [15] Ibn Taymiyyah, [16] na Mawahabi [17] wanachukulia upwekeshaji katika ngazi ya ibada kuwa ni sawa na upwekeshaji katika ngazi ya Uungu, wakiona kwamba; dhana zote mbili kumpwekesha Mungu pekee. Kwa upande mwingine, Ja'afar Subhani, mtafiti na mtafsiri wa Kishia, anapinga mtazamo huu. Na anasisitiza kwamba upwekeshaji katika ngazi ya ibada na upwekeshaji katika ngazi ya Uungu ni dhana mbili tofauti na wala hazipaswi kuchanganywa na kuwekwe kwenye dhana moja. [18]
Hoja na Misingi Juu ya Upwekeshaji Katika Ngazi ya Ibada Kna hoja kadhaa zilizotolewa katika uwanja huu, miongoni mwazo ni kama ifuatavyo: [19] 1. Fungamano Lazimifu Kati ya Uumbaji na Ibada: Upwekeshaji katika ngazi ya ibada unathibitishwa kupitia fungamano lazimifu la kipekee lililopo kati ya Mungu kama Muumba na mwanadamu kama mja. Mungu ndiye Muumba pekee wa viumbe vyote, na hivyo, hakuna muumba mwingine anayestahili kuabudiwa isipokuwa yeye. Kuna Aya kadhaa za Qur'ani kama ile; ya 61 ya Suratu Hud, Aya ya 1 na 102 za Suratu Al-An'am zinazo eleza kwa uwazi kabisa jinsi ya Uumbaji unavyohusiana na ibada. Aya hizi zinathibitisha kwamba kutokana na ukweli kwamba Mungu ndiye Muumba pekee, hivyobasi ibada zote zinapaswa kuelekezwa kwake Yeye tu. [20] 2. Fungamano Lazimifu Kati ya Ulezi (Rububiyya) na Ibada: Mungu ndiye Mlezi (Rabb) pekee wa viumbe, anaye hudumia na kudhamini mwongozo wa maisha yao. Katika kuna Aya Qur'ani zinazotumika kama hoja katika kutetea ukweli huu. Miongoni wanzo ni; Aya ya 21 ya Suratu Al-Baqara, pamoja na aya za 76 hadi 79 za Suratu Al-An'am, ambazo zinathibitisha uwepo wa fungamano lazimifu kati ya ulezi wa Mungu na ibada. [21] Kwa kuwa Mungu ndiye pekee anaye jali na kusimamia viumbe, kwa hiyo yapaswa ibada zote kuelekezwa kwake Yeye peke yake. [22]
3. Funagamano Lazimifu Kati Ibadan a Umiliki wa Maisha na Kifo cha Mwanadamu Mungu ndiye mwenye mamlaka kamili juu ya maisha na vifo vya viumbe vyote. Hakuna mwingine anayemiliki au awezaye athari fulani juu ya maisha na kifo isipokuwa Mungu peke yake.Basi iweje tena awepo mwengine aabudiwaye isipokuwa Yeye. [23] Aya kama ile; Aya ya 104 ya Suratu Yunus, Aya ya 123 ya Suratu Hud, na Aya ya 88 ya Suratu Al-Qasas zimejuja nakubaliana na ukweli huu nazo ni zenye kuthibitisha kwamba ya mamlaka haya yanajenga fungamano lazimifu kati ya Mungu na Ibada, na ni hoja kamili juu ya haki ya upwekeshwaji wa Mungu katika ngazi ya ibada, ambapo ibada zote zinapaswa kuelekezwa kwa Mungu pekee. [24] 4. Aya ya 5 ya Suratu Al-Fatiha (إِيَّاكَ نَعْبُدُ): Aya hii inaweka wazi kwamba ibada zapaswa kuelekezwa kwa Mungu peke Yake. Ujumbe wa Aya hii unathibitishwa na mpangilio wa maneno yake katika kifungu kisemacho (إِيَّاكَ نَعْبُدُ), ambapo kipande cha kiima (إِيَّاكَ) kinatangulia kitenzi (نَعْبُدُ), mpangilio ambao katika lugha ya Kiarabu; huwa una maana ya kufungika na kitu kimoja pekee na kukanusha vyengine vyote isipokuwa hicho tu. Hii inaonyesha kwamba; haki ya kuabusiwa ni ya Mungu tu, na hakuna mwingine anayestahili kuabudiwa. 5. Aya ya 39 na 40 ya Suratu Yusuf: Katika Aya ya 40 ya Suratu Yusuf, Mwenye Ezi Mungu anasisitiza kwamba; hakuna mwingine anayestahili kuabudiwa isipokuwa Yeye mwenyewe. [25] Allama Tabatabai ameichukulia Aya hizi kama ni uthibitisho wa upwekeshaji katika ngazi ya ibada, ambapo Mwenye Ezi Mungu katika Aya hii amesema: “اَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ” “Ameamuru kwamba hamupaswi kuelekeza ibada zenu isipokuwa kwake Yeye tu.” [26] Misingi hii inatoa mwanga wa kina kuhusu upwekeshaji katika ngazi ya ibada unavyo thibitishwa na kuimarishwa katika Qur'ani, na jinsi inavyohusiana na dhana moja kwa moja na dhana ya upwekeshaji wa Mungu katika ngazi ya uumbaji na ulezi. Ayatollah Subhani anasisitiza kwamba, Waislamu wote wanakubaliana ya kwamba, kitendo cha kumuabudu asiyekuwa Mwenye Ezi Mungu ni miongoni mwa vitendo haramu vya ushirikina. Tendo ambalo ni miongoni mwa matendo ya dhambi kubwa ndani ya dini ya Kiislamu, na ni kitendo kinacho mweka mtu nje ya Uislamu. [27] Pia, Murtadha Mutahhari, mwanafikra maarufu wa Kiislamu, naye amethibitisha msimamo huu akisema kwamba; kwa mujibu wa mantiki na sheria za dini, ni jambo lisilokubalika kabisa kuabudu mwengine kinyume na Alla. Kwa Maoni ya Mutahhari, hili ni kosa la kimsingi linalomtoa mtu nje ya mipaka ya Uislamu. [28] Kwa mtazamo wa Mawahabi; vitendo kama vile kutawasali (kuomba msaada kupitia kwa watu wema na bila kumwomba Mungu moja kwa moja), [29] kutabarruk (kutafuta baraka kutoka katika vitu vinavyohusiana na watu wema), [30] kuzuru makaburi (kutembelea makaburi ya watu wema), [31] pamoja na kuomba shufaa, [32] ni miongoni mwa aina za ibada za kuabudu watu, kwa hiyo mambo hayo ni ushirikina, na si mambo yenye kufaa katika Uislamu. [33] Hii imepelekea wao kuwachukulia Waislamu wanaotawasali kupitia kwa Mtume (s.a.w.w) au Ahlul-Bait, pamoja na watu wema wengine kama ni washirikina. [34] Katika kujibu mtazamo wa Mawahabi, imeelezwa kwamba; vitendo kama tawasali (kuomba msaada kupitia kwa watu wema), kutabarruk (kutafuta baraka kwa kutumia vitu vinavyohusiana na watu wema), na ombia shufaa(ombi la kutaka uombezi kupitia mtu mwengine) vinaweza kuwa ni vya kishirikina iwapo mambo hayo yataambatanishwa na nia ya ibada, na katika hali ya kuambatana na imani ya kwamba hao waliotawasuliwa au waliotabarukiwa wana Uungu au wana aina fulani ya sifa ya Urububiyya (utawala wa kimungu). Ila, kama vitendo hivi vinafanyika kwa imani ya kwamba watu hao wema, ni waja wa Mungu na si wamiliki wa sifa yoyote ile ya Uungu, katika hali hii, vitendo hivi havitachukuliwa kuwa ushirikina katika ibada, hata kama vinafanyika kwa unyenyekevu na heshima kwao. [35]
Takwimu ya Kitabu (Monografia): • Upwekeshaji katika Ngazi ya Ibada kwa Mtazamo wa Kishia na Kiwahabi Mwandishi: Mahdi Nikuui Saamaaniy Maelezo ya Kitabu: Kitabu hichi, kilichoandikwa na Mahdi Nikuui Samaniy, kinachunguza kwa kina umuhimu wa upwekeshaji katika ngazi ya Ibada (Tawhidu ‘Ibadiy) na tafsiri potofu zinazohusiana na upwekeshaji katika ngazi ya Ibada, hususan kutoka madhehebu ya Kiwahabi. Kitabu hichi kimeandikwa kikiwa na sehemu mbili pamoja na hitimisho. Mwandishi anatoa mtazamo wa kina juu ya tofauti na uwiano kati ya Shia na Mawahabi kuhusiana na suala hili la msingi katika Uislamu. Sehemu ya Kwanza: Sehemu hii inatoa muhtasari wa dhana mbili kuu za upwekeshaji (tawhid) na shirk (ushirikina). Inafafanua vigezo vya msingi vya imani ya Kiislamu, ikielezea umuhimu wa upwekeshaji katika ngazi ya Ibada na athari za shirk katika imani ya Kiislamu. Inajumuisha tafsiri za kitaalamu na maandiko ya mbali mbali yaliotolea juu ya dhana hizo mbili kulingana na mtazamo wa Shia. Sehemu ya Pili: Katika sehemu hii, mwandishi anajadili mitazamo ya Kishia na Kiwahabi kuhusiana na upwekeshaji katika ngazi ya Ibada na shirk. Inatoa tathmini ya kina kuhusu tofauti na maelezo ya mitazamo ya Kiwahabi kuhusiana na upwekeshaji katika ngazi ya Ibada, ikichambua jinsi tafsiri zao zinavyokinzana na zile za Kishia. Sehemu hii pia inaeleza jinsi tafsiri hizi zinavyoathiri uhusiano kati ya madhehebu haya mawili. Hitimisho: Hitimisho linaweka wazi mapendekezo na muhtasari wa tafiti zilizofanywa katika sehemu za awali. Linatoa tathmini ya jumla kuhusu upwekeshaji katika ngazi ya Ibada na jinsi tafsiri za Kishia na Kiwahabi zinavyoathiri mtindo wa ibada na uhusiano wa kidini. Hitimisho hili pia linaelezea jinsi welewa wa upwekeshaji katika ngazi ya Ibada unavyo weza kuchangia katika kuimarisha umoja wa Waislamu na kupunguza migogoro ya kidini. Malengo ya Kitabu: Kitabu hichi kinakusudia kutoa mtazamo wa kina kuhusu upwekeshaji katika ngazi ya Ibada kulingana na mitazamo ya pande zote mbili za Shia na Kiwahabi. Lengo lake ni kueleza tofauti za msingi katika tafsiri za upwekeshaji katika ngazi ya Ibada na shirk, na hivyo kusaidia kuelewa vizuri zaidi namna ya mitazamo ya kidini inavyowe kuleta uhusiano wa kiimani kati ya madhehebu tofauti. [36]