Umri wa Imamu Mahdi (atfs)
Umri wa Imamu Mahdi (a.t.f.s) (Kiarabu: طول عمر الإمام المهدي (ع)) maana yake ni kuwa hai Imamu Mahdi (a.t.f.s) kuanzia mwaka 255 Hijria mpaka kudhihiri kwake na hizi ni katika itikadi na imani za Shia Imamiyah. Umri wa Imamu Mahdi mpaka kufikia 1446 Hijria umepindukia miaka 1190. Wapinzani wa Shia Imamiya akiwemo Ibn Taymiya na Nassir al-Qifari wamesema ni jambo liililo mbali kwa mtu kuishi umri kama huo na kulifanya hilo kuwa hoja ya kukana kuzaliwa Imamu Mahdi (a.t.f.s).
Maulamaa wa Imamiyah wanasema kuwa, kiakili inawezekana kuweko mtu mwenye umri usio wa kawaida na kwa ajili ya kuthibitisha jambo hilo wanatumia kama hoja umri mrefu wa watu kama Nabii Nuh, mtukufu Khidhr na Nabii Issa Masih (a.s). Kadhalika ili kuthibiitisha umri mrefu wa Imamu Mahdi, kumetumiwa kama hoja mifano ya kihistoria ya watu walioishi umri mrefu na hadithi zinazoonyesha juu ya kuwa na mrefu umri Imamu Mahdi na uwezekano wa umri wa mtu kuwa mrefu kulingana na tajiriba.
Kuna vitabu vya kujitegemea vilivyoandikwa kuhusiana na maudhui ya umri mrefu wa Imamu Mahdi ambapo miongoni mwavyo ni Al-Burhan Ala Sihat Tuli Umri al-Imam Sahib al-Zaman, kilichoandikwa na Abul-Fat'h Karajaki mwaka 427 Hijria. Kadhalika katika baadhi ya vitabu vya hadithi vilivyoandikwa, baada ya mwaka 370 Hijria, kumetengwa sehemu maalumu kwa ajili ya kadhia hii.
Umuhimu na Historia Yake
Umri wa Imamu Mahdi (a.t.f.s) maana yake ni kuendelea kuwa kwake hai tangu alipozaliwa (255 Hijria) mpaka kudhihiri kwake) ambapo hii ni miongoni mwa imani za Shia Imamiyah[1] na baadhi ya Maulamaa wa Ahlu-Sunna.[2] Kwa msingi huo Umri wa Imamu Mahdi tangu alipozaliwa 255 Hijria mpaka 1446 Hijria ni zaidi ya miaka 1190.
Kwa mtazamo wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, kuweko umri ambao ni nje ya ada na mazoea ya watuu ni jambo ambalo linawezekana na kuna mifano ya hilo.[3] Pamoja na hayo, wapinzani wa Mashia wanasema kuwa, haiwezekani mtu akaishi umri mrefu kiasi hiki na kwamba, hilo ni jambo lisilowezekana na hata kulitumia hilo kama hoja ya kukana kuzaliwa Imamu Mahdi (atfs).[4] Miongoni mwa wanaokana hilo ni Ibn Taymiyah Harrani (aliaga dunia: 728 Hijria)[5] na Nassir al-Qiffari mwandishi Muwahabi wa Saudi Arabia.[6]
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika, suala la umri wa Imamu Mahdi (atfs) katika athari zinazohusiana na Umahdi katika Imamiyyah lilianza kuzingatiwa baada ya mwaka 370 Hijria. Katika athari za kabla ya hapo kama Basair al-Darajat, al-Kafi na al-Ghaiba (cha Ibrahim Nu’mani) kutokana na kuwa jambo la kawaida umri wa Imamu Mahdi (a.t.f.s) mpaka wakati huo jambo kama hilo halikuzungumziwa.[7] Kitabu cha kwanza ambacho kilitenga mlango kamili wa suala hili ni Kamal al-Din Watamaam al-Ni’mah cha Sheikh Swaduq (aliaga dunia: 381 Hijria).[8]
Kuthibitisha Uwezekano wa Umri Usio wa Kawaida
Uwezekano wa Kiakili

Kwa mujibu wa hoja hii, suala la umri mrefu usio wa kawaida sio kitu muhali na kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye ujuzi na Muweza, kama akitaka anaweza kumruzuku mtu umri mrefu..[9] Muhammad Baqir Sadr (aliaga dunia: 1400 Hijria) anaamini kwamba, kutokuwa jambo la kawaida jambo hili kunatokana na mlango wa muujiza na usiokuwa muujiza, na hilo halipeleki jambo hilo lisiwezekane.[10]Abdallah Jawadi Amuli (alizaliwa 1312 Hijria Shamsia), mwanafalsafa wa Kishia anaamini kwamba ikiwa nafsi ya mwanadamu itakuwa, basi itapata ukamilifu ambao unaweza kumiliki ulimwengu wa kimaada, ukiwemo mwili wake wenyewe, na kudumisha hali za maisha ya kimaada ndani yake.[11]
Mifano ya Watu Wenye Umri Mrefu katika Qur’ani na Torati
Qur’ani inaashiria Utume wa Nabii Nuhu (as0 wa miaka 950 katika Aya ya 14 ya Surat al-Ankabut. Hili linatumiwa na Maulamaa wa Shia Imamiya kama hoja ya Qur’ani ya kuonyesha uwezekano wa mtu kuishi umri mrefu.[12] Kadhalika mtukufu Khidhr ambaye kwa mujibu wa Qur’ani alikuwa hai katika zama za Nabii Mussa,[13] na kwa mujibu wa nukuu ya Sheikh Mufidu (aliaga dunia 413 Hijria) na ijmaa ya waandishi wa sira, angali anaendelea kuishi mpaka leo.[14] Irbili (aliaga dunia: 692 Hijria) akitumia kama hoja Aya ya 159 ya Surat al-Nisaa, anamuarifisha Nabii Issa kwamba, alikuwa hai mpaka katika kipindi na zama zake.[15]
Kwa mujibu wa Lutfullah Safi Gulpeygani (aliaga dunia 1400 Hijria Shamsia) mmoja wa Marajii na mtafiti wa Umahdi wa Kishia anasema kuwa, katika dini zote za Mwenyezi Mungu kuna imani juu ya uwepo wa watu wenye umri mrefu sana. Kwa mfano katika kitabu cha Taurati kuna maeneo mengi ambayo ndani yake kumzungumziwa suala la watu wenye umri mrefu ambapo wametajwa Manabii na wasiokuwa Manabii. [16]
Hadithi Zinazoashiria Umri wa Imamu Mahdi ni Mrefu
Sheikh Tusi (aliaga dunia: 460 Hijria) anataja katika Kitabu al-Ghaibah hadithi ambazo zinaashiria kuwa mrefu na usio wa kawaida umri wa Imamu Mahdi.[17] Irbili mtaalamu mwengine wa hadithi wa Kishia pia ametaja katika kitabu cha Kashf al-Ghummah juu ya kuwa mrefu umri wa baadhi ya Manabii kama Ilyas (a.s), Issa (a.s) na Mtukufu Khidhr (a.s) kwamba, ni hoja ya uwezekano watu kuwa na umri mrefu na kisha anazungumzia na kutaja hadithi zinazoeleza juu ya kuwa hai Imamu Mahdi (a.t.f.s) mpaka atakapodhihiri.[18] Ibn Maytham Bahrani (aliaga dunia: 679 au 699 Hijria) pia anaashiria juu ya kuweko mtazamo mmoja baina ya Mashia na Masuni juu ya kuwa hai Ilyas, Khidhr (a.s), Samiriy (msamaria) na Dajjal na kubainisha kwamba, watu hawa kuna uwezekano wakawa hai, lakini Mwenyezi Mungu pia anaweza kuufanya umri wa mtu ukawa mrefu.[19] Feydh Kashani (aliaga dunia: 1091 Hijria) anasema kuwa, hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) kuhusiana na umri wa Imamu Mahdi (a.t.f.s) zimefikia kiwango cha mutawatir.[20]
Uwezekano wa Umri Kuwa Mrefu Kwa Mujibu wa Elimu ya Tajiriba
Hoja hii imeelezwa na kutolewa ufafanuzi namna hii kwamba, elimu inataka sababu kwa ajili ya kifo na sio kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kifo ni kutokuweko masharti ya kuishi (uhai). Mwanadamu kutokana na ujahili na kutokuwa na maarifa ya kutosha ya sababu za magonjwa na uzee, hana uwezo wa lazima na unaohitajika kwa ajili ya kudhibiti hayo na hivyo hukumbwa na kifo. Endapo mtu atakuwa na elimu na suhula za lazima kwa ajili ya kudhibiti sababu kama za lishe, mazingira na mambo ya kijenitiki, kwa mtazamo wa kielimu anaweza kuwa na umri mrefu na hata wa mielele.[21]
Uthibitisho wa Kihistoria Juu ya Kuwa Mrefu Umri wa Imamu Mahdi (a.t.f.s)
Katika kitabu cha Kamal al-Din na Tamam al-Ni'mah, Sheikh Swaduq ametenga faslu moja kwa ajili ya kuzungumzia watu walioishi kwa muda mrefu. Katika mlango huu, Sheikh Swaduq ametaja makumi ya watu. Kati ya watu hawa, kuna umri kutoka miaka 120 hadi 3000. Sheikh Swaduq hakuichukulia riwaya ya watu hawa kuwa makhsusi kwa Shia bali anaamini kwamba kuwepo kwa watu hao kumethibitishwa pia katika vitabu vya Sunni.[22] Kwa kutaja mifano hiyo na kutumia hadithi kutoka kwa Mtume (saww) ambayo ndani yake inaashiria kutokea katika Umma wa Kiislamu matukio ya umma zilizotangulia na kueleza kwamba, kuna uwezekano wa kupatikana kwa umri kama huo katika kadhia ya Imam Mahdi (atfs).[23]
Sheikh Mufidu,[24] Karajaki[25](aliaga dunia: 449 H), Sheikh Tusi,ref>Shekh Tusi, al-Ghaibah, uk. 113-126.</ref> Amin al-Islam Tabarsi[26] (aliaga dunia: 548 Hijria), Khwaja Nasiruddin Tusi[27] (aliaga dunia:672 Hijria), Ibn Maytham Bahrani,[28] Allama Hilli (aliaga dunia:726 H),[29] Allama Majlisi[30] (aliaga dunia:1110 H), Lutfullah Safi Gulpeygani[31] na Ibrahim Amini[32] (aliaga dunia: 1399 Hijria Shamsia) ni miongoni mwa Maulamaa wa Kishia ambao wameegemea na kutegemea sababu za kihistoria ili kuthibitisha uwezekano wa kuweko maisha marefu yasiyo ya kawaida.
Monografia

Suala la umri wa Imamu Mahdi (a.t.f.s) limeandikiwa na kujadiliwa katika maudhui yenye kujitegemea katika baadhi ya vitabu na miongoni mwavyo ni:
- Al-Burhan ala sihat Tuli Umri al-Imam Sahib al-Zaman, mwandishi: Abul-Fat'h Karajaki, mmoja wa wanafunzi wa Sheikh Mufid na mwanateolojia wa Shia Imamiyah: Katika kitabu hiki kumetajwa hoja za akili na nakili za siri za umri mrefu na kundi la watu walioishi maisha marefu. Chapa ya kwanza ya kitabu hiki ilichapishwa 1332 H Tabriz Iran ikiwa sehemu ya kitabu cha Kanzul Fawaid na kutarjumiwa na Muhammad Baqir Kamerei kwa anuani ya hazina ya maarifa ya Shia Imamiyah.[33] Kwa mujibu wa mtunzi wa kitabu hiki, mwanzoni mwa kitabu hiki, mwaka wa kuandikwa kwake ni 427 Hijria.[34]
- Daf'u Shubhat Tuli Uumri al-Hujja, mwandishi Mamhmoud bin Muhammad Hassan Shariatmadar.[35]
- Tule Omr Hazrat Valii Asr (atfs), mwandishi Lutfullah Safi Gulpeygani.[36]
- Montazer Jahan va Raz Tile Omr, mwandishi Sayyid Ahmad Alamul-Huda.[37]
- Shegefti dar Chist? mwandishi: Muhammad Salehi Azari.[38]
- Ithbat Tul Umr Imame Zaman (a.t.f.s), mwandishi: Sayyid Murtadha Mir Said Qadhi.[39]
- Bahs Piramun Tul Omr Imam Ghaib, kilisambazwa na Dar al-Tabligh Islami Qom.[40]
- Tul Omr Imame Zaman az Didgah Ulum va Adiyan: Mwandishi: Ali Akbar Mahdipouri.[41]
- Imam Mahdi (a.t.f.s); Tul Omr, mwandishi: Hadi Husseini.[42]
Rejea
- ↑ Rezvani, Tavallud-e Hazrat-e Mahdi, uk. 60-61; Tazama: Kulaini, al-Kafi, juz. 1, uk. 514; Shekh Saduq, al-Irshad, juz. 2, uk. 339; Shekh Tusi, al-Ghaibah, uk. 419; Tabrisi, I'lam al-Wara, uk. 418; Irbili, Kashf al-Ghummah, juz. 2, uk. 437; Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 51, uk. 2.
- ↑ Al-'Amidi, al-Mahdi al-Muntadhar fi al-Fikr al-Islami, uk. 136-141; Mahmud, Wildah al-Imam al-Mahdi fi Kutub al-Fariqain, uk. 357-402; Tazama: Nashibi Shafi'i, Matalib al-Saul, uk. 311-319; Ibnu Jauzi, Tadhkirah al-Khawas, juz. 2, uk. 506-507; Ganji Shafi'i, al-Bayan, uk. 521; Hamui Juwaini, Faraid al-Simtain, juz. 2, uk. 134.
- ↑ Zainali, «Emam Mahdi va Tul-e 'Umr (Pishineh va Dalail)», uk. 222-223.
- ↑ Zainali, «Emam Mahdi va Tul-e 'Umr (Pishineh va Dalail)», uk. 223.
- ↑ Ibnu Taimiyah Harrani, Manhaj al-Sunnah al-Nabawiyah, uk. 91-94.
- ↑ Qifari, Usul Mazhab al-Shiah, juz. 2, uk. 866.
- ↑ Zainali, «Emam Mahdi va Tul-e 'Umr (Pishineh va Dalail)», uk. 223.
- ↑ Zainali, «Emam Mahdi va Tul-e 'Umr (Pishineh va Dalail)», uk. 224.
- ↑ Khaje Nashiruddin al-Tusi, Talkhis al-Muhasal, uk. 433; Allamah Hilli, Manahij al-Yaqin, uk. 482.
- ↑ Sadr, Buhuth Haula al-Mahdi, uk. 53-56.
- ↑ Jawadi Amuli, Ushareh Khelqat, uk. 24.
- ↑ Tazama: Shekh Mufid, al-Masail al-'Ashr, uk. 93; Tabrisi, I'lam al-Wara, uk. 472; Ibnu Maitham Bahrani, Qawaid al-Maram, uk. 191; Faidh Kashani, Ilm al-Yaqin, juz. 2, uk. 966.
- ↑ Surat. Al-Kahfi : 65-82.
- ↑ Shekh Mufid, al-Masail al-Ashr, uk. 83.
- ↑ Irbili, Kashf al-Ghummah, juz. 2, uk. 489.
- ↑ Safi Golpeyghani, Selsele-e Mabahith-e Emamat va Mahdawiyat, juz. 3, uk. 166-167.
- ↑ Shekh Shaduq, al-Ghaibah, hlm. 419-422.
- ↑ Irbili, Kashf al-Ghummah, juz. 2, uk. 489-519.
- ↑ Ibnu Maitham Bahrani, Qawaid al-Maram, uk. 192.
- ↑ Faidh Kashani, Ilm al-Yaqin, juz. 2, uk. 965.
- ↑ Safi Golpeyghani, Muntakhab al-Athar, juz. 2, uk. 276-282; Safi Golpeyghani, Selsele-e Mabahith-e Emamat va Mahdawiyat, juz. 3, uk. 161-217; Amini, Dadgastar-e Jahan, uk. 175-201.
- ↑ Shekh Saduq, Kamal al-Din, juz. 2, uk. 552-576.
- ↑ Shekh Saduq, Kamal al-Din, juz. 2, uk. 576.
- ↑ Shekh Mufid, al-Masail al-Ashr, uk. 94-103.
- ↑ Karajaki, Kanz al-Fawaid, juz. 2, uk. 114.
- ↑ Tabrisi, I'lam al-Wara, uk. 473-476.
- ↑ Khajah Nasiruddin al-Tusi, Talkhis al-Muhasal, uk. 433.
- ↑ Ibnu Maitham al-Bahrani, Qawaid al-Maram, uk. 191.
- ↑ Allamah Hilli, Mihaj al-Yaqin, uk. 482.
- ↑ Allamah Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 51, uk. 225-293.
- ↑ Safi Golpeyghani, Muntakhab al-Athar, juz. 2, uk. 275-276.
- ↑ Amini, Dadgastar-e Jahan, uk. 201-202.
- ↑ Agha Buzurg Tehrani, al-Dhari'ah, juz. 3, uk. 92; Refa'i, Mu'jam Ma Kutiba an al-Rasul wa Ahlilbait, juz. 9, uk. 115; Rey Shahri, Danesh Nameh Emam Mahdi, juz. 10, uk 248.
- ↑ Karajaki, Kanz al-Fawaid, juz. 2, uk. 114.
- ↑ Agha Buzurg Tehrani, al-Dhari'ah, juz. 8, uk. 230; Refa'i, Mu'jam Ma Kutiba an al-Rasul wa Ahlilbait, juz. 9, uk. 160.
- ↑ Safi Golpeyghani, Tul-e Umr Hazrat-e Wali-e 'Asr, (shenasname kitab).
- ↑ Refa'i, Mu'jam Ma Kutiba an al-Rasul wa Ahlilbait, juz. 9, uk. 268.
- ↑ Refa'i, Mu'jam Ma Kutiba an al-Rasul wa Ahlilbait, juz. 9, uk. 194.
- ↑ Refa'i, Mu'jam Ma Kutiba an al-Rasul wa Ahlilbait, juz. 9, uk. 85.
- ↑ Refa'i, Mu'jam Ma Kutiba an al-Rasul wa Ahlilbait, juz. 9, uk. 114.
- ↑ Mahdi Pur, Raz-e Tul-e Umr Emam-e Zaman az Didgah-e Ilm va Adyan, (shenasname kitab).
- ↑ Husaini, Emam-e Mahdi Tul-e Umr, (shenasname kitab).
Vyanzo
- Agha Buzurg Tehrani, Muhammad Muhsin. al-Dhari'ah ila Tasanif al-Shiah. Qom: Ismailiyan, 1408 H.
- Al-'Amidi, Sayid Thamir Hashim. al-Mahdi al-Muntadhar fi al-Fikr al-Islami. Qom: Markaz al-Risalah, 1425 H.
- Allamah Hilli, Hasan bin Yusuf. Minhaj al-Yaqin fi Usul al-Din. Tehran: Mandhumah al-Auqf wa al-Shu'un al-Khairiyah. Dar al-Uswah li al-Tiba'ah wa al-Nashr, 1415 H.
- Allamah Majlisi, Muhammad Baqir. Bihar al-Anwar. Beirut: Dar Ihya al-Turath al-Arabi, 1403 H.
- Faidh Kashani, Muhammad bin Shah Murtadha. Ilm al-Yaqin. Qom: Bidar, 1377 S.
- Ganji Shafi'i, Muhmmad bin Yusuf. al-Bayan fi Akhbar Sahib al-Zaman. Tehran: Dar Ihya Turath Ahlilbait Alaihimusalam, 1404 H.
- Hamawi Juwaini, Ibrahim bin Muhammad. Faraid al-Simtain fi Fadhail al-Murtadha wa al-Batul wa al-Sibtain wa al-Aimmah min Dhuriyatihim Alaihimusalam. Tahqiq: Muhammad Baqir al-Mahmudi. Beirut: Muasasah al-Mahmudi, 1400 H.
- Husaini, Hadi. Emam-e Mahdi - Tul-e Umr. Mashhad: Intisharat Astan-e Quds-e Razavi, Sherkat be Nashr, 1381 S.
- Ibnu Jauzi, Yusuf bin Qazugali. Tadhkirah al-Khawas. Qom: Al-Majma al-'Alami li Ahlilbait Alaihimusalam, Markaz al-Tiba'ah wa al-Nashr, 1426 H.
- Ibnu Maitham Bahrani, Maitham bin Ali. Qawaid al-Maram fi Ilm al-Kalam Qom: maktabah Ayatullah Mar'ashi Najafi, 1406 H.
- Ibnu Taimiyah Harrani, Ahmad bin Abdul Halim. Manhaj al-Sunnah al-Nabawiyah fi Naqd Kalam al-Shiah al-Qadariyah. Riyadh: Jamiah al-Imam Muhammad bin Mas'ud al-Islamiah, 1406 H.
- Irbili, Ali bin Isa. Kashf al-Ghummah fi Ma'rifah al-Aimmah. Tabriz: Bani Hashimi, 1381 H.
- Jawadi Amuli, Abdullah. Usareh Khalqat: Darbare-e Emam Zaman. Qom: Isra, 1390 S.
- Karajaki, Muhammad bin Ali. Kanz al-Fawaid. Tahqiq: Abdullah Ni'amih. Beirut: Dar al-Adhwa, 1405 H.
- Khajah Nasiruddin al-Tusi, Muhammd bin Muhamad. Talkhis al-Muhasal. Beirut: Dar al-Adhwa, 1405 H.
- Kulaini, Muhammad bin Ya'qub. al-Kafi. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiah, 1407 H.
- Mahdi Pur, Ali AKbar. Raz-e Tul-e Umr Emam Zaman az Didgah-e Ilm va Adyan. Tehran: Thawus Behest, 1378 S.
- Mahmud, Irfan. Wiladah al-Imam al-Mahdi fi Kutub al-Fariqin. Qom: Nashr al-Fuqahah, 1390 S.
- Muhammad Reyshahri, Muhammad. Daneshnameh Emam-e Mahdi Ajjalallahu Farajah bar Payeh Quran, Hadith va Tarikh. Qom: Muasasah Ilmi Farhanggi Dar al-Hadith, Sazman chap va Nashr, 1393 S.
- Nasibi Shafi'i, Muhmmad bin Talhah. Matalib al-Saul fi Manaqib Ali al-Rasul. Beirut: Muasasah al-Balagh, 1419 H.
- Qifari, Nasir. Usul Mazhab al-Shiah al-Imamiah al-Ithna Ashariyah. Bija,Bina, 1414 H.
- Refa'i, Abdul Jabbar. Mu'jam Ma Kutiba an al-Rasul wa Ahlilbait. Tehran: Wezarat Farhang va Irshad Eslami, Sazman Chap va Intisharat, 1371 S.
- Rezvani, Ali Asghar. Tavallud-e Hazrat-e Mahdi. 'Qom: Nashr-e Masjid Jamkaran, 1386 S.
- Sadr, Muhammad Baqir Bahth Haula al-Mahdi. Beirut: Markaz al-Ghadir li al-Dirasat al-Islamiah, 1417 H.
- Safi Golpeyghani, Lutfullah. Muntakhab al-Athar fi al-Imam al-Thani Ashar. Qom: Dftar Hazrat-e Ayatullah Safi Golpeyghani, Wahdah al-Nashr al-Alamiah, 1380 S.
- Safi Golpeyghani, Luhfullah. Selsele-e Mabahith-e Emamat va Mahdawiyat. Qom: Daftar Tanzim va Nashr Athar-e Hazrat-e Ayatullah Safi Golpeyghani, 1391 S.
- Safi Golpeyghani, Luhfullah. Tul-e Umr Hazrat-e Wali-e Asr. Qom: Daftar Hazrat-e Ayatullah Haj Shekh Ali Safi Golpeyghani, 1386, S.
- Site hajj.ir. «Derakhshesh-e Nam-e Ahlebait bar Divar-e Masjid al-Nabi Muhmmad al-Mahdi (afs) Zendeh ast». Tarikh darj matalib 25 Murdad 1396 S, Tarikh bazdid 9 Urdibehest 1403 S.
- Shekh Mufid, Muhammad bin Muhammad. al-Irshad fi Ma'rifah Hujajillah ala al-Ibad. Qom: Muasasah Alulbait Alaihimusalam li Ihya al-Turath, 1372 S.
- Shekh Mufid, Muhammad bin Muhammad. al-Masail al-Ashr fi al-Ghaibah. Qom: Dalil-e Ma, 1426 H.
- Shekh Saduq, Muhammad bin ALi. Kamal al-Din wa Tamam al-Ni'mah. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiah, 1395 H.
- Shekh Tusi, Muhammad bin Hasan. al-Ghaibah. Qom: Muasasah al-Ma'arif al-Islamiah, 1425 H.
- Tabrisi, Fadhl bin Hasan. I'lam al-Wara bi A'lam al-Huda. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiah, 1390 H.
- Zainali, Ghulamuhsin. «Emam Mahdi va Tul-e Umr (Pishineh va Dalail)». Majalah Intizar-e Mau'ud, juz. 6, payopi 6 Dey, 1381 S.