Tahaddi

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na changamoto. Ili kujua kuhusiana na changamoto katika Qur'ani, angalia makala ya Ayaat Tahaddi.

Tahaddi (Kiarabu: التحدّي) ni hatua ya Mitume ya kuwapa changamoto na kuwataka wanaokana Utume wao walete mfano wa miujiza yao. Changamoto inafanywa ili kuthibitisha Utume wa Mtume kwa muujiza. Qur'ani imertoa changamoto katika Aya sita, ambazo ni maarufu kwa jina la Ayaat Tahaddi. Katika Aya za Tahaddi (Aya za Changamoto), waliokanusha Utume wa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) wametakiwa kuleta mfano wa Qur'ani au angalau wasome sura inayofanana na sura za Qur'ani.

Kuna maoni tofauti kuhusiana na changamoto ya Qur'ani. Baadhi wanaamini kwamba, Qur'ani imetoa changamoto kupitia fasihi na ufasaha wake na maudhui yake; lakini kundi fulani limesema kuwa Qur'ani ilitoa changamoto tu katika suala la fasihi na ufasaha wake.

Utambuzi wa Maana

Tahaddi ni kumpa changamoto mpinzani na mshindani ili kudhihirisha udhaifu wake. Tahaddi katika istilahi ya sayansi ya Qurani [2] na teolojia ya Kiislamu [3] ina maana ya hatua ya Mitume ya kuwapa changamoto na kuwataka wanaokana Utume wao walete mfano wa miujiza yao.[4]

Tahaddi, Sharti la Muujiza

Kwa mujibu wa Adhduddin al-Aiji, mmoja wa wanateolojia wa karne ya 8 Hijria wa Ahlu-Sunna ni kwamba, baadhi ya wanateolojia wameitambua changamoto kuwa moja ya masharti ya muujiza na tofauti kati ya miujiza ya Mitume na mambo ya kivipaji au karama za mawalii ni kwamba miujiza huambatana na changamoto yaani kuwataka watu waje na muujiza kama huo, lakini mambo mengine ambayo siyo ya muujiza hufanyika pasi ya kuweko changamoto. [5] Imesemekana kuwa hata wale ambao hawakutaja sharti la changamoto katika kutoa fasili na maana ya muujiza, wakitumia maneno mengine walikuwa wakiiashiria maudhui hii hii. [6)

Pamoja na hayo, baadhi ya wanateolojia wanaamini kwamba, kutaja sharti la tahaddi katika kufafanua na kutoa fasili na maana ya muujiza, kwanza kabisa, hakuna ushahidi kutoka katika Qur'ani, Sunna, Ijmaa (maafikiano) na akili, na pili, kunasababisha miujiza mingi ya Mtume (s.a.w.w) ambayo haikuambatana na tahaddi (changamoto) isihesabiwe kuwa ni miujiza [7].

Tahaddi katika Qur'ani

Makala kuu: Ayaat Tahaddi

Qur'ani imetoa changamoto katika Aya sita; yaani inawataka wanaokanusha kuwa ni muujiza waje na mfano kwa ajili yake. Katika Aya hizi changamoto hii ni kwa ajili ya kuthibitisha kwamba, Qur'ani ni muujiiza na kwa ajili ya kuthibitisha ukweli wa Utume wa Mtume (s.a.w.w). Aya hizi zinfahamika kwa jina la Ayaat Tahaddi (Aya za Changamoto). [8] Neno changamoto linatokana na neno «تحدی» ambalo ni neno la Kiarabu lenye maana ya kutoa tangazo la kujizatiti katika kukabiliana na mpinzani, yaani kumtaka mpinzani ajitokeze na aoneshe uhodari wake. Kwa mara ya kwanza kabisa, neno hili lilitumika katika maandishi ya kiteolojia ya karne ya tatu, katika kuthibitisha changamoto ya Qur'an dhidi ya wapinzani wake. Kwa mujibu wa itikadi ya Waislamu ni kwamba; hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuleta kitabu kama Qur'ani, na hii ni ithibati ya muujiza huo wa Qur'an na Utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Qur’an yenyewe nayo ni yenye kusisita kwamba, Qur'an ni maneno ya Mungu, na pia imejizatiti ya kuwa hakuna awezaye kuleta mfano wake. Miujiza ya Qur’an ni miongoni mwa mada zinazojadiliwa katika fani ya sayansi (elimu) za Qur’an inayochunguza na kutafiti ithibati zinazothibitisha kuwa Qur’an ni muujiza wa Mungu. Katika Aya tatu za Tahaddi (changamoto) watu ambao hawaamini kwamba, Qur'ani inatoka kwa Mwenyezi Mungum wametakiwa walete mfano wake [9] katika Aya moja, wanakanusha wametakiwa walete sura kumi mfano wa sura za Qur'ani [10] na katika Aya mbili zingine, wametakkiwa kuleta sura mmoja mfano wa sura ya qur'ani. [11] Wahakikii wametofautiana kuuhusiana na kushuka Aya za changamoto. [12]

Mitazamo Kuhusiana na Changamoto ya Qur'ani

Wanazuoni wa Kiislamu wana mitazamo tofauti juu ya changamoto ya Quran. Baadhi wanaamini kwamba changamoto ya Qur’ani ina kipengele cha kifasihi tu; yaani wapinzani wake wametakiwa kuleta maandishi katika kiwango cha ufasaha wa Qur’an; [13] lakini baadhi ya wengine kama Allama Tabatabai (aliaga dunia 1360 Hijria Shamsia) ambaye ni mfasiri wa Qur'ani tukufu anasema kuwa, utoaji changamoto wa Qur'ani unajumuisha kila kitu kilichomo ndani ya Qur'ani kama vile: elimu, maarifa, Mtume kuwa ni mtu ambaye hajui kusoma na kuandika, habari za ghaiba na kutokuweko tofauti katika Qur'ani na katika balagha na ufasaha wake. [14]

Muhammad Hadi Ma'refat (aliyefariki dunia 1385 Hijria Shamsia) msomi na mtafiti wa masuala ya Qur'ani sambamba kupinga mtazamo wa kwanza ameandika: Lau changamoto ingekuwa ni mahususi kwa maneno na lafudhi za Qur’ani tu, basi Mwenyezi Mungu angeiwekea mpaka changamoto hiyo na kuifanya kuwa inawahusu Waarabu tu na asingeitoa na kuileta kwa sura mutlaki; changamoto ya Qur'ani inapaswa kuwa ni kitu cha jumla na kisichokuwa ni kwa ajili ya kundi maalumu au wakati maalumu. [15]

Kukabiliana na Changamoto ya Qur'ani

Kwa mujibu wa vitabu vya tafsiri na na vyanzo vya sayansi ya Qur'ani (Ulul al-Qur’an), baadhi ya watu ambao walijaribu kukabiliana na changamoto ya Qur'ani waliibua maudhui kama hiyo. Miongoni mwa watu hao walikuwa Musailamah Kadhab [19] na Nadhr bin Harith. [20] Ibn Kathir mfasiri wa Qur'ani tukufu wa karne ya 8 Hijria ameandika, Nadhr bin Harith alinukuu visa vya Rostam na Esfandiar na hivyo akadai kukabiliana na changamoto ya Qur'ani. [21]

Imeeleza kuwa, Abdallah bin Muqaffa'a, alikusudia kuandika kitu ambacho kitakuwa ni jibu lake kwa changamoto ya Qur'ani, lakini baada ya muda akabadilisha uamuzi wake. [22]

Kadhalika Mmarekani Mkristo mwenye mwenye jina la bandia la Nasiruddin Zafar ameandika katika kijitabu kiitwacho «Husn al-Ijaz fi Abtal al-I'jaz» sura mbili kwa kuiga Sura za Hamd na Kauthar, ambazo zilikosolewa na Ayatullah Khoui [23] na Rashid Ridha [24], miongoni mwa wafasiri wa Qur'ani. Rashid anasema, mwandishi wa suura hiii hakuwa na ufahamu kuhusu lugha ya Kiarabu. [25] Katika majarida ya Kifarsi pia, kumeandika makala kwa anuani ya «uchunguzi kuhusiana na ukosoaji wa kitabu cha Husn al-ijaz fi Ibtal al-I'jaz» katika kukosoa kitabu hicho. [26]

Kitabu kinachojulikana kwa jina la al-Furqan al-Haqq kimesambazwa nchini Marekani ambacho yumkini mwandishi wake ni Mayahudi au mkristo kwa jina bandia la al-Safii na al-Mahdi ambapo mwandishi wake hadi Utume lakini anafanya juhudi za kutilia shaka Utume wa mtukufu Muhammad (s.a.w.w). [27] Mwandishi huyu akiiga Qur'ani na kuchanganya Qur'ani na mafundisho ya Kiyahudi na Kikristo ametunga sura. [28] Kumeandikwa ukosoaji dhidi ya kitabu hiki; miongoni mwa vitabu vilivyoandikwa kukosoa kitabu hiki ni «al-Intisar Lil-Qur'an» kilichoandika na Saleh al-Khalidi. [29]

Rejea

Vyanzo