Sijida ya Kusahau
- Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine.
Sijida ya kusahau (Kiarabu: سجدتي السهو) ni sijida mbili zinazoletwa baada ya Swala ya wajibu kwa ajili ya kufidia baadhi ya makosa katika Swala. Sijida ya kusahau inapaswa kutekelezwa mara tu baada ya kutoa salamu ya kumaliza Swala na baada ya sijida ya pili. Ni lazima kutekeleza tashahudi na kutoa salamu ya kumaliza Swala. Dhikri ya sijida ya kusahau inatofautiana na dhikri za sijida za Swala.
Wanazuoni wa fiq'h wametofautiana kimtazamo kuhusiana na mambo ambayo yanapelekea sijida ya kusahau kuwa wajibu. Kuzungumza bila kukusudia (kusikokuwa kwa makusudi) katika Swala, kusahau moja ya sijida na kutoa salamu ya kumaliza Swala bila kukusudia katika mahali ambapo haipasi kufanya hivyo, ni miongoni mwa mambo ambayo yanapelekea sijida ya kusahau kuwa wajibu.
Fasili (ufafanuzi)
Kwa mujibu wa fat'wa za wanazuoni wa fiq'h ni kwamba, ili kufidia baadhi ya makosa katika Swala ni lazima baada ya Swala mtu atekeleze sijida mbili ambazo zinatambulika kama sijida ya kusahau (sijida za makosa yasiyo ya makusudi). [1] Mafaqihi wa Kishia wanajadili na kuzungumzia sijida ya kusahau pamoja na hukumu zake katika hukumu za kusahau (makosa yasiyo ya makusudi) na shaka za Swala. [2]
Namna ya kutekeleza sijida ya kusahau
Baada ya salamu anuie nia ya sijida ya kusahau na kuweka paji la uso juu ya kinachosihi kusujudu juu yake na kuna dhikri maalumu. Baada ya sijida ya pili, kunasomwa tashahudi na kutolewa tena salamu ya kumaliza Swala. [3] Akthari ya mafaqihi wa Kishia wanaamini kwamba, sijida ya kusahau haianzi kwa takbira ya kuhirimia (kusema Allah Akbar); [4] lakini kwa mujibu wa fat'wa ya Sheikh Tusi, inapaswa kutoa takbira ya kuhirimia kabla ya kutekeleza sijida ya kusahau. [5] Swahib al-Jawahir yeye ameuona kuwa dhaifu mtazamo huu wa Sheikh Tusi [6] na ameitambua takbira katika hili kuwa ni mustahabu. [7]
Dhikri ya sijida ya kusahau
Dhikri ya sijida ya kusahau ina tofauti na dhikri za Swala. Katika sijida ya kusahau inapasa kusoma moja ya dhikri zifuatazo:
Dhikr | Tarjama kiswahili |
---|---|
Bismillah wabillah asalamu alayka ayuha nabiyu warahmatu llah wabakatuh | |
Bismillah wa billah allahuma swali alaa muhamadi wa aali Muhamadi [1] | |
Bismillah wa billah wa swala llahu alaa Muhamadi wa aali Muhammad[2] |
Wakati wa sijida ya kusahau
Kwa mujibu wa fat'wa mashuhuri ya wanazuoni wa fiq'h wa Kishia ni kwamba, wakati wa kutekeleza sijida ya kusahau ni baada ya kutoa salamu ya kumaliza Swala. [10] Hata hivyo Sheikh Tusi anasema, kama sijida ya kusahau itakuwa ni kwa ajili ya mapungufu na nakisi (kupungua jambo miongoni mwa vipengee vya Swala), baadhi ya mafaqihi wa Imamiyyah wanasema kuwa, muda wa kutekeleza sijida ya kusahau ni kabla ya kutoa salamu ya kumaliza Swala. [11] Ibn Junayd al-Iskafi faqihi wa karne ya 14 Hijiria amekubaliana na mtazamo huu. [12]
Maeneo ambayo ni wajibu
Mafakihi wa Kishia wana mitazamo tofauti kuhusiana na maeneo ambayo sijida ya kusahau inakuwa wajibu. [13] Kwa kuuzingatia fat'wa mbalimbali, sijida ya wajibu huwa wajibu katika masuala au maeneo manne, matano au sita. [14] Kwa mujibu wa fat'wa mashuhuri, sijida ya kusahau huwa wajibu katika mambo matano yafuatayo au kwa mujibu wa ihtiyat ya wajibu(tahadhari) inapaswa kutekelezwa:
- Kuongea katika Swala kwa makusudi.
- Kusahau sijida moja.
- Shaka baina ya rakaa ya nne na ya tano katika Swala ya rakaa nne.
- Kutoa salamu ya kumaliza Swala bila ya kukusudia (kusiko kwa makusudi) katika mahali ambapo haipasi kufanya hivyo. Kwa mfano katika rakaa ya pili ya Swala ya rakaa nne na baada ya tashahudi anayeswali akatoa kimakosa salamu ya kumaliza Swala.
- Kusahau tashahudi. [15]
Baadhi ya mafakihi wameongezea jambo jingine nalo ni kukaa kusiko kwa makusudi katika sehemu ambayo anayeswali anapaswa kusimama, na kusimama kusiko kwa makusudi katika sehemu ambayo anayeswali anapaswa kukaa. [16] Sheikh Tusi anasema, baadhi ya mafakihi wa Shia Imamiyyah wanaitambua sijida ya kusahau kuwa ni ya lazima katika Swala katika kila ziada na nakisi (katika vipengee vya Swala ambavyo sio nguzo). [17] Allama Hilli ameukubali mtazamo huu. [18] Baadhi ya Marajii Taqlidi wanasema, sijida ya kusahau katika hali hii ni mustahabu. [19]
Hukumu
- Wakati wa kutekeleza sijida ya kusahau, ni lazima viungo vyote saba (viungo ambayo vinapaswa kugusa ardhi wakati wa kusujudu) viguse ardhi. (paji la uso, matumbo ya viganja vya mikono, magoti, na vidole gumba vya miguu). [20]
- Kuna hitilafu baina ya mafakihi kuhusiana na sharti la tohara na kuelekea kibla wakati wa kutekeleza sijida ya kusahau. [21]
- Sijida ya kusahau haifidii kusahau nguzo miongoni mwa nguzo za Swala. [22]
- Wajibu wa sijida ya kusahau ni wa haraka na wa hapo hapo; kwa maana kwamba, sijida ya kusahau inapaswa kutekelezwa mara tu baada ya kumaliza Swala; [23] hata hivyo kwa mtu ambaye hakutekeleza sijida ya kusahau, sio lazima aswali tena; bali anapaswa kutekeleza sijida ya kusahauu tu na kwa kurefuka Swala, wajibu wa sijida ya kusahau hauondoki. [24]
Rejea
Vyanzo
- Banī Hāshimī Khumaynī, Sayyid Muḥammad Ḥasan. Tawḍīh al-masāʾil marājiʿ. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1383 Sh.
- Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Mukhtalaf al-shīʿa fī aḥkām al-sharīʿa. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1413 AH.
- Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Qawaʿid al-aḥkām fī maʿrifat al-ḥalāl wa l-ḥarām. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1413 AH.
- Ḥillī, Ibn Idrīs al-. Ajwiba masāʾil wa rasāʾil fī mukhtalaf funūn al-maʿrifa. Edited by Sayyid Muḥammad Mahdi Musawi al-Khirsan. Qom: Dalīl-e Mā, 1429 AH.
- Ḥillī, Ibn Idrīs al-. Al-Sarāʾir al-ḥāwi li-taḥrīr al-fatāwa. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1410 AH.
- Ibn Junayd al-Iskafī, Muḥammad b. Aḥmad. Majmūʿat fatāwa Ibn Junayd. Edited by Ali Panah Ishtihardi. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1416 AH.
- Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tawḍīḥ al-masāʾil. Qom: Intishārat-i Imam ʿAli b. Abī Ṭālib, 1395 Sh.
- Muḥaqqiq al-Ḥillī, Jaʿfar b. Husayn al-. Al-Mukhtaṣar al-Nāfiʿ fī fiqh al-imāmiyya. Qom: Muʾassisa al-Maṭbūʿāt al-Dīnīyya, 1418 AH.
- Najafī, Muḥammad al-Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām. Edited by ʿAbbās Qūchānī & ʿAlī Ākhūndī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1404 AH.
- Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Al-Muʾtalaf min al-mukhtalaf bayn Aʾimma al-salaf. Edited by Mudirshana et al. Mashhad: Majmaʿ al-Buhūth al-Islāmiyya, 1410 AH.
- Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Mabsūṭ fī fiqh al-imāmīyya. Edited by Sayyid Muḥammad Taqi Kashfi. Tehran: al-Maktabat al-Murtaḍawīyya li-Ihyāʾ al-Āthār al-Ja'fariyya, 1387 AH.
{[End}}