Seyyid Abulqasim Khui

Kutoka wikishia
Sayyid Abulqasim Al-musawi Al-Khui

Sayyid Abulqasim Al-musawi Al-Khui (Aliyezaliwa mwaka 1278 na kufariki mwaka1371 Hijiria) alikuwa mmoja wa wanazuoni mtegemewa wa Kishia, na ni rejeo la wanajamii (mujitahi). Pia alikuwa ni mwanafani wa elimu ya nasaba na sifa za wapokezi wa Hadithi (elmu al-rijal), aliyeandika juzuu 23 za kitabu fani hiyo kiitwacho Muujam Rijali Al-Hadith. Naye vile vile mwandishi wa Tafsir Al-Bayan fi Tafsir. Al-Qur'an. Walimu wake mashuhuri katika fani ya fiqhi na usuli al-fiqhi, ni Mirzai Nainiy na Muhaqqiq Isfahaniy. Mwanzo wa kutambulika kwake rasmi kuwa ni rejeo la jamii katika kufutu masuala ya kidini (na kutambulikana kuwa ni mujtahid), ilikuwa ni baada ya kifo cha Sayyid Hussein Tabatabai Borujerdiy, na kifo cha Sayyid Mohsin Tabatabai Al-Hakim, huo ndio mwanzo wa umaarufu wake, hasa nchini Iraq. Khui katika kipindi cha miaka yake 70 ya ualimu, alifundisha kozi kamili za fiqhi na kozi sita juu ya fani ya misingi mikuu ya fiqhi (usuli al-fiqhi), na pia alifundisha kozi fupi ya kuhusiana na fani ya tafsiri ya Qur'ani. Wanazuoni wakiwemo Muhammad Is-haq Fayadh, Sayyid Muhammad Baqir Al-Sadr, Mirza Jawad Tabriziy, Sayyid Ali Sistani, Hussein Wahid Khorasani, Sayyid Musa Shabiri Zanjani, Sayyid Musa Sadr na Sayyid Abdul Karim Musawi Ardebiliy, ni miongoni mwa wanafunzi maarusu wa Sayyid Khui.

Ayatullah Khui ana nadharia muhimu katika fani ya fiqhi na usuli al-fiqhi, nadaria ambazo wakati wakati mwengine huwa zinatofautiana na nadharia au maoni ya mafaqihi maarufu wa Kishia. Kuna vyanzo vilivyorikodi hadi kufikia nadharia 300 kutoka kwake, ambazo zina mirengo tofauti na mafaqihi wengine wa Kishia. Miongoni mwa nadharia zake tofauti katika fani ya fiqhi na usuli Al-fiqhi, ni kupinga uwajibu wa makafiri katika kutekeleza masuala yanayo fungamana na fiqhi. Yaani kwa mtazamo wake; makafiri hawajibiki wala si lazima wao kutekeleza ibada mbali mbali, kama vile; sala, zaka n.k. Nadharia nyengine ya Ayatullah Khui, inahusiana na mwandamo wa mwezi. Yeye anaamini ya kwamba; Iwapo mwezi utaandama katika nchi fulani, basi ya pia ambayo inashiriaka na nchiyo kwa kiasi fulani cha usiku, basi nao watawajibika kufuata nchi hiyo katika suala hilo la mwandamo wa mwezi. Pia Ayatullah Khui anapinga nadharia ya kufuata mawafikiano ya mafaqihi waliopita katika fatwa zao, naye hakubaliani na mawafikiano ya ijmau ya wanazuoni waliopita. Wakati wa mamlaka yake ya kifiqhi, Ayatullah Khui alichukuiwa hatua mbalimbali za kueneza dini na kuutangaza Ushia pia alifanya juhudi katika suala la kuwasaidia wenye shida. Miongoni mwa juhudi zake, ni pamoja na kujenga maktaba, shule, misikiti, huseiniyyah na hospitali nchini Iran, Iraq, Malaysia, Uingereza, Amerika, India, nk.

Katika miaka ya 1340 Shamsia, Ayatullahi Khui alionekena kuwa na baadhi ya misimamo na kauli dhidi ya serikali ya Pahlawi (Phahlawi). Maandamano ya kupinga tukio la Faiziyyah la mwaka 1342 Shamsia, ni mojawapo ya misimamo yake dhidi ya serikali hiyo. Mwanzoni mwa harakati za Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ya mwaka 1357 Shamsia, Ayatullah Khui alikumbwa na baasdhi ya misukosuko, pia kushakiwa kuwa ana ajendea za siri dhidi ya Iran. Tuhuma hizo zilikuja baada ya yeye kukutana kwa Farah Diba, mke wa Muhammad Reza Pahlawi (mfalme wa Iran wa zama hizo), ambapo kulijitokeza mashaka baada ya mkutano huu. Baadae yeye alionekana kuunga mkono na kutetea masuala kadhaa yanayohusiana na mapinduzi ya Iran, kama vile kura ya maoni ya kuanzishwa kwa Serikali ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran. Pia yeye alisimama upande wa Serikali ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran, katika suala la na vita vya Iraq dhidi ya Iran. Wakati wa maandamano na uasi wa Mashia wa dhidi ya serikali ya Saddam Hussein, na kutaka kuwepo kamati maalumu ya uongozi itakayoongoza na kuendesha mambo mbalimbali chini ya uongozi wa Kishia, Ayatullahi Khui alikuwa chini ya shinikizo la serikali ya Saddam Hussein. Hadi mwishoni mwa maisha yake Ayatullahi Khui alikuwa chini ya kizuizi kudhibitiwa nyumbani kwake.

Maisha Yake

Sayyid Abulqasim Al-Musawi Khui alizaliwa mwezi 15 Rajab mwaka 1317 Hijiria sawa na mwezi 28 Aban 1278 Shamsia, kwenye mji wa Khui katika mkoa wa Azabajani ya Magharibi nchini Iran. [1] Baba yake ambaye ni Sayyid Ali Akbar Khui, alikuwa ni mwanafunzi wa Abdullahi Maamaqaniy. Ambaye Alihama kutoka Iran na kuhamia Iraq katika mji wa Najaf, mwaka 1328 Hijria [3] Mnamo siki ya Jumamosi ya mwezi 8 Safar 1413 Hijiria, ambayo ni sawa na mwezi 17 Mordad mwaka 1328 Shamsia, Sayyid Abulqasim Al-Musawi Khui alifariki dunia katika mji wa Kufa, akiwa na umri wa miaka 96. Kifo chake kilitokana na matatizo ya moyo. Sayyid Abulqasim Al-Musawi Khui alizikwa pembeni mwa Masjidi Al-Khadhraa, kwenye ukumbi aliozikwa ndani yake Amirulmuuminina Ali (a.s). [4]

Mke na Watoto

Sayyid Abulqasim Al-Musawi Khui aliowa mara mbili. Yeye alipata watoto watatu wa kiume na binti watatu, kutoka kwa mke wake wa kwanza. Kupitia mkewe wa pili, alipata watoto wanne wa kiume na binti wawili. [5] Baadhi ya watoto ambao wanatambilikana kuwa ni wanawe ni:

  • Sayyid Jamal Al-Din Khui, naye ni mtoto wake wa kwanza, ambaye alitumia muda mwingi wa maisha yake katika masuala yanayo husiana na mambo ya kielimu katika mambo ambayo watu walikuwa wakimrejea baba katika miongozo ya kidini. Baadhi ya kazi alizojishughulisha nazo ni pamoja na uandishi wa tafsiri na ufafanuzi wa kitabu; Kifayatu Al-Usuli, uandishi wa kitabu kiitwacho Bahthu fi Al-Falsafa wa 'Ilmu Al-Kalam, Taudhihu Al-Muradi fi Sherhr Tajridu Al-Itiqadi pamoja na kitabu cha mashairi kwa lugha ya Kiajemi. [ 6]
  • Sayyid Muhammad Taqiy Khui ni mtoto wake wa pili ambaye alikua ni katibu mkuu wake baada ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Mambo Kheri ya Imam Khui mnamo mwaka 1368. Baada ya uasi na maandamano ya Mashia dhidi ya serikali ya Saddam Hussein (Intifadhatu Al-Shabaniyyah) yaliofanyika mwaka 1369, Seyyed Mohammad Taqiy Khui alikuwa ni mjumbe wa bodi iliyochaguliwa na baba yake kusimamia maeneo yaliyokombolewa. Kufuatia kukandamizwa kwa uasi huo na mauaji ya Mashia, yeye aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani pamoja na baba yake, na hatimae alifariki dunia kupitia ajali ya gari mnamo tarehe 30 Tiir, mwaka 1373 Shamsia. Wengine wamechukulia tukio hili, kuwa ni mipango na njama zilizopangwa na serikali ya Saddam. [7] Mbali na kuhariri masomo ya sheria za kifiqhi ya babake, pia aliandika kitabu kuhusiana na fiqhi, kiitwacho Al-Iltizaamati Al-Taba'iyyah fi Al-'Uquudi.[8]

Hakuna taarifa za kina kuhusu binti za Ayatullahi Khui, lakini baadhi ya wakwe zake ni pamoja na Sayyid Nasrullah Mostanbat, Sayyid Mortadha Hakemiy, Sayid Jalaluddin Faqih Imaniy, Jafar Gharawi Nainiy, na Sayyid Mahmoud Milani. [9]

Maisha Yake ya Kielimu

Mnamo mwaka 1330 Hijria, akiwa na umri wa miaka 13, Abul Qasim Khui yeye akiwa pamoja na kaka yake (Abdullah Khoui), walijiunga na baba yao huko Najaf. [10] Alitumia miaka sita kusoma masomo ya utangulizi na viwango vya juu zaidi vya fani za dini, na kisha akashiriki kwenye masomo ya wanazuoni tofauti katika fani mbalimbali, ikiwemo fani ya fiqhi na usuli al-fiqhi kwa miaka 14. Miongoni mwa wanazuoni aliosoma kwao, kama alivyoelezea katika kitabu alichoandika kuhusiana na maisha yake, ni kwamba yeye alifaidika zaidi kielimu kupitia wanazuoni wawili, nao ni Muhammad Hussein Nainiy na Muhammad Hussein Gharawi Esfahani. [11]

Wanazuoni Waliompa Ijaza ya Ijtihadi

Sayyid Abul-Qasim Al-Khui, pamoja na ukweli wa kwamba, kulingana na maelezo yake, alifaidika zaidi kupitia wanazuoni wawili maarufu ambao ni; Mohammad Hossein Nainiy na Mohammad Hossein Isfahani. Yeye alijifunza kutoka kwao kozi kamili za elimu ya usuli al-fiqhi pamoja na baadhi ya vitabu vya fiqhi.Miongoni mwa wanazuoni wengine aliopata elimu kutoka kwao ni; Sheikh Al-Shari'a (aliyefariki mwaka 1338 Hijiria), Mehdi Mazandarani (aliyefariki mwaka1342 Hijiria) na Agha Dhiaa Al-Iraqiy. [12]

Baadhi ya wanzuoni wengine wa Khui ni pamoja na Muhammad Jawad Balaghiy ambaye alijifunza kutoka kwake fani ya theolojia, akida na tafsiri. Mwengine ni Sayyid Abu Tarab Khansari ambaye alimsomesha fani ya utambuzi wa nasaba na sifa za wapokezi wa Hadihti (fani ya elmu al-rijal na dirayah). Sayyid Abul Qasem Khansari alimsomesha fani ya hesabati, Sayyid Hussein Badkuubei alimpa fani ya falsafa na tasawwuf, pia akiwemo Sayyid Ali Qadhi. [13]

Sayyid Abu Al-Qasim akiwa katika kipidi cha masomo yake ya dini huko Najaf Iraq, alishirikiana na Sayyid Muhammad Hadi Milani (aliyefariki 1395 Hijiria), Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai (aliyefariki 1402 Hijiria), Sayyid Sadruddin Jazayeri, Ali Muhammad Burojerdi (aliyefariki 1395 Hijiria), Sayyid Husseyin Khadimiy pamoja na Sayyid Muhammad Milani Khamidani katika tafiti mbali mbali za kielimu.[14]

Mnamo mwaka 1352 Hijiria, Khui alipata ijaza (ruhusa) ya ijtihad kutoka kwa manazuoni tofauti, akama vile; Mohammad Hussein Naini, Muhammad Hussein Gharavi Esfahani, Agha Zia Iraqi, Muhammad Hussein Balaghi, Mirza Ali Agha Shirazi, na Sayid Abul Hassan Isfahani. [15]

Cheo cha Mujitahidi Mrejelewa (مرجع الدیني)

Haijulikani wazi tarehe au mwaka ambao Khui aliingia katika darja la kuwa yeye ni rejeo katika utowaji wa fatwa, lakini vyanzo vingi vimeeleza ya kwamba; Mwanzo wa yeye kushika mamlaka ya kuwa na cheo hicho, ilikuwa ni baada ya kifo cha Burojerdi na wamesisitiza kwamba sifa ya cheo chake hicho ilikolea rangi zaidi, baada ya kifo cha Sayyid Mohsin Tabatabai Hakim, hasa nchini Iraq.[16] Nafasi na mamlaka hayo ya kidini pia yanaripotiwa kuwa na umuhimu mkubwa miongoni mwa Mashia wa Iran.[17] Khui anajulikana kama ni mmoja mafaqihi wenye mamlaka na uwezo (ijaza na ruhusa) ya kutoa fatwa, ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa Mashia walio wengi, Waarabu na wasio Waarabu. [18]

Wanazuoni 14 Najaf, wenye cheo, sifa na mamlaka ya kutoa fatwa, akiwemo Sadra Badkuubei, Sayyid Muhammad Baqir Al-Sadr, Sayyid Muhammad Ruhani, Mojtaba Lankarani, Musa Zanjani, Yusuf Karbalai, Sayyid Yusuf Hakim, na Sayyid Jafar Marashi, walimtangaza Khui na kumtambua kuwa yeye ni miongoni mwa wanazuoni wakuu wenye hadhi na sifa kufutwa katika fatwa mbali mbali za kidini.[19] Sayyid Musa Al-Sadr alimtangaza Khui mbele kamati kuu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Lebanon, kuwa yeye ni mwanazuoni aliyebobea zaidi kielemu. [20]

Ukufunzi

Wakati alipokuwa masomoni katika Chuo Kikuu cha Najaf nchini Iraq, Abul Qasim Khui pia alikuwa akijishughulisha na ukufunzi chuoni humo. kulingana na vyanzo mbalimbali ni kwamba; Kila alipojifunza kitabu fulani, naye alikifunza kitabu hicho kwa wanafunzi wengine. [21]

Baada ya kifo cha Muhammad Hussein Gharaqi Naini na Muhammad Hussein Gharawi Isfahani, ukumbi wa mihadhara wa Sayyid Abulqasim Khui na Muhammad Ali Kazemi Khorasani, ziligeuka kuwa ndizo kumbi mbili muhimu za masomo mjini Najaf. Kwa msingi huo basi, baada ya kifo cha Kazemi Khorasani, ukumbi wa Khui wa mihadhara ya kielemu ndio ulikuwa ukiongoza mjini humo.[22] Kama Khui mwenye alivyoandika katika wasifu wake, katika kipindi chake chote kirefu cha ukufunzi, hakuna siku alizoacha kufundisha isipokuwa labde awe kakutwa na ugonjwa au kapata dharura ya safari. [23] Alifundisha kiwango na kozi za juu (kozi za ijitihadi ambazo huitwa bahthu al-kharij) kwa jumla ya miaka 70, akiwa katika chuo cha Najaf, na kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, kwa kipindi cha miaka 50 alisimamia jamvi la elimu, na akawa ni mwanazuoni maarufu na ndiye mshika hatamu wa chuo cha Najaf. Wanafunzi kutoka nchi za; Iran, India, Afghanistan, Pakistan, Iraq, Lebanon na baadhi ya nchi nyingine walikuwa wakihudhuria katika darsa zake.[24]

Khui aliwafundisha wanafunzi wake kozi kamili ya nyanja za juu za fani ya fiqhi, na kozi sita za nyanja za juu za fani ya usuli al-fiqhi. Pia kwa kipindi kichache alifundisha tafsiri ya Qur'an.[25]

Njia za Ukufunzi Wake

Khui katika kufundisha mada na fani za, amesifiwa kuwa ni mahiri mwenye ujuzi mkubwa katika uwanja huo. Yeye alikuwa akisomesa kupitia nidhamu maalumu yenye uchambuzi na ufasaha maridadi mno. Hakuwa na kawaida ya kutoka nje ya mada na kujadili mambo ya pembeni ambayo hayahusiani na somo lake. Yeye hakuonekana akiingiza mijadala ya kifalsafa katika mada zake, bali alikuwa akitumia Hadithi kadhaa katika ufafanuzi wake, pia alikuwa akijali sana umakini wa nukuu za Hadithi alizokuwa akizinukuu. [26] Misingi ya darsa zake iliegemea kwenye mihadhara ya Agha Dhiai Iraqi, Muhammad Hussein Gharawi Naini na Muhammad Hussein Gharawi isfahani akiambatanisha na maoni yake mwenyewe. [27]

Kazi na Tafsiri

Makala asili: Orodha ya kazi za Sayyid Abulqasim Musawi Khui

Sayyid Abulqasim Khui ameandika maandishi kadhaa kuhusiana na masomo kwama vile: Fiqhi, usuli al-fiqhi, elmu al-rijal, theolojia na ulumu Al-Qur'ani. Kazi zake zimekusanywa katika juzuu hamsini zilizopewa jina «Mausu'atu Al-Imam Al-Khui». [28] Toleo la kidijitali la mkusanyo huu linapatikana pia kwenye kitengo cha Noor Islamic Sciences Computer Research Center. [29]

Baadhi ya kazi zake zililizo maarufu zaidi ni pamoja na:

Wanafunzi

Khui na wanafunzi wake: kwa mpangilio kutoka kulia: Sayyid Jaafar Khui, Sayyid Musa Sadr, Sayyid Abdallah Shirazi, Abolqasem Khui, Sayyid Nasrullah Mustanabat na Sayyid Murtaza Hakkami.

Abulqasim Khui alikuwa na wanafunzi wengi, kuna vyanzo vingine vimeorodhesha zaidi ya wanafunzi 600 kwa waliosoma kwake.

Baadhi ya wanafunzi wake wengine ni pamoja na:

Mitazamo na Nadharia za Kielimu

Sayyid Abul Qasim Khui, alikuwa na nadharia zenye hadhi maalumu katika fani ya fiqhi na usuli al-fiqhi. Nadharia ambazo wakati mwingine zilitofautiana na fikra za mafaqihi maarufu wa Kishia. Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti, kuna fatwa 300 zinapatikana miongoni mwa fatwa zake, ambazo ziko kinyume na fatwa za wanazuoni au mafaqihi maarufu wa Kishia. [37] Baadhi ya khitilafu za kifatwa zilizopo baina yake na wanazuoni wengine ni:

  • Nadharia isemayo; Makafiri hawawajibiki kutenda matendo yao kulingana na sheria za fiqhi ya Kiislamu: Khui amekwenda kinyume na wanazuoni wengine, kama alivyokwenda Yusuf Bahrani kinyume na rai za wanazuoni wote wa Kishia. Mtazamo wake yeye ni kwamba; Makafiri pia wanawajibika kuamini misingi mikuu ya dini, na pia wanawajibika kutenda matendo yao kulingana na sheria za kifiqhi. [38] Ila nadharia za wanazuoni wengine ni kwamba; Makafiri hawana wajibu wa kutenda matendo yao kwa mjibu wa sheria za Kiislamu kabla ya wao kuukubali Uislamu, isipokuwa watawajibika kufanya hivyo baada ya wao kusilimu. [39]
  • Kutokubaliana na nadharia maarufu za mwandamo wa mwezi: Maoni ya Khui yapo kinyume na maoni ya wanazuoni walio wengi. Kwa mtazamo wa Khui ni kwamba; iwapo mwezi utaandama kwenchi moja, basi nchi nyengine pia watawajibika kufuata mwandamo huo, ila sharti yake ni kwamba, nchi hizo mbili ni lazima ziwe zinashirikia masaa fulani ya usiku baina yao. Kwa sababu kigezo cha mwanzo wa mwezi wa mwandamo, kinazingatia hali ya kuondoka kwa mwezi kutoka kwa ecliptic, ambalo tukio la kijografia na linahusiana na nafasi ya jua, mwezi, na dunia, na halitegemei nchi na mipaka yake dunia. [40]
  • Kutokubali nadharia za kushikamana umaarufu za wanazuoni wa kale, na kutokubali mawafikiano ya wanazuoni (ijmaa): Sayyid Abul Qasim, kuhusu umaarufu wa fatwa, alikuwa na rai tofauti kabisa na rai mashuhuri za wanachuoni wa Kishia. Kwa mujibu wa wanazuoni wengi wa Kishia wanaoshikamana na itikadi ya Usuliyyiina, kama kutakuwa na Fat’wa mashuhuri miongoni mwa mafaqihi waliopita, kisha kukawa na Hadithi sahihi inayopingana na fatwa hiyo, basi Hadithi hiyo haitakuwa na thamani mbele ya fatwa hiyo. Hata hivyo, Khui yeye hakubaliani na nadharia hii. Khui mada ya umaarufu wa fatwa za wanazuoni wa zamani, amelijadili katika elimu ya usuli al-fiqhi kwenye mlango unaohisiana na masuala ya "migongano ya kanuni za kisheria (kifiqhi)". Yeye anaamini ya kwamba; umashuhuri wa fatwa hauwezi ukasababisha Hadithi dhaifu kupata nguvu, Kama vile mafakihi kutoijali Hadith sahihi hakutaifanya Hadithi hiyo kuwa batili. [41]
  • Vile vile ametilia shaka uhalali wa kushikanmana na maafikiano au makubaliano (ijmaa) ya wanazuoni waliopita yaliyonukuliwa na mwanazuoni fulani au hata makubaliano yalioyakinishwa katika kutokea kwa makubaliano hayo. Hata hivyo, Khui amechukwa tahadhari katika fatwa zake, na hakwenda kinyume na makubaliano ya wanazuoni waliopita. [42]
  • Fatwa maarufu zinazopingana na fatwa za wanazuoni wengine: ruhusa ya mwanamke kutoka nje ya nyumba bila ya idhini ya mumewe, ruhusa ya mwanamke kutoa mimba iwapo atakhofia kupoteza maisha kutokana na mimba yake, ruhusa ya ndoa ya kudumu ya mwanamume Mwislamu na mwanamke wa Ahlul-Kitabi, ruhusa ya kuanza Jihadi hata kama zama ambazo Imamu Maasumu hayupo, hakimu si lazima awe mujtahid, Na pia kwa mtazamo wake, ni halali kutumia ngozi zinazoingizwa kutoka nchi zisizokuwa za Kiislamu ambazo uchinjaji wao wa kisharia unatiliwaa mashaka. [43]

Nyenendo za Kisiasa

Kuunga mkono Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

Sayyid Abulqasem Khui alitoa matamshi na matangazo ya kulaani vitendo vya serikali ya Pahlawi tokea hafikia daraja ya ijitihadi. Baada ya hapo kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi, alifuata siasa za ukimya, hatimae akavunja siasa yake hiyo ya ukimya katika siku ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, mnamo mwezi wa Bahman 1357 Shamsia. Ambapo alimuunga mkono Imam Khomeini pamoja na Mapinduzi ya Kiislamu. Pia Sayyid Abulqasem Khui aliunga mkono maandamano na uasi wa Mashia wa Iraq, ujulikanao kwa jina la Intifadha Shabaniyah. Uungwaji mkono wake wa Intifadha Shabaniyah, ulipelekea kukamatwa na kufungwa kifungo cha ndani. [44] Baadhi ya nyenendo za kijamii na kisiasa za Ayatullah Khoui ni:

Nyenendo Dhidi ya Serikali ya Pahlawi

Mnamo mwezi wa Mehr 1341 Shamsia, katika telegramu aliyoituma kwa Mohammad Reza Pahlawi (Shah wa Iran), Khui alipinga muswada wa sheria wa jumuiya za mikoa na wilaya, na akaushutumu ya kuwa, mswaada huo ni mswaada unaokwenda kinyume na Sharia. Azimio za mswaada huo lilikuwa ni kuwapa wanake haki ya kupiga kura, na kutoa ruhusa kwa viongozi wanaotawazwa kutumia kitabu chochote kile wakitakacho, hali kwamba hapo mwanzo waliapishwa kupitia Qur'an. [45] Pia Sayyid Khui, katika ujumbe kwa Sayyid Muhammad Behbahani, alisisitiza ya kwamba; kunyamazisha sauti ya wananchi kwa nguvu za dola, si jambo la kudumu kwa muda mrefu na propaganda za kidanganyifu haziwezi kutatua matatizo na wala hazitaponya maradhi ya uchumi uliofilisika, na katu haitokuwa ya kutibu huzuni za watu na kwarejeshea furaha nyoyoni mwao. [46] Katika radiamali yake Sayyid Abulqasem Khui, kuhusiana na tukio la Faidhiyya lililotokea mwanzoni mwa mwaka 1342 Shamsia. Alimtumia Muhammad Ridha telegramu akionesha masikitiko yake kuhusiana na kuporomoka kwa dola za Kiislamu na nyenendo za viongozi wake. [47] Baada kupita kipinda cha mwezi mmoja, akijibu barua ya jopo la wanazuoni wa Iran, alitoa tamko la kuonesha ubovo wa vingozi na kutostahiki kwao kushika nafasi za uongozi kutokana na ubovo waliokuwa nao, alieleza wajibu mzito wa wanazuoni katika kukabiliana na hali hiyo, akisema ya kwamba ukimya haukubaliki tena katika hali kama hiyo. [48] Baada ya mauaji ya watu ya tarehe 15 Khordad 1342 Shamsia, akiutaja mfumo tawala wa Iran kuwa ni wa kidhalimu, akipiga marufuku kushiriki katika uchaguzi wa 21 wa Majlis (bunge) na kulihisabu bunge hilo kuwa ni buge lisilo na uhalali wa kisheria. Kumuunga kwake mkono Imam Khomeini baada ya kukamatwa na kuanzishwa uvumi wa kumpandsha Imam Khomeini mahakamani, ni baadhi ya misimamo yake mingine ya kisiasa maishani mwake. [49]

Kufukuzwa kwa Wairani Kutoka Nchini Iraq

Makala Asili: Maawidina

Katika tukio la kufukuzwa Wairani kutoka Iraq, lillilotokea mwishoni mwa miaka ya 1340 Shamsia, Khui alikuwa mmoja wa wanazuoni wachache wa Kishia ambao hawakufukuzwa kutoka Iraq. Hata hivyo, kufukuzwa kwa wanafunzi wake wengi kulipunguza ufanisi wa masomo yake. [50] Wengi wa wanafunzi wa Khui, kwa kujiunga kwao chuo kikuu cha Qom kilichoko nchini Iran, waliweza kutangaza na kukuza nadharia mbali mbali za mwalimu wao katika fani ya fiqhi na usuli al-fiqhi. Kabla ya hapo Chuo Kikuu cha Qom, kilikuwa kimeathiria zaidi na mirengo na nadharia za bwana Haeri Yazdi na Borujerdi, ambao ni wanazuoni maarufu wa Iran. Kuingia kwa wanafunzi wa Khui chuoni humo kulileta mchipuko mpya wa kielimu, mchipuko ambao ulileta muowano wa nadharia za kifiqhi na usuli al-fiqhi zenye sura za wanazuoni tofauti; ambao ni Khui, Mirza Naini, Muhaqqiq Isfahani na Agha Dhiyaa-i Iraqiy. [51]

Kipindi cha Ukimya cha Zaidi ya Miaka Kumi

Khui baada kushika nafasi ya mujitahidi mtegemewa (مرجع الدینی), alijiondoa katika uwanja wa kisiasa. [52] Kipindi hiki kiliambatana na miaka ya uwepo wa Imam Khomeini huko Najaf. [53] Ukimya wake dhidi ya matukio ya Mapinduzi ya Iran ya 1357 uliuzua malalamiko kadhaa dhidi yake nchini Iran. [54] Ziara ya Farah Diba, mke wa Mohammad Reza Pahlawi, aliyetembela ofisi yake nchini Iraq mnamo tarehe 28 Aban mwaka 137, kulichochea zaidi malalamiko hayo dhidi yake. Khui akijibu baadhi ya wanazuoni, alisema kuwa; Ziara bibi Farah haikuwa ni ziara rasmi, bali ilikuwa ni ziara isiotarajiwa. [55]

Farah Diba Kukutana na Khui

Farah Diba, mke wa Muhammad Reza Pahlawi, Shah (mfalme) wa Iran wa zama hizo, alimtembelea Sayyid Abul Qasem Khoei mnamo tarehe 28 Aban 1357. Ziara ya Farah Diba ilisadifiana na siku ya maadhimisho ya Eid Al-Ghadir. [56] Mkutano huu ulifanyika katika hali ambapo harakati za kuleta Mapinduzi ya Kiislamu ya watu wa Iran yalikuwa kileleni kabisa, huku Sayyid Ruhollah Mousawi Khomeini akiwa amefukuzwa kutoka Iraq. [57] Mkutano wa Farah Diba na Khui ulipelekea Khui kukosolewa katika vikao mbali mbali vya kimapinduzi nchini Iran. [58] Jammbo ambalo liliwafanya wanazuoni kumjibu bwana Sayyid Sadiq Ruhani, na kumpasha habari yakwamba; Ziara hiyo haikuwa ziara rasmi, bali ilikuwa ni ziara ya ghafla isiyotarajiwa. katika jawabu hiyo walisisitiza wakisema ya kwamba; sisi tulipinga na kukosoa vikali matukio mabaya yasioridhisha pamoja na maafa yaliyotokea nchini Iran. [59] Hussein Fardoost, mtu wa karibu wa Muhammad Reza Pahlawi, alitoa ufafanuzi wake kuhusu mkutano huo akisema: Ayatollah Sayyid Abul Qasim Khui aliyapuza maombi Farah kuhusiana na ziara yake, ila Farah binafsi aliamua kuvaa hijabu ya Kiislamu na kwenda nyumba kwa Ayatollah Khui bila ya kusubiri suhusa kutoka Khui. [60]

Kuandamana na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

Khui baada ya kukutana na Farah Diba katika hali ambayo mapambano ya wananchi wa Iran dhidi ya serikali ya Pahlawi yalikuwa yamezidi kushadidi, aliunga mkono Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kisha kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kadhia mbalimbali. Kabla ya ushindi wa mapinduzi, katika tamko lake rasmi alilolielekeza kwa wanazuoni na wananchi wa Iran, aliwataka wananchi wanazuoni na wannchi kwa jumla, aliwata wachukue haatua kishujaa bila ya kuvunja Sharia za dini. [61] baada ya hapo, Khui katika kadhia ya kura ya maoni kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu, aliwataka watu watie kura ndio juu ya kuuchagua Mfumo Jamuhuri ya Kiislamu. Pia Khui aliwahimiza wanafunzi wake kushiriki katika harakati za kuleta mapinduzi nchini Iran. Katika vita kati ya Iraq na Iran, licha ya shinikizo la serikali ya Saddam la kumtaka aiunge mkono serikali ya Iraq, yeye alitoa fatwa ya kujuzisha kutumia pesa za baitul al-mal (mfuko wa mali za Waislamu) kutumika katika mahitaji ya wapiganaji wa Iran. [62]

Intifadha Shabaniyyah ya Iraq

Makala Kuu: Intifadha Shabaniyyah Iraq

Abulqasim Khui aliteua ujumbe wa watu 9 kusimamia maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Mashia. Kushindwa na kufeli kwa Intifadha Shabaniyyah (uasi wa Mashia waIraq dhidi ya serikali ya Saddam) kulipelekea Khui kufungwa kifungo cha ndani na kukabiliwa na shinikizo kubwa dhidi yake, kutoka serikali ya Iraq katika kipindi cha utawala wa Saddam Hussein. [63] Mnamo mwaka 1991 Miladia, utetezi na uungaji mkono wa Sayda Al-Qasim Khui wa uasi wa Mashia, ulipelekea kukamatwa kwake na chama cha Ba'ath na kupelekwa Baghdad. Siku mbili baada ya kukamatwa kwake, alipelekwa kwa Saddam Hussein kwa nguvu na Saddam Hussein akazungumza naye kwa kutumia lugha ya kejeli na matusi. [64]

Huduma za Kidini na Kijamii

Katika mamlaka yake ya uongozi wa kidini, akiwa ni mmoja wa wanazuoni wanaotegemewa kifatwa, Khui kupitia fedha za baitu al-mali (mfuko au wa fedha za Waislamu) alijenga maktaba, shule, misikiti, husseiniyyah, hospitali, zahanati, mabweni, taasisi za mambo ya kheri na vituo vya kulelea watoto yatima katika nchi tofauti, zikiwemo Iran, Iraq, Malaysia, Uingereza, Amerika na India. Jengo kuu la Shirika la Hisani la Khui liko mjini London. [65] Baadhi ya vituo vya Kiislamu vilivyo chini ya usimamizi wa Shirika la Hisani la Khui ni:

  • Kituo cha Al-Imam Al-Khui mjini London kinajumuisha Kituo Kikuu cha Kiislamu (مرکز اسلامی), skuli ya watoto wa kiume ya Imam Sadiq (a.s), Skuli ya watoto wa kike ya Al-Zahra (a.s), ukumbi wa mikutano, maktaba ya umma (public library), na duka la vitabu. Kuna idadi ya wanafunzi 800 wanasoma katika skuli mbili hizo zilizoko chini ya Kituo cha Al-Imam Al-Khoei mjini London. Jarida la "Al Noor" ni jarida la kituo hicho linalochapishwa kila mwezi kwa lugha ya Kiarabu na Kiingereza. [66]
  • Kituo cha Kiislamu cha Imam Khui mjini New York: Ni kilichokusanya ndani yake ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu elfu tatu, maktaba yenye vitabu zaidi ya elfu kumi, skuli ya chekechea, skuli ya watotot wa kike na watoto wa kiume, kila moja ikiwa na uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 150, Skuli ya Imani, ambayo skuli maalumu kwa ajili ya kusomesha lugha ya Kiarabu, Qur'ani na mafunzo ya amali (tabia njema) kwa watoto. Pia kutuo hicho kana sehemu maluumu ya kukoshea maiti, pamoja na vitengo vyengine kadhaa. [67]
  • Taasisi ya Hisani ya Imam Khui huko Montreal: Taasisi hii ilianzishwa mwaka 1989 Miladia kwa lengo la kutoa huduma za kidini, kitamaduni na kijamii kulingana na madhehebe ya Kishia katika nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu. Jengo la Utamaduni la Imam Khui huko Mumbai: Ni jengo lenye eneo la mita za mraba 100,000, umbali wa kilomita 20 kutoka mji wa Mumbai. Ndani yake linajumuisha ukumbi mkubwa wa mikutano, msikiti wenye uwezo kupokea watu 3,000, maktaba yenye vitabu 50,000 na huseiniyyah yenye uwezo wa kuchukuwa watu 700, skuli ya masomo ya kidini yenye uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 1,000, skuli ya Msingi na sekondari yenye wanafunzi 1,200, pamoja na duka la dawa na zahanati. [68]

Kazi Mbalimbali Kuhusiana na Khui

Filamu itwayo «Ayatullahi» iliongozwa na Sayyid Mustafa Mousawitabar na kutengenezwa kwa msaada wa Ouj Media Art Organization. Filamu hii inahusiana na maisha, elimu na uhusiano wa Ayatollah Khui na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. [69]

Mktaba ya Picha

Vyanzo

  • Anṣārī Qumī, Nāṣir al-Dīn. Nujūm-i ummat – Haḍrat-i Āyat Allāh al-Uzmā Ḥāj Sayyid Abū l-Qāsim-i Khūʾī. Journal of Nūr-i ʿilm, Mihr & Ābān 1373 Sh.
  • Ayyāzī. Chih kasānī murawwij-i maktab-i āyat Allāh Khūʾī shudand?. Interview with Mohammad Ali Ayyāzī in Mehrnameh magazine. 1390 Sh
  • Ḍāhir, Yaʿqūb. Masīrat al-Imām al-Sayyid Mūsā al-Ṣadr. Beirut: Dār Bālil, 2000.
  • Fayyāḍ, Muḥammad Isḥāq. "Nuāwarīhā-yi uṣūlī wa fiqhī-yi Āyatollāh Khūyī". Journal of Kāwishī nu dar fiqh. Autumn & Winter 1377 Sh.
  • Hāshimīyānfar, Sayyid Ḥasan. Gūnashināsī-yi raftār-i sīyāsī-yi marājiʿ-i taqlid-i Shīʿa. Tehran: Dānishgāh-i Imām Ṣādiq, 1390 Sh.
  • Islāmī, Ghulāmriḍā. Ghurūb-i khurshīd-i fiqāhat. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1372 Sh.
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. Khātira-yi khwāndanī darbāra-yi dastgīrī-yi Ayatollāh Khūʾī dar intifāḍa-yi Shaʿbānīyya. https://www.khabaronline.ir, 9 Ābān 1391 Sh.
  • Jaʿfarīyān, Rasūl. Tashayyuʿ dar ʿIrāq, marjaʿīyyat wa Irān. Tehran: Muʾassisa-yi Muṭāliʿāt-i Tārīkh-i Muʿāṣir-i Irān, 1386 Sh.
  • Khātirāt-i Āyatollāh ʿAbbās Khātam-i Yazdī. Tehran: Intishārāt-i Markaz-i Asnād-i Inqilāb-i Islāmī, 1380 Sh.
  • Mudarrisī, Dikhālat-i Ākhund-i Khurāsānī dar Mashrūṭa mutaʿāraf-i Najaf nabūd. http://faridmod.blogfa.com. 22 Shahivar 1390 Sh.
  • Pīrī Sabziwārī, Ḥusayn. Āyat Allāh al-Uzmā Sayyid Abū l-Qāsim Khūyī, Qurʾānshinās-i buzurg-i muʿāṣir. Journal of Gulistān-i Qurʾān, Aban 1381 Sh.
  • Raʾīszāda, Muḥammad. "Khoeī, Abū l-Qāsim". Dānishnāma-yi jahān-i Islam. Tehran: Bunyād-i Dāʾirat al-Maʿārif-i Islāmī, 1375 Sh.
  • Ṣadrāʾī Khūʾī, ʿAlī. Sīmā-yi Khuy. Tehran: Sāzmān-i Tablīqāt-i Islāmī, 1374 Sh.
  • Sharīf Rāzī, Muḥammad. Ganjīna-yi dānishmandān. Tehran: 1352-1354 Sh.
  • Sharif, Sayyid Saʿīd. Talāmidha al-Imām al-Khoeī. In Al-Musim magazine, 1414 AH.
  • Subḥānī Tabrīzī, Jaʿfar. "Marjaʿīyyat dar Shīʿa". Journal of Maktab-i Islām. Mehr 1371 Sh.
  • Ṭabāṭabāyi, Sayyid Hādī. Dīdār-i purmajarā wa riwāyathā-yi mutafāwit. http://mobahesat.ir, 13 Tir 1394 Sh.
  • Tihrānī, Aqā Buzurg al-. Al-Dharīʿa ilā taṣānīf al-Shīʿa. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1403 AH.
  • Tihrānī, Aqā Buzurg. Ṭabaqāt aʿlām al-Shīʿa. Qom: Ismāʿīlīyān, [n/d].
  • Yādnāma-yi Haḍrat-i Āyat Allāh al-ʿUzmā Āqāy-i Ḥāj Sayyid Abū l-Qāsim-i Khoeī, 1372 Sh. (based on the online version available at http://www.alkhoei.net)