Nenda kwa yaliyomo

Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt

Kutoka wikishia

Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt (Kiarabu: سَلْمانُ مِنّا أهل‌َ البيت) ni hadithi mashuhuri, mutawatir (iliyopokewa kwa wingi) na yenye sanadi na mapokezi sahihi iliyopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na fadhila na daraja ya Salman Farsi. Baadhi ya Maimamu wa Kishia kama Imamu Ali (a.s), Imamu Sajjad (a.s) na Imamu Baqir (a.s) wamebainisha hadithi hii kwa sura ya kujitegemea au kwa kunukuu kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w).

Tukio la kuchimbwa handaki katika vita vya Ah’zab na maneno ya Omar bin al-Khattab kuhusiana na Salman kutokuwa Muarabu ni baadhi ya matukio ambayo yametajwa kuwa sababu ya Mtume (s.a.w.w) kusema hadithi hii.

Sheikh Swaduq, Sheikh Tusi na Sheikh Mufid ni baadhi ya Maulamaa wa Kishia na Ibn Saad na Ibn Hisham ni wanazuoni na Maulamaa wa Ahlu-Sunna ambao wameinukuu hadithi hii katika vitabu vyao.

Baadhi wamesema kuwa, makusudio ya Mtume (s.a.w.w) ya hadithi hii ya: “Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt” «سلمان منا اهل البیت» ni kwamba, Salman yupo katika dini yetu. Baadhi ya wengine wanasema kuwa, hadithi hii inabainisha fadhila na daraja ya Salman Farsi kwa upande wa ukaribu na imani yake, maadili na matendo yake kwa Mtume (s.a.w.w).

Muhammad Ali Asbar mwaka 1413 Hijria alitoa kitabu kilichokuwa na anuani ya «سلمان منا اهل البیت» “Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt” huko Beirut kuhusiana na historia na maisha ya Salman Faisi na kusambaza hadithi ya: «سلمان منا اهل البیت» “Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt”.

Utambulisho na Nafasi Yake

«“Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt” «سلمان منا اهل البیت» ni hadithi ambayo kwa mujibu wa wahakiki wa Kishia imenukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w).[1] Kwa mujibu wa vyanzo vya hadithi, baadhi ya Maimamu wameibainisha moja kwa moja au kwa kunukuu kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w).[2] Kwa mfano Imamu Ali (a.s) amemtaja Salman kuwa ni katika Ahlul-Bayt wakati alipokuwa akijibu swali kuhusiana na sahaba huyo wa Mtume.[3] Katika kitabu cha Kafi kilichoandikwa na Sheikh Kulayni (aliaga dunia:329 Hijria) kuna hadithi pia iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s) ambayo ina tofauti kidogo na ambayo ndani yake inamtambua Salman kuwa ni katika Ahlul-Bayt.[4] Kadhalika kwa mujibu wa hadithi kutoka katika kitabu cha Rawdhat al-Waidhin kilichoandikwa na Fattal al-Nayshaburi watu walinukuu maneno mbele ya Imamu Baqir (a.s) kutoka kwa Salman Farsi. Imamu akawataka wanyamaze na kisha akasema, muiteni “Salman Muhammadi”; kwa sababu yeye ni katika Ahlul-Bayt (a.s).[5] Katika kitabu cha Rijal Kashi pia imenukuliwa hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) katika mlango wa: “Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt”.[6]

Asili ya Hadithi

Kuhusiana na kutokea tukio ambalo lilipelekea kutolewa hadithi hii, kuna hitilafu zinazoshuhudiwa katika vyanzo na vitabu.[7] Tabarsi, mfasiri wa Qur’ani wa Kishia na Ibn Saad mwandishi wa sira wa Kisuni wameripoti kwamba, Mtume (s.a.w.w) aliwaainishia Waislamu sehemu ya kuchimba handaki katika Vita vya Ahzab. Muhajirina na Ansari walitofautiana kuhusiana na Salman Farsi ambaye alikuwa mtu mwenye nguvu na kila kundi miongoni mwa makundi hayo likawa linataka Salman awe upande wake ambapo katika hali hii Mtume (s.a.w.w) alisema: “Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt”.[8]

Sheikh Mufid ameandika katika ripoti ya kipekee kwamba: Wakati Mtume (s.a.w.w) aliposikia maneno ya Omar bin al-Khattab akisema kwamba, Salman sio Muarabu, alipanda katika mimbari ambapo sambamba na kutoa hotuba iliyoeleza kwamba, wasifu na ubora wa watu juu ya watu wengine sio katika mbari wala rangi zao, bali ni kwa taqwa na kumcha Mwenyezi Mungu, alimtaja Salman kuwa ni bahari isiyo na kikomo na dafina na hazina isiyo na mwisho na akasema kuwa, Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt.[9] Katika kitabu cha Sulaym Ibn Qays pia kuna hadithi iliyonukuliwa ambapo Mtume (s.a.w.w) aliwataka watu wote waondoke isipokuwa Ahlul-Bayt (a.s). Watu wakaanza kuondoka ambapo Salman naye akawa anaondoka, ambapo Mtume alimtaka abakie; kwani yeye ni katika sisi.[10]

Itibari ya Hadithi na Vyanzo Vyake

Hadithi ya “Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt” «سلمان منا اهل البیت», ni katika hadithi mashuhuri, zenye itibari[11] na mutawatir.[12] Baadhi ya wahakiki wameitambua hadithi hii kuwa mapokezi yake ni sahihi, yenye nguvu si kama hadithi moja bali ni sehemu ya kushirikiana hadithi kadhaa [13] za Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (as).[14]

Sheikh Swaduq katika kitabu cha Uyun Akhbar al-Ridha,[15] Sheikh Tusi katika al-Tibyan na Misbah al-Mujtahid,[16] Sheikh Mufid katika al-Ikhtisas,[17] Ibn Shahrashub katika Manaqib Aal Abi Talib,[18] Ahmad bin Ali Tabarsi katika al-Ihtijaj,[19] na vilevile Sulaym Ibn Qays[20] ni baadhi ya Maulamaa wa Kishia ambao wamenukuu kadithi hii. Ibn Saad katika al-Tabaqat al-Kubra[21] na Ibn Hisham katika al-Sirat al-Nabawiyah[22] nao ni baadhi ya Maulamaa wa Kisuni ambao wameinukuu kadithi hii.

Ufahamu Tofauti

Wanazuoni wa Kiislamu wamekuwa na ufahamu na welewa tofauti kuhusiana na hadithi ya «سلمان منا اهل البیت» yaani “Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt”:

Fadhl bin Hassan Tabarsi na Sheikh Tusi wamesema kuwa, makusudio ya Mtume wa Allah yalikuwa ni kwamba, Salman yupo katika dini yetu.[23] Baadhi ya wengine wameandika kwamba, hadithi hii inabainisha daraja na cheo cha Salman kwa upande wa itikadi, maadili na matendo alikuwa amekaribia kwa Mtume (s.a.w.w).[24]

Ibn Arabi, mmoja wa maurafaa wa Kiislamu anasema kuwa, maneno haya ni ithbati na ushahidi wa Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na daraja ya utakasifu wa Salman Farsi; kwa ushahidi huu kwamba, Mwenyezi Mungu katika aya ya Tat’hir (utakaso) amewatakasa na kuwatoharisha Mtume na Ahlul-Bayt (a.s) na uchafu wa aina yoyote na kila ambaye atafanana nao ataungana na Mtume na Ahlul-Bayt. Kwa muktadha huo, Aya hii inamjumuisha Salman pia;[25] lakini Mulla Muhsin Faydh Kashani amepinga matamshi na maneno haya ya Ibn Arabi ya kujumuishwa Salmna bin Farisi na wengine wasiokuwa Ahlul-Bayt katika Aya ya utakaso na kueleza kwamba, hata haijuzu kutaja jambo hili.[26]

Kundi la watafiti linasema kuwa, hadithi hii inaonyesha nafasi ya kweli ya Ahlul-Bayt (a.s)[27] huku kundi jingine likisema kwamba, hizi ni katika sifa maalumu za Salman Farsi[28] na ni katika siri za kufikia Salman katika daraja ambayo Mtume na Maimamu wanamtaja kuwa yeye ni katika wao.

Monografia

Muhammad Ali Asbar mwaka 1413 Hijria aliandika kitabu kilichokuwa na anuani ya “Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt” «{[Arabic|سلمان منا اهل البیت}}» kwa lugha ya Kiarabu kuhusiana na Salman Farsi na kikasambazwa na Taasisi ya Dar al-Islamiyah Beirut, Lebanon kikiwa na kurasa 354.[29]

Rejea

Vyanzo