Sahihain

Kutoka wikishia
Makala hii inahusiana na istilahi ya Sahihayn. Ili kujua kuhusu vitavu vya Sahihayn, angalia makala ya Sahih Bukhari na Sahih Muslim.

Sahihayn (Kiarabu: الصحيحان) inaashiria vitabu viwili vya Sahih Bukhari na Sahihi Muslim ambavyo kwa mujibu wa mtazamo na msimamo wa Waislamu wa Ahlu-Sunna vinahesabiwa kuwa, vitabu vya hadithi vyenye itibari kabisa. Maulamaa wa Ahlu-Sunna wanavitambua vitabu hivi viwili vya hadithi kwamba, ndio vitabu sahihhi zaidi baada ya Qur'an. Vitabu vya Sahihayn viko katika orodha ya vitabu sita vya hadithi vya Waislamu wa Kisuni vinavyojulikana kama Sahih Sittah (Sahihi Sita).

Ndani ya vitabu vya Sahihayn kuna hadithi zinazohusiana na fadhila za Ahlul-Bayt (a.s). Pamoja na hayo yote, Waislamu wa madhehebu ya Shia wanavikosoa vitabu hivyo. Miongoni mwa ukosoaji wao ni hadithi za baadhi ya wapokezi wa hadithi ambao si watu wa kuaminika na wenye uadui na Ahlu-Bayt (a.s), kutozingatiwaa kama inavyostahiki fadhila za Ahlu-Bayt (a.s), kunukuliwa hadithi chache mno katika vitabu hivyo kutoka kwa Ahlul-Bayt na kunukuliwa hadithi ndani ya vitabu hivyo ambazo zinakinzana na kwenda kinyume na akili na dini.

Utambuzi wa istilahi

Sahihayn ni jina la vitabu ambavyo ndani yake mwandishi amenukuu tu hadithi ambazo kwa mtazamo wake zina sanadi na mapokezi sahihi.[1] Istilahi ya Sahihayn inaashiria vitabu viwili vya Sahih Bukhari na Sahihi Muslim. Wanazuoni wa Kisuni wanavitambua vitabu hivi kuwa vitabu vya hadithi vya kuaminika na vyenye itibari sana.[2]Sahihayn viko katika orodha ya vitabu sita vya hadithi vya Waislamu wa Kisuni vinavyojulikana kama Sahih Sittah (Sahihi Sita).[3]

Istilahi ya Sahihayn inatumika pia kwa vitabu ambavyo vimekusanya Sahih Bukhari na Muslim katika kitabu kimoja; kama kitabu cha Jam'u baina al-Sahihayn kilichoandikwa na Farra al-Baghawi.[4]

Sahih Bukhari

Makala kuu: Sahih Bukhari
Kitabu cha Sahih Bukhari

Sahih Bukhari, iliandikwa na Muhammad bin Ismail Bukhari (194-256 Hijiria) ambaye ni mtaalamu mashuhuri wa elimu ya hadithi wa Ahlu-Sunna. Ukiacha wanazuoni wachache, Maulamaa walio wengi wa Kisuni wanakitambua kitabu kuwa, kina itibari kubwa zaiidi miongoni mwa vitabu vya hadithi na ni kitabu sahihi zaidi baada ya Qur'an.[5]

Idadi ya hadithi zilizoko katika kiitabu hjiki Zimetambuliwa kuwa ni baina ya 7000-9200 ingawa sehemu kubwa ya hadithi hizo ni za kukariri.[6] Imenukuliwa kutoka kwa Bukhar kwamba, alichagua na kutea hadithi zake kutoka katika hadithi 600,000 alizokuwa amekusanya.[7]

Sahih Muslim

Makala kuu: Sahih Muslim
Kitabu cha Sahih Muslim

Sahih Muslim imeandikwa na Muslim bin al-Hajjaj al-Naysaburi (204-261 Hijria) msomi na mtaalamu mtajika wa elimu ya hadithi wa Ahlu-Sunna. Maulamaa wa Kisuni wanakihesabu kitabu hiki kuwa na itibari zaidi miongoni mwa vitabu vya hadithi vya Ahlu-Sunna baada ya Sahih Bukhari. Baadhi pia wamesema ya kwamba, itibari yake ni zaidi ya Sahih Bukhari.[8]

Kitabu cha Sahih Muslim kina hadithi za Mtume 7,275 ambapo kwa kufuta hadithi zilizojikariri, idadi yake itakuwa taribani hadithi 4,000.[9]

Ahlul-Bayt katika Sahihayn

Katika vitabu vya Sahih Bukhari na Sahi Muslim (Sahihayn) kuna hadithi zilizonukuliwa kuhusianan na fadhila za Imam Ali (a.s), Bibi Fatma Zahra (a.s), Hassan na Hussein (a.s), Imamu Sajjad (a.s) na Imam Mahdi (a.t.f.s).[10]

Katika Sahih Bukhari zikifutwa hadithi zilizojikariri kutabakia hadithi mbili au tatu tu hivi zinazohusiana na fadhila za Imamu Ali (a.s)[11] na hadithi nne kuhusiananna fadhila za Bibi Fatma (a.s).[12] Hadithi ya Manzila (daraja)[13], Hadith ya al-Raya (bendera), hadithi ya Bidh'a (Fatma ni pande la nyama yangu)[14], na hadithi ya: "Fatma ni kiongozi wa wanawake wa peponi"[15], ni miongoni mwa hadithi ambazo zinatikana katika kitabu cha hadithi cha Waislamu wa Kisuni cha sahih Bukhari.[16] Katika Sahih Muslim pia kuna hadithi tatu zinazozungumzia fadhila za Imamu Ali (a.s) na hadithi tatu kuhusu fadhila za Bibi Fatma Zahra (a.s);[17] miongoni mwazo ni: Hadithi ya Manzila (daraja),[18] hadithi ya al-Raya na hadithi ya: Fatma ni kiongozi wa wanawakke wa peponi".[19]

Ukosoaji wa Mashia kwa Sahihayn

Baadhi ya ukosoaji wa Mashia kuhusiana na vitabu vya Sahihayn (Bukhari na Muslim) ni:

  • Baadhi ya wapokezi wa hadithi za Sahihayn walikuwa watu waongo, wasio wa kuaminika na wapotovu; kama Abu Hurairah, Abu Mussa al-Ash'ari na Amr al-A's. Watu hawa walikuwa na uadui pia na Imamu Ali (a.s) na kwa mujibu wa hadithi za Sahihayn ni kwamba, kuwa na uaduii na Imam Ali (a.s) ni ishara ya kutokuwa na imani, na kutokuwa na imani kunamdondosha mpokezi wa hadithi, hivyo watu hawa hawana itibari.[20]
  • Bukhari na Muslim ambao ni waandishi wa vitabu vya Sahihayn, walikuwa na taasubi (chuki) za kimadhehebu na baadhi ya hadithi ambazo kimsingi Waislamu walifikia mwafaka na makubaliano juu yake na zimenukuliwa pia katika sahihi zingine za Ahlu-Sunna, waandishi hawa hawakuzileta katika vitabu vyao kutokana tu na hadithi hizo kuonyesha ubora wa Imamu Ali (a.s) kwa makhalifa watatu (Abu Bakr, Omar na Othman). Miongoni mwa hadithi hizo ni hadithi ya ghadir, hadithi inayohusiana na Aya ya Utakaso (Tat'hir), hadithi ya sadd al-Abwab na hadithi ya : (انا مدینةُ العلم و علیٌ بابُها ; Mimi ni mji wa elimu na Ali ni mlango wake).[21] Inaelezwa kuwa, Hakim al-Nayshaburi katika kitabu chake cha Mustadrak al-Wasail (ukamilisho wa Sahihi Bukhari na Sahih Muslim) amenukuu takribani hadithi 260 kuhusiana na fadhila za Imamu Ali (a.s) na Ahlul-Bayt (a.s) ambazo zilitimiza masharti ya kuweko katika Sahihayn lakini hazikunukuliwa katika vitabu hivyo viwili.[22]
  • Katika vitabu vya Sahihayn, kumenukuliwa zaidi ya hadithi 2400 ambapo wapokezi wake wengi ima walikuwa na uadui na Ahlul-Bayt (a.s) au hawafahamiki, lakini hakujanukuliwa hadithi kihivyo kuhusiana na Ahllu-Bayt (a.s).[23]
  • Kuna hadithi katika vitabu hivyo viwili vya Sahihayn ambazo haziendani kabisa na akili na dini. Miongoni mwa hadithi hizo ni zile ambazo zinaonyesha kuwa, inawezekana kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho.[24]

Rejea

  1. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Fatḥ al-bārī, juz. 1, uk. 7.
  2. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Fatḥ al-bārī, juz. 1, uk. 8.
  3. Mudīr Shānachī, ʿIlm al-hadīth, uk. 53.
  4. Mudīr Shānachī, ʿIlm al-hadīth, uk. 69.
  5. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Fatḥ al-bārī, juz. 1, uk. 8.
  6. Mudīr Shānachī, ʿIlm al-hadīth, uk. 63-64.
  7. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Fatḥ al-bārī, juz. 1, uk. 7.
  8. Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Fatḥ al-bārī, juz. 1, uk. 8.
  9. Mudīr Shānachī, ʿIlm al-hadīth, uk. 67-68.
  10. Fāḍilī, Fāḍil-i ʾAhl-i Bayt dar Ṣiḥāḥ-i Sitta, uk. 232-251.
  11. Fāḍilī, Faḍāil-i ʾAhl-i Bayt dar Ṣiḥāḥ-i Sitta, uk. 233.
  12. Fāḍilī, Fāḍil-i ʾAhl-i Bayt dar Ṣiḥāḥ-i Sitta, uk. 237
  13. Bukhārī, Ṣaḥīḥ al-Bukhārī, juz. 5, uk. 19, h. 3706.
  14. Bukhārī, Ṣaḥīḥ al-Bukhārī, juz. 5, uk. 29, h. 3767.
  15. Bukhārī, Ṣaḥīḥ al-Bukhārī, juz. 5, uk. 29, h. 3767.
  16. Fāḍilī, Fāḍil-i ʾAhl-i Bayt dar Ṣiḥāḥ-i Sitta, uk. 232-239.
  17. Fāḍilī, Fāḍil-i ʾAhl-i Bayt dar Ṣiḥāḥ-i Sitta, uk. 246-247.
  18. Nayshābūrī, Ṣaḥīḥ Muslim, juz. 4, uk. 1870, h. 2404.
  19. Fāḍilī, Fāḍil-i ʾAhl-i Bayt dar Ṣiḥāḥ-i Sitta, uk. 245-247.
  20. Najmī, Siyrī dar Ṣaḥīḥayn, uk. 99-107.
  21. Najmī, Siyrī dar Ṣaḥīḥayn, uk. 112-113.
  22. Masʿūdī, Al-Mustadrak ʿalā l-Ṣaḥīḥayn
  23. Najmī, Siyrī dar Ṣaḥīḥayn, uk. 118.
  24. Najmī, Siyrī dar Ṣaḥīḥayn, uk. 145-146.

Vyanzo

  • Bukhārī, Muḥammad b. Ismāʿīl al-. Ṣaḥīḥ al-Bukhārī. Edited by Muḥammad Zuhayr b. Nāṣir al-Nāṣir. [n.p]. Dār Ṭawq al-Najāt, 1422 AH.
  • Fāḍilī, ʿAlī. Fāḍil-i ʾAhl-i Bayt dar Ṣiḥāḥ-i Sitta. Qom: Shīʿashināsī, first edition, 1391 SH.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Fatḥ al-bārī bi sharḥ ṣaḥīḥ al-Bukhārī. Beirut: Dār al-kutub al-ʿilmīyya, 2003.
  • Masʿūdī, Jawād. "Al-Mustadrak ʿalā l-Ṣaḥīḥayn". accessed 16 February 2023.
  • Mudīr Shānachī, Kāzim. ʿIlm al-hadīth. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1381 Sh.
  • Muslim Nayshābūrī. Ṣaḥīḥ Muslim. Edited by Muḥammad fuʾād ʿAbd al-Bāqī . Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Kutub al-ʿArabiyya, 1412 AH.
  • Najmī, Muḥammad Ṣādiq. Siyrī dar Ṣaḥīḥayn. Qom: nashr al-mahdī.