Nenda kwa yaliyomo

Rukn Hajar al-Aswad

Kutoka wikishia


Rukn Hajar al-Aswad
Makala hii inahusiana na Rukn Hajar al-Aswad (moja ya engo za Kaaba). Ili kufahamu kuhusiana na Hajar al-Aswad) na kugusa na kubusu angalia Hajar al-Aswad na kugusa na Istilamu Al-Hajar.

Rukn Hajar al-Aswad (Kiarabu: رُكن الحَجَر الأسوَد), Rukh Hajar, Rukn Aswad au Rukn Sharqi (nguzo ya mashariki) ni moja ya engo ya Kaaba ambayo hapo kuna Hajar al-Aswad (jiwe jeusi). Nguzo hii iko upande wa kuelekea mashariki na kisima cha maji ya zamzam na kila tawafu inaanzia na kumalizikia kando yake.

Wakati wa kufanya Twafu (kuzunguka Kaaba), Mtume (s.a.w.w) alikuwa akigusa na kubusu nguzo ya Jiwe Jeusi (Rukn Hajar al-Aswad) na Nguzo ya Yamani (Rukn al-Yamani), na kwa muktadha huo, mafakihi wanasisitiza na kutilia mkazo juu ya kugusa, kubusu na kukumbatia nguzo ya Hajar na kuomba dua kando yake.

Kwa mujibu wa hadithi zinazohusiana na mwisho wa zama, kuuawa nafsi Zakiyyah (kuuawa mtu miongoni mwa masahaba wa Imam Mahdi) ambayo ni moja ya alama na ishara za kudhihiri Imam Mahdi, kutatokea kando ya nguzo hii na baada ya harakati ya Imam Mahdi (a.t.f.s), baadhi ya Mashia watakusanyika katika eneo hilo kutoa bai ana kiapo cha utii kwa Imam Mahdi (a.t.f.s).

Nafasi na Daraja

Rukn Hajar al-Aswad ambayo inajulikana pia kwa jina la Rukn Hajar na Rukn Aswad, ni moja ya engo za nyumba tukufu ya Kaaba.[1] Rukn ina maana ya nguzo na msingi.[2] Kwa kuwa engo nne za ndani ya Kaaba, zinashikilia eneo la juu, basi kila moja kati ya engo za Kaaba inafahamika kwa jina la nguzo.[3] Rukn Hajar al-Aswad takribani ipo upande wa kuelekea mashariki na katika kisima cha maji ya zamzam ambapo hapo kuna Hajar al-Aswad (jiwe jeusi).[4] Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana inafahamika kwa jina la Rukn Hajar al-Aswad (nguzo ya Jiwe Jeusi).[5] Kila tawafu inaanzia na kumalizikia katika nguzo hii.[6]

Fadhila na Adabu Zake

Angalia pia: Hajar al-Aswad

Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Baqir (a.s) ni kuwa, Mtume (s.a.w.w) na Imam Sajjad (a.s) walikuwa wakiigusa Rukn Hajar al-Aswad kisha wakiibusu na kuweka nyuso zao juu yake kwa ajili ya kutabaruku.[7] Kwa mujibu wa hadithi mbalimbali, kumeusiwa na kutiliwa mkazo kufanya amali kama vile kuigusa kwa mkono, kuikumbatia na kuibusu Rukn Hajar al-Aswad[8] na vilevile kumswalia Mtume (s.a.w.w),[9] kuomba dua, kunong'ona na Mwenyezi Mungu na kufanya toba katika nguzo hiyo.[10]

Uhalali wa Kutabaruku

Angalia pia: Kutabaruku

Wanazuoni wa kundii la Kiwahabi licha ya kuamini kwamba, kugusa na kubusu vitu vitakatifu ni shikr,[11] lakini wamekubaliana na suala la kugusa na kubusu Hajar al-Aswad.[12] Kugusa Rukn Hajar ni miongoni mwa mambo yaliyotumiwa kuhalalisha kutabaruku na kubusu vitu na maeneo matakatifu.[13]

Yatakayotokea Kando yake Wakati wa Kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s)

Katika vitabu na vyanzo vya hadithi kumenukuliwa matukio yatakayotokea kando ya Rukn Hajar al-Aswad wakati wa kudhihiri Imam Mahdi (a.t.f.s).

Kadhalika angalia: Kuuawa Nafs al-Zakiyyah

  • Baadhi ya Mashia watakusanyika katika eneo hilo kutoa baia na kiapo cha utii kwa Imam Mahdi (a.t.f.s): Kwa mujibu wa hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s)[15] na Imamu Muhammad Baqir (a.s)[16] ni kuwa, Imam Mahdi atasimama siku ya Ashura baina ya rukn na maqam na wafuasi wake kutoka maeneo mbalimbali ya dunia watakusanyika hapo na kumpa baia na kiapo cha utii.
Kadhalika angalia: Kudhihiri Imam wa zama.

Rejea

  1. Shāhrūdī, Farhang-i fiqh, juz. 1, uk. 359-360.
  2. Muṣṭafawī, al-Tahqīq, juz. 4, uk. 234.
  3. Ṣādiqī Ardistānī, Ḥajj az mīqāt tā miʿād, uk. 104.
  4. Mishkinī, Muṣṭalaḥāt al-fiqh, uk. 275.
  5. Furqānī, sarzamīn-i yād-hā wa nishān-hā, uk. 59.
  6. Mishkinī, Muṣṭalaḥāt al-fiqh, uk. 275.
  7. Kulaynī, al-Kāfī, juz. 4, uk. 408
  8. Shāhrūdī, Farhang-i fiqh, juz. 1, uk. 359
  9. Kulaynī, al-Kāfī, juz. 4, uk. 408
  10. al-Fiqh al-mansūb ilā l-Imām al-Riḍhā (a.s); al-mushtahir bi-fiqh al-Riḍhā (a.s), uk. 231
  11. Ibn Taymīyya, al-radd ʿalā l-Akhnāʾī qāḍī l-Mālikīyya, juz. 1, uk. 124
  12. Ibn Qayyim al-Jawziyya, Ighāthat al-lahfān, juz. 1, uk. 194.
  13. ʿAynī, ʿUmdat al-qarī, juz. 9, uk. 241
  14. Ṣadūq, Kamāl al-dīn, juz. 1, uk. 331.
  15. Mufīd, al-Irshād, juz. 2, uk. 379
  16. Ṭūsī, al-Ghayba, uk. 453.

Vyanzo

  • Al-Fiqh al-mansūb ilā l-Imām al-Riḍā (a); al-mushtahir bi-fiqh al-Riḍā (a.s), Mashhad: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1406 AH.
  • ʿAynī, Maḥmūd b. Aḥmad, ʿUmdat al-qarī; Sharḥ ṣaḥīḥ al-Bukhārī, Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth, [n.d].
  • Furqānī, Muḥammad. Sarzamīn-i yād-hā wa nishān-hā, Tehran: Mashʿar, 1379 Sh.
  • Ibn Qayyim al-Jawziyya, Muḥammad ibn Abī Bakr. Ighāthat al-lahfān min maṣāyid al-Shayṭān, Riyadh: Maktabat al-ʿĀrif, [n.d].
  • Ibn Taymīyya, Aḥmad b. ʿAbd al-Ḥalīm. Al-Radd ʿalā l-Akhnāʾī qāḍī l-Mālikīyya. Beirut: Al-Maktabat al-ʿAsrīyya, 1423 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-, Al-Kāfī, Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1407 AH.
  • Mishkinī, ʿAlī, Muṣṭalaḥāt al-fiqh, Qom: Nashr al-Hadī, 1377 Sh.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Muṣṭafawī, Ḥassan, Al-Tahqīq fī kalimāt al-Qur'ān al-karīm, Tehran: Bungāh Tarjuma wa Nashr-i Kitāb, 1360 SH.
  • Shāhrūdī, Sayyid Maḥmūd, Farhang-i fiqh muṭābiq bā madhhab-i Ahl al-Bayt, Qom: Muʾassisat Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh al-Islāmī, 1382 Sh.
  • Ṣādiqī Ardistānī, Aḥmad, Ḥajj az mīqāt tā miʿād, Tehran: Mashʿar, 1385 Sh.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAli al-. Kamāl al-dīn wa tamām al-niʿma. Second Edition. Tehran: Islāmīyya, 1395 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥassan al-. Al-Ghayba, Edited by ʿIbād Allāh Tihrānī and ʿAlī Aḥmad Nāṣiḥ, Qom: Muʾassisat al-Maʿārif al-Islāmiyya, 1411 AH.