Nushuzu
Nushuzu (Kiarabu: النشوز) ni neno la Kiarabu lililotumiwa na Qur'ani, ambalo humaanisha uasi wa mwanamke wa kuto tekeleza majukumu ya kisheria kwa ajili ya mumewe. Kulingana na fat'wa za wanachuoni, kuto rahisisha au kuto toa wasaa kwa mwanamke mbele ya mumewe katika kujibu mahitajio ya tendo la ndoa kwa mumuwe, huhisabiwa kuwa ni miongoni mwa ukiukaji wa haki za mume huyo, tendo ambalo kifiqhi hujulikana kwa jina la nushuzu. Kwa upande wa wanaume; Kuto toa huduma za maisha katika kuihudumia familia yake, ni moja ya alaza za nushuzu kwa mwanamme huyo.
Katika hali ya mwanamke kumuasi mumuwe, mume hatakuwa na wajibu wa kutoa huduma kwa mwanamke huyo. Kulingana na maoni ya wanazuoni, iwapo mke atafanya nushuzu, mume atapaswa kwanza kumnasihi mkewe, na ikiwa nasaha zake hazitakuwa na faida, atapaswa kumtenga kitandani, na ikiwa jambo pia halitakuwa na athari, hatua ya mwisho kabisa itakuwa ni kumpiga. Iwapo uasi utatokea upande wa mwanamume, mwanamke atapaswa kwanza kumshauri mumewe na kudai haki zake kutoka kwake, na ikiwa jambo hilo halitakuwa na athari, atapaswa kurejea kwa hakimu wa kidini, ili kupata suluhu na muwafaka juu ya matatizo yao.
Ufafanuzi wa Kisheria na Nafasi Nushuzu katika Sheria za Fiqhi
Nushuzu (نشوز) ni istilahi ya kisheria linalomaanisha kule mume au mke kuyakimbia majukumu ya kisheria mbele ya mwenzi wake. [1] Mwanamke kuto mkutii mumewe, na mwanamume [2] na mwamme kuto toa huduma za maisha kwa mmkewe, ni miongoni mwa mifano ya nusuzu. [3]
Mwanamke anayekataa kutekeleza majukumu ya kindoa kwa mumewe huitwa naashizah (ناشزة), na mwanamume anayekataa au kiuka katika kutimiza majukumu ya kindoa kwa mkewe huitwa nashazu (ناشز). [4]
Vitabu vya fiqhi vimeyajadili masuala yanayo husiana na nusuzu na hukumu zake katika mlango wa masuala ya ndoa. [5] Hata hivyo, vitabu vya sheria za kifiqhi vimejadili zaidi kuhusu hukumu za nusuzu za upande wa wanawake. [6]
Ishara na Dalili za Nushuzu za Wanawake
Baadhi ya mambo ambayo wanazuoni wameyahisabu kuwa ni ishara za nusuzu za wanawake dhidi ya waume zao ni kama ifuatavyo:
- Kutosahilisha tendo la ndoa; Yaani kutotimiza matakwa halali ya kindoa kwa mumewe zao. [7]
- Kuonyesha kutopendezwa na mumewe na kumkabili kwa sura ya kuchuki mbele yake. [8]
- Kutokuzingatia usafi na mapambo ya muonekeno wake, hadi kufikia hatua ya kuondoa raghaba ya mwanamme katika kumtamani mkewe. [9]
- Kutoka nje ya nyumba bila ya ruhusa ya mumewe. [10]
Ishara za nusuzu kwa upande wa waume
Wanazuoni wametaja mambo yafuatayo kama ishara za nushuzu kwa waume:
- Kuto toa huduma za maisha. [11]
- Kupiga na kuwanyanyasa wake bila sababu. [12]
- Kutokuzingatia zamu (katika kugawanya masiku baina ya wake zake), ikiwa mwanamume ana mke zaidi ya mmoja. [13]
Majukumu ya Mwanamke na Mwanamme katika Kukabiliana na Nushuzu Baina yao
Kwa mujibu wa Fat’wa za wanazuoni, ikiwa mwanamke ni ناشزة (mvunja sharia za kindoa) hatua ya kwanza kwa mumewe ni kumpa ushauri wa nasaha, na ikiwa haikusaidia, ampe mgongo kitandani (yaani asilale naye) na ikiwa bado hakukupatikana faida, hatua ya mwinsho ni kumpa adhabu ya kimwili (kumpiga). [14] Ikiwa suala la nusuzu ni kutoka upande wa mume, mwanamke hutakiwa kumnasihi mumewe na kudai haki zake kutoka kwake, na ikiwa haikusaidia, aende kwa hakimu wa kisheria (kadhi). [15]
Hukumu za Ziada Juu ya Nushuzu
Hukmu nyengine zinazohusiana na nushuzu ni kama ifuatavyo:
- Ikiwa mwanamke ni mkiukaji wa haki za kindoa (ناشزة), mumewe atakuwa hana wajibu wa kumpa huduma za kimaisha mwanamke huyo. [16]
- Ikiwa mwanamume atakuwa mkiukaji wa haki za kindoa (ناشز), mwanamke hatakuwa na haki ya kuacha majukumu yake ya ndoa kwa mumewe[17] au kumpa adhabu ya kimwili (kipigo). [18]
- Adhabu ya kimwili kwa mwanamke haipaswi kuwa nzito na kusababisha kuvunjika, kupata majeraha na mitisiko ya mwili. [19]
- Kwa upande wa mwanamke, suala la kukataa kufanya kazi ambazo si lazima kwake, kama vile kupika, kushona na kusafisha na nyumba, si kati ya ishara za nusHuzu ya mwanamke huyo. [20]
- Kutoka kwa mwanamke nje ya nyumba bila idhini ya mumewe, ili kupata mafunzo ya imani na sheria za kifiqhi kwa kiwango kinachohitajika, [21] au kwa ajili ya matibabu katika hali ambayo matibabu hayawezekani kupatikana nyumbani kwake [22] au kukimbia kutokana na hatari kwa ajili ya kusalimisha mwili pamoja na roho yake, mali na kwa nia ya kulinda heshima yake, si miongoni mwa mambo yanayo husiana na nusuzu. [23]