Muujiza wa hisabati katika Qur’an
Muujiza wa hisabati katika Qur'an (Kiarabu: الإعجاز العددي للقرآن) au muujiza wa namba ndani ya Qur’an, ni nadharia ambayo inabainisha nidhamu na mpangilio wa Kimuujiza wa Qur’an. Kwa mujibu wa nadharia hii, idadi ya herufi na maneno ya Qur’an yana mpangilio wenye umakini wa hali ya juu na wenye umakini na kutokana na kuwa, hakuna mwandishi anayeweza kuwa na nidhamu na mpangilio kama huu katika kuandika kitabu, mpangilio huu ni ishara ya muujiza wake. Kwa mara ya kwanza nadharia hii ambayo ina wapinzani wengi ilizungumziwa na Rashad Khalifa, mtaalamu wa Qur’an wa Kimisri. Akthari ya wapinzani wanaokosoa nadharia hii wanasema kuwa, takwimu zinazotolewa sio sahihi na kwa uoni wao zina mapungufu mengi.
Kutambulisha nadharia yenyewe
Kulingana na nadharia ya muujiza wa kihisabati au kihesabu wa Qur’an, idadi ya herufi na maneno ya Qur’an yana mpangilio wenye umahiri wa hali ya juu na wenye umakini na kutokana na kuwa, hakuna mwandishi anayeweza kuwa na nidhamu na mpangilio kama huu katika kuandika kitabu, mpangilio huo ni ishara ya muujiza. [1] Nadharia hii inaitambua namba 19 kuwa ufunguo wa siri wa muujiza wa Qur’an. [2]
Kwa mujibu wa nadharia hii, ibara ya : بسم الله الرحمن الرحیم ina herufi 19 na jumla ya maneno yake yaliyokaririwa katika Qur’an ni namba na idadi ambayo imepatikana baada ya kuzidishwa namba 19 mara kadhaa yaani ni zidisho la namba 19 au ni namba ambayo ukiigawa mara 19 utapata namba ambayo ina 19 kadhaa. Bismillah imekaririwa mara 19, Allah mara 2698, Rahman mara 57 na Rahim mara 114 ambazo namba zote hizo ni zidisho la 19. Kadhalika idadi ya herufi za sura zote za Qur’an ni zidisho la 19.
Historia fupi ya nadharia hii na aliyeileta
Kwa mujibu wa baadhi ya wahakiki na watafiti, kwa mara ya kwanza nadharia ya muujiza wa hisabati wa Qur’an iliashiriwa katika kitabu cha al-Itiqan cha Jalal al-Din Suyuti (849-911 Hijiria) mmoja wa Maulamaa wa Kisuni; [4] hata hivyo nadharia hii kwa uwazi wake kwa mara ya kwanza ililetwa na kuzungumziwa na Rashad Khalifa, mtafiti wea masuala ya Qur’an wa Kimisri. Alifanya utafiti katika uga wa utafiti wa Kiqur’an katika kipindi cha miaka mitatu akitumia compyuta ambapo mwaka 1972 alitangaza mbele ya vyombo vya habari natija na matokeo ya utafiti wake. Mwaka 1983 pia kitabu chake kilichojulikana kwa jina la Mu’jizat al-Qur’an al-Karim kilichaopishwa Beirut na Marekani. [5] Rashad Khalifa alidai kwamba, hata amefanikiwa kujua siku ya kutokea Siku ya Kiyama kupitia kuhesabu idadi na namba zilizoko katika Qur’an. [6]
Baada ya Rashad Khalifa, alikuja Abdul-Razaq Naufal, msomi na mtafiti mwingine wa Kimisri wa masuala ya Qur’an ambaye aliendeleza njia ya Rashad Khalifa na akazungumzia nukta na mambo mengine ya muujiza wa hisabati na namba katika Qur’an; kama vile maneno ambayo yapo kinyume na yanayokinzana kama vile uhai na kifo kadhalika dunia na akhera yametumika katika Qur’an kwa idadi sawa. Baada yake alikuja Abu Zahra al-najdi, mtafiti wa Qur’an wa Kishia ambaye alisema kuwa, katika Qur’an neno (الساعة) limetumika mara 24 katika Qu’ran idadi ambayo ni ya masaa 24 ya siku yaani mchana na usiku. Kadhalika alisema kuwa, neno Shia limetuka mara 12 katika Qur’an idadi ambayo ni sawa na idadi ya Maimamu 12 wa Mashia. [7]
Hii leo nadharia ya muujiza wa kihisabati na kiidadi wa Qur’an iunazingatiwa sana na watafiti wa masuala ya Qur’an. [8]
Mifano ya muujiza wa kihisabati wa Qur’an
Baadhi ya takwimu ambazo zimetolewa na wafuasi wa nadharia hii ni kama ifuatavyo:
- Katika Qur’an herufi za mkato (Huruf al-Muqatta’ah) za kila sura zimerudiwa zaidi ya herufi zingine.
- Herufi za mkato za kila surah zimerudiwa zaidi katika surah hiyo kuliko katika surah zingine.
- Idadi ya herufi za mkato katika sura zote zenye herufi za mkato ni zidisho la namba 19.
- Maneno mawili ya “dunia” na “akhera” yamekuja na kukaririwa katika Qur’an kwa idadi sawa.
- Neno al-Sa’ah (الساعة) limekaririwa kwa idadi ya masaa ya siku moja yaani masaa 24 ambayo ya nundwa kwa usiku na mchana.
- Neno “uhai” na “kifo” pamoja na maneno yanayotokana nayo yametumika kwa idadi ambayo ni sawa na idadi ya neno “kifo”.
- Neno Shahar “mwezi’ limetumika mara 12 ambayo ni idadi ya miezi katika mwaka.
- Ibara ya (السموات السبع) imetumika mara 7 katika Qur’an.
- Neno “sijdah” limetumika mara 34 katika Qur’an idadi ambayo ni sawa na sijida anazosujudu mtu katika Sala za wajibu kila siku. [9]
Ukosoaji
Nadharia ya muujiza wa namba na kihisabati katika Qur’an imekabiliwa na upinzani mkubwa. [10] wakosoaji wa nadhari hii wanaamini kwamba, Mwenyezi Mungu hakuishusha Qur’an kwa namna ya kimafumbo na kuwa nje ya ufahamu wa watu. Kitabu hiki ni kwa ajili ya uongofu kwa watu na maneno haya hayana uhusiano na suala la hidaya na uongofu.
Kwa kuongezea ni kuwa, wakosoaji wamezingatia takwimu nyingi zinazowasilishwa na watetezi wa nadharia hii kuwa sio sahihi [12] na wamegundua mapungufu mengi. Baadhi yao ni:
- Idadi ya herufi za mkato katika Surat Yasin yaani herufi mbili za Yaa na siin, ndiko kukaririwa kuchache zaidi; kwa maana kwamba, Sureat Yassin ndio yenye idadi ndogo ya kukaririwa herufi za mkato; hii ni katika hali ambayo, kwa mujibu wa nadhari hii, idadi ya herufi za mkato katika kila sura ni zaidi ya herufi zingine.
- Idadi ya kukaririwa herufi Qaaf (ق), herufi ya mkato katika Surat Qaaf, idadi yake ni nyingi katika surat Shams, Kiyana na Falaq kuliko idadi yake katika Surat Qaaf.
- Madai kwamba, idadi ya kutumiwa maneno ya Bismillah Rahmar Rahim katika Qur’an ni zisho la namba 19, si kweli na madai hayo yanathibiti tu katika neno Rahman.
- Idadi ya herufi katika Surat al-Nas sio zidisho la namba 19.
- Idadi ya herufi za mkato katika Surat al-Qalam na Tah sio zidisho la namba 19. [13]
Bibliografia
Makala ya Kitabshinasi-yi i'jaz-i 'adadi wa riyadi-yi Qur'an ni bibliografia ambayo imebainisha kwa mapana na marefu kuhusiana na muujiza wa kihisabati wa Quran. Makala hii imetambulisha vitabu 118, makala 36 na mitandao 6 ya Intaneti kuhusiana na maudhui hii. Baadhi ya vitabu hivyo vilivyoarifishwa ni:
- Mu’jizat al-Qur’an al-Karim: Rashad Khalifa
- Mu’jizat al-Arqam Wal-Taraqim Fil Qur’an al-Karim; Abdul-Razaq Naufal
- Minal I’jaz al-Balaghi wal-Adadi Lil-Qur’an al-Karim; Dokta Abu Zahra al-Najdi
- I’jaz Qur’an; Sayyid Ridha Muaddab. [14]