Nenda kwa yaliyomo

Musabbihat

Kutoka wikishia

Musabbihati (Kiarabu: المُسَبِّحات) Ni Sura za Qur'ani zinazianza na kumsabihi Mwenyezi Mungu. Kuna idadi ya Sura saba zinazoanza na mojawapo ya mizizi ya neno "Sabbaha" nazo ni; Surat Israa, Hadiid, Hashr, Saf, Jumu'a, Taghabun na A'ala. Hata hivyo, kuna tofauti ya maoni kuhusu ikiwa Musabbihat inajumuisha Sura hizi zote.

Kuzungumzia misingi ya dini ni mojawapo ya mada za pamoja au mada shirikisho za Sura hizi. Sura ya Israa inahisabiwa kuwa ndiyo mhimili wa Musabbihat na kushuka kwa Sura hizi kulikuwa ni kwa muda wote wa maisha ya utume wa Mtume wa Muhammda (s.a.w.w) huko Makkah na Madina.

Kwa mujibu wa moja ya Hadithi, ni kwamba; Bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa akisoma Sura hizi za Musabbihat kila usiku kabla ya kulala na alisema kuwa: "Katika Musabbihat kuna Aya moja ambayo ni bora kuliko Aya elfu moja.

Majina

Musabbihati ni jina la Sura za Qur’ani zinazo anza na kumsabihi Mwenye Ezi Mungu. [1] Kufanya tashbihi inamaanisha kumtakasa [2] na kumsabihi Mwenyezi Mungu (kumdhukuru au kutaja majina ya Alla) kwa kumtakasa na aina yoyote ile ya mapungufu. [3]

Mifano Hai

Katika Hadithi, hakukutajwa majina ya Sura za Musabbihati; hivyo kuna mitazamo tofauti kuhusiana na idadi ya Sura hizi. Mitazamo juu ya idadi ya Sura hizi ni kama ifuatavyo:

  1. Sura tano: Hadid, Hashr, Saf, Jumu'a, na Taghabun ambazo zinaanza na سَبَّحَ (Sabbaha) au یسَبِّحُ (Yusabbihu) . [4]
  2. Sura sita: Hadid, Hashr, Saf, Jumu'a, Taghabun, na A'ala. [5] Kwa sababu katika sura hizi, baada ya Bismillah, ndani yake kuna moja ya vitenzi vinavyotokana na neno "Sabbaha", ambavyo ni; "Yusabbihu", au "Sabbih". Sayyid Ali Qadhi Tabatabai aliwashauri wanafunzi wake kusoma Sura hizi sita kila usiku akizitambua kama ni Musabbihati. [6]
  3. Sura saba: Israa, Hadid, Hashr, Saf, Jumu'a, Taghabun, na A'ala. [7] Sura ambazo zinaanza na mojawapo ya mizizi ya neno (Sabbaha) س ب ح. [8]
  4. Sura tisa: Muhammad Hadi Ma'rifat, (aliye ishi kati ya mwaka 1309 na 1385 Shamsia) ambaye ni mtafiti wa Sayansi za Qur’ani, aliongeza Sura za Furqani na Mulk, ambazo zinaanza na "Tabaraka", kwenye sura saba zilizotajwa. [9]

Sifa

Sura za MusabbihatI zina sifa shirikisho na maudhui za pamoja ambazo ni kama ifuatavyo:

  • Kujumuisha Kanuni za Dini: Maudhui ya sura za Musabbihat ni Tawhidi, Utume, Ufufuo, Uadilifu, na Uimamu. [10]
  • Nafasi ya Mhimili ya Surat al-Israa: Baadhi wanaamini kuwa kuna uhusiano maalum kati ya maudhui ya Musabbihati na Suratu al-Israa, na kwamba Sura hii ni mhimili wa Sura nyingine za Musabbihati. Kulingana na mtazamo huu, Musabbihat ni kama kitabu ambacho utangulizi wake ni Suratu al-Israa, milango yake ni Sura tano nyingine, na hitimisho lake ni Suratu al-A'ala. [11]
  • Kushuka Katika Kipindi Chote Endelevu cha Ufunuo: Katika kushuka na kuteremka kwake, Sura hizi zimefunika na kutanda kwenye kipindi chote cha utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.w); Sura ya A'la ni Sura ya 87 kushuka mjini Makka, Israa ni Sura ya hamsini kushuka Makka, na Sura za Hadid, Hashr, Saf, Jumu'a, na Taghabun zilishuka Madina nazo kimpangilio katika Quran ni kuanzia Sura ya tisini na nne hadi ya mia moja na kumi zilizoteremshwa kwa bwana Mtume (s.a.w.w). [12]

Thamani Yake

  • Aya Moja ni Bora Kuliko Aya Elfu: Kwa mujibu wa moja ya Hadithi, ni kwamba bwana Mtume (s.a.w.w) alikuwa akisoma Sura za Musabbihati kila usiku kabla ya kulala na akasema kwamba: "Katika Musabbihati kuna Aya moja ambayo ni bora kuliko Aya elfu moja. [13]
  • Kumuona Imam wa Zama (Imamu Mahdi (a.f)): Katika moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Muhammad Baqir (a.s), imesimuliwa kwamba; "Yeyote atakayesoma Musabbihati kabla ya kulala kwake, yeye hatakufa mpaka aonane na Imamu Mahdi (a.f) na akifa, atakuwa pamoja na Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w). [14]

Rejea

Vyanzo