Mkopo:Dua ya arubaini na tisa ya Sahifa Sajjadiya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Ahmad Nayrizi, iliyoandikwa mnamo 1145 AH. | |
| Mada | Dua iliyokuwa ikitumiwa na Imam Sajjad (a.s), wakati wa kumuombwa Mola wake hifadhi dhidi ya ujanja na njama za maadui zake. |
|---|---|
| Ina Mapokezi au Haina Mapokezi | Ina Mapokezi |
| Imenukuliwa Kutoka kwa | Imamu Sajjad (a.s) |
| Mpokezi | Mutawakkil ibn Harun |
| Vyanzo vya Kishia | Sahifa Sajjadiyah |
| Dua ya Tawassuli • Dua ya Kumaili • Dua ya Nudba • Dua ya Samati • Dua ya Faraji • Dua ya Abu Hamza Thumali • Ziara ya Ashura • Ziara ya Jamiat Kabira • Ziara ya Warith • Ziara ya Aminu-Llah • Ziara ya Arobaini | |
Dua ya Arubaini na Tisa ya Sahifa Sajjadiya (Kiarabu: الدعاء التاسع والأربعون من الصحيفة السجادية) ni miongoni mwa dua alizoripotiwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Kulingana na nukuu zilizowasilisha dua hii ni kwamba; Imamu Sajjad (a.s) alikuwa akiisoma kwa ajili ya kujikinga dhidi ya shari na njama za maadui zake. Ndani ya dua hii, Mwenye Ezi Mungu, Subhanahu wa Ta'ala, anatajwa kuwa ndiye hifadhi na kimbilio la kweli kwa mja dhidi ya maadui mbali mbali akiwemo Shetani aliyelaaniwa na Mwenye Ezi Mungu. Kadhalika katika dua hii, Imam Sajjad (a.s) anaweka wazi ya kwamba; Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kuyaepusha na kuyaondoa masaibu pamoja na mabalaa yote yanayomkabili mja Wake.
Kuna tafsiri mbali mbali zilizoandikwa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa dua ya arubaini na tisa smabamba na dua nyengine zilizomo ndani ya Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa waandishi walioandika vitabu vya tafsiri ya dua za Sahifa Sajjadiyya lugha ya Kiajemi, ni bwana Hassan Mamdouhi Kermanshahi, mwandishi wa kitabu kiitwacho Shuhud wa Shenakht. Ama kwa upande wa lugha ya Kiarabu, kitabu mashuri kilichotoa tafsiri ya dua ya arubaini na tisa, sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya, ni kile kitabu kiitwacho Riadhu as-Salikin kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani.
Mafunzo Yaliomo Ndani ya Dua ya Arubaini na Tisa
Dua ya arubaini na tisa ni miongoni mwa dua tukufu za kitabu cha Sahifa Sajjadiya, nayo ni ile dua iliyokuwa ikitumiwa na Imam Sajjad (a.s), wakati wa kumuombwa Mola wake hifadhi dhidi ya ujanja na njama za maadui zake.[1]
Miongoni mwa hekima na mafunzo yaliyomo ndani ya dua hii adhimu ni kama ifuatavyo:
- Shukrani na sifa kwa Mwenye Ezi Mungu kutokana na sifa yake ya kusitiri mapungufu na kusamehe ukengeufu wa waja Wake.
- Dhambi ni mlango wa kuingia kwenye upotevu na niyo mwelekeo wa kuelekea ndani ya mabonde ya angamizi.
- Mwenye Ezi Mungu ndiye hifadhi halisi kwa mwanadamu.
- Uokovu wa kutoka na adhabu ya Mwenye Ezi Mungu hupatikana kupitia imani ya kuamini Mungu mmoja.
- Kujiepusha na adhabu ya Mungu na kutafuta hifadhi kupitia rehema Zake.
- Neema ya kipekee ya Mwenyezi Mungu katika kuwatizama waja wake wema kwa jicho la rehema.
- Kung'oa mizizi ya kukata tamaa na kuvunjika moyo chini ya nuru ya mafundisho ya Uislamu.
- Mwenye Ezi Mungu pekee ndiye muepushaji wa matukio hatarishi.
- Kutafuta hifadhi ya Mwenye Ezi Mungu dhidi ya uovu wa maadui walioinua mikono yao kwa ajili ya hujuma.
- Ujuzi wa Mwenye Ezi Mungu kuhusiana na uadui wa maadui fulani.
- Uokovu wa kuokoka na shari ya maadui na vitimbi vyao chini ya kivuli cha rehema za Mwenye Ezi Mungu.
- Msaada wa Mwenye Ezi Mungu kwa waja Wake waumini kabla ya hata wao kuomba kitu fulani kutoka kwa Mola wao.
- Kutafuta hifadhi kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu kutokana na unafiki na kujipendekeza kunakofanya na baadhi wanafiki katika kutafua urafiki na maadui wa Uislamu.
- Maadui wa Uislamu kunaswa na mitego yao wenyewe walioitayarisha dhidi ya Waislamu.
- Mahasidi kukumbwa na huzuni pamoja na simanzi, zinazo sababishwa na uadui wao dhidi ya waumini.
- Kutafuta ya hifadhi ya rehema za Mwenye Ezi Mungu, ndiyo ngao imara ya kupata amani dhidi ya hofu na dhuluma za wengine.
- Dhana njema kwa Mwenye Ezi Mungu na fidia ya kuondolewa kwa umaskini na uhitaji kutokana na dhana njema hiyo.
- Kukiri mapungufu katika utekelezaji wa majukumu ya utumishi, licha ya kuwepo wingi wa baraka tele za Mwenye Ezi Mungu.
- Uasi wa waja licha ya kuwepo kwa wingi wa vipawa na fadhila kadhaa zitokazo kwa Mola wao.
- Kumshukuru Mwenye Ezi Mungu kwa kutowaharakishia waja Wake adhabu Zake kutokana na uasi wao.
- Kukiri makosa ni miongoni mwa mifano ya adabu katika kutumikia utumishi wa Mwenye Ezi Mungu.
- Kujitambua ndio chanzo msingi cha wokovu dhidi ya maangamizi.
- Kukata tamaa ndiyo chanzo halisi cha kutumbukia kwenye bonde la tabia zisizofaa.
- Ulazima na umuhimu wa kumtambua adui.
- Kukiri wingi wa neema na upungufu wa kushukuru zetu mbele ya Mwenye Ezi Mungu.
- Kujikurubisha kwa Mwenye Ezi Mungu na kutafuta hifadhi dhidi ya uovu wa maadui, kupitia mwanga wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), pamoja na mamlaka ya Ali (a.s).
- Kuomba njia ya kufikia radhi za Mwenye Ezi Mungu chini ya kivuli cha rehema na taufiki ya Mwenye Ezi Mungu.[2]
Tafsiri Chambuzi za Dua ya Arubaini na Tisa
Kuna waandishi mbali mbali waliotumia muda wao kwa ajili ya kufasiri dua ya Dua ya arubaini na tisa, sambamba na dua nyengine zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiya. Miongo mwa vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiajemi kwa ajili ya kutoa tafiri chambuzi ya dua hiyo, pamoja na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya, ni pamoja na; kitabu kiitwacho Shuhud wa Shinakht, cha bwana Muhammad Hassan Mamduhi Kermanshahi[3] na Sharh wa Tarjomeye Sahifeh Sajjadiyeh, kilichoandikwa na bwana Sayyid Ahmad Fahri.[4]
Tukija kwenye upande wa lugha ya Kiarabu, pia tutakukana vitabu kadhaa vilivyofanya kazi ya kutoa tafsiri chambuzi ya Dua ya arubaini na tisa, sambamba na dua zilizosalia ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiya. Miongoni mwa kazi maridadi zilizoandikwa kwa lugha ya Kiarabu ni pamoja na; kitabu kiitwacho Riadhu al-Salikin cha Sayyid Ali Khan Madani,[5] Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyya cha Muhammad Jawad Mughniyya,[6] Riadhu al-Arifin cha Muhammad bin Muhammad Darabi,[7] na Afaqu al-Ruh kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[8] Kadhalika kuna vitabu maalumu vilivyoandikwa kwa ajili ya ya kufasiri msamiati na maneno ya dua hii sambamba na dua nyengine za Sahisa Sajjadiyya. Vitabu viwili maarufu vilivyo andikwa kuhusiana na kazi hii ya kilugha ni: Ta'liqat ala al-Sahifati al-Sajjadiyya cha Faidhu Kashani,[9] na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya kilichoandikwa na Izz al-Din al-Jaza'iri.[10]
Matini ya Dua ya Arubaini na Tisa Pamoja na Maelezoi Yake kwa Kiswahili
وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي دِفَاعِ كَيْدِ الْأَعْدَاءِ، وَ رَدِّ بَأْسِهِمْ
إِلَهِي هَدَيْتَنِي فَلَهَوْتُ، وَ وَعَظْتَ فَقَسَوْتُ، وَ أَبْلَيْتَ الْجَمِيلَ فَعَصَيْتُ، ثُمَّ عَرَفْتُ مَا أَصْدَرْتَ إِذْ عَرَّفْتَنِيهِ، فَاسْتَغْفَرْتُ فَأَقَلْتَ، فَعُدْتُ فَسَتَرْتَ، فَلَكَ- إِلَهِي- الْحَمْدُ.
تَقَحَّمْتُ أَوْدِيَةَ الْهَلَاكِ، وَ حَلَلْتُ شِعَابَ تَلَفٍ، تَعَرَّضْتُ فِيهَا لِسَطَوَاتِكَ وَ بِحُلُولِهَا عُقُوبَاتِكَ.
وَ وَسِيلَتِي إِلَيْكَ التَّوْحِيدُ، وَ ذَرِيعَتِي أَنِّي لَمْ أُشْرِكْ بِكَ شَيْئاً، وَ لَمْ أَتَّخِذْ مَعَكَ إِلَهاً، وَ قَدْ فَرَرْتُ إِلَيْكَ بِنَفْسِي، وَ إِلَيْكَ مَفَرُّ الْمُسيءِ، وَ مَفْزَعُ الْمُضَيِّعِ لِحَظِّ نَفْسِهِ الْمُلْتَجِئِ.
فَكَمْ مِنْ عَدُوٍّ انْتَضَى عَلَيَّ سَيْفَ عَدَاوَتِهِ، وَ شَحَذَ لِي ظُبَةَ مُدْيَتِهِ، وَ أَرْهَفَ لِي شَبَا حَدِّهِ، وَ دَافَ لِي قَوَاتِلَ سُمُومِهِ، وَ سَدَّدَ نَحْوِي صَوَائِبَ سِهَامِهِ، وَ لَمْ تَنَمْ عَنِّي عَيْنُ حِرَاسَتِهِ، وَ أَضْمَرَ أَنْ يَسُومَنِي الْمَكْرُوهَ، وَ يُجَرِّعَنِي زُعَاقَ مَرَارَتِهِ.
فَنَظَرْتَ- يَا إِلَهِي- إِلَى ضَعْفِي عَنِ احْتِمَالِ الْفَوَادِحِ، وَ عَجْزِي عَنِ الِانْتِصَارِ مِمَّنْ قَصَدَنِي بِمُحَارَبَتِهِ، وَ وَحْدَتِي فِي كَثِيرِ عَدَدِ مَنْ نَاوَانِي، وَ أَرْصَدَ لِي بِالْبَلَاءِ فِيمَا لَمْ أُعْمِلْ فِيهِ فِكْرِي.
فَابْتَدَأْتَنِي بِنَصْرِكَ، وَ شَدَدْتَ أَزْرِي بِقُوَّتِكَ، ثُمَّ فَلَلْتَ لِي حَدَّهُ، وَ صَيَّرْتَهُ مِنْ بَعْدِ جَمْعٍ عَدِيدٍ وَحْدَهُ، وَ أَعْلَيْتَ كَعْبِي عَلَيْهِ، وَ جَعَلْتَ مَا سَدَّدَهُ مَرْدُوداً عَلَيْهِ، فَرَدَدْتَهُ لَمْ يَشْفِ غَيْظَهُ، وَ لَمْ يَسْكُنْ غَلِيلُهُ، قَدْ عَضَّ عَلَى شَوَاهُ وَ أَدْبَرَ مُوَلِّياً قَدْ أَخْلَفَتْ سَرَايَاهُ.
وَ كَمْ مِنْ بَاغٍ بَغَانِي بِمَكَايِدِهِ، وَ نَصَبَ لِي شَرَكَ مَصَايِدِهِ، وَ وَكَّلَ بِي تَفَقُّدَ رِعَايَتِهِ، وَ أَضْبَأَ إِلَيَّ إِضْبَاءَ السَّبُعِ لِطَرِيدَتِهِ انْتِظَاراً لِانْتِهَازِ الْفُرْصَةِ لِفَرِيسَتِهِ، وَ هُوَ يُظْهِرُ لِي بَشَاشَةَ الْمَلَقِ، وَ يَنْظُرُنِي عَلَى شِدَّةِ الْحَنَقِ.
فَلَمَّا رَأَيْتَ- يَا إِلَهِي تَبَاركْتَ وَ تَعَالَيْتَ- دَغَلَ سَرِيرَتِهِ، وَ قُبْحَ مَا انْطَوَى عَلَيهِ، أَرْكَسْتَهُ لِأُمِّ رَأْسِهِ فِي زُبْيَتِهِ، وَ رَدَدْتَهُ فِي مَهْوَى حُفْرَتِهِ، فَانْقَمَعَ بَعْدَ اسْتِطَالَتِهِ ذَلِيلًا فِي رِبَقِ حِبَالَتِهِ الَّتِي كَانَ يُقَدِّرُ أَنْ يَرَانِي فِيهَا، وَ قَدْ كَادَ أَنْ يَحُلَّ بِي لَوْ لَا رَحْمَتُكَ مَا حَلَّ بِسَاحَتِهِ.
وَ كَمْ مِنْ حَاسِدٍ قَدْ شَرِقَ بِي بِغُصَّتِهِ، وَ شَجِيَ مِنِّي بِغَيْظِهِ، وَ سَلَقَنِي بِحَدِّ لِسَانِهِ، وَ وَحَرَنِي بِقَرْفِ عُيُوبِهِ، وَ جَعَلَ عِرْضِي غَرَضاً لِمَرَامِيهِ، وَ قَلَّدَنِي خِلَالًا لَمْ تَزَلْ فِيهِ، وَ وَحَرَنِي بِكَيْدِهِ، وَ قَصَدَنِي بِمَكِيدَتِهِ.
فَنَادَيْتُكَ- يَا إِلَهِي- مُسْتَغِيثاً بِكَ، وَاثِقاً بِسُرْعَةِ إِجَابَتِكَ، عَالِماً أَنَّهُ لَا يُضْطَهَدُ مَنْ أَوَى إِلَى ظِلِّ كَنَفِكَ، وَ لَا يَفْزَعُ مَنْ لَجَأَ إِلَى مَعْقِلِ انْتِصَارِكَ، فَحَصَّنْتَنِي مِنْ بَأْسِهِ بِقُدْرَتِكَ.
وَ كَمْ مِنْ سَحَائِبِ مَكْرُوهٍ جَلَّيْتَهَا عَنِّي، وَ سَحَائِبِ نِعَمٍ أَمْطَرْتَهَا عَلَيَّ، وَ جَدَاوِلِ رَحْمَةٍ نَشَرْتَهَا، وَ عَافِيَةٍ أَلْبَسْتَهَا، وَ أَعْيُنِ أَحْدَاثٍ طَمَسْتَهَا، وَ غَوَاشِي كُرُبَاتٍ كَشَفْتَهَا.
وَ كَمْ مِنْ ظَنٍّ حَسَنٍ حَقَّقْتَ، وَ عَدَمٍ جَبَرْتَ، وَ صَرْعَةٍ أَنْعَشْتَ، وَ مَسْكَنَةٍ حَوَّلْتَ.
كُلُّ ذَلِكَ إِنْعَاماً وَ تَطَوُّلًا مِنْكَ، وَ فِي جَمِيعِهِ انْهِمَاكاً مِنِّي عَلَى مَعَاصِيكَ، لَمْ تَمْنَعْكَ إِسَاءَتِي عَنْ إِتْمَامِ إِحْسَانِكَ، وَ لَا حَجَرَنِي ذَلِكَ عَنِ ارْتِكَابِ مَسَاخِطِكَ، لَا تُسْأَلُ عَمَّا تَفْعَلُ.
وَ لَقَدْ سُئِلْتَ فَأَعْطَيْتَ، وَ لَمْ تُسْأَلْ فَابْتَدَأْتَ، وَ اسْتُمِيحَ فَضْلُكَ فَمَا أَكْدَيْتَ، أَبَيْتَ- يَا مَوْلَايَ- إِلَّا إِحْسَاناً وَ امْتِنَاناً وَ تَطَوُّلًا وَ إِنْعَاماً، وَ أَبَيْتُ إِلَّا تَقَحُّماً لِحُرُمَاتِكَ، وَ تَعَدِّياً لِحُدُودِكَ، وَ غَفْلَةً عَنْ وَعِيدِكَ، فَلَكَ الْحَمْدُ- إِلَهِي- مِنْ مُقْتَدِرٍ لَا يُغْلَبُ، وَ ذِي أَنَاةٍ لَا يَعْجَلُ.
هَذَا مَقَامُ مَنِ اعْتَرَفَ بِسُبُوغِ النِّعَمِ، وَ قَابَلَهَا بِالتَّقْصِيرِ، وَ شَهِدَ عَلَى نَفْسِهِ بِالتَّضْيِيعِ.
اللَّهُمَّ فَإِنِّي أَتَقَرَّبُ إِلَيْكَ بِالْمُحَمَّدِيَّةِ الرَّفِيعَةِ، وَ الْعَلَوِيَّةِ الْبَيْضَاءِ، وَ أَتَوَجَّهُ إِلَيْكَ بِهِمَا أَنْ تُعِيذَنِي مِنْ شَرِّ كَذَا وَ كَذَا، فَإِنَّ ذَلِكَ لَا يَضِيقُ عَلَيْكَ فِي وُجْدِكَ، وَ لَا يَتَكَأَّدُكَ فِي قُدْرَتِكَ وَ أَنْتَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
فَهَبْ لِي- يَا إِلَهِي- مِنْ رَحْمَتِكَ وَ دَوَامِ تَوْفِيقِكَ مَا أَتَّخِذُهُ سُلَّماً أَعْرُجُ بِهِ إِلَى رِضْوَانِكَ، وَ آمَنُ بِهِ مِنْ عِقَابِكَ، يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ.
Na (ifuatayo ilikuwa ni) miongoni mwa dua zake, amani iwe juu yake, (aliyokuwa akiitumia) kwa ajili ya kujilinda dhidi ya njama za maadui, pamoja na kurudisha numa madhara yao.
Ee Mola wangu, Uliniongoza, nami nikajisahau (nikacheza na dunia). Ukaniwaidhi (ukanisemeza), nami nikakaidi (nikajitia ununda). Ukanikirimu kwa fadhila (Zako), nami (badala ya kushukuru) nikaasi. Hatimaye, nilikuja kufahamu yale niliyoyafanya pale Uliponijulisha makasa yangu hayo. Hivyo nikaomba radhi Nawe, ukanikubalia (ukanisamehe). Na ukawa na mwenye kunisitiri hata pale niliporejea katika makosa yangu. Basi shukurani zote ni Zako Wewe, Ee Mungu wangu.
(Ewe Mola wangu! Hakika mimi) nimejivurumisha kwenye mabonde ya maafa, na nikatumbukia ndani ya mapito ya upotevu; ambamo nilihatarika na kukumbwa na (hatari za) nguvu Zako, na kutumbukia kwangu humo, kulinistahikisha kupata adhabu Zako.
Na Tauhidi (upwekeshaji) ndiyo nyenzo yangu kwa ajili ya kukufikia Wewe, na hoja yangu (na kisingizio changu tetezi) ni kwamaba mimi sikuwahi kukushirikisha na kitu chochote, na wala sikuwahi kutwaa (kuchagua au kumtawalisha moyoni mwangu) mungu mwingine (yeyote yule) sambamba Nawe. Hakika, nimekimbilia Kwako kwa maamuzi kamili ya nafsi yangu (Na nimekimbilia Kwako na fafsi yangu ikiwa kibindoni mwangu). (Na bila shaka) kwako Wewe ndio kimbilio la muovu, na kwako Wewe ndio rejeo la yule anayetafuta kimbilio, ambaye amepoteza fungu la nafsi yake (ambaye amepoteza bahati ya nafsi yake).
Ni maadui wangapi walionichomoa panga za uhasama wao (dhidi yangu), na wakanoa makali ya visu vyao (wakavinoa visu vyao dhidi yangu), wakachonga ncha za mishale yao, wakaniandalia sumu ziangamizazo (ziuazo), na wakanilekezea mishale yao yenye kusibu (shabaha zake). Macho yao angalizi kamwe hayapatwi na usinzigi katika ulinzi wake wa kuniangaza mimi, na tayari wameshanuia (wameshadhamiria) kuniletea madhara na kuninywesha machungu ya madhara (ya uadui wao).
Hapo basi, Ewe Mola wangu, uliungalia udhaifu wangu katika kuhimili majanga, na ushindwaji wangu wa kujipatia ushindi katika mapamabano yangu na yule anayenikusudia mabaya. Kadhalika, ukaiangalia hali yangu ya upweke wangu ndani (mbele) ya kundi kubwa la wale wanaonifanyia uadui, na (ukaona) jinsi (maadui zangu) walivyonitegea mitego ya mabalaa, kwa njia ambayo katu sikuwa na fikra nayo.
Hapo basi ukanianzia kwa kunipa msaada Wako (kabla ya mimi kuomba msaada Huo), na ukaniimarishia uwezo wangu kwa nguvu Zako. Baadaye, ukanipunguzia ukali wake (ukali wa maadui zangu hao), na ukawabadilisha kutoka hali ya kuwa na kundi kubwa (mkusanyiko wa nguvu kubwa), hadi kufikia nguvu pweke. Kisha ukaniinua dhidi yake, na ukamuelekezea mwenyewe ile mipango yake mibaya aliyokuwa ameipanga dhidi yangu. Na hatima yake, ukamrejesha bila ya kuponya chuki zake, na bila kuiponya ghadhabu yake. Akaondoka na kujitafuna kidole (kwa hasira), huku majeshi yake yakiwa yameshindwa kutimiza malengo yao.
Ni maadui wangapi walionipangia njama kwa hila zao, na wakanitegea mitego yao. Wakaniwekea mtu maalumu wa kunichunguza kwa makini nyenendo zangu, huku wakinyemelea kama simba anavyomkizia kiwindwa chake, akingoja fursa nzuri ya kumshambulia. Hutabasamu mbele yangu kwa tabasamu ya kinafiki, huku wakinitizama kwa jicho la chuki kupita kiasi.
Na Ewe Mola wangu, Uliyetuka na Muadhamu, baada ya Wewe kubaini ubaya wa nafsi ya daui yangu huyu, pamoja uovu alioficha kifuani mwake, ulimwangusha kifudifudi kwenye mtego wake mwenyewe, kisha ukamrudisha kwenye shimo la maangamizi yake mwenyewe (ayoyatayarisha kwa ajili yangu). Hivyo basi, baada ya majivuno yake, alidhibitiwa na kudhalilishwa vikali ndani ya tanzi za mtego wake ambao alikadiria kuniona mimi nikiwa ndani yake. Na laiti si huruma yako, bila shaka yaliyomfika yeye yangekuwa ndiyo yaliyonifika mimi.
Na kuna hasidi wangapi ambao wamesongwa na chuki (balaa) zao wenyewe walizokuwanzao dhidi yangu, na wakakosa raha kwa sababu ya hasira zao kwangu. Wamenichapa kwa ukali wa ndimi zao, na kunichafua kwa kunisingizia (kunipchika) mimi aibu zao weo. Wameifanya heshima yangu kuwa shabaha ya mashambulizi yao, na (wakajitahidi) kunivika tabia mbaya ambazo daima zilikuwa ni tabia zao wao. Wamejaribu kunitia katika dhiki kwa hila zao, na kunilenga kwa njama zao ovu (halifu).
Hivyo basi (baada kukabiliwa na njama hizo), nilikuelekezea maombi yangu, Ewe Mola wangu, kwa lengo la kuomba msaada Wako, (nilifanya hivyo) nikiwa na imani thabiti juu ya kupata majibu ya haraka kutoka Kwako. (Na nilifanya hivyo) nikifamu fika kwamba; katu hatowezi kukumbwa na dhuluma, yule anayetafuta ulinzi chini ya kivuli cha himaya Yako, na wala hatakumbwa na hofu, yeyote yule anayekimbilio katika ngome ya ushindi Wako. (Nami baada ya kukimbilia kwenye mamlaka yako), umenikinga dhidi ya madhara yake (dhidi ya madhara ya adui zangu).
Na ni mawingu mangapi ya karaha kunikengeusha nayo (Na ni mawingu mangapi ya ya madhara ulionipambazulia), na (ni mawingu mangapi ya neema) ulinielekezea, na (ni makunjuo mangapi) ya rehema (Zako) ulionikunjulia, na (ni aina ngapi za afya) ulizonivika nazo, na (ni macho mangapi ya fitina (dhidi yangu) uliyonifumbia, na ni magubiko mangapi ya kero (dhidi yangu) uliyoniondolea.
Na ni matumaini mangapi mema uliyoyatimiza (Na ni dhana ngapi chanya ulizonitimizia), na ni hali ngapi za uhitaji ulizoziondoa, na ni maanguko ngapi (dhidi yangu) ulilolinyanyua (ulinishika mkono na kuninyanyua nikaweza kusimama), na ni aina ngapi za umasikini (zilizkuwa zikinikabili nawe) (Nawe) ulizigeuza (kuwa ni utajiri badala ya umaskini).
Yote hayo ni neema na fadhila zitokazi Kwako. Na katika yote hayo, mimi nilikuwa nimezama katika kukuasi. Uovu wangu haukukuzuia Wewe kuendelea kunifanyia hisani, wala hilo (wala hisani Zako juu yangu) hazikunizuia kufanya mambo yanayokukasirisha. (Bila shaka) Wewe haulizwi juu ya unachokifanya (juu ya maamuzi Yako).
Hakika Uliombwa nawe Ukatoa, na hata kabla hujaombwa Ulianza kutoa. Fadhila (hisani) Zako ziliombwa nawe hukuchoka kutoa (Nawe hukuwa mbahili katika kutoa hisani hizo). Ewe Bwana wangu, umekataa (kufanya jengine lolote lile), isipokuwa kutenda Hisani, kuneemesha, kutoa kwa wingi na kuneemesha kupita kifani. Nami nimekataa (kutende jengine lolote lile) isipokuwa kukiuka matakatifu Yako, kuvuka mipaka Yako na kusahau maonyo Yako. Basi, sifa zote njema ni Zako, Ewe Mungu wangu, Mwenye uwezo usioshindwa, na Mwenye upole usiye na haraka.
Hii ni nafasi (hali) ya yule aliyekiri wingi wa neema (Zako juu yake), kisha akazikabili kwa mapungufu (mbali mbali), na yeye mwenyewe ametoa ushuhuda dhidi ya nafsi yake juu (tendo lake la) upotezaji (wa haki zako).
Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika mimi ninajikurubisha Kwako kupitia hadhi ya juu ya Muhammadiyya (aliyonayo mtume Wako Muhammad), (pia ninajikurubisha Kwako kupitia hadhi) na nasaba tukufu na safi ya Ali (Kwa lulgha nyengine: Ninajikurubisha Kwako kupitia cheo cha nafasi ya Uimamu wa Ali). Na ninaelekea Kwako kupitia (watukufu) wawili hawa ili uniepushe na shari ya hili na lile (kadha wa kadha). Hakika jambo hilo halikukanzi ndani ya uwezo Wako, wala halikulemei katika nguvu Zako, Nawe ni Muweza juu ya kila kitu.
Hivyo basi, Ee Mola wangu, niruzuku kutoka katika hazina ya rehema yako na ufanisi wako usio na kikomo, kile kitakachokitumia kama nyenzo (ngazi) ya kupanda daraja hadi kufikia radhi Zako, na niweze kupata amani kwacho dhidi ya adhabu Yako, Ewe Mrehemevu kuliko warehemevu wote.
Rejea
- ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 275.
- ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 275-292.
- ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 3, uk. 269-292.
- ↑ Fahri, Sherh wa Tafsir Sahifa Sajjadih, 1388, juz. 3, uk. 525-529.
- ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 6, uk. 243-296.
- ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 625-635.
- ↑ Darabi, Riyadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 681-698.
- ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 2, uk. 573-591.
- ↑ Faydh Kashani, Ta'baqat al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 99-101.
- ↑ Jazairi, Sharh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1402 AH, uk. 278-284.
Vyanzo
- Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
- Jazairi, Izu-Din, Sherh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Beirut, Dar al-Taaruf Lil-Matbuat, 1402 AH.
- Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
- Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
- Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
- Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
- Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
- Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
- Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.