Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Dua ya Hamsini na Moja ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Hamsini na Moja ya Sahifa Sajjadiyya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Ahmad Nayrizi, iliyoandikwa mnamo 1145 AH.

MadaDua ya kuonesha unyenyekevu na shukrani kwa Mwenyezi Mungu kutokana na neema mbalimbali.
Ina Mapokezi au Haina MapokeziIna Mapokezi
Imenukuliwa Kutoka kwaImamu Sajjad (a.s)
MpokeziMutawakkil ibn Harun
Vyanzo vya KishiaSahifa Sajjadiyah
Dua ya Tawassuli • Dua ya Kumaili • Dua ya Nudba • Dua ya Samati • Dua ya Faraji • Dua ya Abu Hamza Thumali • Ziara ya Ashura • Ziara ya Jamiat Kabira • Ziara ya Warith • Ziara ya Aminu-Llah • Ziara ya Arobaini

Dua ya Hamsini na Moja ya Sahifa Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء الواحد والخمسون من الصحيفة السجادية) ni miongoni mwa dua za maarufu iliyonukuliwa kutoka kwa Imam Sajjad (a.s). Nayo ni dua yenye kuakisi hali ya unyenyekevu wa mja anayotakiwa kuwa nayo mbele ya Mola wake. Katika dua hii tukufu, kwanza kabisa Imamu Sajjad (a.s) anamshukuru Allah kwa neema Zake zisizohesabika alizowaneemesha Waja wake. Hata hivyo, Iamu Sajjad anakiri uhaba wa shukrani za mja juu neema hizo, na kukuli kwamba mwanadamu ni dhaifu katika kumshukuru Mola wake ipasavyo. Vilevile, dua hii inamtambulisha Allah kuwa ndiye Mlinzi na Msaidizi pekee wa mwanadamu. Aidha dua hii inatufunza kwamba; Kutawakali (kumtegemea Mwenye Ezi Mungu), ndiyo njia pekee ya uokovu kutokana mitihani mbali mbali. Miongoni mwa mafuzo mengine ya dua hii ni kwamba; Uhai na endelevu wa maisha ya kijamii, uko chini ya dhamana ya Allah ya kusitiri aibu za waja Wake, na kwa ukombozi wa Mwenye Ezi huwafikia waja wake, pale waja Wake wanapojitambua kuwa wapo katika hali ya dharura (yaani wanapogonga mlango wa Mola wao huku wakiachana na milango mengine ya asiyekuwa Yeye).

Tafsiri na ufafanuzi wa Dua ya Hamsini na Moja unapatikana ndani ya vitabu mbali mbali vya tafsiri za Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu hivyo ni kama vile; Shuhud wa Shenakht kilichoandikwa kwa lugha ya Kiajemi na Hassan Mamdouhi Kermanshahi. Aidha, kwa watumiaji wa lugha ya Kiarabu, wanaweza kupata uchambuzi wa Kiarabu wa dua hii katika kitabu kiitwacho Riyadh as-Salikin, kilichondikwa na Sayyid Ali Khan Madani.

Mafunzo Yaliomo Ndani ya Dua ya Hamsini na Moja

Mada za Dua ya Hamsini na Moja, kutoka katika kitabu cha Sahifa Sajjadiyya, zinajumuisha vipengele tofauti ndani yake. Miongoni mwavyo ni; sifa kwa Mwenye Ezi Mungu, kuomba haja kutoka kwa yule Mwenye Kujitosheleza kwa Dhati (Mwenye Ezi Mungu), kutafuta kimbilio kwenye mlango wa Mwenye Ezi Mungu, kuomba msamaha, kuomba afya njema, ombi la kuomba majaaliwa (taufiki), kumshukuru Mungu na kukiri uwezo mdogo wa mwanadamu katika ufanisi wa kutoa shukurani kwa Mola wake.[1] Kwa mujibu wa Hassan Mamdouhi Kermanshahi katika uchambuzi wake wa dua hii, ni kwamba; maneno ya Maimamu Watoharifu (a.s) waliyoyatumi ndani ya dua zao mbali mbali, ni maneno yawakilishayo kilele cha uzuri wa maneno ya mja yanayoweza kutumika katika mawasiliano ya mja na Mola wake. Hii inatokana na kule wao kutilia maanani zaidi dhana ya ufukara wa dhati aliyonao binadamu mbele ya Mwenye Ezi Mungu, pamoja na kusisitiza na kukiri ukwasi kamili wa Mwenye Ezi Mungu. Kutokana na hilo, wameweza kuainisha na kuwasilisha mahitaji yote ya viumbe mbele ya Mola wao, na wakaweza ibara bora zaidi na zenye ufasaha wa hali ya juu zaidi katika kuomba rehema za Mwenye Ezi Mungu.[2]

Mafunzo ya dua hii yamekuja katika vipengele vifuatavyo:

  • Dhana ya Shukrani: Wajibu wa kumshukuru Mungu kwa hisani Zake.
  • Fadhila za Awali: Neema za Mwenye Ezi Mungu kwa viumbe hutangulia kabla ya maombi yao.
  • Wingi wa Neema: Neema za Mwenye Ezi Mungu kwa wanadamu ni nyingi mno kiasi cha kutoweza kuhesabika.
  • Upungufu wa Kibinadamu: Kukiri kutokuwa na uwezo kamili wa kutoa shukrani stahiki kwa neema za Mwenye Ezi Mungu.
  • Maisha na Maendeleo ya Nafsi: Utumiaji wa maisha na urekebishaji wa nafsi kama matokeo ya kutambua na kushukuru hisani na neema za Mwenye Ezi Mungu.
  • Uzembe wa Kibinadamu: Tabia ya wanadamu ya kuzoea neema na kusahau wajibu wa kutoa shukrani.
  • Uingiliaji wa Kiungu: Mwitikio wa Mwenye Ezi Mungu katika kujibu dua za wanadamu katika nyakati za shida na dhiki.
  • Ulinzi dhidi ya Maafa: Uwezo wa Mwenye Ezi Mungu wa kuwaepushia wanadamu majanga makubwa mbali mbali.
  • Neema Maalum: Fadhila za kipekee za Mwenye Ezi Mungu kwa waja wake.
  • Matumaini ya Milele: Kutokukata tamaa kwa waja wa Mwenye Ezi Mungu katika kumuomba Mola wao.
  • Mlinzi Mkuu: Mwenye Ezi Mungu ndiye mlinzi pekee dhidi ya maadui.
  • Shukrani za Kina: Sifa na shukrani kwa Mwenye Ezi Mungu kwa kutumia viungo vyote vya mwili pamoja na akili.
  • Kupata ukombozi kupitia Shukrani: Kuepuka ghadhabu za Mwenye Ezi Mungu kwa njia ya kumsifa na kumshuku.
  • Shukrani ya Kweli: Sifa ya kweli na kamilifu inaambatana na shukrani pamoja na kuleta radhi za Mwenye Ezi Mungu.
  • Msamaha wa Kiungu: Mwenye Ezi Mungu ni msamehevu wa makosa.
  • Utulivu wa Kijamii: Umuhimu wa Mungu wa kuficha aibu za waja Wake katika kudumisha na kudhamini utulivu wa kijamii na heshima yake.
  • Madhara ya Dhambi: Udhalili na fedheha kwa mwanadamu kama matokeo ya dhambi zake.
  • Unyenyekevu na Hofu: Heshima na unyenyekevu mbele ya Mwenye Ezi Mungu, na hofu ya watawala mbele ya uwezo Wake.
  • Toba na Marejeo: Kuepuka dhambi zinazodhuru na kurejea kwa Mwenye Ezi Mungu kikamilifu.
  • Malalamiko kwa Mungu: Kumwelezea Mungu wingi wa huzuni na vishawishi vya nafsi vyenye kumhadaa mwanadamu.
  • Uendelevu wa Fadhila: Fadhila za Mwenye Ezi Mungu kwa wanadamu ni za kudumu na zisizo na kifani.
  • Utegemezi Kamili: Haja ya mwanadamu ya kumtegemea Mwenye Ezi Mungu ni utegemezi kamili na wa lazima usioepukika.
  • Ombi la Kuomba Hifadhi: Kuomba hifadhi na ulinzi kutokana na fedheha inayosababishwa na uovu wa ndani (nafsi).
  • Hila za Shetani: Uvivu katika kutekeleza majukumu ni moja miongoni mwa mbinu za Shetani.
  • Utegemezi kwa Mungu: Kumtegemea Mungu kama njia pekee ya kupata ukombozi kutokana na shida tofauti.
  • Kuomba Neema: Kuomba kutonyimwa baraka za dunia pamoja na Akhera kwa sababu ya kuwa na shukrani chache.
  • Uchache wa Shukrani: Kukiri kuwa shukrani ya mwanadamu ni ndogo mno ikilinganishwa na neema za Mwenye Ezi Mungu.
  • Uadilifu Kiungu: Adhabu ya Mwenye Ezi Mungu ni kielelezo cha uadilifu wake na si dhulma kwa waja Wake.[3]

Tafsiri Chambuzi za Dua ya Hamsini na Moja

Tafsiri chambuzi za Dua ya hamsini na moja ya Sahifa Sajjadiyya, inapatikana ndani kwa lugha mbali mbali kupitia vitabu vilivyofasiri na kuchambua dua zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu vilivyofanya kazi hiyo kwa lugha ya Kiajemi ni pamoja na; Shahud wa Shenakht kazi ya Muhammad Hassan Mamduhi Kermanshahi,[4] na Sharh wa Tarjome Sahife Sajjadiyye, kazi ya Sayyid Ahmad Fehri.[5]

Pia kuna kazi kadhaa za lugha ya Kiarabu zinazohusiana na tafsiri chambuzi za Dua ya hamsini na moja sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiya. Miongoni mwa kazi hizo ni; kitabu kiitwacho Riadhu as-Salikina kazi ya Sayyid Ali Khan Madani,[6] Fi Dhilali al-Sahifati al-Sajjadiyya kazi ya Muhammad Jawad Mughniyya,[7] Riadhu al-Arifina kitabu kilichoandikwa na Muhammad bin Muhammad Darabi,[8] na Afaqi al-Ruh kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[9] Halikadhalika kuna kazi maalumu zilizofanywa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa maneno na msamiati wa dua hii sambamba na dua nyengine za Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa kazi hizi za kilugha ni kama vile; Ta'liqat Ala al-Sahifati al-Sajjadiyya kazi ya Faidhu Kashani[10] pamoja na Sharhu al-Sahifat al-Sajjadiyya kazi iliyiofanywa na Ezzuddin Al-Jaza’iri.[11]

Matini ya Dua ya Hamsini na Moja na Maelezo Yake kwa Kiswahili

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي التَّضَرُّعِ وَ الِاسْتِكَانَةِ

إِلَهِي أَحْمَدُكَ وَ أَنْتَ لِلْحَمْدِ أَهْلٌ عَلَى حُسْنِ صَنِيعِكَ إِلَيَّ، وَ سُبُوغِ نَعْمَائِكَ عَلَيَّ، وَ جَزِيلِ عَطَائِكَ عِنْدِي، وَ عَلَى مَا فَضَّلْتَنِي بِهِ مِنْ رَحْمَتِكَ، وَ أَسْبَغْتَ عَلَيَّ مِنْ نِعْمَتِكَ، فَقَدِ اصْطَنَعْتَ عِنْدِي مَا يَعْجِزُ عَنْهُ شُكْرِي.

وَ لَوْ لَا إِحْسَانُكَ إِلَيَّ وَ سُبُوغُ نَعْمَائِكَ عَلَيَّ مَا بَلَغْتُ إِحْرَازَ حَظِّي، وَ لَا إِصْلَاحَ نَفْسِي، وَ لَكِنَّكَ ابْتَدَأْتَنِي بِالْإِحْسَانِ، وَ رَزَقْتَنِي فِي أُمُورِي كُلِّهَا الْكِفَايَةَ، وَ صَرَفْتَ عَنِّي جَهْدَ الْبَلَاءِ، وَ مَنَعْتَ مِنِّي مَحْذُورَ الْقَضَاءِ.

إِلَهِي فَكَمْ مِنْ بَلَاءٍ جَاهِدٍ قَدْ صَرَفْتَ عَنِّي، وَ كَمْ مِنْ نِعْمَةٍ سَابِغَةٍ أَقْرَرْتَ بِهَا عَيْنِي، وَ كَمْ مِنْ صَنِيعَةٍ كَرِيمَةٍ لَكَ عِنْدِي

أَنْتَ الَّذِي أَجَبْتَ عِنْدَ الِاضْطِرَارِ دَعْوَتِي، وَ أَقَلْتَ عِنْدَ الْعِثَارِ زَلَّتِي، وَ أَخَذْتَ لِي مِنَ الْأَعْدَاءِ بِظُلَامَتِي.

إِلَهِي مَا وَجَدْتُكَ بَخِيلًا حِينَ سَأَلْتُكَ، وَ لَا مُنْقَبِضاً حِينَ أَرَدْتُكَ، بَلْ وَجَدْتُكَ لِدُعَائِي سَامِعاً، وَ لِمَطَالِبِي مُعْطِياً، وَ وَجَدْتُ نُعْمَاكَ عَلَيَّ سَابِغَةً فِي كُلِّ شَأْنٍ مِنْ شَأْنِي وَ كُلِّ زَمَانٍ مِنْ زَمَانِي، فَأَنْتَ عِنْدِي مَحْمُودٌ، وَ صَنِيعُكَ لَدَيَّ مَبْرُورٌ.

تَحْمَدُكَ نَفْسِي وَ لِسَانِي وَ عَقْلِي، حَمْداً يَبْلُغُ الْوَفَاءَ وَ حَقِيقَةَ الشُّكْرِ، حَمْداً يَكُونُ مَبْلَغَ رِضَاكَ عَنِّي، فَنَجِّنِي مِنْ سُخْطِكَ.

يَا كَهْفِي حِينَ تُعْيِينِي الْمَذَاهِبُ وَ يَا مُقِيلِي عَثْرَتِي، فَلَوْ لَا سَتْرُكَ عَوْرَتِي لَكُنْتُ مِنَ الْمَفْضُوحِينَ، وَ يَا مُؤَيِّدِي بِالنَّصْرِ، فَلَوْ لَا نَصْرُكَ إِيَّايَ لَكُنْتُ مِنَ الْمَغْلُوبِينَ، وَ يَا مَنْ وَضَعَتْ لَهُ الْمُلُوكُ نِيرَ الْمَذَلَّةِ عَلَى أَعْنَاقِهَا، فَهُمْ مِنْ سَطَوَاتِهِ خَائِفُونَ، وَ يَا أَهْلَ التَّقْوَى، وَ يَا مَنْ‏ «لَهُ الْأَسْماءُ الْحُسْنى»‏، أَسْأَلُكَ أَنْ تَعْفُوَ عَنِّي، وَ تَغْفِرَ لِي فَلَسْتُ بَرِيئاً فَأَعْتَذِرَ، وَ لَا بِذِي قُوَّةٍ فَأَنْتَصِرَ، وَ لَا مَفَرَّ لِي فَأَفِرَّ.

وَ أَسْتَقِيلُكَ عَثَرَاتِي، وَ أَتَنَصَّلُ إِلَيْكَ مِنْ ذُنُوبِيَ الَّتِي قَدْ أَوْبَقَتْنِي، وَ أَحَاطَتْ بِي فَأَهْلَكَتْنِي، مِنْهَا فَرَرْتُ إِلَيْكَ- رَبِّ- تَائِباً فَتُبْ عَلَيَّ، مُتَعَوِّذاً فَأَعِذْنِي، مُسْتَجِيراً فَلَا تَخْذُلْنِي، سَائِلًا فَلَا تَحْرِمْنِي مُعْتَصِماً فَلَا تُسْلِمْنِي، دَاعِياً فَلَا تَرُدَّنِي خَائِباً.

دَعَوْتُكَ- يَا رَبِّ- مِسْكِيناً، مُسْتَكِيناً، مُشْفِقاً، خَائِفاً، وَجِلًا، فَقِيراً، مُضْطَرّاً إِلَيْكَ.

أَشْكُو إِلَيْكَ يَا إِلَهِي ضَعْفَ نَفْسِي عَنِ الْمُسَارَعَةِ فِيمَا وَعَدْتَهُ أَوْلِيَاءَكَ، وَ الْمُجَانَبَةِ عَمَّا حَذَّرْتَهُ أَعْدَاءَكَ، وَ كَثْرَةَ هُمُومِي، وَ وَسْوَسَةَ نَفْسِي.

إِلَهِي لَمْ تَفْضَحْنِي بِسَرِيرَتِي، وَ لَمْ تُهْلِكْنِي بِجَرِيرَتِي، أَدْعُوكَ فَتُجِيبُنِي وَ إِنْ كُنْتُ بَطِيئاً حِينَ تَدْعُونِي، وَ أَسْأَلُكَ كُلَّمَا شِئْتُ مِنْ حَوَائِجِي، وَ حَيْثُ مَا كُنْتُ وَضَعْتُ عِنْدَكَ سِرِّي، فَلَا أَدْعُو سِوَاكَ، وَ لَا أَرْجُو غَيْرَكَ

لَبَّيْكَ لَبَّيْكَ، تَسْمَعُ مَنْ شَكَا إِلَيْكَ، وَ تَلْقَى مَنْ تَوَكَّلَ عَلَيْكَ، وَ تُخَلِّصُ مَنِ اعْتَصَمَ بِكَ، وَ تُفَرِّجُ عَمَّنْ لَاذَ بِكَ.

إِلَهِي فَلَا تَحْرِمْنِي خَيْرَ الْآخِرَةِ وَ الْأُولَى لِقِلَّةِ شُكْرِي، وَ اغْفِرْ لِي مَا تَعْلَمُ مِنْ ذُنُوبِي.

إِنْ تُعَذِّبْ فَأَنَا الظَّالِمُ الْمُفَرِّطُ الْمُضَيِّعُ الْآثِمُ الْمُقَصِّرُ الْمُضَجِّعُ الْمُغْفِلُ حَظَّ نَفْسِي، وَ إِنْ تَغْفِرْ فَأَنْتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ.

Na (ifuatayo ni) miongoni mwa dua zake (zinazohusishwa naye) (alayhi as-salaam), aliokuwa akiitumia wakati wa mchakato wa kujenga unyenyekevu na utiifu (mbele ya Mola wake).

Ewe Mola wangu, ninakushukuru (ninakuhimidi), na Wewe ndiye mwenye haki ya kutushukuriwa (kuhimidiwa) kwa ubora wa utendaji Wako kwangu, na kwa wingi wa neema Zako juu yangu, pia kwa wingi wa takrima Zako kwangu, na kwa kunipa nafasi (fungu) maalumu katika rehema Zako, vilevile (nakushukuru) kwa kunifunika kwa neema Zako; bila shaka, Umeanzisha katika nafsini mwangu yale yanayokwaza na kupiku uwezo wa shukrani zangu juu yake.

Lau si (wingi wa) fadhila zako kwangu na ukamilifu wa baraka zako juu yangu, (bila shaka) nisingefanikiwa kufikia malengo yangu, wala nisikuwa na uwezo wa kuirekebisha nafsi yangu. Hata hivyo, Wewe ndiye ulianza kunipa hisani (uliyenianza kwa hisani kabla ya mimi kuomba kitu kutoka Kwako), ukanijalia utoshelevu katika nyanja zote za maisha yangu, ukaniepushia mbali mzigo wa majanga, na ukanizuilia maamuzi (kadari) ya hatari (kutoka Kwako).

Ewe Mungu wangu, ni mabalaa mangap makubwa uliyoniepusha nayo, na ni neema nyingi kiasi gani uliyafurahisha macho yangu kwazo, na ni fadhila njema nyingi zilizoje nilizonazo (zilizonifikia) kutoka Kwako.

Wewe ndiye uliyenijibu maombi yangu katika wakati wa dhiki, na ukanisamehe kosa langu wakati wa kuteleza kwangu, na ukanichukulia haki yangu kutoka kwa maadui zangu (walionidhulumu haki yangu).

Ewe Mola wangu, sikukutua ukiwa bakhili pale nilipokuinulia mikono yangu kukuomba, wala sikuwa ni mwenye kukata tamaa pale nilipokuelekea Wewe. Bali, daima nilikukuta ukiwa ni Mwenye kuvisikia (kuviitikia) vilio vyangu na ni Mwenye kuyajibu maombi yangu. Nimeziona neema Zako zikinienea katika kila hali na katika kila nyakati miongoni mwa nyakati zangu. Kwangu mimi, Wewe ndiwe Mwenye kustahiki shukrani, na ukarimu Wako kwangu ni ukarimu mtukufu ulioje.

Nafsi yangu, ulimi wangu, na akili yangu, vyote ni vyenye kukuhimidi Wewe, (vyakuhimidi kwa) himdi zifikiazo utimilifu na haki ya shukrani, (vyakuhimidi kwa) himdi (zenye lengo la) kufikia kilele cha ridhaa Yako juu yangu, basi niokoe na ghadhabu Zako.

Ewe kimbilio langu la hakika pale nichoshwapo (nikwamishwapo) na njia za dunia (zisizo na uhakika). Ewe unayenisamehe madhambi yangu, kama si sitara yako juu ya aibu zangu, basi ningekuwa miongoni mwa walioaibishwa. Ewe muokozi (muungaji mkono) wangu kwa nusra yako; bila ya msaada wako, ningelikuwa miongoni mwa waliolemewa. Ewe ambaye wafalme na watawala hunyenyekea mbele ya utukufu wako kwa kidhalili kabisa, huku wakiogopa adhabu yako. Ewe Mola Mwenye kustahiki takwa, na Ewe Mwenye Asma-ul-Husna (Majina Mazuri), nakuomba unihurumie na unighufirie (dhambi zangu), kwani mimi si mja asiye na dhambi, kiasi ya kwamba niwe na haki au fursa ya kutoa udhuru, wala sina uwezo wa kujinusuru, wala sina mahali (pengine) pa kukimbilia isipokuwa Kwako.

Na ninakuomba unighufirie makosa yangu, na ninajitenga (ninajikinga) mbele Yako na madhambi zangu zenye kunihiliki, dhambi ambazo zimenizunguka (zimenivaa) na kunimaliza (kuniangamiza). Ewe Mola wangu (Bila shaka) nimekimbilia Kwako nikizikimbia dhambi hizo, hali nikiwa ni mwenye kutubu (kutokana na dhambi hizo), hivyo basi (ninakuomba) uipokee toba yangu. (Nimekimbilia Kwako nikiwa ni) mwenye kuomba hifadhi, basi (ninakuomba) unihifadhi. (Nimekimbilia Kwako nikiwa ni) mwenye kuomba nusra, basi (ninakuomba) usinidhadhilishe (kwa kutonipa nusra Yako). (Nimekimbilia Kwako nikiwa ni) mwenye kuombaji, basi (ninakuomba) usininyime (fadhila Zako). (Nimekimbilia Kwako nikiwa ni) mwenye kushikamana nawe, basi (ninakuomba) usinikabidhishe (kwa adui zangu). (Nimekimbilia Kwako nikiwa ni) kwenye kukuita, basi usinirudishe nikiwa nimevunjika moyo.

Nimekuomba Wewe, Ewe Mola wangu Mlezi, hali nikiwa katika hali ya umaskini, mwenye unyenyekevu, mwenye hofu, muoga, mwenye kutetemeka, fukara, na mwenye shida nawe.

Ee Mola wangu Mlezi! Ninakushtakia Wewe udhaifu wa nafsi yangu, kutokana na kushindwa kwangu kwenye uwanja wa mashindano ya amali na mbio za kukimbilia yale uliyowaahidi mawalii (wapenzi) wako, na kujiepusha na yale uliyowakataza maadui zako. Na (ninakushtakia Wewe) wingi wa majonzi zangu na wasiwasi wa nafsi yangu.

Ewe Mola wangu, hukunifedhehesha kwa aibu zale nizifichazo, na wala hukuniteketeza (hukuniangamiza) kwa maovu yangu. Ninakuomba nawe unaitikia maombi yangu, ijapokuwa mimi ni mzito katika kuitikia wito wako. Ninakuomba kila hitaji langu nilipendalo, na mahali popote pale nilipo huamua kuzitandaza siri zangu mbele yako. Hivyo basi, simwabudu mwingine yeyote yule asiyekuwa Wewe, na wala simtaji mwengine yeyote yule isipokuwa Wewe.

Ewe Mola, Labbaika (ninaitikia wito Wako), Labbaika (ninaitikia wito Wako). Nawe ni Mwenye kusikia malalamiko ya anayekuelekezea shida zake, na ni Mwenye kumpokea (kumdiriki) yule anayekuwekea kwa kutawakali kwako Wewe, na ni Mwenye kumnusuru yule anayejikinga Kwako, na ni Mwenye kumwondolea dhiki yule anayetafuta hifadhi Kwako.

Ewe Mola wangu, usiniharamishie kheri za maisha ya duniani na ya Akhera kutokana uchache wa shukrani zangu (Kawako), na (ninakuomba) unighufirie dhambi zangu unazozijua (zilizo wazi mbele ya elimu Yako).

Ukinuadhibu, basi mimi ndiye niliyejidhulumu, niliyepindukia mipaka, mzembe, mtenda dhambi, niliyepuuza na kusahau maslahi ya nafsi yangu. Na ukisamehe, basi Wewe ndiye Mrehemevu zaidi warehemevu wote.

🌞
🔄
➖
➕

Rejea

  1. ↑ Ansarian, Diyar Asheqan, 1373, juz. 7, uk. 607.
  2. ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 311.
  3. ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 311-336.
    Sherh Farzahaye Duaye Panjo Yekom Sahife Az Site Irfan.
  4. ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 307-336.
  5. ↑ Fahri, Sherh wa Tafsir Sahifa Sajjadih, 1388, juz. 3, uk. 547-552.
  6. ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 6, uk. 333-364.
  7. ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 641-646.
  8. ↑ Darabi, Riyadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 707-715.
  9. ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 2, uk. 601-613.
  10. ↑ Faydh Kashani, Ta'baqat al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 102-103.
  11. ↑ Jazairi, Sharh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1402 AH, uk. 288-292.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Jazairi, Izu-Din, Sherh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Beirut, Dar al-Taaruf Lil-Matbuat, 1402 AH.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.