Hal Min Nasirin Yansuruni

Kutoka wikishia

Hal Min Nasirin Yansuruni (Kiarabu: هَلْ مِنْ ناصِرٍ یَنْصُرُني) ina maana kwamba: Je, kuna mwenye kunusuru aninusuru. Maneno haya yamenukuliwa kutoka kwa Imamu Hussein (a.s) katika lahadha za mwisho za uhai wake siku ya Ashura. Jawad Muhadathi anasema katika kitabu cha Farhgang Ashura (Utamaduni wa Ashura) maneno haya ni nukuu ya kimaana na haijaja namna hii katika vitabu vya historia. [1] Hata hivyo, vyanzo vinavyohusiana na tukio la Ashura, vimenukuu ibara na maneno yanayoshabihiana na madhumuni hii. [2]

Kwa mujibu wa nukuu ya wasimuliaji na waliandika kuhusiana na matukio tukio la Ashura ni kuwa, wakati masahaba wa Imamu Hussein (a.s) walipouawa shahidi na Imamu Hussein akawa amebakia peke yake alisema maneno haya: ((هَلْ مِنْ ذَابٍّ يَذُبُّ عَنْ حَرَمِ رَسُولِ اللَّهِ هَلْ مِنْ مُوَحِّدٍ يَخَافُ اللَّهَ فِينَا هَلْ مِنْ مُغِيثٍ يَرْجُو اللَّهَ بِإِغَاثَتِنَا هَلْ مِنْ مُعِينٍ يَرْجُو مَا عِنْدَاللَّهِ فِي إِعَانَتِنَا ; Je, kuna mtu mwenye kuhami ili ahamu haram ya Mtume wa Mwenyezi Mungu? Je, kuna muabudu Mungu mmoja ili kuhusiana na sisi amuogope Mwenyezi Mungu? Je, kuna mfikishaji sauti ambaye kwa kufikisha sauti yetu awe na matarajio ya Mwenyezi Mungu? Je, kuna msaidizi ambaye kwa kutusaidia sisi ili awe na matumaini kwa kile akitarajiacho kwa Mwenyezi Mungu? [3]

Imamu Hussein (a.s) alitaka msaada zaidi wakati alipokuwa katika mashukio ya Qasr Bani Muqatil ambapo wakati alipomtaka Abdallah bin Hurr Ju’fi amsaidie na yeye akakataa kufanya hivyo kwa kutoa udhuru, Imamu alimtaka Abdallah aondoke hapo, kwani kama atatasikia sauti ya Imamu ya kuomba msaada na kisha asiitikie na kujibu, Mwenyezi Mungu atamuangamiza. [4] Baadhi ya watu wanatambua nara ya Labayyka ya Hussein kwamba ni jibu la kuitikia wito wa Imamu Husewein wa kutaka msaada siku ya Ashura. [5]

Katika filamu ya Ruze Ashura (Siku ya Ashura) iliyotengenezwa na Bahram Asadi na ambayo inazungumzia tukio la Karbala, muigizaji mkuu wa filamu hii ni kijana ambaye ndio kwanza amesilimu ambapo anasikia sauti ya mzungumzaji wa ghaibu na anaikariri “Nani wa kuninusuru?” Kijana huyo anaifuata sauti hiyo na alasiri ya siku ya Ashura anawasili katika jangwa la Karbala. [6]