Kuuawa Kwa Habili
Kuuawa kwa Habili (Kiarabu: مقتل هابيل) ni mojawapo ya hadithi zilizomo ndani ya Qur’ani kuhusiana na kuuawa kwa mmoja kati ya watoto wawili wa Nabii Adamu, kilichofanywa na mwana mwingine wa Nabii Adamu. Katika vyanzo vya kidini, mauaji haya yanachukuliwa kuwa ndio mauaji ya kwanza ya binadamu duniani humu. Inasemekana kwamba; Qabili ambaye ni mwana wa pili wa Nabii Adamu, alipinga uteuzi wa Habili kama ni mrithi wa Nabii Adamu, na ili kumaliza mzozo huu, Mwenye Ezi Mungu alimwambia kila mmoja wao atoe dhabihu kwa ajili ya Mola wake. Kulingana na Hadithi, kichinjwa cha Qabili hakikukubaliwa na Mwenye Ezi Mungu. Kwa hivyo, wakati wa kuteulia kwa mrithi wa Nabii Adamu, Qabili alimwonea wivu Habili na hatimae kumsababishia kifo. Kulingana na Aya ya 31 ya Surat Al-Ma’ida, Mwenye Ezi Mungu alimfundisha Qabili jinsi ya kumzika Habili kupitia ndege wa aina ya kunguru.
Mauaji ya Kwanza Kabisa Ulimwenguni
Mauwaji ya Habili yametambuliwa kama ndiyo mauaji ya kwanza ulimwenguni.[1] Aya ya 27 hadi 31 za Surat Al-Maida zinahusiana na kisa cha mauaji haya ya Habili. Mwenyezi Mungu katika Aya hizi anaelezea kwamba; wana wawili wa Adamu, walifanya ya ibada fulani kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenye Ezi Mungu, moja wao akakubaliwa amali na mwengine akakataliwa. Ndugu ambaye amali yake haikukubaliwa, alimtishia ndugu yake kumuua kisha akamshambulia na hatimaye akamuua.[2] Kulingana na maelezo ya wafasiri wa Qur’ani, jina la ndugu aliyefanya mauaji hayo ni Qabili na yule aliyeuawa ni Habili.[3]
Shauku na Sababu ya Qabili Kutekeleza Mauaji Haya
Hadithi zinaeleza kwamba; sababu ya mauaji ya Habili ni husuda ya ndugu yake dhidi yake, husuda ambao inahusiana na suala la kumteuliwa kwake kama ni mrithi wa Mtume wa Adamu (a.s).[5] Kulingana na baadhi ya watafiti, wakati Mwenye Ezi Mungu alipomshushia wahyi Nabii Adamu (a.s) na kumwamuru alikabidhi jina kuu (Ismu al-A’adham) la Mwenye Ezi Mungu kwa Habili, na kumtambua kama ni mrithi wake wa kushika nafsi ya baba yake, Qabili alipinga; hii ni kwa sababu yeye alikuwa ndiye mtoto mkubwa katika familia, na aliamini kuwa urithi na huo unapaswa kuja kwake yeye; kwa upande mwingine, yeye (Qabili) aliona kuwa, mapenzi yake binafsi ya Nabi Adamu (a.s), na upendeleo wake kwa Habili, ndio sababu ya uteuzi huo, na wala si amri itokayo kwa Mwenye Ezi Mungu. Ili kumaliza mzozo huu, Mwenye Ezi Mungu alishusha wahyi ya kwamba kila mmoja atoe kitu fulani kwa ajili ya Mola wake.[6]
Ufafanuzi Juu ya Kichinjwa cha Habili na Qabili
Kulingana na maelezo ya Hadithi, Qabili alikuwa ni mkulima, naye katoa sadaka ile sehemu mbaya zaidi ya mazao yake, na Habili ambaye alikuwa ni mchungaji, alimtoa kondoo bora aliye bora zaidi kama ni sadaka kwa ajili ya Mola wake. Kuteketezwa kwa sadaka ilikuwa ndio ishara ya kukubalika kwa sadaka hiyo mbele ya Mwenye Ezi Mungu, hivyo basi sadaka ya Habili ikakubaliwa, lakini sadaka ya Qabili haikukubaliwa.[7]
Husuda Ndiyo Chanzo cha Mauaji ya Habili
Kulingana na Hadithi na riwaya za Kiislamu, baada ya kukubaliwa kwa sadaka ya Habil, Qabili alimwonea hasadi ndugu yake, na akatoa kiapo ya kwamba atamuua Habili.[8] Kulingana na Aya za Qur’ani, Habili aligusia suala la kumcha Mungu (taqwa), na kwamba Mwenyezi Mungu hukubali sadaka za watu wenye taqwa (wachamungu), alimwambia Qabili akisema kwamba; yeye hatanyosha mkono wake kwa nia ya kumuua, kwani yeye hataki kuwa mhalifu; pia alimwonya Qabili kwamba ikiwa atamuua, basi atakuwa miongoni mwa wahalifu na atastahili Jahannam.[9] Kulingana na riwaya ya Tabari (iliyohaririwa mwaka 303 Hijiria), ni kwamba; wakati Habili alipokuwa akichunga kondoo wake mlimani, alishambuliwa na Qabili hali akiwa amejipumzisha machungani humo, na akauawa kwa kupigwa na jiwe kichwani mwake.[10]
Baadhi ya watafiti na wanazuoni wakifafanua sababu ya husda ya Qabili dhidi ya Habili, wamesema kwamba; Husda ya hii ilitokana na amri ya baba yao Adamu (a.s) ya kumtaka kila mmoja kati yao kumwoa dada pacha wa mwenzake, ila kwa kuwa dada wa Qabili alikuwa ni mzuri zaidi kuliko dada wa Habili, hilo lilipelekea Qabili kuhisi wivu na kuto ridhia dada yake kuolewa na Habili, naye akawa amepinga amri ya baba yake juu ya maamuzi hayo. Kutokana na upinzani huo, Mwenye Ezi Mungu alitoa amri ya kuwataka kila mmoja kati yao watoe muhamga kwa ajili ya Mola wao, na yule atakaye kuliwa muhanga wake ndiye atakaye kuwa na haki ya kumwoa dada wa Qabili. Hatimaye muhanga wa Qabili ukawa ndio uliokubalika mbele ya Mwenye Ezi Mungu, na hiyo ikawa ndiyo sababu ya Habili kumuua Qabili kupitia jiwe alilompiga kichwani mwake.[11]
Kisa huchi cha ndugu hawa wawili kuhusiana na utoaji wao muhanga kwa ajili ya Mola wao, pia kinapatikana ndani Taurati.[12]
Mazishi ya Habili
Kulingana na ripoti ya Muhammad bin Jarir Tabari, mwanahistoria wa karne ya tatu Hijria, ni kwamba; mwili wa Habili ulikuwa katika hatari ya kuliwa na wanyama pori kutokana Qabili kutofahamu jinsi ya kuustiri mwili huo na kukosa ufahamu wa jinsi ya kuzika mwili wa binadamu.[13] Kulingana na Aya ya 31 ya Surat Al-Ma’idah ni kwamba; Qabili alitumiwa kunguru na Mola wake, ambaye alikuja na kuchimbua ardhi na kuficha mwili wa kunguru ambaye alikuwa amefariki, ili amwonyeshe Qabili jinsi ya kumzika ndugu yake.[14]
Rejea
- ↑ Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, juz. 4, uk. 345.
- ↑ Tazama: Surat al-Maidah, Aya ya 27-31.
- ↑ Sheikh Tusi, At-Tibyān, juz. 3, uk. 492; Tabatabai, al-Mīzān, juz. 5, uk. 315; Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, juz. 4, uk. 348.
- ↑ Nishaburi, Qisas al-Anbiyai, Hati ya mkono.
- ↑ Ayāshi, Tafsīr al-'Ayāshī, juz. 1, 1380 S, uk. 312.
- ↑ Sadiqi Fadaki, Irtidad; Bazgasht Be Tarikh, uk. 270.
- ↑ Kulaini, al-Kāfī, juz. 8, uk. 113.
- ↑ Ayāshi, Tafsīr al-'Ayāshī, juz. 1, 1380 S, uk. 312.
- ↑ Surat al-Maidah, Aya ya 29.
- ↑ Tabari, Tārīkh al-Umam Wa al-Mulūk, juz. 1, uk. 138.
- ↑ Tusi, at-Tibyān, juz. 3, uk. 493; Tabari, Tārīkh al-Umam Wa al-Mulūk, juz. 1, uk. 138.
- ↑ Taurati, Kitabu cha Mwanzo, Sura ya 4, Aya ya 3-8.
- ↑ Tabari, Tārīkh al-Umam Wa al-Mulūk, juz. 1, uk. 86.
- ↑ Makarim Shirazi, Tafsir Nemune, juz. 4, uk. 351.
Vyanzo
- Al-Qur'an
- 'Ayāshī, Muhammad bin Mas'ud, Tafsīr al-'Ayāshī, Mhakiki: Hashim Rasuli, Tehran: Perpustakaan al-Ilmiyyah al-Islamiyyah, Chapa ya kwanza, 1380 H.
- Kulaini, Muhammad bin Ya'qub, Al-Kāfī, Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyyah, 1407 H.
- Makarim Shirazi, Nashir, Tafsir Nemune, Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyyah, 1407 H.
- Sadiqi Fadaki, Ja'far, Irtidad; Bazgasht Be Tarikh; Negareshi Be Mauzu'-e Irtidad Az Negahaye Qur'an, Qom: Pazuheshgah Ulum wa Farhange Islami, Chapa ya kwanza, 1388 HS/2010.
- Tabari, Muhammad bin Jarir, Tārīkh al-Umam wa al-Mulūk, Mhakiki: Muhammad Abul-Fadhl Ibrahim, Beirut: Dar at-Turath, Chapa ya pili, 1387 H.
- Tabatabai, Sayyid Muhammad Husein, Al-Mīzān Fī Tafsīr al-Qur'ān, Beirut: Muasasat al-A'lami Lil-Mathbu'at, Chapa ya pili, 1390 H.
- Tusi, Muhammad bin Hassan, At-Tibyān Fī Tafsīr al-Qur'ān, Beirut: Dar Ihya' at-Turath al-Arabi.