Kufuta au kupaka juu ya viatu

Kutoka wikishia

Kupaka juu ya viatu (Kifarsi: مسح بر خفین) Dhana ya kupaka juu ya viatu (khuffaini) katika kutia udhu, ni dhana inayo maanisha kuchukua udhu kwa kufuta viatu au juu ya viatu katika amali ya kutia udhu, badala ya kupaka juu ya miguu, jambo ambalo kulingana na fat'wa za wanachuoni wa Shia ni batili na lililo sahihi ni kupaka moja kwa moja juu ya ngozi ya miguu bila ya kuwepo aina yoyote ile ya kizuizi. Walakini, jambo hilo linajuzu katika kesi ya taqiyyah na dharura.

Wanazuoni wa madhehebu ya Shia wakipinga huku hii, wamenukuu Aya ya 6 ya Surat al-Maida isemayo; ((وَ امْسَحُوا بِرُؤُسِکُمْ وَ أَرْجُلَکُمْ إِلَی الْکَعْبَیْنِ ; Na futeni vichwa vyenu na miguu yenu hadi vifundoni mwa miguu)). Kulingana na Aya ii, Mashia wanaamini kwamba; kufuta huko ni lazima iwe ni juu ya miguu yenyewe, na viatu sio miguu. Pia kwa kusisitiza hoja hii, wao wametoa baadhi ya Hadithi ili kuthibitisha madai yao, Hadithi ambazo aghalabu yake ni kutoka kwa Imam Ali (a.s). Kulingana na Hadithi hizo, ruhusa ya kufuta juu ya viatu imefutwa na Aya ya udhu.

Kwa upande mwingine, Waislamu kotoka madhehebu ya Sunni, wao wanakubaliana kwa kauli moja, kwamba kufuta juu ya viatu ni halali hata katika hali ya kawaida (bila ya kuwepo sinikizo la dharura). Waislamu wa Sunni wanaamini kwamba katika kutia udhu, miguu ni lazima ioshwe, iwapo miguu hiyo itakuwa haikuvikwa khufi, na haijuzu kufuta juu ya miguu hiyo, ambayo iko nje ya khufi. Ila suala la kufuta juu ya miguu limeruhusiwa katika hali ambayo miguu hiyo itakuwa imo kwenye khuri.

Ufafanuzi wa Mofolojia

Neno masaha ((مسح)) ni neno la Kiarabu ambalo humaanisha kitendo cha kupitisha mkono juu ya kitu. [1] Khufi ((خف)) ni neno la Kiarabu linalomaanisha viatu ambavyo vinafunika mguu mzima. [2] Kinyume cha khufi ni ndala, ambazo haziifunika miguu yote. [3]

Hukumu za Kifiqhi

Kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wa madhehebu ya Shia, tendo la kupangusa katika udhu ni lazima lipite juu ya miguu yenyewe, yaani juu ya ngozi ya miguu hiyo, [4] na sio juu ya viatu vya ngozi (khuffaini), kwa hiyo si halali kufuta juu ya viatu na wala haisihi kufanya hivyo. [5] Hata hivyo, wameruhusu kufanya hivyo katika hali mbili; katika hali ya taqiyyah [6] na katika hali ya dharura. [7]. Kwa hivyo kupangusa juu ya viatu, kwa maoni yao, itajuzu katika hali ambayo mtu atakuwa na hofu ya kudhuriwa, au kutakutwa na dharura fulani, kama vile wakati wa baridi. [8]

Masunni wao wana makubaliano (ijmaa) ya kwamba; kupagusa juu ya viatu vya ngozi ni halali; iwe katika hali ya dharura au katika hali ya kawaida. [9]

Ithibati za kisheria (kifiqhi)

Mafakihi katika kuharamisha kumpaka juu ya viatu (khuffaini) wametegemea ithibati ya Aya isemayo; ((وَ امْسَحُوا بِرُؤُسِکُمْ وَ أَرْجُلَکُمْ إِلَی الْکَعْبَیْنِ ; Na mpake vichwa vyenu na miguu yenu hadi kwenye vifundo viwili)). [10] [11] Kwa kuzingatia Aya hii, Mashia wanaamini kwamba; tende la kupaka linapaswa kufanywa juu ya miguu, kwa hiyo viatu havizingatiwi kuwa ni sawa na miguu. [12] Kama ilivyo kwamba suala la kupangusa kichwa linatakiwa kufanywa juu ya kichwa, na sio juu ya kilemba au kofia. [13] Katika Hadithi, Ahlul-Bayt (a.s) wameichukulia Aya hii kuwa ni hoja na ithibati dhidi ya imani ya kupangusa juu ya viatu. [14]

Kwa mujibu wa maelezo ya Hadithi ni kwamba; Imam Ali (a.s) alikuwa akiamini kwamba Mtume (s.a.w.w) alikuwa akipaka viatu vyake kabla ya kuteremshwa kwa Surat al-Maidah; Hata hivyo, baada ya kuteremka kwa Aya hii, hakufuta tena juu ya viatu, [15] na Aya hii ibatilishwa suala la kupaka juu ya viatu katika amali ya udhu. [16] Kwa upande wa madhehebu ya Shia, kuna idadi kubwa ya Hadithi zenye kukataza kupaka juu ya viatu. [17]

Kwa upande wa pili Masunni Ili kuthibitisha madai yao juu ya kuruhusiwa kupaka juu ya viatu, wao wanaamini ya kwamba; hata baada ya kuteremka Aya ya sita ya Sura Maida, bwana Mtume (s.a.w.w) bado alikuwa akipangusa viatu vyake katika amaili yake ya udhu. [18] Baadhi ya Masunni wameifungamanisha Aya na wale mtu wanaotia udhu hali wakiwa hawakuvaa viatu. [19] Fakhr Razi, Miongoni mwa wafasiri wa Kisunni, pia anaamini kwamba baadhi ya Masahaba walikuwa wakiamaini kwamba; si tatizo kupangusa juu ya viatu wakati wa kufanya amali ya kutia udhu. Akiendelea kufafanua, amesema kwamba; Masahaba hawakuonekana kupingana na amali hiyo, nayo moja ya dalili madhubuti juu ya kukubalika kwa amali hii. [20]

Rejea

{{Rejea}

Vyanzo

  • Āmulī, Mīrzā Hāshim. Al-Maʿālim al-maʾthūra.First edition. Qom: Nashr-i Muʾallif, 1406 AH.
  • Āmadī, Muḥammad Ḥasan. Al-masḥ fī wūdūʾ al-Rasūl. [n.p], [n.d].
  • ʿAyyāshī, Muḥammad b. Masʿūd al-. Tafsīr al-ʿAyyāshī. Edited by Rasūlī Maḥallātī. Tehran: al-Maktaba al-ʿIlmiyya al-Islāmiyya, 1380 Sh.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-. Mafātīḥ al-ghayb (al-Tafsīr al-Kabīr). Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Jazīrī, ʿAbd al-Raḥmān. Al-Fiqh ʿalā al-madhāhib al-arbaʿa. First edition. Beirut: Dār al-Thaqalayn, 1419 AH.
  • Khoeī, Sayyid Abū l-Qāsim al-. Mawsūʿat al-Imām al-Khūʾī. First edition. Qom: Muʾassisa Ihyāʾ Āthar al-Imām al-Khūʾī, 1418 AH.
  • Mūsawī Sabziwārī, Sayyīd ʿAbd al-Aʿlā. Mawāhib al-Raḥmān fī tafsīr al-Qur'ān. Beirut: Muʾassisat Ahl al-Bayt (a), 1409 AH.
  • Nawawī, Yaḥyā b. Sharaf. Al-minhāj sharḥ ṣaḥīḥ Muslim b.Ḥajjāj. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1392 AH.
  • Qurashī Bunābī, Sayyīd ʿAlī Akbar. Qāmūs-i Qurān. Sixth edition. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1371 Sh.
  • Ruḥānī, Sayyid Ṣādiq. Fiqh al-Ṣādiq. Qom: Dār al-Kitāb, 1412 AH.
  • Shahīd al-Awwal, Muḥammad b. Makkī. Al-Dhikrā al-shīʿa fī aḥkām al-sharīʿa. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt, 1419 AH.
  • Shāhrūdī, Sayyid Maḥmūd. Farhang-i fiqh muṭābiq bā madhhab-i Ahl al-Bayt. Qom: Muʾassisat Dāʾirat al-Maʿārif al-Fiqh al-Islāmī, 1426 AH.
  • Subḥānī, Jaʿfar. Sīlsīlat al-masāʾil al-Fiqhiyya. Qom: [n.p], [n.d].
  • Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1417 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Tibyān fī tafsīr al-Qurʾān. Edited by Aḥmad Qaṣīr al-ʿĀmilī. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].