Inqilab (Ya kifiq'hi)

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Inqilab)

Inqilab (Kiarabu: انقلاب) au mabadiliko katika elimu ya fiqhi: ni mchakato maalumu wa pombe hubadilika kuwa siki. Wanazuoni wa fiqhi wanauhisabu mchakato huu kama ni mojawapo ya njia za kutahirisha vitu. Katika istilahi za kifiq-hi vitoharishi huitwa Mutahhirat. Kwa mujibu wa fat’wa za wanazuoni wa fiq-hi, iwapo pombe itabadilika yenyewe au kwa kuongezewa vitu kama vile siki na chumvi na kuwa siki, basi siki hiyo itakuwa tahir (safi) na halali kisheria.

Uelewa wa Dhana ya Inqilab

Katika istilahi ya wanazuoni wa fiqhi, mchakato wa "inqilab" unamaanisha kubadilika kwa pombe kuwa siki, mchakato unaotokea kutokana na kuchemshwa au kuongezewa chumvi na siki kwenye pombe hiyo.[1] Wanazuoni wa fiqhi wanaihisabu "inqilab" kama ni mojawapo ya njia za kutahirisha vitu mutahhirat.[2] Neno "mutahhir" linatumika kwa maana ya vitu vinavyo tumika katika kusafisha kisheria kitu ambacho ni najisi.[3]

Tofauti Kati ya Inqilab na Istihalah

Makala Asili: Istihala

Katika tafsiri za kifiqhi zinajadiliwa na wanazuoni wa Shia, huwa kuna tofauti kati ya "inqilab" na "istihalah". Tofauti hizi zinawakilishwa kwa mitazamo miwili kuu:

  • Mtazamo wa Kwanza: Kwa mujibu wa baadhi ya wanazuoni kama vile Sayyid Kadhim Yazdi, mwandishi wa kitabu cha Al-Uruwatul Wuthqa, ni kwamba; kuna tofauti ya kimsingi kati ya "inqilab" na "istihalah". Kwa mtazamo wake, "istihalah" inahusisha mabadiliko ya asili ya kitu fulani, ambapo kitu hicho hugeuka na kuwa kitu chengine asili tofauti na ile asili yake ya mwanzo. Hii ina maana kwamba mchakato wa "istihalah" unahusisha mabadiliko ya kihalisia. Kwa upande mwingine, "inqilab" hutokea pale ambapo sura au muonekano wa kitu hubadilika bila mabadiliko ya asili ya kitu hicho. Katika hali hii, pombe inabadilika kuwa siki lakini asili ya mfumo pombe inabaki kama ilivyo.[4]
  • Mtazamo wa Pili: Baadhi ya wanazuoni kama vile Seyyid Abulqasim Khui wanaona kwamba mchakato wa "inqilab" ni aina ile ile ya mchakato "istihalah". kwa sababu katika muktadha wa kijamii na kisheria, asili ya pombe hubadilika na kuwa siki, jambo ambalo hupelekea pombe hiyo kuwa ni halali kisheria baada ya kupitia mchakato huo. [5]

Hukumu za Kisheria Kuhusiana na Mchakato wa Inqilab

Kwa mujibu wa vitabu vya maelezo ya sheria za Kiislamu, hukumu zifuatazo zimeelezwa kuhusiana mchakato wa inqilab:

  • Mabadiliko ya pombe kuwa siki: Ikiwa pombe itageuka kuwa siki wenyewe kwa yenyewe au kwa kuongeza vitu fulani kama siki na chumvi, pombe hiyo huhisabiwa kuwa ni safi na halali kisheria. Hii ina maana kwamba, baada ya mchakato huu, pombe haitachukuliwa kuwa najisi tena na inaruhusiwa kutumi kwa matumizi mengine kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. [6]
  • Pombe iliyotayarishwa kwa matunda najisi: Kwa mujibu wa maoni ya baadhi ya wanazuoni, pombe inayotokana na zabibu au matunda fulani ambayo ni najisi, haiwezi kuondoka hali ya unajisi kupitia njia ya inqilab.[7] Hii inamaanisha kwamba, hata kama pombe hiyo imegeuka kuwa siki, haitakuwa safi kisheria kutokana na chanzo chake cha awali kuwa najisi.

Rejea

  1. Tazama: Yazdi, al-'Urwah al-Wuthqa, juz. 1, uk. 258, 1419 H.
  2. Tazama: Imam Khomeini, Taudhih Masa'il Maraji', juz. 1, uk. 153, 1392 S.
  3. Tazama: Imam Khomeini, Taudhih Masa'il Maraji', juz. 1, uk. 123, 1392 S.
  4. Tazama: Yazdi, al-'Urwah al-Wuthqa, juz. 1, uk. 261, 1419 H.
  5. Tazama: Khu'i, Mausu'ah al-Imam al-Khu'i, juz. 14, uk. 159, 1418 H; Muasasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh, juz. 1, uk. 742, 1390 S.
  6. Taudhih Masa'il Maraji', Bakhsh Mutaharat Masail 198.
  7. Tazama: Imam Khomeini, Taudhih Masa'il Maraji', juz. 1, uk. 153, 1392 S.

Vyanzo

  • Imam Khomeini,. Taudhih al-Masa'il Maraji' Mutabeq Ba Fatawa Shanzdah Nafar Az Maraje' Muadham Taqlid. Tandhim Sayid Muhammad Hassan Bani Hashimi Khomeini. Qom: Daftar-e Entesharat-e Eslami. juz. 1, 1392 S.
  • Taudhih al-Masa'il Maraji'. Qom: Daftar-e Entesharat-e Eslami, 1385 S.
  • Khu'i, Sayid Abul Qasim. Mausu'ah al-Imam al-Khui. Qom: Muasasah Ihya' Athar al-Imam al-Khu'i. juz. 1, 1418 H.
  • Muasasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Eslami. Farhang Fiqh Mutabeq Ba Madhhab Ahl- Beit 'Alaihim as-Salam. juz. 1, 1390 S.
  • Yazdi, Sayid Muhammad Kadhim. Al-'Urwah al-Wuthqa (al-Muhassha). Tahqiq: Ahmad Muhseni Sabzawari. Qom: Daftar Entesharat Islami. juz. 1, 1419 H.