Nenda kwa yaliyomo

Ikrimah bin Abi Jahl

Kutoka wikishia

Ikrimah bin Abi Jahl (Kiarabu: عكرمة بن أبي جهل) alikuwa mmoja wa shakhsia wakubwa wa Kikureshi ambaye alikuwa akimfanyia uadui Mtume Muhammad (s.a.w.w). Hata hivyo alisilimu baada ya Fat’h Makka (kukombolewa Makka) na akawa miongoni mwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w). Mwanzoni mwa mab’ath ya Muhammad (s.a.w.w)(kupewa Utume) Ikrimah alikuwa miongoni mwa maadui wa Mtume na alipiaga vita vya Badr, Uhud na Khandaq dhidi ya Waislamu. Abu Jahl ambaye ni baba yake, naye pia, alikuwa miongoni mwa shakhsia wakubwa wa Makka na mmoja wa maadui wa Mtume (s.a.w.w).

Baada ya kukombolewa Makka, Mtume (s.a.w.w) aliwapa amani watu wote wa Makka, isipokuwa watu wachache, mmoja wao akiwa Ikrimah bin Abi Jahl. Ikrimah alikimbilia Yemen, lakini mkewe alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w) na kumuombea amani kwake, na kwa amani ya Mtume, Ikrimah alirejea Makka na akasilimu. Baada ya kifo cha Mtume, Abu Bakr alimfanya Ikrimah kuwa mmoja wa makamanda wa vita vya Ridda. Ikrimah hatimaye aliuawa katika vita vya Yarmouk.

Familia na sifa maalumu

Ikrimah alikuwa mtoto wa Abu Jahl, kutoka kabila la Kuraishi na ukoo wa Bani Makhzoom. [1] Kizazi cha Ikrimah hakikuendelea; [2] kwa sababu mtoto wake Umar aliuawa katika vita vya Yarmouk [3]

Ikrimah amechukuliwa kuwa mmoja wa watu wakubwa wa Makka [4] na wazee wa zama za Ujahilia. [5] Pia ametambulishwa kama mpiganaji maarufu [6] na shujaa. [7] Ummu Halim [8] au Ummu Hakim, binti ya Harith bin Hisham ndiye, aliyekuwa mke wake [9] ambaye alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w) na kumuombea amani Ikrimah. [10]

Uadui wake dhidi ya Mtume (s.a.w.w)

Ikrimah kama baba yake Abu Jahl, yeye pia alikuwa na uadui na Mtume wa Uislamu. [11] Alikuwepo katika jeshi la washirikina katika vita vya Badr na akamuua mtu kutoka kwa Ansari. [12] Pia aliukata mkono wa mtu ambaye alikuwa miongoni mwa waliohusika katika mauaji ya baba yake. [13]

Katika vita vya Uhud, Ikrimah alikuwa kamanda wa sehemu ya jeshi la washirikina. [14] Baada ya warushaji mishale wa Kiislamu kuondoka mlimani, akiwa pamoja na Khalid bin al-Walid aliwashambulia Waislamu kwa nyuma na kusababisha kushindwa jeshi la Uislamu. [15]

Baada ya vita vya Uhud, Ikrimah, pamoja na Abu Sufyan na Abu al-A’war al-Sulami, waliomba amani kwa Mtume na wakaenda Madina kwa ajili ya mazungumzo na wakamtaka Mtume aache kuyasema vibaya masanamu ya al-Lat, al-Uzza na al-Manat na atangaze kwamba, yana manufaa, ili kwamba wao pia wasiseme lolote kuhusu Mungu wa Waislamu. Maneno haya yalikuwa yalimuudhi  Mtume na akawaamuru waondoke Madina. Ni wakati huu ambapo iliteremshwa Aya ya kwanza ya Sura Al-Ahzab:

یا أَیُّهَا النَّبِیُّ اتَّقِ اللَّهَ وَ لا تُطِعِ الْکافِرِینَ وَ الْمُنافِقِینَ
(Ewe Nabii! Mche Mwenyezi Mungu wala usiwat'ii makafiri na wanaafiki.)[16]

Ikrimah alikuwepo pia katika vita vya Khandaq na akavuka handaki pamoja na Amr bin Abd Wudd na akaenda kwa jeshi la Waislamu na akarejea baada ya kuuawa Amr. [17]

Kusilimu kwake

Baada ya kukombolewa Makka, Mtume (s.a.w.w) aliwapa amani watu wote wa Makka, isipokuwa watu wachache, mmoja wao akiwa Ikrimahh bin Abi Jahl. [19] Ikrimah alikimbilia Yemen, lakini mkewe alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w) na kumuombea amani kwake, na kwa amani ya Mtume. Kisha akamfuata Ikrimah na kumleta Makka kwa Mtume. [20] Ikrimah aliporejea Makka alisilimu mbele ya Mtume na akala kaipo kwamba, kila alichogharamia dhidi ya Uislamu atakakitoa maradufu katika njia ya Mwenyezi Mungu. [21]

Baada ya vita vya Hunain, Mtume (s.a.w.w) aligawanya ngawira miongoni mwa Makureshi tu ili kutia nguvu nyoyo, mmoja wao akiwa Ikrimah bin Abi Jahl. [22] Wakati wa Hijjat al-Wada (Hija ya kuaga), Mtume alimfanya Ikrimah kuwa msimamizi wa ukusanyaji Zaka miongoni mwa kabila la Hawazin [23]

Baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w), Abu Bakr alimtuma kwenda katika vita vya Ridda na watu kama Ash'ath bin Qays [24] na Musaylamah [25] na baadhi ya walioritadi huko Oman [26] na akamfanya mtawala wa baadhi ya maeneo ya Sham. [27]

Kuaga dunia

Ikrimah hatimaye aliuawa katika vita vya Yarmouk mwaka wa 15 Hijiria katika zama za Khalifa wa Pili. [28] Mwanawe pia aliyekuwa akiitwa Omar aliuawa katika vita hivi. [29] Baadhi ya vyanzo vinasema kuwa, Ikrimah aliaga dunia katika vita vya Ajnadayn huku baadhi vikisema, aliuawa katika vita vya Marj al-Suffar. [30]

Rejea

Vyanzo

  • Balādhurī, Aḥmad b. Yaḥyā al-. Ansāb al-ashrāf. Edited by Suhayl Zakār & Riyāḍ al-Ziriklī. Beirut: Dār al-Fikr, 1417 AH.
  • Dhahabī, Muḥammad b. al-Aḥmad al-. Tārīkh al-Islām. Edited by ʿUmar ʿAbd al-Salām al-Tadmurī. Second edition. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1409 AH.
  • Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Muḥammad. Usd al-ghāba fī maʿrifat al-ṣaḥāba. Edited by Muḥammad Ibrāhīm Bannā, Muḥammad Aḥmad Āshūr, Muḥmūd ʿAbd al-Wahhāb Fāyid. Beirut: 1409 AH.
  • Ibn al-Athīr al-Jazarī, ʿAlī b. Abī l-Karam. Al-Kāmil fī l-tārīkh. Beirut: Dār Ṣādir, 1385 AH-1965.
  • Ibn Aʿtham al-Kūfī, Aḥmad b. Aʿtham. Kitāb al-Futūḥ. Edited by ʿAlī Shīrī. Beirut: Dār al-Aḍwaʾ, 1411AH-1991.
  • Ibn al-Jawzī, ʿAbd al-Raḥmān b. ʿAlī. Al-Muntaẓam fī tārīkh al-umam wa l-mulūk. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1412 AH.
  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad b. ʿAlī. Al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Ibn Saʿd, Muḥammad. Al-Ṭabaqāt al-kabīr. Edited by ʿAbd al-Qādir Aḥmad ʿAṭā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1410 AH/1990.
  • Ibn Sayyid al-Nās, Muḥammad b. Muḥammad. ʿUyūn al-athar fī funūn al-magghāzī wa al-shamāʾil wa al-sīyar. Edited by Ibrāhīm Muḥammad Ramaḍān. 1st edition. Beirut: Dār al-Qalam, 1414 AH.
  • Ibn ʿAbd al-Barr, Yūsuf b. ʿAbd Allāh. Al-Istīʿāb fī maʿrifat al-aṣḥāb. Edited by ʿAlī Muḥammad al-Bajāwī. Beirut: Dār al-Jīl, 1412 AH.
  • Ibn Qutayba al-Dīnawarī, ʿAbd Allāh b. Muslim . Al-Maʿārif. Edited by Tharwat ʿAkkāsha. Cairo: al-Hayʾat al-Misrīyya al-ʿĀmma li l-Kitāb, 1992 CE.
  • Ibn Kalbī, Hisham b. Muḥammad. Jumhurat al-nasab. Edited by Nājī Ḥasan. Beirut: 1407 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿalā l-ʿibād. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-.Tārīkh al-umam wa l-mulūk. Edited by Muḥammad Abu l-faḍl Ibrāhīm. Second edition. Beirut: Dar al-Turāth, 1387 AH.
  • Wāḥidī, Alī b. Aḥmad. Asbāb al-nuzūl al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1411 AH.
  • Wāqidī, Muḥammad b. ʿUmar al-. Al-Maghāzī. Edited by Marsden Jones. Beirut: Muʾassisa al-Aʿlām, 1409 AH.
  • Ziriklī, Khayr al-Dīn al-. Al-Aʿlām. Eighth edition. Beirut: Dār al-ʿIlm li-l-Malāyyīn, 1989.